Home
Unlabelled
sarakasi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Muhidin,
ReplyDeleteWale ambao hawakuwahi kuliona hilo kundi sijui tuwaelezee vipi? Miye nilibahatika kuliona kwenye maonyesho yake ya kwanza 1974 Msimbazi Centre na ya mwisho 1980 Diamond Jubilee Hall na Jumba la Makumbusho ya Taifa. Pia nilibahatika kufundishwa sarakasi na wanachama wa kundi hili nilipokuwa chuoni Bagamoyo kama Marehemu Mwalimu Thomas Umila na Mwalimu David Twalib
Pia nilibahatika kuliona kundi la taifa la Urusi, Moscow Circus Assembly kabla halijasambaratika. Kilichowatofautisha Moscow Circus Assembly na Kikundi cha Taifa cha Sarakasi cha Tanzania ni contortionists wa Kirusi walikuwa wanajinyonga mpaka hujui kama huyu ni binadamu au kolokolo fulani. Jugglers yule wa Kirusi alikuwa anarusha mipira mingi mno! Balancing ya kipipa Warusi walikuwa wanapandisha mpaka meza nne halafu huku wanabalance wanaendeleza machejo mengine, na taofauti ya mwisho ilikuwa katika bendi, Warusi walikuwa wamekamilika zaidi kuliko sisi. Sijawahi kuona drummer boy yoyote anayepiga kit ya ngoma kumi na mbili, double bass drums, cymbal nne, cowbell, na latin percussion. Ile solo ya drummer boy wa Kirusi sijaiona tena maishani mwangu tangu siku nilipoiona ukumbi wa IFM takribani miaka ishirini na saba iliyopita.
Ijumaa na Jumamosi (15 na 16 Sept) ijayo natumaini tutajumuika pamoja mjini Bagamoyo katika wingi wetu na baadhi hawa jamaa wa kikundi cha taifa watakuwepo kwa hiyo tutakuwa na mengi zaidi kusogoa.
Masalaam,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Mtimkubwa, ni Fidelis Tungaraza?
ReplyDeleteMambo ya k'nyembe!!!?
Wewe Tungaraza, nakuuliza swali..kuna jamaa mmoja anaitwa Issa Yasini...yuko wapi? nae alikuwa kwenye kundi hilo la sarakasi...nataka kufahamu kwani tuliachana miaka mingi kule Uchina..
ReplyDeleteMichuzi hiyo picha kweli ni mwaka 1983? maanake ukiangalia background, watu, baadhi ya vitu inaonekana kama ni kwenye 60's au 70's achilia mbali suala la kusafiri kwa meli tokea China.
ReplyDeleteHii sio picha ya 80's.
ReplyDeleteMichuzi kamba hizo bwana.
Michuzi, seriously, umetudanganya bwana....that is not cool...credibility mjomba......
ReplyDeleteJamani hayo masanduku yamenichekesha sana.
ReplyDeleteTumsamehe Michuzi labda kalamu iliteleza kidogo. Ukweli hiyo picha ni ya mwaka 1969 kama sijakosea sana na hao jamaa walikuwa wamekwenda China miaka mitatu kabla kwenye miaka 1965/66 kutokana na mwaliko wa serikali ya China kwa mwalimu JKN.
ReplyDeleteHuyo jamaa wa mbele mfupi sikumbuki jina lake kwa sasa hivi lakini baada ya kundi hilo kuvunjwa rasmi yeye na wenzake walikuja kuanzisha kundi la BANTU ACROBATICS ambalo lilivuma sana mwanzoni mwa miaka ya 80 na yule wa mwisho kushoto ni bwana mmoja anaitwa BADI OMAR ambaye miaka ya 80 hadi 90 alikuwa afisa utamaduni wa Kigoma mjini lakini sasa ni Meneja wa hoteli moja ya kitalii kule Bangwe, Kigoma.
Michuzi dear get real sometimes eeh!
ReplyDeletekulaleki,hapo nilikuwa na miaka 2....
ReplyDeletePS:nice blog,michuzi....
chesi (,pilipili?) asante kwa sahihisho kwani ni kweli kalamu iliteleza. huo ulikuwa ni mwaka 1969. samahani wadau kwa usumbufu
ReplyDelete