
hili ni bango la filamu mpya inayozinduliwa kesho, katika kile jkinachoonekana mwamko mpya wa wasanii wa kizazi kipya wengi wao wakiwa wamejikita kwenye fani hii kwa sasa. prodyuza wa filamu hii iendayo kwa jina la sauti ya manka ni huyo gwamaka kaihula a.k.a. king crazy gk (anaekula saluti) na imeongozwa na dairekta donald mugisha toka uganda. mazungumzo yanaendelea nami kuona ni jinsi gani kopi zitaweza kuuzw huko ughaibuni...


Haya ndio maneno Michuzi. Toka wimbo, albamu, hadi filamu. Ukiweza kutuletea picha za uzinduzi tutashukuru.
ReplyDeletehivi!, Sirikali si imepia marufuku raia kuvaa mavazi ya kisoja????
ReplyDeletesasa GK mbona anajitafutia balaa???
MIchuzieeeeeee! OOngeeni fast fasta wape jamaa namna ya kufikisha filamu yao huku. Unjajua wasanii wetu wanajikita mno humo ndani kwa ndani ili hali hata huku ughaibuni soko la filamu za Kiswahili lipo. Tunatamani kuona kazi za vijana wetu, pliiiiiiiiiiiiiz tuone picha za uzinduzi mkuu.
ReplyDeleteSafi sana, ningekuwa Bongo, ningeenda. Kwa kweli wanajiathidi siku hizi.
ReplyDeletenashukuru sana Michuzi kwa mwamko wa vijana wa kitanzania,mimi mwenyewe ni mshabiki wa Bongo flava,Ila kuna kitu kimoja nataka kuwaelimisha vijana wa Kibongo(Hao wanaojiita masupa star).Nadhani kama sijakosea hilo bango linatangaza uzinduzi wa filamu hiyo ya "MANKA",sasa sikuzote hilo bango linatakiwa liwe na picha ya kitu kinachoenda kufanyika.Kwa mfano ningetegemea labda liwe bango fulani na picha ya msichana mmoja(MANKA)inayooenyesha huzuni fulani,yaani kuonyesha mabalaa yaliyomkuta huyo manka,Sasa cha kushangaza tunaona picha ya GK na nguo za kijeshi sasa hapo GK ndo unapokosea au kama unapenda sana jeshi au bado una mambo yale ya EAST COAST na WEST COAST ambayo hata huko Marekani wameshaanza kusahau,ndo maana nawafananisha hao wanaojiita masupa staa wa Bongo kama mtu fulani anayejifunza kucheza wakati ndo kwanza mziki unaishia.ANYWAY GK JARIBU KUTAFUTA USHAURI NI PICHA GANI INAFAA KU-ADVERTISE HIYO FILAMU HALAFU USIJE UKAJISAU KWENYE HIZO TAPES,CDs,DVDs UKAWEKA PICHA KAMA HIYO YA BANGO,MAANA UTATENGENEZA KITU WATAALAMU WANAITA 'CONTRADICTION'.
ReplyDeleteNi kweli nakuballiana na mzee wa sheffield.
ReplyDeleteTunaisubiri hiyo movie yenu huku....ila next time ...tafuta jinsi ya kumarket. Kama movie inaitwa Manka na kuna General nje ya cover ukweli mimi ninazania hii ni movie ya kejeshi au vita...Cambodia au vietnam vile
hongereni tunajua wote kuwa mwanzo mgumu na ndio hivyo tunajaribu kuchangia mawazo yetu kwa jinsi tunavyoona ulimwengu wa kucatch unavyosema....
all in all mkiileta nitanunua...kwasababu kila kukiwa na concernt ya watu kutoka africa especially south huwa nanunua tape zao just kusupport vipaji vyetu.....