watoto wa kibongo wakicheza ngoma za nyumbani kuukaribisha mwaka mpya huko kanada katika kitongoji cha richmond hill, ontario

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hii safi sana, muhimu kukumbuka nyumbani na kuwafundisha watoto wetu ngoma zetu, hongereni sana tu!

    ReplyDelete
  2. Mwanzo mzuri sana msisahau na lugha tu wakija kututembelea wasijisikie wapweke huku kwenye asili yao.

    ReplyDelete
  3. Hiki kitongoji kiko kaskazini mwa jiji la Toronto, inahesabika kama sehemu ya Greater Toronto

    ReplyDelete
  4. Wewe anony wa pili. Unaposema msisahau na lugha, nikuuluze swali. Pale Dar, kwa wale waliozaliwa Dar, au popote Tanzania kwenye mji mkubwa kwa sababu wazazi wako mjini kikazi kwa sababu walisoma, ni wangapi wanaongea lugha za wazazi wao? Karibu wote wanaongea kiswahili, na hawaongei kisukuma, au kisambaa. Hii inatokana na urbanization. Watoto wamezaliwa mjini (e.g. Dar, au elsewhere) wataongea lugha ya hapo mjini (kiswahili). Sasa ukitegemea mtu aliyezaliwa Canada, au U.S. aongee kiswahili, wakati TV,majirani, watoto wenzake, shuleni, vitabu, radio, vyote viko in english haitakuwa fair. Mimi binafsi mtoto wangu kazaliwa U.S., kwa hiyo ni mmarekani mwenye asili ya Tanzania. Na wala haongei kiswahili kwa sababu anaoshinda nao (day care), shule,vitabu, TV, vyote viko kwenye english. Mimi naweza kurudi Tanzania kama nikichoka maisha ya huku. Lakini mtoto wangu hawezi kurudi Tanzania, kwa sababu yeye ni raia hapa,na ataenda shule hapa, tena kwa uhakika hana haja ya kuhofia migomo ya wanafunzi, au kusumbuliwa na wenye dala dala akienda shule, au lecturer kumkamata(kum disco) mwaka wa mwisho. Kama una mtoto kazaliwa nje, mwache ale matunda ya kuwa raia wa hiyo nchi. Mimi kama mzazi,ninafurahi kuona mtoto wangu atakuwa na maisha bora zaidi ya yale niliyopitia nikiwa Tanzania. Angalau mtoto wangu hataumwa malaria, au kipindupindu, au kushushwa kwenye dala dala.

    ReplyDelete
  5. Anon 5:22:33 hapo juu acha kuandika pumba hapa. Yaani nimesoma nimeboreka kabisa kutokana na utumbo uliouandika. Wangapi wana watoto hapa US, Canada, UK na sehemu nyingine kibao na utakuta wanajaribu kuwafundisha watoto wao lugha ya nyumbani(Kiswahili) na utawakuta hao watoto wanajitahidi kuongea kidogo. Nyinyi ndio tunawaita malimbukeni mkifika abroad tu, kazi yenu inakuwaga kujizalisha mitoto kibao kisa tu wawe wamarekani au wacanada ili muanze kuombaomba kwenye Govt Sponsored Social Programs.

    ReplyDelete
  6. Mtoto akizaliwa Tanzania=malaria, kipindipindu,kero za daladala, migomo ya shule. Mtoto akizaliwa U.S.=no malaria, no cholera, no harassment from city buses.

    Swahili is so limited, with very poor vocabulary. English has rich vocabulary. Either you agree or not, english is more important than english. That's why when you go to secondary schools and colleges in Tanzania, you WILL NEVER FIND A TEXT BOOK IN SWAHILI. That's a proof that Swahili is too poor in vocabulary to be used in TEXT BOOKS.

