miss tz 1998 basilla mwanukuzi alivyo leo.

WADAU KUNRADHI. KWANZA NASHUKURU KWA MAONI YENU YOOOTE MLIOTOA KWENYE MADA YA URAIA WA NCHI MBILI. KWA KWELI NIMEFARIJIKA KUONA WENGI MMECHANGIA, ILA SEMA KUNA MAHALI TUMEPIGA KONA NA KUANZA KUJADILI MADA YA KUBAKI UGHAIBUNI AMA KURUDI BONGO. NAKILI KWAMBA HATA MIMI NILIJISAHAU NA KUELEKEA KUSHOTO. NAOMBA RADHI KWA HILO.
KWA MSEMO MWINGINE NI KWAMBA TOPIKI HAPA NI NINI FAIDA/HASARA YA URAIA WA NCHI MBILI. MADA YA KUBAKI AMA KURUDI ITAKUJA KWA WAKATI WAKE.
VILE VILE NAOMBA KUKANUSHA TUHUMA KWAMBA NAWAKEJELI WANAOSHUKIWA 'KUZAMIA' KWANI SI KWELI. MIE NAWAHESHIMU NA KUWAPENDA WADAU WOTE, SITHUBUTU KUMMBEZA MTU. HIVYO KILA NITALOSEMA SINA MAANA INGINE ILA KUFIKISHA UJUMBE NYUMBANI. SAMAHANI KAMA KUNA WANAODHANIA NAENDA KINYUME. HAKUNA BINADAMU ALIYE PAFEKTI.
KWA SASA NAWASIHI NA NAOMBA TUENDELEEE NA HII YA FAIDA/HASARA YA URAIA WA NCHI MBILI. JUMA LIJALO, MUNGU AKITUWEKA HAI, NITAFUNGUA MJADALA MWINGINE. NAOMBA NISIUTAJE SASA....
NAOMBA KUWASILISHA...
NA SIO VIBAYA UKICHUNGULIA HAPO CHINI KAMA ILIVYOLETWA NA DOGO MIKE MUSHI:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. WEWE MICHUZI MWISHO UTAANZA KUSEMA WACHEZA SOKA WOTE WA AFRIKA WARUDI KWAO KUCHEZEA TIMU ZA NCHI ZAO BADAYA YA KUCHEZA SOKA YA KULIPWA NA TIMU NZURI ZENYE MASRAHI. MICHUZI KABLA YA KUULIZA FAIDA NA HASARA WAULIZE HAO WAHINDI WANAOINGIA TANZANIA KILA SIKU WATAKUPA JIBU LA FAIDA YA KUWA NJE YA NCHI. WABONGO MMELALA MAHINDI YANATANUA HAPO MA SOUZI YANAKULA KILA KITU, MAKENYA YANAKOMBA KAZI KISA UMBEYA UMBEYA KAMA WAKO NA TU CHANGE KIDOGO TWA TRIP ZA KIKWETE ANGALIA ASIKUBASHIE, MTOTO WA KIHUNI HUYO KIKWETE...ENDELEA KUTUZARAU TULIO UGHAIBUNI LAKINI UNGEANZA KWA WAHINDI, WASAUZI NA WAKENYA WANAOTAMBA HAPO BONGO WASOMESHE WAENDE NCHI ZAO WASIKALIE KUTANUA BONGO USIKIE JIBU LAKE WEWE MICHUZI KIKWETE!

    ReplyDelete
  2. Michuzi angalia hapa uone wenzetu Wakenya walio nje wanavyopeleka pesa kwao kwa wingi kuliko hata DFI (direct foreign investment) za kutoka wawezekezaji wote waliowekeza Kenya. Na si ajabu wengi wao wana uraia wa huko waliko
    http://www.mshale.com/article.cfm?articleID=1248

    Je ni hasara gani watu kama hawa wakiruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili? Kuna hasara kweli ya nchi yoyote katika Afrika kuwanyima watu kama hawa uraia wa nchi mbili?

    Kuna uwezekano mkubwa kiasi cha fedha ambacho Watanzania walio nje wanaleta nyumbani kila mwaka kikawashangaza wengi kama kitapatikana (Hebu tumia umaarufu wako utafute kiasi cha pesa kilicholetwa na Wabongo walio nje katika miaka ya 2004 na 2005 toka bank ya posta ambao wanashirikiana na Western Union).

