dk. asha-rose migiro akiwa na jk na mama salma kikwete na mumewe profesa cleophas migiro na watoto wao chansa (8) na twalame (20) ikulu leo baada ya kuwasili toka sauzi na kupata mapokezi makubwa kwa kuteuliwa kwake kuwa naibu katibu mkuu umoja wa mataifa. safari hii bongo tumepiga bao la kisigino...yaani watani wetu wa jadi kama nawaona vile....hahahaaa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Duh! First lady aanze mazoezi amenenepa sana. Afya itunzwe, unene unaweza lete maradhi (i.e ugonjwa wa moyo, kisukari) na mengine mengi. Inaweza kuliletea taifa hasara (i.e, gharama za matibabu kutibiwa nchi za nje. Tafadhali mlio karibu na First Lady hebu mwambieni.

    ReplyDelete
  2. bao hili inaelekea limeenda mbali zaidi ya kwa watani wa jadi.bbc wameandika sentensi saba tu kuhusu hii habari na katika hizo saba ni moja tu ndio inayomzungumzia mama Migiro moja kwa moja!http://news.bbc.co.uk/2/hi/in_depth/6235907.stm

    ReplyDelete
  3. Hongera Dr.Asha-Rose, hilo ni bao la kisigino wandugu,hao watani wa jadi kama nawaona vile macho yamewatoka!!,wao wanajua jina lao tu ndio liko ngazi za juu...wamesahamu kama TZ ni ari mpya kasi mpya na nguvu mpya.....tuwakilishe vema mama...

    ReplyDelete
  4. Michuzi watani wetu,hawatuwezi si mnakumbuka Dr Salim nae alikua akalie kiti cha kabla ya Annan kama sio USA kutia kauzibe.Beijing kwenye mkutano wa wanawake nako nako tulipeleka mtu(Mongela);OAU nako ndio usisema mpaka lugha tumeipeleka na wameikubali.Watani wataishia kula kuwa Mbuzi kula kunapoishia kamba (east africa)bahari hawavuki.

    Hila msisahau nyumbani bado kuna harufu kali sana ya RICHMONDULI; Hii harufu hata wakitumia manemane bado haitaisha.Mbona wameanza kiuba mapema sana? wanatafuta pesa za kujiandaa na kampeni za uraisi 2015 au wanarudisha madeni ya kampeni zilizopita.Naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete
  5. Hata nyie mlitilia mtu kauzibe ili Mkorea ashinde

    ReplyDelete
  6. HURAAAA HURAAAAAAAAA ROSE... STRENGTH OF WOMEN!!! GO ON GIRL SHOW THEM WHAT YOU HAVE MADE OF!!
    TUNAHITAJI WANAWAKE WOTE TZ TUFUATE MIKONDO HII KITABU KWA SANA NA KUONYESHA UMAHIRI MPAKA UN INASALUTE!! NA BADO WAKO WANAWAKE WENGI WA SHOKA - NATUMAINI WATAENDELEA IBULIWA HUKO WALIKO!! YOUNG WOMEN OUT THERE THIS WOMAN IS A REAL SUPER ROLE MODEL...

    ILA KWA WALE AKINA NANIHIII WANATAFUTA UMAARUFU KWA NGONO NADHANI HAWATUFAI NA WALA HAWAFIKA MBALI.

    ReplyDelete
  7. duuu ila first lady kavimba halafu ndio mavazi gani hayo kuvaa ikulu over katokea kwenye alaiki..!! Hata kama casual wear basi kuna vitu vinakwendana na umbo lake bwana sio lifulana jalo... huyo mshauri wake anafanya nini???

    Kuhusu unene hamna noma ndo alivyo walao twajua hajaupatia ikulu... zoezi kiasi kujiweka fit tuu mama nona weeeeeee!!

    ReplyDelete
  8. DOCTOR.
    CONGRATULATION DR. MIGIRO I TAKE THIS OPPORTUNITY TO WISH YOU SUCCESSFUL CAREER IN INTERNATION AFFAIRS .I HOPE YOU WILL BE GOOD TANZANIAN ENVOY AND MOTHER OF AFRICA BUT IRON -LADY DIPLOMAT...
    for my people congraturation to have exposure person in the world...at last Tanzania hoyeee... (my self so proud of that)
    DOCTOR.

