baada ya wabongo kujikomboa kutoka kwenye makucha ya ndombolo na mayenu za kongo kwa silaha iitwayo bongofleva, sasa wametangaza vita dhidi ya sinema za naijeria zilizotawala kila kona kwa kuanza kutengeza filamu zao wenyewe. hapa prodyuza nassir anayesoma uingereza kwa sasa akisimamia shuting ya sinema yake sehemu za mikadi bichi kigamboni, dar. kumbuka kaka josiah kibira aliyeko minnesota tayari keshamwaga 'bongoland' na 'tusamehe' ambazo zimepokelewa vyema nyumbani na ughaibuni. sasa anaandaa 'bongoland II' ambayo ataishuti bongo karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ndo hapo hutoweza sikia kitu mzee,mawimbi ya baharini yote yako kwenye hiyo filamu.

    ReplyDelete
  2. Nassir CONGRATS from NYC unajua ni nani.....PEACE!!!

    ReplyDelete
  3. Nassir CONGRATS from NYC unajua ni nani.....PEACE!!!

    ReplyDelete
  4. Hii inafurahisha na kutia moyo. Ni kweli kuwa tunatengeneza filamu za Kitanzania ziwe kama za Ki-Nigeria wakati filamu za Ki-Nigeria zimejaa sokoni, kisha tunalalamika kuwa filamu za Kitanzania hazina soko. Nani anataka kununua kopi ya filamu wakati orijino ipo?!

    ReplyDelete
  5. na huyo mshika MIC ametoa mimacho hio doh si atawatisha hao wanao act

    ReplyDelete
  6. Huyo mshika MIC alikuwa na zinga la kikwapa bora walivyosuhuti bichi.

    ReplyDelete
  7. bado tuko mbali sana na sanaa hii ya cinema, lakini ndiyo mwanzo kesho tutafika na sisi walau walipo wahindi na picha zao, tusione aibu ku shoot japo kwa zana duni na mazingira duni kama haya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...