MWILI WA MAREHEMU JUMA AKUKWETI UNATARAJIWA KUWASILI LEO JIONI SAA MOJA NA NUSU UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE TERMINAL ONE.

MWILI UNATARAJIWA KUSAFIRISHWA KESHO ASUBUHI KUELEKEA TUNDURU KWA MAZISHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ni msiba Mkubwa kwa taifa kumpoteza kiongozi ambaye bado mchango wake ulikuwa bado unahitajika. Tumesikitishwa kuona kwamba yeye alikuwa kazini na ndipo ajali ilipompata ambayo hatimaye ilipeleka katika dunia nyingine.

    Tunaiombea familia ili Mungu awape faraja ya kweli katika wakati huu wa Msiba mkubwa. Pia kwa Viongozi wenzake ambao walikuwa karibu naye kikazi nao ninawapa pole. Mwisho kwa Watanzania wote. Wote tumeguswa na msiba huu kwa namna ya kipekee.

    Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe

    Nyangusi Ndukai - Dublin

    ReplyDelete
  2. Asha-Rose Migiro bosi UN
    Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu
    Na Mwandishi Wetu
    KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro (50), kuwa Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo.
    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Maura Mwingira, uteuzi wa Dk. Asha-Rose ulifanywa na kutangazwa jana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.
    Dk. Asha-Rose anachukua nafasi ya Mark Malloch Brown wa Uingereza aliyekaa katika wadhifa huo tangu Aprili, mwaka jana. Kabla ya Brown, nafasi hiyo ilikuwa ikishikwa na mwana mama Louise Frechette wa Canada.
    Kutokana na kuteuliwa huko, Rais Jakaya Kikwete, alisema hiyo ni heshima kwa Tanzania na Afrika kwa jumla kwa sababu ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo tangu kuanzishwa kwa umoja huo mwaka 1945.
    Rais Kikwete alimsifu Dk. Asha-Rose kwa kusema anajua ameteuliwa kwa sababu ana uwezo wa kushika wadhifa huo na kutekeleza dhamana aliyopewa.
    Kufuatia kuteuliwa katika wadhifa huo mpya, nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa aliyokuwa akiishikilia, sasa inabaki wazi.
    Uteuzi huo unaweka historia mpya kwa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini katika Umoja wa Mataifa kwa kutoa mtu wa kushika wadhifa huo.
    Kabla ya uteuzi huo, Dk Asha pia alikuwa ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje nchini tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.
    Dk. Asha-Rose Migoro alizaliwa mwaka 1956 na kupata elimu ya msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuanzia mwaka 1963 hadi 1966 na baadaye kuendelea na elimu hiyo katika shule ya Korogwe kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1969.
    Baada ya hapo aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Weruweru mkoani Kilimanjaro mwaka 1970 na kuhitimu mwaka 1973. mwaka uliofuata alijiunga na shule ya sekondari ya Korogwe kwa masomo ya kidato cha tano na cha sita ambapo alihitimu mwaka 1975.
    Mwaka 1977, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya kwanza ya sheria ambayo alitunukiwa miaka mitatu baadaye.
    Alijiunga na chuo hicho hicho mwaka 1982 kwa shahada ya pili ya sheria na kuhitimu mwaka 1984. Mwaka 1988, alihitimu shahada ya uzamivu (Ph.D) katika sheria kwenye Chuo Kikuu cha Konstanz nchini Ujerumani.
    Kwa upande wa ajira, aliajiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mkufunzi msaidizi mwaka 1981 na baadaye kupanda katika ngazi za mhadhiri msaidizi, mhadhiri hadi mhadhiri mwandamizi, cheo alichokuwa nacho mpaka mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa.
    Katika mwaka huo, aliamua kuingia kwenye siasa na kugombea ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa taasisi za elimu ya juu.
    Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, aliteuliwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nafasi aliyoishika hadi mwaka 2005.
    Januari, mwaka huu, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hadi kuteuliwa katika wadhifa wake mpya kwenye Umoja wa Mataifa.
    Vile vile, Dk. Asha-Rose kisiasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Katibu wa Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa ya NEC. Kwa nafasi hiyo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

    JK kuongoza mazishi ya Akukweti kesho

    ReplyDelete
  3. Ewe binti wa Kitanzania, hongera! Umepewa wadhifa wa myamba ya Umoja wa Mataifa waliokutangulia.