    ReplyDelete
  7. We anony wa 7:19 hujui tu umuhimu wa kuzaa mtoto U.S. Mtoto akizaliwa U.S. ni raia wa U.S. Anakuwa na haki zote za kiraia, ikiwemo kuwa na passport ambayo haitaji kuhonga kama mlivyozoea huko Tanzania. Anakuwa na uhakika wa elimu mpaka college mradi tu afaulu mitihani. Anakuwa na uwezo wa kuongea lugha na kueleweka na jamii inayomzunguka. Mzazi hatakuwa na hofu kuwa mtoto atapata malaria, au kipindupindu, au surua, au kichocho n.k. Mtoto atafika shule kwa wakati kwa sababu atapanda school bus, na sio daladala. Kama hujui faida ya kuwa na mtoto U.S.,au Canada, au U.K. waulize wanawake wajawazito ambao husafiri kwenda huko ili tu watoto wao wazaliwe huko, na wapate all benefits. Na kwa taarifa yako, hicho kiswahili hakina VENUE kwa watoto wanaozaliwa mahali kama U.S., Canada, au U.K. We zaa watoto wako huko Dar alafu wakaombe visa kuja huku. Mwanangu akienda Tanzania, anaomba visa ya kuingilia Tanzania, na akirudi huku U.S. haitaji visa, anakaa kwenye mstari wa raia pale airport port of entry, wakati wewe na wanao walizaliwa Tanzania mnakuwa kwenye foleni ya wageni, na kama mmebeba vitu vibaya hamruhusiwi kuingia U.S. Mtarudishwa Tanzania na very next flight.

    ReplyDelete
  8. Picha kama hii inaonyesha kuwa dunia ishakuwa kijiji na Watanzania tuko kila kona ya kijiji hicho.

    Tanzania itafaidika kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili maana watoto kama hao si ajabu ni wazaliwa wa Canada, wanajifunza asili yao hapo(japokuwa tunachoona hapo ni kucheza ngoma tu). Siku moja pengine wangependa kwenda Tanzania kufanya kile ambacho huku kinaitwa "to give back to the community" sasa wakiwa na uraia wa nchi mbili hawa wanaweza kuwa wawekezaji wazuri sana baadaye.

    Kila nchi inaangalia maslahi yake hivyo na sisi Tanzania tusizubae tukabaki nyuma halafu miaka 50 baadaye, wenzetu washapeta sana na dual citizenship ndio sisi tuamke(baada ya kusulubiwa na hiyo EA Federation inayokuja)!

    ReplyDelete
  9. Ama kweli mtu asiyesoma utamjua tu. Mtu anadharau kwao alikotoka maana anamuona hata baba na mama yake wanaoishi Tz ni wapumbavu kwa vile kuna mbu! Lakini kumbukumbu zinaonyesha nchi yenye wafungwa wengi duniani walio magerezani(tena weusi) ni Marekani. Watoto wako tunawatakia jela njema huko wakishakua na sisi huku tutaendelea kutumia doom kuua mbu.

    ReplyDelete
  10. Wanaoishi Tanzania si wapumbavu. Ila kiswahili huku nje, esp. U.S., U.K., Canada na kwengine hakina VENUE. Kinazungumzwa among waTanzania, lakini sio mitaani. Kwa watoto wa waTanzania wanaozaliwa nje, kiswahili hakiwasaidii. Watakiongea wapi, na nani? Jiulizeni kwa nini text books kwenye secondary schools, na college huko Tanzania haziko kwenye kiswahili? Jibu ni wazi kuwa kiswahili ni lugha changa, ambayo vocabulary yake ni POOR.
    Ukweli ni huu: Kiswahili=Poor/Weak language with very limited vocabulary.

    ReplyDelete
  11. Bwana, Michuzi naona Watanzania wanaoishi nje baadhi yao wanajisahau kabisa.
    Nhi hii ndio iliyowakuza pamoja na ubaya woote wanaoipa na hawalioni hili.Mimi binafsi nimekulia Tanzania na sasa naishi Kanada na familia yangu, na najivunia kuwa MTANZANIA, na watoto wangu wanaogea kiswahili fasaha, na kingereza fasaha, na kifaransa kidogo.Najivunia hilo , na hawapungui kitu kujua lugha zote hizo.
    Huu ni ulimbukeni kwanza kusema MTOTO WANGU KAZALIWA CANADA/US hivyo ni mkanada au mmarekani.Mbona wakizaliwa INDIA AU PAKISTANI AU IRAQ hampigi kelele kuwa watoto wangu ni WAHINDI, AU WAPAKISTANI?Acheni ujinga nyie!!!

    ReplyDelete
  12. watu wengine bwana wamebahatika kwenda US,UK....imekuwa taaabu kweli kweli...sasa wanaponda kila kitu cha home...wengine wanadai bongo hawajui kuvaa,wengine wanaponda lugha....home sweet home...kiswahili ni bomba ndio maana wanajifunza kwa kila hali hao mnaowaabudu na kudhani ni miungu yenu!!!!!