    Pia haitakuwa vibaya kama zikatolewa hasara za kuruhusu uraia wa nchi mbili. Naomba zisiwe za ujasusi na usaliti kwani majasusi na wasaliti wanaweza pia kuwepo hata Tanzania na tunaona mikataba inayosaliti nchi yetu kama ya Net Group Problems (makaburu wa Tanesco, IPTL, uchimbaji dhahabu, uwekezaji wa wageni n.k.) Hii yote inasaliti/imesaliti nchi yetu na hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa dhidi ya walioboronga.

    ReplyDelete
  3. Njadala huu ni mzuri na kuna mifano ya kuiga ama kutazama e.g. :

    Dual Citizenship for Overseas Indians Considered
    The Indian Prime Minister announced new regulations affecting Indians abroad in order to encourage the diaspora to invest in the country. India’s domestic industry raised objections to the possibility of dual citizenship.

    In advance of legislation granting Indians abroad dual citizenship, the Indian government announced a Persons of Indian Origin (PIO) card scheme. The cards will provide visa-free entry and a number of educational and financial benefits over such things as property and income earned on dividends. The scheme would also enable overseas Indians to cut through much of the country’s tangle of regulations.

    Prime Minister A.B. Vajpayee launched the card scheme while addressing the Global Indian Entrepreneurs Conference in New Delhi. The issue was also raised by the Union Urban Affairs Minister, Ram Jethmalani, at the 18th International Conference of Non Resident Indians in the same city in December. Vajpayee noted that Indians abroad had contributed over $12 billion a year in remittances for the past two years. The Resurgent Bond Issue alone raised $4.2 billion in a matter of weeks (see Traces #3). Members of the diaspora had been calling for dual nationality for a number of years.

    The Prime Minister also announced in November that a dual nationality policy would be implemented early in 1999. He also called on Non-Resident Indians (NRI) to invest in India’s new highway network, while Jethmalani asked for assistance in the country’s low-cost housing sector.

    These moves are regarded as part of a concerted effort by the BJP government to restore and strengthen links with Non-Resident Indians – objectives which were part of their election manifesto. They envisage not just economic links, following the success of China in tapping the overseas Chinese, but also enhancing ‘social, cultural, emotional and spiritual’ ties. They may involve reviving the NRI Consultative Committee under the chairmanship of the Minister of Finance, Yashwant Sinha. There may be modifications in investment rules and regulations, as well as more involvement of NRI entrepreneurs in advisory positions close to government. Some overseas figures have suggested that NRIs should be nominated to India’s Upper House of parliament.

    Opposition to the proposals for dual nationality has come from Indian industry, concerned about the threat of foreign competition if NRI investors are allowed greater access to India’s markets. Among the suspicions directed towards NRIs is the question of their divided loyalty, and whether dual nationality gives too many benefits to residents abroad. Spokesmen for Indian industry question whether the desirability of opening up investment opportunities also requires granting citizenship.

    Indian PM launches PIO card scheme to woo Indians abroad, Asia Pulse 12.11.98; PM Vajpayee assures dual nationality, benefits to expat Indians, Agence France Presse 12.11.98; New Delhi pledges greater emphasis on NRIs, Anand Sagar Gulf News 13.11.98; Industry upset over 'dual citizenship', V. Jayanth The Hindu 16.11.98; Tapping the Indian diaspora, The Hindu 23.12.98; 'Govt. considering dual citizenship for NRIs', The Hindu 26.12.98; Private transfers Spectacular turnaround, Harish Damodaran Business Line 9.11.98

    ReplyDelete
  4. 1.Nashukuru kwa apology michuzi na kuweka mambo sawa - Hivi hiyo picha ya basila mwanukuzi hapo juu ina uhusiano gani na mada husika nisaidieni?
    2.Kusema kweli nafikiri its high time sasa tuwe na dual nationality kwani inatoa sana nafasi ya uhuru na haki ya binadamu kujichagulia mambo HASA YALIYO MAZURI , nasema yaliyo mazuri kwa mantiko ya kutumia vizuri utaifa wa nchi mbili.Mfano mtoto anayezaliwa na mama mtanzania marekani anakuwa moja kwa moja ni raia wa marekani, sasa akitaka kuwa raia wa tanzania kwa sheria za hapa atatakiwa kuukana ule wa marekani WE NEED TO CHANGE !

