waziri mkuu el akiongoza waheshimiwa wabunge kula tizi dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2006

    Mh hawa wanataka kujiletea heart attack,maana hawana tabia kabisa ya mazoezi,wao ni vitambi tu.sasa sijui mzuka nani kawapa semina ya mazoezi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2006

    Namba tisa kweli naona kaishiwa pumzi haraka, naona alivutwa hili zoezi haliwezi, je huyo ndo JANET KAHAMA? yule alosaidiwa na dada yake na kuishi nae akaanza ngono na shemeji yake (Mzee Kahama) na kupindua ndoa ya dada yake wa damu? maana nasikia ni kati ya wabunge. Nakubaliana na Anony wa kwanza kabisa kuwa wanataka kujipatia heart attack maana bwana jadi ya mazoezi hawa hawana ni vitambi tu. sio kama wenzetu wazungu mpaka vibabu na vibibi unaona wamo tu kujikipu na mazoezi. Haya basi naona maendeleo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2006

    Asante mheshimia prime minister, wape mzigo ili akili zichangamke hizo mambo ya kulala hayatakiwi kipindi hiki cha kasi mpya na nguvu mpya, na kwa taarifa yao mwili uliochangamka ndio msingi mzuri wa akili kuchangamka na kuwa na straight thinking.
    nitafurahi kama hii ni shughuli ya at least every weekend. kwa kipindi chote wanachokuwa bungeni..
    ni kwa faida yao.....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2006

    Walikuwa wako kwenye competition maana na namba au ni mazoezi ya kawaida tu....
    sasa muheshimiwa mwema nae angeliona hili akafanya mabo kwenye jeshi letu la police kupunguza yale matumbo ya maafisa yanayo ning'inia kama ndizi mkunguni...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2006

    Kweli hii ni kasi mpya hivi mzee wa matrioni kuna siku alifanya hivi zaidi ya kufikiria kibaigwa na kugombana na wanakijiji wa mvomero kule Moro. Tuombe huyu EL asibadilike.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2006

    Trio Kaka hayo manguo si ajabu mhindi ama mwarabu mmoja kawapa ili kutengeneza mazingira ya kufanya biashara, rushwa hizi zipo sana hapa Bongo ndio maana unasikia mtu kanunua peni ya rais kwa milioni mbili kumbe ni mtaji wa kuficha maovu.Haya manguo peleleza utajua katoa nani na uone anataka nini.Ajabu sana nchi hii, kila kitu hakiendi bure.

    ReplyDelete
  7. Mchaka mchaka CHINJA mchaka mchaka CHINJA adimselema HADIJA kitambi matata hiya HIYA hiiiya hiiiya HIYA -hivi ndivyo walivyokuwa wanaimba hawa jamaa inaelekea walikosa nauli wakaanzisha mtindo huu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2006

    Kigerere upo serious na hiyo statement yako? Unaweza kutuambia umetumia vigezo gani kutoa hiyo 95% ukilinganisha na bunge lililopita. Kwani ni kipi hasa walichofanya cha maana, kupitisha bajeti zenye utata hivyo au? Aise watanzania sijui tutaamka lini na kuona ukweli wa mambo. Tuwe tunarison na kuchambua mambo kabla ya kuanza kubwabwaja.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2006

    Hiyo tenda ya pamba zote hizo za mashindano amekula bwana Malinzi, huyu naye amijikita vizuri kwenye system. Nilibahatika kuwa hapo siku ya mchakamchaka huo na kuokota machache.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2006

    Kigerera unao uhuru wa kuoa mawazo, lakini hili ulilotoa naliita wazo chokozi, unataka tuseme safi kabisa na ndiyo hasa lengo letu katika blog hii. Hizo asilimia tano ndizo walizofanya so far, tusubiri hizo 95 mwaka 2010.Huwezi kuwapa asilimia 95 wakati mambo yanaendeshwa kana kwamba wageni kabisa wa mambo, spika nafanya mambo kienyeji kuacha kiti kumpisha naibu wake eti kwa vile mkewe anaenda kutoa bajeti yake, hii ni failure katika itifaki za Bunge,wabunge hawajui hata sheria za bunge juu ya mavazi, ushabiki tu umeawala na kuwalima watu eti walete ushahidi je ikiwa kweli wanauwezo wa kufungua mashtaka.Mimi ninachoweza kusema, wana asilimia tano tu, nyingine tusubiri 2010.Ukitaka kujua busara ya Bunge walau sikiliza kambi ya upinzani hasa pale DR.Slaa anapochangia,utaona jinsi wapinzani walivyona busara.CCM kinachowaponza woga kwa rais na kile wanachokiita "collective responsibility" ambacho ni adui wa kuchangia hoja.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2006

    Malinzi yupi Jamali ama kaka yake?hawa jamaa nao wanafaa kujiingiza katika biashara hiyo maana wanauzoefu wa michezo, ila yatokanayo basi tuyaache kwa mtunza pesa wa Bunge na faida itakayotokea hapo, waulizeni Simba ile mipira waliyokuwa wanabeba akutoka TZ kwenda nayo Ufaransa kwenye mazoezi walifaidika vipi,ajabu na kweli.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2006

