sanamu ya mwalimu chuo cha sanaa bagamoyo. je unakumbuka oktoba 14 tutakumbuka siku ya kufa kwake?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yes Michuzi kaka, tunaikumbuka siku ya Mwalimu, 14th Oct. pia je unamjua aliyetengeneza sanamu hiyo ya mwalimu pale Bagamoyo chuo cha sanaa? Ni rafiki yako mmoja aliyetengeneza masanamu ya sigara ya Safari.
    Pia tunaiomba serikali ikiangalie zaidi chuo hicho na ikiwezekana ifikirie kuanzisha vyuo vingine vya muundo huo, kwani kwa kuwa na chuo kimoja tu cha sanaa nchini, kunapelekea kuwepo kwa rushwa katika uchaguzi wa wanafunzi na pia kunarudisha nyuma maendeleo ya nnchi kwakuwa ubunifu ndiyo chachu ya sayansi, na maendeleo mengine. Tunawahitaji wasanii wawe wengi ili kuwezesha research na shuguli zingine za ubunifu ukiwemo ule wa kisayansi.
    Ukienda Europe, America nk. utakuta kila mwanasayansi, mfanyibiashara na watu wengi waliofanikiwa, wana background ya sanaa, ikiwemo uchoraji, music, na uumbaji sanamu etc.

    ReplyDelete
  2. Tanzania tuna hitaji kuwaenzi watu wengine wengi tu kama hivi. Hapo chuoni ningependa siku moja kuona sanamu la Hukwe Zawose.

    ReplyDelete
  3. Sijui kwanini hakuwaachia watoto wake akili na busara alizokuwa nazo yeye mwenyewe. kwasababu some of his kids if not all of them are a real disgrace to our country. Mungu azidi kumlaza mahala pema peponi.

    ReplyDelete
  4. Nakubaliana na mwandishi huyu tunapoelekea October 14;

    Hello Brothers n Sisters.,
    Hii barua niliipenda, nikaona nii-copy, paste nanyi muone.
    Asanteni.
    --------------------------

    Mbuya ori tata?
    Katika kuadhimisha miaka saba tangu Marehemu Mwalimu
    Julius Kambarage Nyerere ututoke, nimeamua kufanya
    hivyo kabla ya tarehe yenyewe kufika ili lau nikupe
    nafasi ya kutafakari nitakayoyasema.

    Kwanza Mwalimu watanzania wako bado wanakukukumbuka
    sana hasa wanapopambana na matatizo ambayo wakati wa
    uhai wako uliyatatua au kuyashiriki sawa na
    wao.Wanaikumbuka falsafa yako ya usawa wa binadamu.
    Kwa sasa kuna binadamu zaidi ya binadamu kutegemea una
    nini na nafasi gani.

    Tangu utuondoke Mwalimu watu wameanza kuona jinsi
    ulivyokuwa na mapenzi ya dhati na ya aina yake kwa
    nchi na watanzania. Kwani kama tulivyoambiwa kuwa
    wakati ukikata roho ulikuwa unasema kuwa unawaacha
    pabaya watanzania wako. Badala ya kumtaja mkeo mpendwa
    Mama Maria na watoto wako, ulikuwa unawalilia
    watanzania wako.

    Hayo ni mapenzi yaliyotukuka kiasi cha kuwafanya
    baadhi ya matapeli wa kidini kutaka sifa kwa kukutumia
    eti wakutangaze mtakatifu. Wale uliowaacha laiti kama
    wangefikia hatua ya kukata roho, wangesema "maskini
    wawekezaji wetu tunawaacha pa baya"

    Kitu kingine kinachofanya watanzania wakukumbuke ni
    utabiri wako kutimia wakati ukikata roho kule Guy and
    St. Thomas London tarehe ambayo haijulikani vizuri
    mwezi wa kumi 1999.

