jk akipozi na wadau chuo kikuu cha boston univesti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Ni vizuri sana JK kutembelea vyuo vikuu vya nnje, lakini mbona sijawahi kumsikia akitembelea vyuo vikuu vya hapa bongo?

    JK anaona vyuo vya nnje tu

    Je huu ni ustaarabu????????????????

    ReplyDelete
  2. Michuzi hapo kuna wanaotoka bongo? Mbona sura zote zijawahi kuziona bongo kabisa?

    Aliyeandika hapo juu nafikiri now we are learning in the future tunabadilika mambo taratibu.

    ReplyDelete
  3. Nadhani Rais anaogopa kurudisha Gentlemen degree yake pale alipoipata.
    Haiwezekana baba mwenye nyumba wanao wanapata tabu nyumbani wewe uko busy na watoto wa jirani, hata kama mwanao mmoja ancheza katika nyumba ya jirani. Mimi nadhani ustaarabu ni kuwajulia hari wale waliopo nyumbani 'then' ndio unamjulia hari yule aliyoko nje ya nyumba. KIJU!

    ReplyDelete
  4. Inabidi sasa kuanza kuheshimiana kuna watanzania wengi tu wana kwenda shule tena vyuo vikubwa tu hapa marekani na wengi wetu tuna jisomesha kwa kubeba hayo mabox na kuosha vizee kama mnavyo tutukana kila siku lakini nakukumbusha kitu kimoja wewe unayetoa matusi nitarudi Bongo siku moja na dollar na vyeti vyangu utanikimbia kama siyo kwenye interview basi hata barabarani, nachotaka kukwambia hapa marekani kazi zote zinalipa na tunaweza kujisomesha na kuendeleza familia zetu nyumbani kitu cha msingi unacho takiwa kujua kila corner ya dunia watu wote hawana focus sawa kumbe utakuta wengine vichwa ngumu na wengine smart na kama utakuwa smart utaosha wazee sana na kesho utakuwa na maisha mazuri kama siyo tanzania basi hapa hapa. Cha msingi ni kujipanga vizuri, hata wazungu wenyewe hapa hapa wana chamba mikundu na kujilipia shule mpaka wana maliza. Nina amini kabisa kama malipo ya kuchamba mikundu ingekuwa ni dollar 10 ama 15 per hour Bongo ni watu wengi sana wangeenda kuchamba na kujipatia riziki yao si ajabu hata baadhi ya mawaziri hasa wanaotemwa kabla ya kujiandaa. Sasa wajomba tulieni acheni longo longo fanyeni kweli saa ya ukombozi ni sasa.Chapa kazi kumbukeni hata nyumbani kuna omba omba, wasukuma mikokoteni wakulima vijijini na wasomi matajiri na kila mtu hapo anamheshimu mwenzake na maisha yanaendelea. Ndugu watanzania mkiendekeza ushua mtakuwa mnawaona wahindi kila siku wanaendelea na mtanzania wa kawaida anazidi kudidimia kisa USHUA/UCHEKIBOBU...AIBU TUPU!

    ReplyDelete
  5. Ewe MTANZANIA UGHAIBUNI!
    Mbona hueleweki, aliyetoa hayo maneno ya kukukashifu mbona hatumuoni hapo juu, au ndio njia ya kuwatusi wale wote wanafanya hayo uliyoyataja. Tafadhali andika mambo yasiyo na unyume wa maana!
    KIJU!

    ReplyDelete
  6. WEWE WATANZANIA UGHAIBUNI, STOP THAT NON-SENCE!! HIYO SPEACH YAKO WAJUMUISHE HAO HAO WATANZANIA MBUMBUMBU WENZIO ULIOKUWA NAO HUKO HUKO UNYONYWAJI SIO KWENGINE...OK? WEWE NADHANI ILITOKA BONGO DIRECT TO STATES, NA UKINYANYUKA HAPO NI BONGO TU!! GET A LIFE BABE! SHUT UR F*** UP OK!!!