    ReplyDelete
  9. Asha-Rose Mtengeti Migiro:
    Do The Millennium Fire Dance!
    Copright: Born Again Pagan, 2007


    Asha-Rose Mtengeti Migiro,
    As a woman,
    You have come a long way,
    Baby!

    Time was when Leon Bukassa
    Of then Congo-Leopoldville
    Composed and sang
    In 1960’s "Bibi Sultani"
    A disparage of African woman
    And her empowerment
    To take charge
    Amid advantaged masculine-skewed
    Gender inequality.

    In Bibi Sultani
    A man either marries
    A traditional rural wife
    And moves into the city
    With her
    Or he returns into his village
    To marry a traditional wife
    And brings her
    In the city.

    The new city sophistications
    Lead to her self-discovery;
    They liberate her to question
    The arresting traditional shackles
    And she responds;
    She shades off
    Her rural imageries,
    As a subservient woman
    To the chagrin
    Of her husband machismo
    And his disparaging reaction
    Singing in amazement:

    Bandugu wapenzi
    Ninataka kuwapa habari
    Bandugu wapenzi
    Inakuwa namna hiyo
    Wanasema
    Sultani ni mwanamke!
    Wapi wandugu
    Mliona habari hiyo?
    Bibi Josephina
    Kwa mapendo,
    Nilikupenda
    Njoo ville
    Unataka kuwa
    Sultani wangu!

    Akili ya bibi
    Haiwezi kushinda ya bwana
    Akili ya bibi
    Iko sawa mtoto mdogo!

    Like Okot p'Bitek “Lawino”,
    Picking up machismo baton,
    Fela Anikulapo-Kuti song "Lady"
    Elucidates Bukassa song;
    The multi-standard song
    Glorifies yet denigrates
    African woman
    Prescribes how she occupies space
    And carries herself
    Her proper relationship
    Ridicules foreign trait aping
    Of being a “Lady”!

    She remains submissive
    She is a subordinate wife,
    She sheds off idea of "lady":
    Lady is anaemic
    Lady is untraditional
    Lady is spiritless dancer
    Of the African fire dance
    For her man!

    Asha-Rose Mtengeti-Migiro,
    You have proved
    Omugasi nyangubho
    (A no nosense woman)
    Keep on climbing
    You daughter of African soil
    For you are not climbing iron pole
    Wearing iron shoes and gloves
    Where man is climbing
    Wearing rubber shoes and gloves!

    Mama wa Tanzania,
    Emulate Asha new day dawning
    Reinvigorate Asha new day dawning
    Rise to protect your rights
    For the time is now:
    Reform, transform, and change
    That conscripting life
    That condemning life
    Which reverberates
    Your passive entity format
    In society
    As if "ordained” life!

    Your man intransigence
    Continues perceiving you
    As a non-starter in matters
    Affecting Tanzanian total ticking,
    As Tanzania does;
    Your existentiality
    Prescribed and described
    Reduces you to a passive format!

    You are understood
    Along a dichotomized
    Linguistic milieu or context
    In which you are not the main
    But a dependent sentence part,
    A dependent clause or phrase;
    Your operational contents
    Derive from and reflect
    Into a context of a passive
    Not an active entity:
    Unaolewa!

    You are understood
    Along a dichotomized
    Linguistic structure or context
    That conscripts you
    Into a passive linguistic format;
    The format elevates
    And reserves the active role
    For your man
    Anakuoa!

    Your daily chores conscript you
    On statistical measure or scale,
    Along the horizontal axis,
    As a dependent variable
    Manipulated by thevertical axis,
    The independent variable,
    Which is reserved for your man!

    You suffered along lamentations
    Of Mwalimu Julius Nyerere:
    During Anglo-colonialism
    An African woman suffered
    From a double-domination dose
    Of Anglo-colonialism
    And from colonialism
    Of African man!

    The time of colonialism is over;
    Last century industrialization
    Replaced human muscles
    Yours were disadvantaged
    For strenuous tasks;
    You do not need a muscular man
    To chase impalas
    All day long to eke out a living
    This century digital information
    Is even replacing human brain
    Sequential linearity;
    Its software is beyond
    The gender divide!

