
mabaki ya ndege iloanguka mbeya jana na kuchukua maisha ya dada teddy nyantori mpiga picha wa maelezo dar, na kujeruhi vibaya abiria wengine akiwemo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu mh. juma akukweti. kada ya wapiga picha imempoteza mwenzao na mmoja wa wapiga picha wanawake wachache nchini. kwa picha na maelezo memgine mtembelee baragumu aliyetupatia picha hii


Pole kwa wafiwa, aidha sio rahisi kuamini kuwa alisalimika mtu katika ndege hiyo.
ReplyDeleteAidha shukrani kwa waakazi wa karibu na eneo la tukio kwa kuweza kuzima moto
Inasikitisha kusikia ajali hii mbaya imetokea, Pia napenda kuwapa pole kwa familia za watu walio poteza maisha au kupata majeruhi.
ReplyDeleteWote tupo gizani kwamba nini tatizo la kuanguka kwa hii ndege. Ukweli utapatikana kama wakiweza kupata Black box ili kujua mazungumzo ya mwisho ya marubani na kujua nini ilikuwa tatizo zaidi.
Nadhani serikali itaweza kutoa hizo sababu mapema iwezekanavyo.
Mwisho, Napenda kutoa tena pole kwa familia na wote walio kumbwa na hili tatizo.
Nashukuru.
pole kwa Familia ya marehemu wote waliopoteza maisha (nasikia mpaka sasa waliofariki wamefikia wawili ukiachia mbali na Terddy), pole kwa wanahabari. Nimefarijika kuona kuwa wapiga picha wenzie wamejipanga kumuenzi mwenzo, ni moyo mzuri na uendelezwe kwa wengine na na hata makanjanja.. Waliojeruhiwa nawatakia kila la kheri waweze kupona na kuendelea na shughuli zao harka iwezekanvyo. Nikiangalia hayo mabaki ya hiyo ndege, sijui hata hao waliopona walitokea mlango/mpenyo upi lakini yote hii ni kazi yake mungu.
ReplyDeleteMichuzi, tafadhali jaribu ku-contact mapaparazi wenzako walioko MB wakupe picha zaidi za hili tukio tujue nini kilitokea, mara nyingi hapa bongo ndege huangukia maporini ambako kupata picha na hali halisi ya tukio inakuwa ngumu. lakini hili nimetokea mahali ambapo ni richabo.
MICHUZI,
ReplyDeleteNaomba utuelekeze, kama unajua juu ya namna ndege hii ilivodhuru wengine ukiachilia mbali abiria waliokuwemo. Ina maana ilidondokea mahala peupe tu? Kama ni mtaani MBY, nahisi watu au vitu vilidhurika pia. Mbona hili halizungumzwi? Au kila kitu kilikuwa shwari tu, isipokuwa ndege na abairia wake? Maana umuhimu wa habari umekuwa tu kwa upande mmoja.
Nitafurahi kujulishwa.
MLALAHOI.