    Kama wahenga walivyowahi kusema kuwa si ajabu panya
    wakala viatu hata ngao ya shujaa maarufu kwa uuaji wa
    simba. Kwani tangu uondoke, wale ulioamini kuwa
    uliwafundisha wakakuelewa kumbe siyo, waliigeuza nchi
    chaka la wezi.

    Nguchiro, vinyamkera, vicheche na vinyama vyote vya
    usiku vilivamia nchi iliyokuwa ya watu na kuigeuza
    nchi ya wanyama. Yale maonyo yako kuwa Ikulu ni sehemu
    takatifu yalionekana upuuzi kwao.

    Kwanza tangu uondoke shilingi Bilioni tatu
    zilishatumika kuitia mkorogo Ikulu ukiachia mbali
    ulaji na matumizi mengine mabaya juu ya ununuzi eti wa
    mashine za kuditekti moto!

    Mwalimu sijui katika kuzinunua walitumia kiasi gani
    lakini najua kuwa Mungu aliwaumbua baada ya kutenda
    dhambi ile. Maana chumba cha Rais kiliungua wakati
    yeye na mkewe wakiwa nje wakitanua. Hatujui kama hata
    kwenye hekelu lao la kule Lushoto nako wameweka
    manjonjo haya.

    Pia tangu uondoke matumizi mabaya yamekuwa ndiyo
    mtindo wa maisha. Kwani kuna mdege mkubwa ya kisasa
    amenunuliwa Rais baada ya wananchi kupinga kuwa ni
    aghali sana. Unaitwa Gulf stream na hauwezi kutua
    kwenye viwanja visivyo vya kisasa kama wenyewe. Ili
    ujue hali ilikuwaje, Mwalimu bado nadhani unakumbuka
    kuwa kipindi fulani washamba wetu walikuwa
    wanashindana kununua mipete ya dhahabu na mikufu
    utadhani ni akina Defao. Kwa ushamba wao hawakujua
    kuwa mikufu ya Tanzanite na almas wanavyochezewa
    ndivyo mali kama wakiamua kuwa malimbukeni.

    Mwalimu wahenga waliwahi kusema kuwa simba aweza kuzaa
    mbwa. Haya ni kweli tangu uondoke. Kwani wale
    tuliowaamini kutokana na wewe kutuambia kuwa ni
    wasafi, walikuangusha vibaya wakageuka vibaka na
    manyang'au walioshirikiana na watu wanaoitwa
    wagenishaji na wawekezaji kuiibia nchi yetu. Wakati
    wakiingia tuliwajua kama mabwana na mabibi wasafi
    lakini wakati wa kutoka wameondoka wakiwa mabingwa wa
    uchafu tena waliondoka kimya kimya hata bila kuaga!
    Wangemuaga nani iwapo hata inzi walikuwa wakiwazomea?

    Kwa mfano, wao na mashemeji wao waliiweka rehani
    TANESCO. Ilipoingia serikali mpya ambayo samahani kuwa
    nilikuwa sijakuelezea kuwa kuna Rais wa nne, nayo
    serikali mpya inataka kuleta Makampuni wake wa Kigeni.
    Hii haikuingia na uwazi na ukweli bali kasi mpya nguvu
    mpya na ari mpya lakini kwa bahati mbaya wasaidizi wa
    jenerali wa batiani hii ni re-cycled sometimes or
    completely re-cycled.

    Hao waliokuwa wamekopa TANESCO kujua hivyo waliamua
    kufungulia maji yote kwenye mabwawa kiasi cha
    kusababisha ukame wakati wa masika.

    Hivyo Mwalimu kama ulivyotabiri, watanzania wanaishi
    kama nungunungu au popo kwenye kiza takriban kwa mwaka
    huu wote. Majenereta yanafuka moshi na kupiga mikelele
    utadhani Baghdad.

    Wahenga mwalimu walisema kuwa kutu hutafuna chuma.
    Najua kuwa uliacha marehemu NBC, DAHACO hata baadhi ya
    migodi vikiwa vimeishapigwa mnada. Nakumbuka
    ulivyokinusuru kiwanda cha nguo cha URAFIKI
    kisinyakuliwe na manyang'au na wakora.