    Unarithi wadhifa wa bin wa Kiingerreza Mark Malloch Brown, ambaye wadhifa wake ni pamoja kufanya kazi na Secretary-General and the Deputy-Secretary General on all aspects of UN work, including helping to set out an ambitious reform agenda for the United Nations. He was once the Administrator of the United Nations Development Programme (UNDP), the UN's global development network, from July 1999 to August 2005. He worked for the UN system’s efforts to help support the achievement of the Millennium Development Goals -- eight, time-bound development targets with the overarching goal of halving extreme poverty by 2015 -- which were approved by world leaders at the UN Millennium Summit of September 2000. Before that he was at the World Bank as Vice-President for External Affairs, and Vice-President for United Nations Affairs from 1996 to 1999. He joined the World Bank as Director of External Affairs in 1994. He is credited with having helped the Bank enhance its outreach and expand its partnership with the United Nations and non-governmental organizations. In 1997, he chaired the United Nations Secretary-General's task force on the reform of United Nations communications.

    Hapo awali Mr. Malloch Brown had his own strategic communications management firm, the Sawyer-Miller Group, where he worked with corporations and governments. He advised Corazon Aquino of the Philippines when she ran against Ferdinand Marcos. Before that he published The Economist Development Report, a monthly report on the aid community and the political economy for development. He served as the Report's editor from 1983 to 1986. Previously, from 1977 to 1979, he had been the political correspondent of The Economist. From 1979 to 1983, he worked for the Office of the United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR). From 1979 to 1981, he was stationed in Thailand, where he was in charge of field operations for Cambodian refugees. He was appointed Deputy Chief of UNHCR's Emergency Unit in Geneva, undertaking extensive missions in the Horn of Africa and Central America. In 1981, the UNHCR and its staff were awarded the Nobel Peace Prize.

    Kabla ya Brown, nafasi hiyo ilikuwa ikishikwa na binti wa Kikanada, Louise Frechette. Mama Frechette alikabiliwa na scandal ya Iraq-UN Oil for Food baada ya ku-intervene directly by telephone to stop report ya Volcker isipelekwe mbele ya United Nations auditors from forwarding their Iraq-UN Oil for Food scandal investigations to the U.N. Security Council.

    ReplyDelete
  4. Kazi aliyokua ameenda kufanya Mhe. Akikweti Dodoma lazima ilikua na mambo,yaani soko alilokwenda kufungua limeungua na ndege aliyokua anasafiria imeanguka?Something is wrong mungu mwenyewe ndo ana_intervene.
    Orkakwi. London.

    ReplyDelete
  5. HII BULOGU INACHEKESHA SANA, MAONI YANAYOTOLEWA HAYAHUSIANI NA PICHA ILIYOTOLEWA NA MICHUZI HAPO JUU.
    TAFADHALI HAPA TOA MAONI YA MAREHEMU MHESHIMIWA AKUKWETI.
    HALAFU NENDA KWENYE PICHA ZA ASHAROSE MTENGETI-MIGIRO. UTOE MAONI YAKO HAPO. PICHA ZIPO MICHUZI KAZITOA. MSICHANGANYE WATU HAPA. AAAH!

    ReplyDelete
  6. WASEME UKWELI, SEREKALI MUSIFICHE KITU, NI CONISIDENCE GANI HII, BABA WA WATU SOKO ALILOENDA KUFUNGUA -LIKAUNGUA- HALAFU, KULIKONI?? NDEGE ANAYORUDI NAYO NYUMBANI PIA IMEKUTWA NA MKASA ULIOSABABISHA KIFO CHAKE HIKI. MH! WAJAMENI, TUSAIDIENI HAPA, HII SIO BURE, KUNA MKONO WA MTU HAPA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...