    Asee umenikumbusha mambo ya top layer nyakati hizo nikiwa St.Peter's pale MG, any way, kama utazingatia makelele waliyopiga so far ni katika kujihami na kujijengea kitu kiitwacho"trust", lakini makele yenyewe hayana maana sana kwetu sisi, angalia mambo ya mikataba, tuliyaongelea sana katika blog mbalimbali hasa ya Darhot wire, mambo ya takrima tulishayaongelea, mambo ya mikopo ya wanachuo ndio usiseme tumechangia sana katika blog ya darhotwire, labda tushukuru kwamba sasa wanasoma mawazo yetu ktk blog hizi na wanashirikishana, ona tulivyomjengea confidence dada Chifupa mpaka akawa mchangiaji mzuri kwasasa, hivyo hayo makelele ni mbinu ya kasi mpya utaona mwakani kasi itapungua hii ni sawa na mtu anayeoa atafanya kila kitu mwanzoni lakini baada ya muda mmh, ulionaje mambo yalivyokuwa kwa asjari wa miavuli si uliona kasi yao hakuna chochote cha uaskari wa miavuli na mbaya zaidi hata waheshimika wa nchi nao walikuwa huko bila kuonyesha uaskari wao wa miavuli, hizi ni mbinu za kisiasa umakiaveri huu, subiri utaona hakuna chochote pale, ubabaishaji tu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2006

    Timu nzima ya mawaziri wanajifanya wemetumwa na Mungu kuikomboa TZ, kumbe si chochote wala si lolote.Mbaya zaidi kila mmoja anajifanya anaijua Tz na kwa kutumia kasi mpya basi wanataka kuleta vya kuleta, unajua Watanzania tuko watulivu sana , leo hii ingekuwa nchi za wenzetu, Mramba na Wassira wangetakiwa kujiuzuru nyadhifa zao, huwezi kutumia pesa ya umma kutoa TAKRIMA katika jimbo lako, utashangaa wabunge maskini hata wa upinzani wamepitisha bajeti hiyo,Nendeni Manyoni na Itigi mkaone taabu ya maji,badala ya kutetea mradi wa Ziwa Victoria, Wassira anatetea pale Bunda. N a huyu Mramba bado anataka afanywe chifu wa sehemu yao, ni AIBU kabisa, nashangaa JK kanyamaza, huu sio uamuzi wa busara asilee mambo kama haya, tutafika wapi tusio na mawaziri?Jmani kwanini tunanyamaza hata katika hili, na huyo Sita wenu asilete utani, wabunge wote sio watani zake yeye awatanie watu wa pwani sisi tunataka awe seriuos na kwanza huyo mama sita si mwali wa kutangaziwa birthday yake, je angekuwa firts lady ingekuwaje? nadhani wangekuwa wanarudi Urammbo kila jioni kutoka Ikulu.Maskini, Tanzania, Tnaznia,nakupenda kwa moyo wote. Nadhani Mzee Kaduma inabidi awapelekee kitabu chake wakasome wawe na uzalendo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2006

    Kigerera upo soma waliyosema waunwana hapo ndio maana mwanzo nilikuambia unabwabwaja bila kufanya uchunguzi. Sio lazima uchangie kila jambo. Wewe ni mzuri sana kwenye kuchangia mada za UREMBO keep it up kwenye umiss. Masuala ya uchumi waachie wachumi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2006

    Kigerera UTANISAMEHE kama wewe ni muheshimiwa mmojawapo, ninachotaka kusema ni wazo lako ulilotoa kuwa Tyson na Muramba hawakufanya cha ajabu ili mradi kinawafaa wananchi, si kweli, kusema hivyo ni kutetea ubinafsi, mimi ni mmoja wapo wa wananchi wa jimbo la Mramba, unajua kwasasa kesha jenga chuki na majirani zetu na hili mimi silitetei, kwani kama ni hivi sasa hivi MUSOMA na Bitiama zingekuwa MBINGU, Mwalimu angetumia urais wake katika miaka ya mwanzo kupendelea kwake, unajua kwa watu wenye HEKIMA NA AKILI NA UPEO wa kuona mbali, watatumia methali ya charity begins at home kwa busara lakini si kama walivyofanya hawa waasi wa maendeleo ya taifa, Kigerera kama kweli una mtazammo wa kitaifa utaona kuwa hilo ni kosa ambalo lilipaswa kukemewa na hata muongoza shughuli za Bunge, hiyo ni takrima kwa kutumia pesa za umma, Bunda haina taabu sana ya maji kama Itigi ama Manyoni, na hata hizo barabara za Mramba hazina matatizo kama zile za kwenda Mtwara, ndipo hapa utaona mtindio wa ubongo unawagusa watendaji wetu, fikiria enzi za Magufuli, nadhani kama angefanya hivyo basi Bukoba sasa hivi ingekuwa British Kingdom, hawa hawakuwa na UBINAFSI, walikuwa na uzalendo, sasa ninachoomba ni kuwa wakweli, wamechemsha sana hawa akina Mramba, katolewa wizara ya fedha sasa analeta ubinafsi wa kabila lake! ajabu sana,sitaomboleza kwa hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...