konda anapowabania madenti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hivyo ndio vitu vinavyonitoaga machozi huko Bongo. Hawa watoto wanataka kusoma kwa nia moja! Wanataka wawe na usafiri wao kama wenzao wa private school! Lakini angalia mateso haya wanayopata hawa malaika, kwa sababu ya serikali yetu!
    Ina uwezo wa kutoa mabasi ya shule, kwa wanafunzi atleast wa primary!
    Lakini hela zao wanazila tena bila ya huruma!

    ReplyDelete
  2. Kwa jinsi mambo yalivyo ndio maana wakati nipo Bongo nasoma pale Aza Boy Makonda walikuwa wanakoma kishenzi yaani ni mkong'oto kila siku. Sijui siku hizi nani anawapa fundisho hawa watu.

    Serikali na wadau wengine wangeliangalia hili swala la Usafiri maana ni shida tupu kwa wakazi wa Tanzania kwa ujumla au wao hawafahamu kwa sababu wanapanda mashangingi?

    ReplyDelete
  3. Kikwete anatakiwa aseme something kuhusiana na tabia hii ya makonda wa daladala kunyanyasa wanafunzi tena watoto wadogo kama hawa. sasa kama hawa watoto wanakosa masomo kwa sababu ya usafiri na rais wetu anakaa kimya, si ndiyo kurudisha maendeleo ya kesho. Au ndiyo janja ya kupunguza idadi ya wasomi nchini? Kikwete, Lowassa na Mama Sitta siyo tu mkae kimya, mmechaguliwa kuwakilisha nchi kumbe sasa jaribuni kuwasaidia hawa ni watoto wenu, ni TAIFA la kesho. Wapigeni Mkwala hao wenye madaladala kama ufanyavyo kwenye UJAMBAZI. Kwangu mimi huu pia ni UJAMBAZI!

    ReplyDelete
  4. Msami mkwala hautoshi maana hawa wapo kibiashara, tuulize ule mradi wa mabasi ya wanafunzi chini ya Umoja wa Vijana uliishia wapi, tazama wabunge kila mmoja ana gari la thamani sana , lakini hawajali kabisa huduma za jamii ikiwemo hii ya wanafunzi.Pelekeni mtetezi wa wanafunzi bungeni, waziri hatowatetea kamwe, mbaya hana mtoto au mjukuu anayeteseka atetee watoto wa jirani ambao wote wanapelekwa na magari ya baba zao. Hapa ndipo inaonekana wazi mawaziri wakae nasi mitaani ili waone tabu hizi

    ReplyDelete
  5. Wewe Michuzi hebu toa hii hoja yetu sisi watu tuliokuwa mbali, kwenye daily news au vyombo vyovyote vya habari, kuhusu wanafunzi na usafiri KIKWETE anampango gani? Tunahitaji interview! Nipo hapa am ready! Monica Kiliba, Stockholm.
    Other wise tunaenda UN kuwashitaki.
    We need some percent za kodi ziende kwenye usafiri wa wanafunzi! Sio wote wazazi wao wanaoweza kununua magari au kuwapeleka privates! Hii sio haki special kwa mtoto wa kimasikini ambaye usikute alilala bila ya kula, halafu mchana anafight na watu wazima wenye TB zao! no, no, no, this is crime!

    ReplyDelete
  6. Katika blog yako hii Michuzi uliyotuambia awali kuwa tuppeane mawazo ya kuendeleza nchi yetu na kusaidiana kama MTANZANIA. Mpaka sasa hivi watu ambao wanamawazo ambayo ningependa tushirikiane kuandika barua kwa Rais wetu mtukufu kuhusu mateso ya mwanafunzi wa Tanzania, ambaye yeye ndiye dhamana, ni Huyo TRIOKAKA na KIGERERA.

    ReplyDelete
  7. Hiyo barua ambayo unataka kumshirikisha Trio kaka na kigerera itakuwa ni pumba tupu!! bora ungesema MK,ESPIONAGE,SAM NA KIDUME HAPO ZINGEPATIKANA POINTS ZA MAANA ZA KUPELEKA KWA HAWA WAKOLONI MAMBOLEO CCM NA SERIKALI YAKE! NAJUA MTAKUWA NA HASIRA SANA LAKINI HUO NDIO UKWELI, HAKUNA HAJA YA KUFAGILIANA BILA SABABU HAPA!!

