Home
Unlabelled
mwalimu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ni: Mwitongo
ReplyDeleteSi: Mitongo
wewe uliyemkosoa michuzi hapo juu pia umekosea!
ReplyDeleteSIO: MWITONGO
NI : MWINTONGO
MIMI NAISHI HAPA, SASA BISHA....
Nilitundika Saa Wednesday, October 11, 2006 6:15:59 PM. Nikaandika si Mwitogo bali ni Mwitongo. Mimi natoka huko huko. Sisi tunaita, Mwitongo. Nyerere si Mkurya ni Mzanaki. Wazanaki wanaita "mwitongo", kama waitavyo Wajita kwa maana kwamba ni mahali palipohamwa but relics zake bado zipo, kwa mfano, in terms of makaburi ya mababu, miti ya matunda, na mabaki ya nyumba. Case closed!
ReplyDeleteMnabishania nini maana ya hilo jina ni kuwa ni sehemu ya watu waliojaa matongotongo.Kuitwe mwintongo au mwitongo kikurya au kizanaki hakubadilishi hali ya kutopenda kunawa uso asubuhi kuondoa tongotongo kwenye macho ya watu wa eneo hilo wawe wakurya au wazanaki asubuhi huwa hawanawi uso wala kupiga mswaki wanakurupuka tu kwenda kwenye shughuli zao.
ReplyDeleteNyinyi watu wa Musoma Kwa ubishi msije mkaanza kushikiana ubishi hapa.Case Close!!
ReplyDeleteMBONA KAMA LINASOGEA KULIA TARATIBU LENYEWE?
ReplyDeleteAkikasirika mpaka leo kifimbo chake kinacheza na yeye anasogea, siku ya mwisho alikishika kulia, shauri yenu.
ReplyDeleteWe Butiama,
ReplyDeletehata kama umezaliwa huko, lakini anavyosema Trio kaka ndivyo tulivyofundishwa shule kwenye history.
Sasa wewe kama unataka kuchokonoa vile unavyojua wewe, inabidi ukabadilishe vitabu vyote na uitishe breaking news.
vitabu gani hivyo vya historia? historia ya mwafrika imeandikwa na mzungu.Mnaambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro umegunduliwa na wazungu wakati wachaga walikuwa pale siku zote na nyie mnakubali.
ReplyDeleteRadioButiama,
ReplyDeleteTunajua Mwalimu Nyerere alikuwa Mzanaki, wewe hatuna hakika. Alivyoelezea kuhusu Mwitongo ni kama anavyokuambia Trio Kaka sasa hiyo unayojaribu kusema wewe labda baadaye itakuja kukubalika. Tafuta kama utaweza pata hotuba yake aliyotoa siku anakabidhiwa ile nyumba aliyojengewa na jeshi. Alielezea kuhusu Mwitongo. Anasema kuwa mwitongo ni mahame. Kuhama siyo mpaka lazima uende kilometa alfu hata mita kumi ni kuhama. Na walihama pale baada ya Chief Burito kufariki. Sasa kama Mwlm ni hakuwa anajua Kizanaki hilo mimi simo.
asante sana kuona mjadala wa Butiama umenoga.
ReplyDeleteMimi naitwa Manyerere Nyembereka, ingawa mara zote nimekuwa nikitumia jina la Jackton kama jina la baba yangu mzazi.
Kwetu ni Muhunda, Butiama, jirani kabisa na Mwitongo mnayoijadili! Mwitongo maana yake ni mahameni. Si kweli kwamba Mwitongo ni mahali pa kuzikia. Mwitongo ni mahali popote ambako mtu/familia iliishi, kisha ikahamia mahali pengine. Hapo palipohamwa ndipo panapoitwa mwitongo. Kwa hiyo, wapo watu wanaodhani kuwa Mwitongo ni kijiji! Hapana. Mwitongo ni kijisehemu tu cha mahame. kwa kuwa siku hizi maeneo yamekuwa finyu, ni wazanaki wachache wana Mwitongo, maana wakitoka walipo, wataenda kuishi wapi? Kila mahali pana mwenyewe!
Pia neno Mwitongo, hata Wanyarwanda-Watutsi na Wahutu, wanalitumia kwa maana hiyo hiyo ya mahameni! Kweli, inawezekana asili ya Wazanaki ni huko huko! Sina uhakika na hili.
Mchangiaji mmoja kataja makabila yanayoshabihiana na Wazanaki. Ni kweli kabisa kuwa Wazanaki, wangoreme, wakurya na kadhalika, wanasikilizana sana. Mimi naweza kuzungumza Kizanati, mwingine akazungumza kikura, mwingine akatwanga Kingoreme, au Kiikizu, sote tutaelewana tu! Kimsingi, haya si makabila, bali ni 'clan', yaani koo! Lakini Wajaruo, Wanandi, Wamaragori na makabila mengine ya aina hiyo, hatusikilizani nao kwa lugha. Lakini ajabu ni kwamba Wakisii tunasikilizana barabara!
asanteni,
Manyerere
+255 713 335 469