raha na karaha ya staili mpya ya twanga pepeta iitwayo 'mugongo-mugongo'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Huu ndiyo naita ujinga wa Waafrika. Ni upuuzi mtupu!!

    ReplyDelete
  2. balaa tupu alafu tunalia kwanini ukimwi umetusakama,

    ReplyDelete
  3. Ahhh wandugu hapo juu, hasira za nini lakini? Vitu kama hivi hulazimishwi kujiunga navyo na kama ukimwi, nani atapata ukimwi kwa kuangalia "mugongo-mugongo". Mbona Amsterdam watu wanauza nyuchi kama karanga na husikii ukimwi ukimwi. Hivyo ni vijisababu tu na kama una chuki binafsi sema bwana au sio. Ni kweli kwamba ukimwi unatupagawisha, lakini huwezi kusema kila kitu ni ukimwi. Na huu sio upuuzi, hizi ni burudani na utamaduni wetu. Tumebarikiwa kuwa na kina dada waliobarikiwa mugongo na wanaojua kukata mauno, basi tujivunie, kitu cha muhimu tujikinge na ukimwi, na sio tuache kuangalia utamaduni na kuuita upuuzi, hiyo nimekataa na huu sio upuuzi

    ReplyDelete
  4. we anony wa juu yangu! vitu vya maendeleo ndio muige na kufananisha africa na europe.....sio vitu vya starehe!

    ReplyDelete
  5. huyo anona anayeongelea amsterdam wanauza nyuchi ila umesikia wakifa kama sie ??? aibu tu starehe na utamaduni wetu unatuponza ukiangalia kwa sana sie hatujali kujikinga unadhani huo mgongo mgongo mwanaume mwenye kinywaji atawaza hata ndomu tamaa tu wataishia kumalziana !!!

    ReplyDelete
  6. huyo jamaa alipatwa na mfadhaiko akawavamia wacheza shoo au? heheeh

    ReplyDelete
  7. Staili nyingine inabidi zipigwe marufuku haziendani na utamaduni wa kiafrika, kwa kifupi zinadhalilisha wanawake. Hivi wanawake wale wanaopigania hali za wnawake hivi kweli haya huwa wanayaona au huwa wanatengeneza pesa (NGO).

    Assume ni demu wako si unaweza kurusha ngumi bure hapa na kuatarisha amani na utulivu wa nchi yetu!

    ReplyDelete
  8. anony wa tatu hakuna mtu anayeshikwa na hasira humu ila kila mtu anaruhusiwa kutoa maoni yake kulingana na uwezo wake wa kuangalia na kuchambua mambo...

    ReplyDelete
  9. Hivi tunaelekea wapi jamani maana mimi ninavyo jua utamaduni wetu hauruhu baadhi ya mambo kuanikwa hadharani namna hivi, ila sasa naona kile kiugwanjwa cha kwenda na wakati na kuiga kila lifanywalo na wenzetu wa magharibi(ughaibuni, kinaanza kutukolea vichwani.

    kabla ya kufanya mambo haya mchana kweupe na hadharani namna hii kwa kisingizio cha starehe na mitindo ya uchezaji, mimi binafsi ningedhani ni busara kama sex education ingeanza kuwa maongezi ya kawaida miongoni mwa jamii na hasa from family level.

    ReplyDelete
  10. Hii inachochea ULAWITI.Hatuwezi kukemea ulawiti wakati kuna staili hii ya mugongo mugongo, huyo jamaa analenga wapi unafikiri!TZ ngono inachochewa na vingi, Wizara iko wapi maana kuna wakati kulikuwa na Wimbo wa ASOSA wa Bomoa tutajenga kesho ulipigwa marufuku sasa hii MUGONGO MUGONGO VIPI!

    ReplyDelete
  11. Jamani watanzania saa nyingine tumezidi kutafuta mtu wa kumuonyeshea kidole.
    We ushasikia wapi mtu ambaye alikuwa yuko makini, hataki kujishughulisha na ngono, lakini baada ya kuona mwanamuziki fulani akicheza kwa staili fulani akaamua kufanya ngono? Tusidanganyane bwana.

    Mugongo or no Mugongo, kama we ni fuska utafanya ufuska tu; na kama we ni mtu wa kujilinda utajilinda tu.

    Sikatai kama wanamuziki wana jukumu la kuielemisha jamii. Lakini fasihi huburudisha pia. Na mara 1, 1 burudani kama hizi sio mbaya. Mila zetu enzi hizo kukatika ndio ilikuwa cheza yetu.
    I am not implying kuwa kila mila iendelee kufuatawa tu blindly hata zisizofaa.. lakini tusikimbia karibia kila kitu ktk utamaduni kwa kuhofia kuwa tutachoche ngono au jambo jingine lolote.

    Mtu anaenda kwenye sherehe kama za Twanga nahope atakuwa ni mtu mzima mwenye akili zake na kujua jema na baya. Na kama we ukienda muziki unajiskia kufanya ngono, basi unahitaji msaada wa kiakili kwa kweli.

    ReplyDelete
  12. Peter!

    Kweli huko makini? Sina uhakika!

    Je ni watoto wangapi wa kitanzania wanajua miziki yote na jinsi ya kuicheza? kama kweli ulisha kaa tanzania na mitaa ya kawaida!

    ReplyDelete
  13. ndugu yangu anony wa hapo juu samahami sijaelewa swali lako linalenga nini hasa. Na kwanini umedai siko makini... na suala la watoto kujua miziki ya Tanzania linahusiana nini na hoja zangu; au hoja za post hii kiujumla?

    Na ndio nimekaa Tanzania mitaa ya kawaida, maana mitaa ya ajabu siifahamu ni ipi hiyo

    ReplyDelete
  14. What the f-k ?!!! Hivi huyo dume anataka kufanya nini hapo! LOH! Ama kweli akina dada wkicheza ngoma zingine inabidi wawe na mabodegadi! Bila shaka alipatwa na mkong'oto!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...