    ReplyDelete
  8. Kama tanzania imefutiwa madeni na IMF na WORLD BANK kwa nini pesa walizo kuwa wanatumia kulipia madeni wasizipeleke kwenye kununua daladala za wanafunzi? Mzee mkapa aliacha akiba nyingi tu kabla ya kumaliza awamu yake sasa hizo pesa ziko wapi? Jamani serikali inashindwa kutoa angalau USD 20 million kununulia mabasi ya wanafunzi wa primary na sekondary? Mbona magali ya wabunge yamefanikiwa kununuliwa? mbona wenyewe wameuziana nyumba kwa bei poa? Kumbe ni wakati umefika wanafunzi kwa pamoja waweke mgomo wasiende mashuleni mpaka hapo suala lao la usafiri litakapo tatuliwa. Ikiwa serikali inaweza kukopesha wabunge magari ya kifahali ambayo wangeweza kujinunulia bila mkopo basi na shule zikopeshwe mabasi ambayo yatatumika kuwapeleka mashuleni. Hivi hizo pesa walizo uziana nyumba za Oysterbay serikali imezipeleka wapi? Hizo pesa za kodi zinaenda wapi hasa hizo walizo kuwa wana lipa madeni IMF na Benki ya dunia? Wanafunzi na Wazazi Bongo amkeni kumekucha anzeni mgomo wabaki watoto wa hao vigogo peke yao madarasani tuone kama hayo mabasi ya wanafunzi hayata nunuliwa?

    ReplyDelete
  9. Ndio askofu sawa sawa MGOMO, MGOMO na maandamano kama inawezekana! Tunataka support Michuzi! Usikalie mamiss tu, kumind watu matajiri!
    Lift up the poor kids also!

    ReplyDelete
  10. Wewe anony #2, hapo juu uliyesoma Aza boys na kupiga makondakta. Kwanza wewe ulisoma enzi hizo mkishafeli darasa la saba huko kwenu Tubuke basi unakuja kurudia darasa la tano Muhimbili primary au Ubungo NH, na unafanikiwa kuingia Aza boys au Tambaza. Siku hizi hakuna mambo hayo. Wakati wa enzi zenu za kurudia rudia shule, mlikuwa mkifika Form IV, mlikuwa na miaka 21. Ndo maana mlikuwa mnawaweza makonda. Form IV siku hizi wana miaka 16, hawawezi shuruba zenu babaake.

    ReplyDelete
  11. Wewe, Miaka haichagui Shule, Pia Maumbile ya Mtu na Nguvu za mtu sio lazima yaendane na Miaka. Kuna Wengi wana miaka 18+ lakini wana miili na nguvu za kutisha. Usitake kuniambia kutoka Form I mpaka VI hakuna atakae kuwa na nguvu au maumbile makubwa.

    Makonda kama hawajatafutiwa mikakati na Serikali au wadau wengine basi ni kuwa chapa tu kama hawapo Aza Boys wajeshi wako wapi? Wachapeni mpaka wajue uchungu wa wanafunzi wengi wao ni vijana hawana watoto ndio sababu hawajui uchungu wa mwana.

    Hakuna mtu anaye rudia rudia shule pale Aza Boy 99.9% wote ni vichwa au haujui kwa undani?

    ReplyDelete
  12. This is a real democracy in the making, people are freely expressing their Ideas, supporting/challenge their fellow citizens.

    The only downside that comes with this freedom though is cursing! I think it would be great if people will continue to agree to disagree without cursing or looking down on other people.

    ReplyDelete
  13. Ndio wandugu na jamaa, naomba nitoe maoni yangu kuhusiana na hili “janga la usafiri wa wanafunzi”. Lakini kabla sijatoa maoni yangu, ningependa kutoa koments’ kuhusiana na maoni mazuri ya hapo juu yenye lengo la kutendua kitendawili hiki cha usafiri.

    Kwanza kupiga makonda sio solusheni. Mimi nimesoma Azania, na ni kweli kuwa wakati ule niko shule nilishiriki kupigana na makonda, na nilishuhudia konda mmoja akichomwa na mwamvuli mbavuni. Nilishangilia, lakini ukiangalia kwa undani, yule jamaa ametoka nyumbani, labda hata chai hajapata, anaenda kupiga debe, usiku inabidi afikishe quota, asipofikisha, hana chake siku imeenda bure, na zaidi ana donda kuuubwa la mwamvuli mbavuni. Ukweli ni kwamba hawapendi kuwakataza watoto, ila Mwamba ngoma, huvutia kwake. Kama binadamu, jiweke kwenye nafasi ya huyu Konda, maskini wa watu anajaribu kufanya siku zisogee halafu wazalendo wenzake, maskini kama yeye tunaotumia mabasi, tunapanga kumdunda kwa sababu anataka kupata shilingi 200 badala ya shilingi 50. Mtanzania mwenzangu ungependa kuwa kwenye pozisheni ya huyu jamaa?, kumbuka yeye hakupenda kuwa hapo.