    ReplyDelete
  7. Huyo JK lakini anajifunza? Au anapita na kukenua meno kwenye vyuo vya wenzetu? Anaona jinsi University zinavyotakiwa kuwa? Siyo UDSM kwa idadi ile ya watu maji yanapatikana masaa mawili asubuhi na masaa mawili jioni

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli mimi tangia mhesh. Jakaya ameanza ziara yake huko majuu kitu ambacho amekuwa akinivutia ni kutembelea vyuo vikuu.Nashukuru sababu nafahamu labda akirudi8 bongo kwa kuwa amekwenda na wanazuoni lukuki huko basi matatizo ya vyuo vya Bongo yatapungua kidogo iwe kwa kuiga mamabo mazuri toka huko.

    Lakini mimi bado niko naye Mhesh Jakaya.Sijamuelewa.Hivi lini alikuja kusikiliza wanafunzi wa vyuo vya Bongo wanayapi ya kutoa kwa taifa zima.TAbia hi imejengeka kwa viongozi wa juu wengi sana.

    Mfano hapa chuoni kwetu hatab ukimwita tu Mkuu wa Chuo Visingizio havishi sasa mkuu wa chuo hawezi kukubaliana na Raisi wake kuja kutembelea wanafunzi tena haamna gharama kubwa kama inayofanyika huyko ughaibuni.

    Sasa hivi wanafunzi wa vyuo vikuu TAnzania waainshi wa "kukomunika" yaani makate na chai asubuhi hadi jioni,lakini sijasikia achilia mabali raisi Kikwete hao viongozi wake wa chini wakihoji kwanini wasomi wa kesho wanishi maisha ya ajabu.Lkini andio haoi wa kwanza kuandamana na RAisi Kikwete hadi ughaibuni eti kutembelea vyuo vya huko.HIVI HUKO WANALIPWA?.

    Na hao watanzania wanaosoma huko naomba haya maswali muwaulizae hasa raisi jakaya mumuulize kwa nini Hatembelei vyuo vya nchini kwake kwanza?

    Inauma na inakera.

    ReplyDelete
  9. MR. NDABAGOYE pole sana umeongea kitu muhimu sana kwamba inashangaza kuona Mheshimiwa Rais na msafala mzito anazunguka miji mbalimbali marekani akitembelea vyuo vikuu na kudiliki kukaa na wanafunzi mbali mbali wa kibongo huku akipiga nao picha na mapozi ya kila aina, lakini ikija vyuo ya nyumbani anaingia mitini, mzee kiwanja noma hujui kama na yeye ana enjoy kuwa kiwanja? Anyway nisiende mbali nafikiri watanzania wengi nyumbani kila mkikutana na VIONGOZI kinacho tawala huo mkusanyiko ni malalamiko kem kem tumezoea sana kulalamika tunataka tufanyiwe kila kitu. Sasa mzee kikwete akija lets say Mzumbe ama mlimani utakuta kitakacho tawala vikao ni Chakula kibaya, hatuna fwedha za kujikimu, hatuna madawati, mkopo umechelewa sasa naona viongozi wengi wamechoka, hiyo mikopo yenyewe mkipewa hamrudishi hizo pesa za vitabu hamnunui, mnaenda kutanulia unafikiri yeye mjinga hataki ma frustrations yasiyo na msingi.Huku marekani akifika anaambiwa mzee tukuchangie walau $ 3000 za sunami bongo, mzee unapenda kupata BBQ kwa Abdallah, Mzee zawadi hii ya mama Salma na kila aina ya mambo matamu. Mkiacha lawama atawatembelea lakini mkitaka mpaka awatawanye kwa mabomu ya machozi itakuwa ngumu saaaanaaa kuja wakati labda ni jana tu amesign mpigwe mabomu ili mtawanyike na kuondoa kero. Nadhani mzee Ndabagoye hii tabia ya lawama inakera na kuuma sana acheni haka kamchezo atawatembelea na kupiga story nzuri nzuri tu!

