mchora katuni maarufu masoud kipanya (shoto) akipata mlo na mkewe na wapambe wao siku ya harusi yao wikiendi ilopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Duh Kipanya amependeza aswa!??????

    ReplyDelete
  2. We Masudi unaoa mara ngapi...Hongera sana

    ReplyDelete
  3. Brother Masoud Ki-mouse,
    Hongera sana kwa kupata jiko.

    ReplyDelete
  4. Duu jamani huyo mpambe wa bwana harusi mbona amejaza sana sahani hiyo?au ndiyo mara yake ya kwanza kuona hivyo vyakula nini?

    Huyu maasoud naye ameoa na vimwana wa Cloudz utawaachia nani?mwana mama unakazi za kila kulia maana huyo atakudanganya yupo kipindi cha kuchekesha watoto usiku wakati wameshalala.

    Nafikiri huyo masoud amshamprpmoti even muheshimiwa.

    Ila hongera sasa kama umeamua KUFUNGA ZIPU YA SURUALI.

    ReplyDelete
  5. Sasa bwana Michuzi mbona taarifa yenyewe hujaikamilisha? Huyo KP amefunga ndoa nani na shughuli ilifanyika wapi?

    ReplyDelete
  6. We anon 3:44:04 hata hujui matumizi ya punctuation marks.Hebu angalia ulivyochemsha!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. we kp umeamua kuoa utulie, funga zipu ya sarawali yako hiyo, harusi ya masoud ilifanyikia aghiti ipo maeneo ya victoria

    ReplyDelete
  8. Jamani hizi suit zikiwekwa label, mkononi kwa nje (kwa kushikizwa na uzi) label hizo huwa tunatoa tukitaka kuivaa!! Sio li label la HUGO BOSS unaliacha linaning'inia kama kengele ya ng'ombe!! Kaka Masoud hongera kwa uamwuzi wako wa kuepukana na UZINZI. Ushauri binafsi: Next time hiyo label itoe!!!!

    ReplyDelete
  9. Kwani huyu Masoud si Muislamu, inakuwaje glasi za bia? au Masoud jina tu sio dini? au ndi Waichilamu ta Bongo?

    ReplyDelete
  10. Kheeee heeee heeeeeH!
    Sikujua kama ukiitwa Masoud, shurti usinywe Bia...

    ReplyDelete
  11. Hongera sana masoud,naona na bonda boy hakuwa mbali,all the best guys!

    ReplyDelete
  12. jamani masoud hongera lakini mkewe mbona jina hatupewi, kafanana na shemeji yangu kwa mbali......kaka asije lia akirudi.....ha ha a hongera na kila la kheri this time....

    ReplyDelete
  13. Yule msichana wake aliyewahi kuwa Miss Dar City Centre, yule aliyeshiriki katika video ya profesa Jay si anaitwa nani Nargis? Waliachana?

    ReplyDelete
  14. Kp hongera babake na watakia kila la heri najua umechagua weweeeeeeeeee hapo ukafika mwisho natumai umeona mengi na sasa umeamua Mwenyezi Mungu awabariki.
    Na huyo Mrs Kp(jina hatujapewa) ila sio mbaya ni Mrs Kp au mama Malcom inabidi awe mwelewa wewe ni mtu wa Media there4 ni mtu wa watu wivu wivu usiokuwa na mpango utamnyima raha inabidi awe mwelewa wivu uwepo coz wewe ni something yake lakini sio wa kijinga akiwa hivyo mtaishi kwa amani sana. Kila la kheri

    ReplyDelete
  15. ACHA UPUMBAVU kwani ukiwa muislaam ndio huruhusiwi kunywa bia, unaonekana kabisa wewe ni TALIBAN kama inakukera kuona KIPANYA anabia nenda MSITUNI NYAMBAFU MKUBWA, huna cha kuchangia kaa kimya

    ReplyDelete
  16. Hongera Masoud!Mimi mshabiki wa kazi zako pia.

