
JAHAZI LA WASOMI TANZANIA LIMEGUBIKWA NA HUZUNI NZITO KWA KUONDOKEWA NA MDAU WAKE PROFESSA SEITHY CHACHAGE ALIYEFARIKI DUNIA GAHFLA USIKU KUAMKIA JANA. HESHIMA ZA MWISHO ZA MSOMI-MWANAHARAKATI HUYU NI KESHO JUMATANO UKUMBI WA NKRUMAH KUANZIA SAA SABA MCHANA. ATAKUMBUKWA KWA KUKATAA KUITA SEPETU KIJIKO KIKUBWA.
MUNGU AILAZE PEMA ROHO YAKE PEPONI - AMINA
Pumzika kwa Amani. Amina.
ReplyDeleteTutakukumbuka...
Kwa heri Komredi Chachage! Umemaliza vita vyako pumzika kwa amani.
ReplyDeleteBinafsi sitamsahau baba huyu maana alinipa changamoto kubwa sana nikiandaa safari yangu ya kuja huku ughaibuni bila shaka Bwana ametoa na ametwaa jina lake libarikiwe.utakumbukwa kwa mema mengi.Rambirambi kwa familia.
ReplyDeleteAlikuwa hana uchoyo na elimu yake, na amesaidia wengi, binafsi najuwa nilipokuwa Mlimani. Mwenyezi Mungu amlaze pahali pema peponi. Amina.
ReplyDeleteMbona kafa kama marehemu Horace Kolimba alivyokufa! Mungu amlaze mahala pema mbinghuni! Nchi yetu imepata hasara.
ReplyDeletePumzika Comred,
ReplyDeleteHuyu alikua bingwa wa kutoa tafsiri kwa vifupisho vya maneno kufikisha ujumbe murua na maridhawa.E.g NGO(Non governmental organization yeye alikua akiziita NEW GOVERNMENT OFFICERS)
Uliyoamini,Uliyokemea,uliyotuasa na kuyapigania tutayaenzi na kuyaendeleza daima.
AMEN.
Wewe FIKRATHABITI umekosea Prof Chachage NGO alikuwa anaziita Nothing Going On. Na sio New Government Officers. Pia Vifupisho e.t.c alisema huo ni uvivu wa kufikiri na akaviita End o Thinking Capacity. Utandawazi aliuita Utandawizi. Na sitamsahau kwa msimamo wake wa kusimama kwenye ukweli hata akisema kitu nani. Ndio Maana Bw Ben alikuwa hampendi lakini kwa sasa naona JK alimuelewa dhamira yake na alimuunga mkono, ndio maana alipokuwa anaagwa pale Nkuruma Hall, JK alituma ujumbe kuwa asipelekwe Njombe hadi yeye afike ili auage mwili wake. Ofcourse ni pengo kubwa katuachia
ReplyDeleteYes anony wa july 17 9.38:57AM umepatia kabisa kabisa huyu prof. chachage alivyokuwa anatafsiri baadhi ya maneno. NGO alitafsiri hivyo akiwa na maana kuwa watu kwenye NGO hawafanyi chochote cha maana hila pesa kibao. Na wakati huo huo alisema ukipenda pesa ya haraka join politics.
ReplyDeleteHAngeweza kumpeda mkapa maana alikuwa na ile hali ya nyerere. na alitaja tabia za watu bongo kuweka mageti na kuta zenye miiba kuwa hizo ni dalili za kuwaibia watu. Ukiisha waibia watu unatafuta njia ya kujilinda hili wasikuingilie. life differences ndio inatufanya hivyo. Tunajihami baada ya kunyanganya waliotuzunguka.
kuna komredi moja amesema kwamba Prof. amemaliza vita vyake.mimi napenda kusema kwamba naingana naye katika hili.........ingekuwa ni hivyo basi leo tusingezungumzia ukoloni mambo leo unaokuja kwa style ya global economy.
ReplyDeleteninachoweza sema, ni kwamba prof. ameweka balaza kwa ajili ya wapigania haki. muda umefika kwa sisi tuliobaki tukikubaliana naye tufuate alichokisemaau kukifanya ,tukiona kuna makosa basi tukosoe ili kwenda vizuri na wakati.
mapinduzi daima.