si mamboksi tu, kuna wadau wanakamata bango la matangazo kutwa nzima mitaani ukerewe kujipatia riziki. huyu ni mbongo ambaye baada ya kuniona akavunga kufa mtaa wa oksfodi striti...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Michuzi, umekunywa nini leo? maana yake kwanza ulianza na sex toys,sasa hii?!! sasa unakoelekea naona pabaya, wewe hata kama jamaa ndio kazi yake kinakuwasha nini? wewe jamaa unapenda sana sifa na comment kama hizo kwenye picha yako zinadhirihisha, si bora ya yeye kafika ulaya mwenyewe kwa nguvu zake na siyo kudandia misafara ya JK au study tour, saa nyingine unaonekana kama mtoto wa mjini kumbe bado bonge la mshamba, japokuwa jamaa simjui lakini sio freshi kulengesha watu namna hiyo, anatafuta rizki yake haibi wala hajipendekezi kwa mjinga mjinga yeyote yule, kua blaza! ukitaka minya tu hii comment lakini ujumbe wewe binafsi ushaupata.

    ReplyDelete
  2. Oyaa, Michuzi mi nakuzimia sana. Unajua sie wabongo tuliko nje kazi yetu kutuma picha nzuri za magari ya kukopa na safari zetu za Vegas. Kumbe tunachofanya hatukipendi!! Kwa nini jamaa anajificha?? jua hapendi anachofanya. Let's be honest we are slaving huku ughaibuni tupange mbinu za kurudi bongo. Kazi zetu ni kuchamaba mavi, kubeba mabox, kupokea simu na ... kubeba mabango!! Holaa

    ReplyDelete
  3. kazi ni kazi kama ni kuuza mihogo uza, kama ni kukwara samaki kwara tu bora mkono wako uende kinywani,( ali choki na wimbo wake ule....)...huna haja ya kuficha kazi yako....bilashaka 95 percent watanzania waishio ughaibuni hawafanyi kazi professional, sasa nyoote mkificha tutafikia wapi?.....JIVUNIE KAAZI YAKO

    ReplyDelete
  4. sidhani kama ni ustaarabu kumpiga mtu picha kama yeye hataki,anaweza kukufunga,kwani kila mtu anahitaji privacy, no wonder watu wanalalamika Rais anawatu wengi kwenye msafara wake abroad!kwa sioni faida ya mtu kaka wewe uwende then ufuatilie upuuzi !just try to be serious.Then sioni faida ya hii blog kwani its too personal! i hope unanielewa kaka!Halafu nataka kukomenti pia kwa huyu jama anayesema kuwa yeye kama mtumwa huku mbona hajarudi nyumbani?
    stop being silly!

    ReplyDelete
  5. Huyo jamaa achana naye sicho kilichokuleta hapo london,Fuatilia yule mhindi manake kesi yake iko hapo ulipo uhandishi wenu wa habari kazi yenu ni nini?

    ReplyDelete
  6. Ive always regarded you so highly muchuzi! you are such a thick motherfish! you are meant to talking positive things about TZ. kazi kazi

    ReplyDelete
  7. Wewe Michuzi umekosa kazi kweli. Yaani badala ya kufanya kazi zilizokupeleka huko unashinda kutwa kuangalia PICHA ZA UCHI na kutembea mitaani kuangalia watu ambao wanajitafutia riziki. Kama mtu mmoja alivyosema, no bora ungetafuta yule Mhindi aliunganisha RUSHWA ya milioni 12 dolali. Wewe kazi yako kula hela za walipa KODI tu, siku moja zitakutokea PUANI.

    ReplyDelete
  8. Wajameni kwa mtazamo wangu, Michuzi yupo sawa. Kama kazi ni kazi, huyu jamaa kwa nini alivunga kufa baada ya kumuona Michuzi? Yeye mwenyewe kwenye picha anaionea aibu kazi anayofanya wakati inampatia kula na kuishi ugaibuni. Tatizo siyo Michuzi, tatizo ni huyu muhusika kwa picha. Nina hakika kama asingevunga kufa, Michuzi wala asingempiga picha kwa ajili ya kuitoa kwa blog. Watanzania popote tulipo, ama ni bongo au ugaibuni tujifunze kuzipenda na kujivunia kazi tunazofanya. Kama unaionea aibu kazi yako, acha kazi vinginevyo nayo itakuonea aibu. Ndiyo maana kutwa mnatukanana na wabeba mabox ugaibuni, shida ipo wapi kama wenyewe wanaifurahia na kuipenda kazi yao! Onyesheni kupenda kazi zenu na kuziheshimu hakuna atakaye wadhihaki, hata kama ni kuosha vizee vya kizungu. Bora mkono uende kinywani na hawaaibiki kwa kugeuka omba omba.

    ReplyDelete
  9. MICHUZI UMENIFURAHISHA SANA! HAWA JAMAA WA UGHAIBUNI LEO UMEWAGUSA IMEWAUMA MAANA WAMEZOEA KUKANDIA BONGO KUMBE HAWANA LOLOTE.NA HUU NDIO UANDISHI KAMA HAMJUI,UANDISHI SIO MPAKA MTU AKUPE KIBALI KUMPIGA PICHA WALA KUTOA HABARI YAKE.