    ReplyDelete
  17. Jamani mi naitwa MASOUD KIPANYA, kwanza natamani kumlaumu michuzi kwa kuiweka hii picha humu kwa sababu najua mbali ya hongera najua nitapigwa madongo SANA lakini powa, nshazoea.
    kilichonifanya niandike ni kutaka mawazo yenu kutokana na ushauri niliopewa na mchangiaji mmoja kuhusu lebo za suti. eti mbona kuna watu wanasema hizo lebo za mikononi kwenye suti hazitakiwi kutolewa? nisaidieni mi si mjuaji wa kila kitu ndo mana sikutoa lebo.KP.

    ReplyDelete
  18. hiyo label siyo lazima uitoe Kipanya.huyo aliyeishangaa inawezekana alidhani hiyo ni price tag au nayeye mambo ya suti siyo richabo.hukufanya kosa kuiwacha hiyo label hapo...

    ReplyDelete
  19. Kama kweli wewe ndo MASOUD KIPANYA, basi ukweli ni kama alivyonanii Revd. EVM. Label huwa zinatolewa!!!

    ReplyDelete
  20. ebwanaee kama utani ulivyoanza kusema unamuoa SALMA sasa imekua kweli,du mchizi wangu hongera sana.

    ReplyDelete
  21. Uncle Zemarcopolo naona hapo umekosea kabisa...., label ya trade mark ya suti huwa inatolewa kama walivyoshauri hao jamaa.

    ReplyDelete
  22. Soko lililoungua ni la Mbeya si la Dodoma!

    Hizo label za nguo huwa zinaondolewa! Kuziacha ni overt mfano wa kutoa show-off "statement", penda tusipende!

    Label za mito ya kulalia, kukalia, magodoro na viti huwa zina maelezo kuwa zising'ofuliwe na kuondolewa. Hii ina maana ya kuhakiki ni kutoka material gani vitu hivyo vilitengenezwa. Na kinga kwa any lawsuit in case watengenezaji watapelekwa kortini.
    Lakini mnunuzi anweza kuondoa tu, kama akipenda.

    Kuna vijana wa nchi moja iliyoendelea ambao hupenda kuonyesha hizo labels kwa kuvaa nguo (hasa fulana na chupi)inside out ili maelezo kama hayo yaonekane, na kutangaza certain designer labels. Simply put: Navaa ya Chanel, Donna Karan, Dior, Gucci, Oscar de Relanta,
    Polo or Yves Saint Laurent!

    ReplyDelete
  23. Hii itakwambia jinsi gani wabongo wanavyoendekeza majungu ziko hoja nyingine nzito tuu za kutoa maoni imewekwa picha masudi kipanya angalia watu walivyojazana kurusha matusi na wengine utawajua tuu kwa kauli zao kuwa huyu inaonesha kuwa ni mtoto wa kiume aliyetandika viboko dada yake sasa anajaribu kufurahisha roho yake kwa kutusi shemeji zake kisa tuu kapindiwa dada yake

    ReplyDelete
  24. Masoud Kipanya umeangaika sana baba Umetangaza ndoa kwa baby Nargis,tukawa tuna kuona na kale ka baby MC Miss tz Fancy tukajua utakaoa mara umempata Salma haya kaka maisha ni yako na uamuzi ni wako tulia nae sasa usije ukamzalisha na kutengana najua uislam unaruhusiwa lakini si kiivyo unavyofanya magonjwa mengi sana siku izi.Hongera sana kwa uamzi wako wa kimaisha.Napenda kazi yako unavyotangaza na ndio maana nimeamua kuandika ivyo nikiwa kama mshabiki wako.Maisha mema ya ndoa.Thankx

    ReplyDelete
  25. Haya kazi kwako dada salma kwa kumridhisha uyo mumeo Masoud.Maana ameacha wa2 kibao kama Nargis,Fancy,Sarah na wngin hatuwajuai ambao amechukua chap chap.Masoud tulia bwana aaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  26. Watanzania tuache ujinga ,na umasikini wa mawazo ,wewe mwanaume unaacha kumtakia MASUDI afya njema na maisha bora na mkewe wewe unaongelea Label,wakati wewe unayeongeleo hayo umezoea kuona suti za baba yako za mwaka 1947 hazikuwa na label hiyo.....ACHENI UMASIKINI WA MAWAZO.....{Masoud BIG UP}