    ReplyDelete
  10. Asante sana Mboroyasolo umejuaje kuhusu hii tabia? Nashukuru umenijibia hili swali vizuri kabisa nimejifunza hapa kwenu hakuna tabia ya kulalamika lalamika, lakini hawa wenzetu kila kukicha lawama kila wanachopewa hawalidhiki? sasa tufanyeje? Sikio la kufa halisikii dawa, nimeamua sasa na wenyewe wachangie walau kipesa kidogo maana gharama za elimu zimepanda, na nitaweka mikakati nimeongea na waziri muhusika ahakikishe tunarejeshewa hiyo mikopo pindi tu wamalizapo masomo kutakuwa na utaratibu muafaka, kopa uripe bwana. Sina zaidi nitajitahidi kadri niwezavyo kuwatembelea hapo vyuoni pindi nitakapo ridhika na tabia yenu hiyo ya kulalamika na maneno mengi bila vitendo.

    ReplyDelete
  11. hahaha, hahaha, ha ha hahahaha. Jamani acheni utani. Mnajua wengine mnafaa kuwa comedians, kama wewe MBORO-YA-SOLO. Umeongea point sana, lakini umeongea kiutani mno. Ndugu yetu NDAGABOYE ameongea kitu muhimu sana. na kwa majibu yako Mb...solo, bado hujamjibu, kwamba kama yeye mheshimiwa anapenda vijizawadi huko ughaibuni, basi japo angewatuma wafagizi wake wa Ikulu kwenda kuwatembelea wasomi wanaishi kwa sacrament ya bwana kila siku. Au woote walio kwenye uongozi serikali hii wanasafiri kwa wakati mmoja? wapeane basi zamu za kusikiliza makelele ya wanavyuo japo nao waumie masikio kwa zamu.

    hahaha, mnanifurahisha sana, hahaha hahahaha hahahahaha

    ReplyDelete
  12. MZEE KIKWETE UNAYASIKIA HAYO?
    Govt under fire for ’neglecting’ higher education

    2006-09-28 08:35:57
    By Hannah Mwandoloma and Lydia Shekighenda


    Perennial students’ problems at the University of Dar es Salaam have downgraded the once premier learning institution in the country to ’a great high school,’ a retired educationist Sekelaga Mwanjisi, has said.


    Mwanjisi blamed the government for sweeping the problems under the carpet, which she said had adversely compromised the quality of education at the institution.

    ’’UDSM is slowly becoming a one big high school and not a university anymore,’’ she said.

    The educationist’s views tally with the students’, who on Monday complained about overcrowding in lecture halls and halls of residence.
    They said some students are forced to sit on dusty floors to take notes during lecture sessions.

    Yesterday, The Guardian made its way into one of the lecture rooms and found students sitting on the floor during lectures.

    Mwanjisi said the education sector needs massive infusion funds to enable more deserving students to access higher education.

    She dismissed as baseless excuses that the government’s budget is hamstrung and proposed that the funds allocated to non-core sectors in the economy should be channelled to education.

    ’’It hurts me as a mother and a citizen to see that no one supports the students who are suffering,’’ she said.

    She said many people don’t understand when students complain about lack of government support in their education. She said inadequate financing to higher education is a serious problem the government must tackle urgently.

    ’’The government is to blame for the recent chaos at the University of Dar es Salaam over students’ loans,’’ she said.

    In an interview, the Dar es Salaam University Student Organisation (DARUSO) minister for academic affairs, Lession Goodluck, said lecture halls cannot accommodate the large population of students.
    Goodluck said the university has few lecture rooms, which cannot accommodate more than 1,000 at a go.

