JAHAZI LA WASOMI TANZANIA LIMEGUBIKWA NA HUZUNI NZITO KWA KUONDOKEWA NA MDAU WAKE PROFESSA SEITHY CHACHAGE ALIYEFARIKI DUNIA GAHFLA USIKU KUAMKIA JANA. HESHIMA ZA MWISHO ZA MSOMI-MWANAHARAKATI HUYU NI KESHO JUMATANO UKUMBI WA NKRUMAH KUANZIA SAA SABA MCHANA. ATAKUMBUKWA KWA KUKATAA KUITA SEPETU KIJIKO KIKUBWA.

MUNGU AILAZE PEMA ROHO YAKE PEPONI - AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2006

    Pumzika kwa Amani. Amina.
    Tutakukumbuka...

    ReplyDelete
  2. Kwa heri Komredi Chachage! Umemaliza vita vyako pumzika kwa amani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2006

    Binafsi sitamsahau baba huyu maana alinipa changamoto kubwa sana nikiandaa safari yangu ya kuja huku ughaibuni bila shaka Bwana ametoa na ametwaa jina lake libarikiwe.utakumbukwa kwa mema mengi.Rambirambi kwa familia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2006

    Alikuwa hana uchoyo na elimu yake, na amesaidia wengi, binafsi najuwa nilipokuwa Mlimani. Mwenyezi Mungu amlaze pahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2006

    Mbona kafa kama marehemu Horace Kolimba alivyokufa! Mungu amlaze mahala pema mbinghuni! Nchi yetu imepata hasara.

    ReplyDelete
  6. Pumzika Comred,
    Huyu alikua bingwa wa kutoa tafsiri kwa vifupisho vya maneno kufikisha ujumbe murua na maridhawa.E.g NGO(Non governmental organization yeye alikua akiziita NEW GOVERNMENT OFFICERS)

    Uliyoamini,Uliyokemea,uliyotuasa na kuyapigania tutayaenzi na kuyaendeleza daima.
    AMEN.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2006

    Wewe FIKRATHABITI umekosea Prof Chachage NGO alikuwa anaziita Nothing Going On. Na sio New Government Officers. Pia Vifupisho e.t.c alisema huo ni uvivu wa kufikiri na akaviita End o Thinking Capacity. Utandawazi aliuita Utandawizi. Na sitamsahau kwa msimamo wake wa kusimama kwenye ukweli hata akisema kitu nani. Ndio Maana Bw Ben alikuwa hampendi lakini kwa sasa naona JK alimuelewa dhamira yake na alimuunga mkono, ndio maana alipokuwa anaagwa pale Nkuruma Hall, JK alituma ujumbe kuwa asipelekwe Njombe hadi yeye afike ili auage mwili wake. Ofcourse ni pengo kubwa katuachia

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2006

    Yes anony wa july 17 9.38:57AM umepatia kabisa kabisa huyu prof. chachage alivyokuwa anatafsiri baadhi ya maneno. NGO alitafsiri hivyo akiwa na maana kuwa watu kwenye NGO hawafanyi chochote cha maana hila pesa kibao. Na wakati huo huo alisema ukipenda pesa ya haraka join politics.

    HAngeweza kumpeda mkapa maana alikuwa na ile hali ya nyerere. na alitaja tabia za watu bongo kuweka mageti na kuta zenye miiba kuwa hizo ni dalili za kuwaibia watu. Ukiisha waibia watu unatafuta njia ya kujilinda hili wasikuingilie. life differences ndio inatufanya hivyo. Tunajihami baada ya kunyanganya waliotuzunguka.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2006

    kuna komredi moja amesema kwamba Prof. amemaliza vita vyake.mimi napenda kusema kwamba naingana naye katika hili.........ingekuwa ni hivyo basi leo tusingezungumzia ukoloni mambo leo unaokuja kwa style ya global economy.

    ninachoweza sema, ni kwamba prof. ameweka balaza kwa ajili ya wapigania haki. muda umefika kwa sisi tuliobaki tukikubaliana naye tufuate alichokisemaau kukifanya ,tukiona kuna makosa basi tukosoe ili kwenda vizuri na wakati.

    mapinduzi daima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...