    ReplyDelete
  13. we anony Monday, January 08, 2007 11:35:07 AM huna akili na ni mtumwa wa kimawazo,uliyoyaongea hapo yananichefua inavoonekana wewe ni type ya wat ambao wanaweza kuwatoa wake zao ili kushibisha njaa ya siku moja. nimetoa kauli hii kwa jazba kutokana na kutoamini ni kiasi gani mtu anaweza akawa si mzalendo ktk kiwango hiko! alamsik!

    ReplyDelete
  14. Hapa si kwamba watu wanadharau kwao. Ni kwamba tu watu wanaongea ukweli. Na ukweli ni huu: Kiswahili nje kama U.S., U.K., Canada etc huzungumzwa miongoni mwa wa Tanzania kwa sana. Lakini nje ya hiyo Tanzanian community kiswahili hakizungumzwi, si mitaani, si makazini, si popote. Pia, Kiswahili ni lugha changa mno, mkubali au msikubali, kiswahili ni lugha ambayo ina limited vocabulary. Ukitaka kujua kuwa kiswahili ni lugha changa, jiulize kwa nini secondary schools, na colleges hazitumii text books ambazo ziko kwenye kiswahili? Hatujaona bado kitabu cha Economics, au Physics kilichoandikwa in Swahili. Kwa mlio Tanzania hivi sasa ambao mna mpango wa kuja nje kama U.S., U.K., Canada etc, nawashauri mtilie mkazo English jamani. Kwani kuna waTanzania wako huku wanatia aibu, kwani hawawezi kuongea hata sentesi moja iliyo kamili in english. Kinachotokea ni kwamba watoto wadogo, na watu wazima wanabaki wanaangua kicheko kwa sababu waTanzania hawawezi kuwasiliana kwa english. Inasikitisha kuona waTanzania wamemaliza university, hawapati kazi kwa sababu hawawezi kuongea english. Nawapa hint tena. ENGLISH IS HIGHLY IMPORTANT especially if you have plans of moving to the U.S., U.K., or Canada etc. TRUST ME ON THIS ONE.

    ReplyDelete
  15. we anoy wa hapo juu 11:35,umenichafua sana kwani hizo text book za kiswahili zenye poor vocabulary ndio ulizosoma,na sasa ukafika hapa ulipo,na kwa jinsi ulivyochangia nina uhakika huna hata degree.Sasa hao watoto walioko kwenye picha hapo juu walikuwa wanaimba sindimba kwa kiingereza?je inapofika mahali pakuonyesha asili yako huko Canada unaonyesha,asili ya Aboriginal?au ni hii ya kiswahili chenye poor vocabulary?,kama wanaweza kuimba sindimba kwanini msiwafundishe lugha hii,jamani hapa A frica miaka ijayo tutaungana na kutumia lugha ya kiswahili kwa Africa nzima,uliza Dar university,wakueleze!!! .Hata maneno ya mwalimu Nyerere, yasema, "jivune na chako".

    ReplyDelete
  16. Nadhani baadhi ya wachangiaji hapa uwezo wao wa kufikiri bado umekwazwa.
    1.Yaani huwezi kuwafundisha watotot wako kiswahili kwa kuwa watakosa kazi wakikuwa wakubwa?Haingii akilini .Mtoto anakuwa shuleni\Day care muda mwingi sana unaomfanya ajue kiingereza auotomatically.Unachotakiwa kama mzazi ni kuongea KISWAHILI nyumbani kwako na kumsaidia kumuelewesha baana ya maneno kila wakati asipokuelewa.Hii inatosha kabisa kumfanya mtoto ajue lugha yake.Haiihitaji kumpeleka shule ya kiswahili kujua kiswahili.
    2.Kama wewe ni MUHA, mkeo\mumeo MUHA.mkizalia mtoto DSM, Haifanyi mtoto yule awe Mzaramo.Kuacha kufundisha Kiha, ni dharau na ujinga tu.Atabakia kuwa MUHA asilia, hata kama Wazazi wake wajinga mmegoma kumfunza mtoto KIHA.
    3.Namuunga mkono mchangiaji fulani hapo juu kuwa mtoto hapungui chochote kwa kujua lugha nyingi.Na watoto wakizaliwa nchi zisizoendeelea mbona hatusikii hii milelelya kijinga ya OOHH mwanangu mmarekani , au mwingereza?
    Tunataka tusikie mwanangu MSUDANI , AU MUHINDI sasa kwa kuwa kazaliwa kule.
    Tumieni akili kidogo ,na muwe na heshima kwa nchi iliyowakuza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...