    Sasa Mwalimu huwezi kuamini kinachoendelea kwani hata
    pale Musoma watu wameishapigwa risasi na kufa! Ya
    Bulyankhulu uliayaacha. Kisa eti wanakatiza au
    kujitafutia riziki kwenye sehemu zinazomilikiwa na
    wawekezaji.

    Mwalimu, huwezi kuamini kuwa hata wale uliowabwatukia
    kuwa wamejilimbikizia mali za wizi ambazo hawawezi
    kuzitolea maelezo sasa ndiyo viranja na manabii wa
    kuwahubiria watanzania wako injii ya watawavusha na
    kuwafikisha Kanani! Wenye akili wameishaanza kuonya
    kuwa huu ni mvinyo ule ule bwate lile lile au kanzu
    mpya lakini shehe yule yule.

    Kwa sasa viranja ambao wengi wao uliwasomesha kwa pesa
    ya mlipa kodi kutokana na wazazi wao kuwa makapuku, ni
    mabilionea wenye harufu ya utajiri na ukwasi utokanao
    na ujambazi na umalaya wa kiuchumi.

    Kitu kingine Mwalimu ni kwamba zile nyumba
    ulizowanyang'anya majambazi wa kiuchumi pale mwaka
    1967 zimeishatokomea. Kwani wale manyang'au si
    walizigawana na kuanzisha upuuzi mwingine eti kujenga
    nyumba za watumishi wa serikali.

    Mwalimu namshukuru Mungu kwani alikupenda mno na
    kukulindia heshima kwa kukuchukua mapema ili
    usishuhudie makufuru yaliyofanywa na wale uliodhani
    kuwa ni watu kumbe ni aina ya wanyama waitwao
    masupials. Wao na wake zao ni watu wa kutanua kwani ni
    matajiri kwa kutupwa. Watoto wao wanatanua ughaibuni,
    wakiugua mafua wao hata hawara zao hupelekwa majuu
    kupima hata mafua na uchovu wa kawaida.

    Kama kuna sehemu Mwalimu walikudhalilisha si kwingine
    bali kwenye msiba wako. Maana walitumia jina lako na
    kulinajisi. Eti walitwambia kuwa walitumia shilingi
    Bilioni moja na ushee kwa ajili ya mazishi yako
    utadhani ulikuwa Bilionea au mfalme.

    Walikutumia kutuibia pesa maana tunakujua ulivyochukia
    makuu ungekuwa hai usingekubali isirafu hii hata huu
    utakatifu wa kuchongwa unaotaka kupewa.

    Kabla sijasahau Mwalimu, kumbe ni kweli kuwa paka
    akiondoka mipanya hujitawala. Kwani baada ya kuondoka,
    ule mpapure uliotuachia uliota mabawa baada ya kunywa
    kwenye kombe la madaraka. Najua Mwalimu ulipenda
    kuchanganya na umombo kwenye hotuba zako. "Do you know
    what? The dugong-like thing played God and holier than
    thou to commit all buffoonery" The guy brought his
    gang of goons and kit of caboodle of devils in the
    sacred place. The holy of the holy was defamed God
    knows Mwalimu.

    Wapo vijana waliojaribu kuhoji hii Infallibility and
    corruption, unajua waliambiwaje? "Nyinyi ni wavivu wa
    kufikiri. Kwanza mna wivu wa kike. Basi kama
    hamnisifii wafadhili watanisifia" Huwezi kuamini
    Mwalimu kuwa utumbo huu ulisemwa na mtu aliyewahi
    kuingia kwenye darasa lako! Lakini ilitokea huu ndiyo
    ukweli. Kuwa kumbe ulikuwa unaishi na kulea michui
    iliyokuwa imevaa ngozi ya fisi.