    KAZI YAO NI KUKANDIA BONGO TU NA KUSIFIA KWA WATU,WAKIJA HUKU BONGO NA MAJINZI YAO NA VIPAFYUMU WANATOA STORI NYIIINGI KWAMBA HUKO NJE MAMBO YAO SAFI,WANA-PARTY KILA SIKU,MARA PICHA KIBAO OOH HAPA NILIKUWA NIMEDRAIVU KWENDA WEST LONDON KULA MAISHA,OOH MARA ANAKUPIGIA SIMU ETI NDIO KATOKEA OFISINI KACHOKA SANA NA MACHO YANAMUUMA KWA KUTUMIA KOMPYUTA MUDA MREFU KUMBE FIKSI TU KATOKA KWENYE MABANGO NA MABOKSI.Haahaaahaaahaaaaa!!!!

    CHUMBA KIMOJA WANAKAA NANE KAMA VILE WAITING ROOM.RUDINI NYUMBANI MSIONE NOMA TUTAWAPENI MICHONGO.

    ReplyDelete
  10. Ili mradi mtu haiibi kazi ni kazi. Vijana walioko bongo au ulaya waacheni watafute maisha hapa Michuzi sijafurahi na hiyo picha kwanza yeye hataki pili ni kama vile unamkashifu sio vizuri. Hata walio maboss leo tz waliposoma ulaya walifanya hizo kazi so tusi discourage vijana, jamani ili mradi wawe organized na wakimaliza masomo warudi tujenga taifa letu. I love u all.
    Aurely

    ReplyDelete
  11. Michuzi hujaua hiyo ni sehemu ya taarifa ,kwa mtizamo wangu kama anabeba bango for schools fees big up my brother seen on the picture lakini kama ni kujikimu kimaisha there are better jobs at home
    Tafakari !!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. hata Rais wa kwanza wa Ghana Kwame Nkrumah pia ilibidi afanye kazi za 'box' maana ukweli kuanza maisha upya nje ya nchi yahitaji uvumulivu. Hivyo wabongo msiogope kufanya kazi za halali za aina yoyote mradi zinawapatia mlo, kulipia karo vyuoni, na baada ya muda mambo yatakaa vyema kama wenyeji wa Amerika na Ulaya. kumbuka siku zote mwanzo mgumu uwe umehamia London, New york au hata Dar-es-Salaam.

    ReplyDelete
  13. Hii picha itawanusuru wengi kukimbilia Ulaya bila ya kuwa na plan za kueleweka. Wengi tunaacha kazi za maana nyumbani na baadhi waweka maisha rehani kwa kuzamia kisa kuja Ulaya. Labda comment yako iko too rude lakini ndio ukweli wenyewe....watu inabidi tuukubali. Kwani inamaana huyu jamaa analipwa pesa ngapi hizo kumfanya mtu hata akimbie nyumbani. Twende Ulaya kwa malengo....maisha ni magumu tu kila kona ya dunia....tena ni bora kupambana nayo ukiwa nyumbani.

    ReplyDelete
  14. Hata hapa nyumbani kuna watu wanafanya hizo kazi mnazozidharau.Sijui wenzetu mna maisha gani maana tuliwafahamu toka zamani hamkua hivyo sasa hivi mmeendelea kelele kibao

    ReplyDelete
  15. Hey mimi sijui wanavyolipwa UK lakini USA kuvaa tu "winnie the pooh" au any other disney character suit ukae nje ucheke cheke na watoto ni $13 an hour. Summer time ni $11-$12 na unapewa free season tickets. Sasa kama una akili unawapa watu pass yako na wanakulipa hata half price of the ticket per day. At the end of summer you are talking about $2000 to $3000 extra. Kwenda disney land au anyother amusement parks sio cheap in the USA.

    Sasa sijui mnalalamika nini.

    Hii picha ni ya kuwaonyesha wabunge bungeni wakiwa kwenye session....Kweli watoto wao ambao ni good citizen na ni very smart kids wanaona ni bora wakafanye hizi kazi nje ya nchi kuliko kuishi TZ na kufanya kazi za kubeba briefcase.... Ni sad but it is true.

    ReplyDelete
  16. support to annony hapo juu,tatizo ni upumbavu wa watu hasa sisi wabongo,kuna ubaya gani jamaa akifanya hiyo kazi na kupata mshahara unaoringana na waziri huko bongo?Au ni bora awe officer bongo lakini yuko choka mbaya sana?

    ReplyDelete
  17. Akirudi Bongo utamuajiri akutangazie photo point? At the end of the day jamaa anapata pesa yake.

    ReplyDelete
  18. Hata Prince William kafanya u tea Boy enzi za shule.Ni kawaida huko UK.
    Michuzi mpe kazi afagie photo point umlipe £3 kwa mwezi.