    As an example, he said, Nkrumah Hall, renowned for hosting heated intellectual debates, was designed for 500 people, but it has become a lecture theatre for over a thousand students.

    He said the semester system at the university also contributes to the problem because there are core courses that are taught in a single semester only, which forces most students to enrol for them.

    ’’This compels many students to register for the courses, resulting in congestion in the lecture halls,’’ he said

    Goodluck pointed out the Educational Media and Technology course, (code CT 201), which he said had attracted many students as a result of recent changes in the duration of the course from four to three years.

    ’’Usually, students are taught this course in the second year. However, this year all second and fourth year students taking education-based Bachelors of Arts and Sciences registered for the course,’’ he said.

    He said although there are more than 1,000 students who registered for the course, the university has no lecture rooms for such large population of students.

    He said the courses are popular because the students are assured of jobs upon graduating.

    ’’Business Administration Management (BM 100) is among the courses that attract many students because it is marketable,’’ Goodluck said.

    He said that, although they tried to divide the students into two groups and allocate the programmes more time, the university shelved the plan because it was straining available human resources.

    He said there are two lecture halls under construction near Hall Six at the university which will have a capacity of 1,000 students each.

    ’’We expected these buildings to be completed this year to alleviate overcrowding problems,’’ he said.

    Mwanjisi supported the students saying, ’’It is the responsibility of the government to provide loans to students joining the university, to offset accommodation, subsistence and transport problems,’’ she said.

    ’’The government must increase the education budget if it really cares for the people and the country,’’ she said.

    The scholar lamented that UDSM has been losing its clout in the region because of the myriad of problems students go through.

    ’’More students, especially girls, are joining the university today. Unfortunately, facilities at UDSM have remained the same for years without taking into consideration the growing population,’’ she said.

    SOURCE: Guardian

    Comment on this article

    ReplyDelete
  13. Ulichomwandikia JK ndugu yangu Ughaibuni haitoshi, nadhani ajaribu kupata ujumbe kwa njia ya picha pia ktk IPPMEDIA. Watu wamekaa chini na baadhi wanaonekana kupitia mlangoni wako nje ya Lecture theatre, tukumbuke hawa ndio anawatafutia hiyo mikopo nje ili waje kuipangalia vizuri katika utekelezaji wa majukumu ya serikari yake na kuondoa umasikini kama si kupunguza. Nadhani hawa wataalamu wakitoka vyuoni badala ya kuwa busy kufanya kaza watakuwa busy kuondoa machungu waliyoyapata.

    ReplyDelete
  14. Mh. Jk naomba hii tabia nzuri ya kuongea na wanachuo uionyeshe na hapa nyumbani. Asinyanyapae wanae wa Tanzania. Usikane kwenu. Kwenu ni kwenu tu hata kama Wazazi wako wamejenga Jangwani ambapo mvua ikinyesha kuna mafuliko.

    Mh. JK naongea haya kwa masikitiko makubwa kuona kwamba haufurahii watoto wako bongo.

    Mr. Michuchi forum hii inafana na ile ya kule uingereza ambako wenzetu wanafanya openly. Napenda Kujua kama JK anasoma maoni haya.

    ReplyDelete
  15. Sasa mzee JK ni mtu mmoja mnafikiri atayamaliza matatizo yote ya tanzania? Ni vigumu sana wenzangu inabidi tusaidiane katika haya matatizo ndugu zanguni. matatizo ni mengi mno.

    Inabidi katika suala la gharama za elimu watanzania wote waliosoma kuanzia wakati wa uhuru walazimishwe kulipia kiasi fulani angalau katika mfuko wa Elimu kwani mnafikiri Mwalimu nyerere alifanya vibaya kuwasomesheni bure.

    Mimi nitafurahi siku moja tanzania mkijenga jengo/tume/bodi itakayokuwa inapokea michango mbali mbali kutoka kwa kila mtanzania aliyesoma iwe tanzania iwe nje ya nchi kama ulisoma kwa mgongo wa serikali huna budi kuchangia kujenga tanzania yenye watu walioelimika vizuri.