    Kuhusu Kikwete kusema kitu, jamani jamani nini maana ya Serikali. Serikali sio raisi pekee. Ni ukweli kwamba tuko nyuma katika uendeshaji wa shughuli za kila siku. Kuna chama cha wenye vyombo vya usafirishaji, kuna wizara ya elimu, kuna wizara ya maendeleo ya jamii, wanawake na watoto, wizara ya maendeleo ya vijana na zaidi. Na kila wizara ina waziri, (ma)naibu waziri na (ma) katibu wakuu. Watu kama kina Amina Chifupa, wanafanya nini Bungeni badala ya kuwatetea vijana, lakini bado tunataka Kikwete aseme kitu, au tuandike barua…mhhh.

    Miji yote mikubwa ina komwuniti transpoti. Dar, moja ya majiji makubwa Afrika na Duniani, tumemaliza UDA. Kitu kama UDA inabidi kirejeshwe na kiendeshwe kibiashara. Hata kama kutakuwa na m’bia atakayeendesha chombo kama hicho, basi apewe. Kitu muhimu ni kuwa serikali iwe na nguvu ya kudhibiti nauli. Duniani kote usafirishaji unatumika sana, na ni biashara moja kubwa sana. Serikali ingetakiwa kuangalia uwezekano wa ku-unify usafirishaji ili kuwe na kampuni moja kubwa au mbili ambazo zitafuata sheria na kuondoa adha kama hii ya wanafunzi. Na madereva wa sasa hivi wapatiwe kipaumbele kupata kazi kwenye makampuni hayo. Serikali haina uwezo wa kuunda tena chombo kama UDA. Sina maana serikali ni masikini ila ufanikishwaji na sustainability ya projekti kubwa kama hio itakuwa ngumu kwa serikali. Watafutwe wadau, sana sana wa ndani ili waweze kuendeleza usafirishaji Dar. Kwa hiyo bwa’ Askofu, hela sio tatizo, tatizo ni utendaji wa kazi, UDA ilikuwa inafanya kazi vizuri lakini nakumbuka nilikuwa napanda kwa shilingi 10 badala ya shilingi 20, namwambia konda asinikatie tiketi, basi shilingi kumi yake mfukoni, na kumbuka sikuwa peke yangu. ni rushwa ndogo ndogo ambazo zinakuja kututesa wote bila ya kujua.

    Halafu kitu kingine pia ni wazazi jamani, watoto wa shule za msingi kwa nini tuwapeleke wakapande mabasi. Mimi nimekaa Mburahati. Kuna shule za msingi kama tatu ambazo zinafikika kwa kutembea. Mimi nimesoma Mburahati shule ya Msingi na nilikuwa natembea lakini majirani zangu wamesoma Muhimbili, Bunge, Oysterbay, Upanga, Forodhani na Zanaki na walikuwa wanapanda mabasi. Kama sio kumtesa mtoto ni nini? Sehemu gani ambayo kuna makazi ya watu na hakuna shule ya msingi inayofikika kwa kutembea? Nimesoma Mburahati na nimefaulu kuliko wao waliosoma shule za mjini. Nilikuwa natoka shule saa nane, saa nane na nusu niko nyumbani wakati wenzangu wanarudi saa kumi au saa kumi na moja, na wamechoka kama walikuwa wanalima. Kweli mtoto kama huyu ataendelea vizuri shuleni? Hizi kasumba kuwa shule za mjini ni bora sio za kweli na zinawaumiza sana watoto.

    Ehh wajameni, hili ligazeti limekuwa kubwa mno ngoja niishiage hapa, nipeni maoni yenu na kwa pamoja tuliendeleze hili litaifa letu, Tanzania.
    dida

    ReplyDelete
  14. Asante sana trio kaka hilo bange la point! We knew you are something! Mabus ya private Tanzania yapigwe marufuku......unless kama ulivyosema.
    Nchi zote za maendeleo ndio hivyo hivyo, hakuna mtu binafsi anayekuwa na bus la abiria hivi hivi tu! Hiyo ndio njia ya kutokubagua abiria. Or school busses.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...