    ReplyDelete
  27. masoud kaka.we ni binadam, kila hatua unayopitia unapitia kama binadam na si malaika, unapoacha mwanamke mara nyingi unalaumiwa wewe, hawatazami makosa ya mwanamke, hawatazami ukicheche wa vitoto vya siku hizi vilivyojaa tamaa.NAMJUA NARGIS, ALIANZA KUDANGANYWA NA WACHIMBA CHUMVI AMBAO HAWAKUWEPO WAKATI UNAMPANDISHA CHATI. mi nakuelewa sana, una misimamo yako, naiheshimu kwa sababu wewe ni wewe. big up, i love what u doing brother. i always look up to you. and i concentrate on your strength. udhaifu wako haunihusu kwa sababu sote ni dhaifu. keep it that way kudadadadadadeki!! wanaopiga kelele wakamulie ndimu za macho. HONGERA!

    ReplyDelete
  28. Acha kumtia ujinga kwani wanaoandika hapa wote ni wanyama? Si binadamu?Mtu akifanya kazi au tabia nzuri lazima asifiwe na mtu akiboronga lazima aambiwe Isitoshe Mtu kama yy kioo cha jamii,ww unajifanya unamjua sana Masoud ilo halituhusu sasa mie ndiye ndugu yake wa karibu sana na inaniuma.Unajua ukiwa na mchumba lazima mchunguzane na mpaka mnatangaza ndoa mmeridhiana sasa iweje aache kama si kuchezee watoto wa watu 2.Haya Kp unachotakiwa sasa ni kutulia nae na sio uzae nae umuache kama sarah couz ana mtoto wako yule usimsahau ila na ww salma unamtoto na ulisha kuwa na mtu mkaachana kwa hiyo wote mnaakili za maisha.Nawatakia afya njema na maisha mema kwenye ndoa yenu mlioifunga majuzi.Ila unaujasili sana unafunga ndoa na kazini ulienda kama kawaida.Salma mme umepata kaka anaongea uyo kama amekula pili pili.Yoote hayo yamepita ninachotaka kuwaambia je mmepima HIV kujua afya zenu?.Kp usiseme umezoea madongo mengine yanakuwa ya kweli na ww unaye muambia akamue ndimu za macho sababu si ww ndio maana mbona ww unayemtu wako na mmetulia nae.haya nina mengi ila ngoja niishie hapa.Mjm

    ReplyDelete
  29. aaaaaah Aminia BABAKE. Hongera kwa kuoa. Ila jamani mkono wa suti yenye lebo si wa masoud ni wa mshkaji Francis Bonda, au Bonda Boy Kadogoo ambaye alikuwa anakula kwa utuliiivu saaana, hahahaha. kulia kwake kuna bibie..... mh mh!! hahahaha, We Bonda we!!

    ReplyDelete
  30. Dini ya Uislamu imekataza kunywa bia. Kama ukinywa bia basi huna Uislamu. Au umewahi kumuona Michuzi kunywa bia?
    Lakini nilichotaka kujua ni kuwa huyu Masoud ni Muislamu au la. Kwani kuna ubaya gani kuulizia? Mbona watu wengine kama anavyosema Michuzi hukosa adabu wanapotoa mchango.au ufudu huo?

    ReplyDelete
  31. Masoud ni muislamu na hajakosea.Koran inasema kama maji ya kunywa hamna muislamu anaruhusiwa kunywa chochote kukata kiu.Hivi huoni kuwa hapo mezani maji ya kunywa hamna? Ndio maana yeye na mkewe na wapambe wanakunywa bia kukata kiu maana ndio kinywaji pekee kilichopo hapo.
    From Sheikh Maulid Kibatari
    KIGOMA,TANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...