    Serikali haina pesa lakini inawatu waliosoma katika mgongo wa serikali, hivi ni watanzania wangapi wamesoma bure. Tukianzia na waheshimiwa wabunge wa bunge la tanzania, Africa, africa mashariki. Nitafurahi siku moja kuona michuzi anatuwekea picha za watu baada ya vikao vya bunge, wakati wa kiinua mgongo wakiandamana kupeleka michango yao katika bodi ya elimu tanzania hii hiwe ktk kujenga nchi na shukrani kwa mwalimu kuwapa akiri bure.

    wanakwambia sisi wote kuna siku tutakuwa hatupo lakini tanzania itaendelea kuwepo lakini itaendelea kuwepo kama watu wake wataweza kushindana na ulimwengu wa sasa. Na kushindana ni elimu tu itawakomboa ni vinginevyo.

    Kama tutaendelea hivi nafikiri zile nyimbo"tazama ramani" "tanzania tanzania" kuna siku zitafutika.

    ReplyDelete
  16. jamani fungueni IPP MEDIA leo muone hali inavyosikitisha pale mlimani!

    ReplyDelete
  17. Inasikitisha sana ni balaa ndugu kabisa hivyo vyuo rais watu anavyotembelea wakiona nafikiri wanaweza kumkimbia kabisa. Tuwaombe IPP media waiondoe hiyo picha ni noma.

    ReplyDelete
  18. Anony 4:34,
    Picha hiyo( tazama hapa http://ippmedia.com/ipp/guardian/2006/09/28/75318.html) si muhimu sana kuotoa cha muhimu ni wahusika wote waone hali hiyo ilivyo.Kwa hiyo wategemee wasomi watokao kwa kukaa chini kama hao hapo pichani.

    Raisi wetu kama angekuwa kweli anvitembelea vyuo vyetu kama anavyovitemebelea hivyo vya huko ughaibuni basi sidhani kama hali hiyo ya hapo mlimni ingekuwepo.Kama ingekuwepo lakini kwa kiwango cha kukaa hivyo chini!

    Sasa achilia hapo kama vifaa vidogo tu kama viti hakuna je facilities nyingine kama vitabu zitakuwepo kweli?.Watanzania tujiulize kuwa generation ya wasomi itakuwaje hapo baadae.TUTAWEZA KUPAMBANA NA MBIO VURUGU VURUGU ZA UTANDAWAZI?


    TUNAOMBA RAISI WETU KIKWETE AONE MAMBO HAYA ILI KUWEZA KUJENGA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

    ReplyDelete
  19. Hivi nyie mnaosema JK hawezi kufanya yote huwa mna maana gani? Yeye si ndio anaongoza serikali? Serikali inaingia mkataba na raia wake na moja ya mambo yaliyomo kwenye mkataba ni kuhakikisha huduma za jamii zinatolewa. Wananchi wanalipa kodi kama wajibu wao na serikali ina shughulikia elimu, afya utajirisho (hali bora kiuchumi). Hii habari ati JK hawezi sasa alitafuta Urais wa nini? Kodi si watu wanalipa kwa kila kitu? Iwe unanua kiberiti, chumvi, dagaa vyote hivyo vinalipiwa kodi watasemaje pesa hakuna? Hizo bahati nasibu zote zinazochezwa sijui celtel, nipashe motomoto, Mwl Nyerere Foundation lottery n.k kwanini wasitoe asilimia 35 nakuipeleka kwenye elimu? Watawala wetu ni wajinga sana, uzuri nikuwa wanaongoza wajinga vilevile.

    ReplyDelete
  20. Mkuu Samora nakuona hapo mzee !!! mwili haukuwa hivyo ulivyokuwa pale Jitegemee!! wapi mwaipungu???