    ReplyDelete
  19. MICHUZI UNASEMA NI MBONGO, UMEJUAJE? UMEONGEA NAYE?

    ReplyDelete
  20. MICHUZI!! KIINGEREZA NOT REACHABLE NINI? AU WE NI MTU WA PANDE.
    UNAMAANISHA NINI UNAPOSEMA"huyu jamaa akiwa mtaa wa okisfod stiriti" wakati mtaa si ndio stiriti!!

    ReplyDelete
  21. MY DEAR TANZANIAN .
    Kweli watanzania waishio ngambo wamekeleketwa na jicha hii ..ni kweli.Sijuhi kwa sheria za mass-media in Tanzania lakini kwa international journalism umevunja sheria(ethics of journalism) ..kwa kumpiga picha mtu bila ya hisani yake ...kwa madhumuni ya kumdharaulisha...Pili kutoa habari bila kuwa na uhakika, maana how sure you are that huyu mtu ni Mtanzania?hata kama umeona Passport yake au umeongea naye kiswahili siyo grant kwamba huyo ni mzaliwa wa nchi hii .Hivyo basi kama sikosei wewe ni journalist tena photo-journalist hivyo sheria kama hizo inabidi uwe makini nazo.
    Ok hata kama ni kweli sioni maajabu yaliyopo kwamba Mtanzania anabeba maboksi mbona ni jambo la kawaida sana . Basi wewe hujuhi huyu mtu wenzake wanavyo mwonea wivu hiyo ni kazi babukubwa mtoni..hizo HIACE unazoziona basi zinatoka kwenye mabango....halafu Bongo zinaleta ajira kwa maelfu ya watu ambao serikali haiwezi kuwapa kazi.Sie tupo mtoni lakini maisha ya nyumbani yanasikitisha sana.
    DOCTOR/////

    ReplyDelete
  22. Mtaa wa oxford strit ndio lugha gani wewe?

    ReplyDelete
  23. Ndugu michuzi nafurahi kwamba wewe ni liverpool fan kama mimi,lakini hii tabia yako ya kuweka picha nyingine ambazo hata hazisaidii kutujenga bali kubomoa,sasa kuna ubaya gani watu wakishika mabango,inawezekana hiyo ndio kazi aliyoipenda kama wewe unavyoipenda hii kazi yako ya kupiga picha na umbea,nina hakika kuna watu wasioipenda kazi yako ambayo wewe unajivunia,ni vizuri kuheshimu kazi ya mtu ambayo inamsaidia,wenzetu nchi zilizoendelea hawadharauliani kwenye kazi sababu watu wanategemeana kwa kazi wanazofanya.
    SAMAHANI NIKUULIZE MICHUZI ELIMU YAKO NI YA LEVEL GANI?INAWEZEKANA IKAWA SIO KOSA LAKO ILA NI ELIMU NDOGO ULIYONAYO NDO MAANA UNAPOST VITU VYA AJABU AJABU,JIREKEBISHE NDUGU NA KUMBUKA USIMDHARAU MTU SABABU BINADAMU HUJAFA HUJAUMBIKA.

    ReplyDelete
  24. Issa, safi sana kwa hiyo information ambao nadhani ni nzuri kwa vijana wetu wanaochipukia na wana mawazo ya kuzamia.

    Huku majuu kuna wengine wanafanya kazi za ajabu zaidi ya hizo na eti wadai bongo hawana uwezo wa kupata ajira! Wanatia huruma sana sana sana ukiwaona!. Ninachowashangaa zaidi eti wanadai wanapata hela nyingi kuliko hata mawaziri (kama mmojawapo alivyojigamba hapo juu,, bila hata soni). Lakini hela yenyewe inaishia kwenye kodi, chakula na kulipia monthly ticket za usafiri. Lengo langu ni kuwakumbusha wale walio BONGO na wanaowaza kuja Ughaibuni, jaribu kutafakari, je hao walioenda huko Majuu, wamefanyia nini familia zao zilizobaki huku? Tunaona ndugu zao wanakufa na wanashindwa hata kuja kuhani misiba kwa sababu eti watashindwa kurudi majuu! Ni jambo la ajabu sana!. Siamini, lakini hata kama kuna wazamiaji wasomi huku majuu, mimi wote naona hawajasoma ila wameenda shule! Kuna jamaa hapa wanaishi kwa dhiki kubwa sana sana. Kazi za kubahatisha, makarati ya kuuungaunga na hawana mwelekeo kabisa! Tafadhali vijana, tufanye kazi bongo. Zipo nyingi sana kama mnafikiria. Kama akili aifikirii kama ilivyo kwa hawa wa huku majuu, siwezi kukusaidia. Utaishia kutamba kuwa uko majuu, ili hali ndugu zako wanakufa akiwemo baba na mama yako, nyumba yenu imeanguka au inavuja, huwezi tuma hata hela. KISA, ETI MAJUU! Kila mtu anachagua maisha, lakini mengine, ya ajabu na yata watu wa ajabu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...