    ReplyDelete
  5. KWELI HII BLOG YA KIKWELI KWELI.
    MAANA KAMA KAWAIDA, MIJADALA HAIENDANI NA PICHA ILIYOTOLEWA HAPO JUU. HEEEE HEEE HEEEEEEEEEE.
    TUENDELEE.
    HAYA TENA WABONGO WANAWAPAPATIKIA SANA WA SAUZI NA WAKENYA.

    ReplyDelete
  6. Michuzi kaweka mjadala wa kitoto!
    Ati walioko nje warudi!!!!!!

    Je, walio ndani wanaoamisha mapesa yao nje?

    Halafu anatukanya tusizungmzie mambo ya Dito!!!!! Kama hataki, ni vizuri afunge blog lake hili.

    ReplyDelete
  7. michuzi binadamu wa kweli ni yule mwenye kutambua kosa lake sasa wewe umenifurahisha kwani umetambua kosa lako la kukejeli ndugu zako sasa mimi nasema hivi ulaiya wa nchi mbili ni mzuri kwani umeona juzi juzi yule mtoto ongara ameshindwa kuchezea timu yetu ya taifa kwa sababu hilibidi eti aukane ulaiya wa uingereza kitu ambocho kilikuwa kigumu kwani laitikama tungelikuwa na utaratibu wa ulaiya wa nchi mbili isingekuwa tabu kwahiyo imebidi tumkose kwa sababu ya sela zetu, huo ni mfano mfupi tu , thnx michuzi

    ReplyDelete
  8. we anony hapo juu kwani mada ni ya Dito tuuuuuuuuu!au na wewe ni wale ambao ulichukuliwa mke na Dito?tuambie kaka maana maada imewekwa hapo juu lakini wewe unataka kila siku tujadili habari ya dito unashangaza sana,mimi nadhani hujamuelewa michuzi yeye alichoonya ni watu kutohukumu wakati wa kujadsili lakini hajakataza kuijadili.Nadhani wewe ni moja ya watu ambao walimu wako walipata shida sana kwenye kufundisha nadhani unahitji majedwali ili uelewe michuzi anataka nini?

    ReplyDelete
  9. Watanzania
    Dual citizenship can have distinct advantages. In particular, a person with dual citizenship has greater flexibility in his or her choice of where to live and work. Thus, it behoves anyone with dual or multiple citizenship -- or with the possibility of claiming such a status -- to investigate the pros and cons of the specific situation very carefully.

    ReplyDelete
  10. Michuzi

    Ah! Bassila bado yumo kweli. Toto la kiafrika linang'ara! Ndiyo Michuzi tupatie vitu kama hivi.

    ReplyDelete
  11. Michuzi naomba weka picha ya Ms Mercy Galabawa , huyu mrembo siku bahatika kumfahamu au hata kumuona kwa picha, sababu nilikwu anje ya nchi akiwa kune kinyanganyiro cha u miss TZ, nasikia ni moto wa kuota mbali !

    ReplyDelete
  12. KUMBUKA MICHUZI 85% YA WASOMAJI WA BLOG YAKO WAKO UGHAIBUNI, NA UNATUMIA NAFASI YAKO KUWAKEJELI, MIMI NAONA PAMOJA NA KUOMBA RADHI LAKINI DAMAGE IMESHAFANYIKA.UMETUTUKANA HALAFU UNATUOMBA RADHI, MIMI NAONA KWA UPANDE WAKO ULIJUA UNATENDA NINI ("ACHA NIWAPASHE HALAFU SI NTAOMBA RADHI NA YATAKWISHA?")MICHUZI MICHUZI, MICHUZI, UNASAHAU WEWE UMEKWENDA MAREKANI KWA PESA YA WALALA HOI? HIVI TUKIAMUA KURUDI NA KUFUNGUA STUDIO MORDEN KULIKO YAKO SI UTATUENDEA BAGAMOYO? NAONA NIISHIE HAPO MAANA ..............??????!!!!!!!""""

    ReplyDelete
  13. WAO I LOVE THIS GIRL...SHE IS THE BEST MISS TANZANIA EVER
    KWANZA SHE IS BEAUTIFUL..SHE IS CLASSIC AND SHE COMES FROM A GOOD FAMILY..hivi ameolewa huyu dada michuzi niangalizie basi mie namfagilia sio siri

    ReplyDelete
  14. Aka kabinti kweli hakakudanganya umri tofauti na mamiss wa siku hizi wanadanganya miaka yao sasa ona toka 98 hadi sasa hivi bado kachanga na kanamvuto kweli alistahili kushinda...yupo wapi siku hizi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...