    ReplyDelete
  21. JK je unasoma haya maoni??? Huu ni ushauri wa bure, chukua ukaufanyie kazi.
    mwananchi

    ReplyDelete
  22. Ndabagoye elimu katika nchi yetu ni kitendawili nafikiri hata michuzi aliyeenda vyuo vya marekani anaweza kutwambia ni watanzania wangapi wako hata hivyo vyuo wanasoma. Sisi miaka ijayo ni watu wa kutawaliwa tu.

    Utaona sasa hivi badala ya kusoma watu wanachukua/wanatafuta vyeti tu. Na ndio maana utaona na vyuo vya nchini sasa vinaelekezwa huko. Tafuta cheti tu na huwe director, matokeo yake hakuna ubunifu wa aina yoyote. Kazi hata ukiwa na kampuni imbayo ni moja tu inatoa huduma ni kuomba ruzuku au kuomba wageni waje kutuendeshea.

    Wazee wetu akikwambia ana diploma kweli ukiona mambo anayoyafanya utagundua kuwa kweli amekwenda shule. Akiamua kuharibu anaharibu kimakusudi. Lakini sasa hivi tunakabiliwa na changamoto nyingine ambayo watu wanapata vyeti tu na siyo elimu matokeo yake tutakuwa na wataalamu hewa.

    Hakuna kitu kibaya kama hiki maana nchi zilizoendelea zina watu kibao nchini mwetu na haya wanayaona matokeo yake ktk utandawazi tutakuwa tunaibiwa hivi hivi. Tunasainishwa mikataba tusiyoweza kungamua kitu gani tunasaini.

    Viongozi wetu kila kukicha wanaimba nyimbo za kufufua elimu hila kinachokosa ni target. wapi hasa kuna tatizo hili palekebishwe hawajajua. Kwa sababu tayari elimu imeoza hawajui ni wapi waanzie. Hili tusubili miaka kumi ijayo kama hakujakuwa na mbinu za makusudi mtaona.

    Swali la kujiuliza tanzania kwa nini wataalamu ni wachache lakini hata hao wachache wakati mwingine wanakosa kazi. jibu walioshika dira/wadau ubunifu hakuna sababu elimu walioipata haikuwasaidia kuona mbali.matokeo yake ofisini ni kusaini makablasha tu na kusukuma mbele siku imeisha.

    ReplyDelete
  23. Punch...a.k.a Mzee Punch
    Nitamalizia makala hii pale yaforum, ... youngafrican.com/360
    kati ya watu wote kwenye hii picha wengi hawasomi pale Boston, wengi hawana elimu, kati yao na majina yao ni sita (6) tu wana degree, wengine ni wazamia meli, wngine ni wanaishi USA kwa kufanya $ 7 mpaka 11 kwa saa.
    Kikwete ndani ya protocali alitakiwa kuchuja audience, 2% of those people got residence in USA, most of them are illegals, non educated, and never been to any college.

    ReplyDelete
  24. kwanza kabisa ningependa kumpa hongera zake JK, pili kumshukuru kwa kujitahidi kujitolea kwa kila dakika ambayo anaweza kuspea kwa wananchi wake walio mbali na TZ.Japo sisi wa Uk hatujamuona ila angejaribu kutuonyesha kuna nia ya kurudi nyumbani as how can he help us kurejea nyumbani NOT PROMISING BUT HOPES WOULD DO na pia kwa KUTUONGEZEA % ZA EXCEMPTION FOR RETURNING RESIDENTS ILI TUSIUMIE PALE BANDARINI KWANI TUKIRUDI NA VISENTI VYETU VIKIISHIA BANDARINI BASI MAISHA TENA BACK TO SQUARE 1. and as we all know we`ve been out of TZ for a very long time sasa fwedha yote ikiishia bandarini itakuwa ngumu sana kwetu.

    au mnaonaje waugaibuni`s

    kk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...