    Enhee! Mwalimu ule Muungano uliouasisi mwaka 1964 kwa
    sasa umebaki kama kichekesho. Kwani serikali ya
    mapinduzi ya jimbo la Zanzibar hivi karibuni ilitoa
    amri ya kuwataka wabara kuwa na vibali kuingia huko.
    Huwezi kuamini kuwa hata kwenye uchaguzi wa 2005,
    wakati mtoto wa Rafiki yako aking'ang'ania kuendelea
    kukalia ulaji, wanajeshi na polisi waliwapiga
    watanzania wako kile kipigo cha mbwa mwizi.

    Najua wewe hukupenda cheo ambacho ni dhamana kurithiwa
    na mtu ndiyo maana hakuna mwanao uliyemuandaa kuwa
    mwanasiasa.

    Usishangae siku moja nikakuletea salamu toka nchi ya
    Tanganyika, Pemba na Zanzibar. Wala Mwalimu usishangae
    ukisikia msamiati wa Wazanzipemba,Wazanziafrika na
    wazanziarabu.

    Pia Mwalimu katika uchaguzi huo chama chako cha
    Mapinduzi kulipewa sifa na majina lukuki. Kwani
    kiliitwa chama cha Matajiri, Majambazi hata
    magabacholi maana pesa zilimwagwa kama njugu. Kumbe
    ule utabiri wako kuwa kuna kipindi Rais wa nchi
    ataamuliwa na mfuko wake. Hatusemi kuwa ilikuwa hivyo
    japo ndo hiyvo hivyo, ni kwamba uchanguzi huu ulikuwa
    ni matanuzi si kawaida.

    Hatujui hadi leo nani alimnunua nani kati ya watawala
    wetu na washitiri wao na wapiga kura wetu! Mwalimu si
    uliacha migodi ishapigwa mnada tena kwa bei ya "Tajiri
    leo kapata kichaa anagawa bure".Kwa taarifa zilizopo
    ni kwamba hata mbuga za wanyama na misitu na mapori
    hata vichochoro vya Msasai kama wawekezaji watavitaka
    vitauzwa kama utawala uliopo nao utaendekeza ulevi wa
    madaraka.

    Sisi tunasema watauza hadi kaburi lako Mwalimu kama
    hawatajitofautisha na wale waliofanya makufuru yote
    tuliyokusimulia.
    Enhee Mwalimu, pia tukukumbushe kitu kingine muhimu.
    Wewe ulishutumiwa kuwa ulibana uhuru wa vyombo vya
    habari. Afadhali yako maana kwa sasa huwezi ukajua
    vyombo vya habari viko wapi. Waandishi siku hizi
    wanaukwaa ukuu wa mkoa hata wilaya. Hii ni baada ya
    kutembeza kampeni hadi mtu wao kupita. Maadili ya
    vyombo vya habari hakuna.

    Kwani kama waandishi wapewavyo mishiko midogo ya elfu
    tano, waandamizi wanapewa maulaji ya vyeo. Hayo
    tuyaache. Ili tusikuchoshe sana, ndiyo maana
    tumekukumbuka mwezi mmoja kabla ya siku yenyewe ili
    uwe unajisomea taratibu.
    Pia nisisahau miaka kama miwili iliyopita, ilifikia
    mahali hotuba zako marehemu zikawa na mantiki na akili
    kuliko viumbe waliokuwa hai wakitangaza injili ya
    ubinafsishaji, ujambasishaji, ugenishaji,
    ushemesishaji.

    Kwanza walijifanya mabingwa wakawa wanaandika mihotuba
    mirefu, kavu na yenye ukali utadhani walikuwa
    wakihutubia wafungwa.

    Mwisho, ukimwi bado unaua. Ila ajabu Mwalimu si unajua
    wale TACAIDS. Basi Mwalimu wao wanachofanya ni kununua
    mishangingi ya bei mbaya, kuandaa masemina kwenye
    mahoteli ya kifahari na kupiga picha za Makete na
    kusambaza na kupata mshiko huku watu wanateketea.

    Mwalimu ile ajali ya kisiasa uliyokuwa ukitufundisha
    pale Pugu kumbe ilikuja kutokea ambapo wananchi
    walijuta na kusaga meno. Maana ilitokea hata watu
    wakaanza kuamini kuwa kumbe mtaua aweza kuzaa jambazi
    na bikira kuzaa kahaba!

    Kwa vile ulikuwa mtu wa kimataifa, hatuwezi kumaliza
    barua yetu bila kukupa lau salamu kidogo. Mzee Mandela
    na Rafiki yako Kenneth ni wazima. Yule rafiki yako wa
    zamani Obote na hasimu wako Amin waliishakufa.

    Pia kule Malawi yule Rais mfanyabiashara Bakili
    aling'olewa kwa aibu kama Chiluba walipong'ang'ania
    kunya sorry kuchafua katiba. Charles Taylor, yule
    jambazi wa kimarekani si unamkumbuka? Yuko ananonihino
    kwenye debe. Walimwengu wanawangojea majambazi wengine
    kama Meles Zenawi, Yoel Museveni, Paulo Kagame,
    Theodore Obiang Ngwema, Dennis Sassou Ngweso, Omar
    Bashir na Yahaya Jammeh.

    Kule Rwanda yule Rais Kibaraka aitwaye Pasteur
    Bizimungu aliishapinduliwa na mfalme Paul Kagame wa
    ukoo wa kifalme wa MUSEVENI ndiye anatawala akitumia
    vitisho na kutunza mafuvu ili dunia imuonee huruma na
    kumchukulia kama mtu aliyeituliza ile nchi ilhali
    ndiye alifanya mauaji ya marais watatu.

    Pia Marekani ilizivamia Afghanistan na Irak
    ikazipindua na inaendelea kuzikalia. Ila nayo sasa
    inajuta maana inapokea kipigo cha mbwa sawa na
    watanzania wako kule Zanzibar.

    Mama Maria ni mzima hata vijana wako nao pia.
    Watanzania hao maskini hawana uzima wowote zaidi ya
    kuishi kwa matumaini tu. Mzee Mwinyi naye ni mzima ila
    mvi zinamsumbua sana. Rashid hajambo jambo japo haishi
    kulazwa. Kingunge bado anaendelea kuwa kijana maana ni
    waziri! Hata John yupo na siku hizi amepoa si haba ila
    Ben amejificha sana maana alichowafanyia watu wako
    sijui!

    Mwlimu naona kwa taadhima na unyenyekevu nikuage
    nikikutakia mapumziko mema.
    Wasalimie Kwame Nkruma, Patrick Lumumba,Modibo Keita,
    Obafemi Owolowo, Nnandi Azikiwe,Ken Saro Wiwa, Gamal
    Nasser, Oliver Thambo, Walter Sisulu, Govan Mbeki,
    Steve Biko, Seletse Khama,Augustino Netto, John Garang
    de Mabior na mashujaa wengine uwajuao.

    Hizo ndizo habari za huku Mwalimu.
    Ni Binti yako akupendaye daima na watanzania wako
    Nthelezi Nesaa

    ReplyDelete
  5. Binti hongera kwa hiyo barua kwa Mwalimu.Labda kwa kuongezea tu ni kwamba hata elimu ya juu kwa sasa imekuwa ni tabu tu Mwalimu maana kwa kile2 chuo kikuu cha DSM ulichokianzisha kuna zaidi ya wanafunzi 17,000.Kwa hiyo pale ni kama sokoni na si chuoni tena.Kijana wako bado hajapatembelea.
    Pumzika baba.."AMIN"

    ReplyDelete
  6. kwakweli inasikitisha, ila nawaomba watanzania wenzangu tusikubali na kusubiri eti mungu au mwalimu aje afufuke atuokoe, kwani yeye mwenyewe hakusubiri ndio maana akatukomboa kwenye makucha ya wakoloni. KWA HESHIMA YAKE TUPAPAMBANE NA HAWA WANYONYAJI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...