    Mama wa Tanzania,
    Mine is a call on you
    For a diplomatic revolt:
    Liberate yourselves,
    Empower yourselves
    From all traditional shackles
    That bind you
    To macho intransigence
    As a passive recipient
    And entity of Mtendewa!

    Sweet mama,
    Rise to sensitize,
    Rise to sharpen,
    Rise to crystallize
    Tanzanian women questions
    Tanzanian women problems
    Tanzanian women issues
    Tanzanian women concerns!

    Rise to usher in women
    New vistas of hope
    And empower new optimism open up,
    Like buds of rose flowers;
    Let this renaissance release
    Its timely fragrant smell
    To deodorize stinking negativism
    That humiliates
    That marginalizes
    That neglects
    Your humanity
    And your endowed rights!

    Mama wa Tanzania,
    Rise wikukumure (shake off)
    The rainwater of such debasement,
    Like bird shakes off rainwater
    To warm up!
    Rise to compose a new symphony
    Of women-centred empowerment
    And women-centred gender equality
    In Tanzanian liberty re-conquered
    Along ari mpya, nguvu mpya
    Na kasi mpya that new leadership
    Espouses!

    Rise,
    Tanzanian women virtuoso
    Tanzania women repertoire,
    Rise to organize a musical concert
    In newly erected Dodoma Parliament
    And do the fire dance
    For your own self-discovery
    For the larger community
    To dance, too.

    Let the new Tanzania,
    In one accord,
    Join in to sing this song
    Of women liberty re-conquered
    For the corridors and walls
    Of Dodoma Parliament
    To reverberate all
    With uplifting echoes
    Of gender democratization
    And gender equality!

    Where are wakina baba wa Tanzania
    That Tanzanian new breed virtuoso
    The new adept repertoire
    That new Tanzanian adroit ensemble
    Liberated out of machismo cacoons
    To play ready-arrayed
    Musical instruments of ebhikuri,
    Jifilimbi, jicheche, jinandala
    Jiinong'o, amatungu,
    Jingoma and jimarimba?

    Let Tanzania and yonder hear
    The seasoned Tanzanian new song
    Of women-centred liberation
    Women-centred empowerment
    And gender equality
    To dissipate all cluttering noises
    Of helplessness of wakina mama all!

    Establish and instil:
    Wakina baba wa Tanzania
    Na wakina mama wa Tanzania
    That pair of sharp scissors
    Cut the ribbon
    Of women empowerment
    Gender equality
    And shall forever
    Remain gender partners
    For future generations
    To emulate!

    Fantastic!

    ReplyDelete
  10. Hao watoto watasomeshwa best schools duniani na United Nations! Wana bahati kweli. Je, wanaelewa mama yao kawa nani?

    Picha safi sana. Mume upande wa kushoto, Kikwete upande wa kulia!

    ReplyDelete
  11. Shule na uchapakazi ndivyo vimemfanya afike hapo. Kwa hiyo, tunaojifanya wasomi,kuvimbisha matumbo, kukaa tu ofisini na kunyanyasa wengine tubadilike. Na wale wanaopata nafasi za kusoma (wanaume kwa wanawake)wakazembea na kufeli badilikeni pia. Changamoto hiyo kinamama tuwe busy na shule siyo "u-miss" hautufikishi popote. Hongera Asha. KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA.

    ReplyDelete
  12. hongera migiro, hongera sana.
    ila first lady aangaliwe kula kula, ananenepa sana,haijatulia kwa mama wa nchi,nasisitiza zoezi,pfffffffffffff

    ReplyDelete
  13. Jamani huyo Twalame mzuri, what does she do?

    ReplyDelete
  14. Yaaaap hii inaitwa kama kawa! haya sasa hakina dada kaza msuli dunia imepania kuwainua, piga kitabu acha porojo na kwenda kwanja kwa saana kwa wale wa 'bodingi skuli', piga shule, shule muhimu vijana hata na nyie wanaume kaza buti, who knows one day will be YES, ila ni kweli ni changamoto kwa wenye kisomo na ajira! CHAPA KAZI one day the society inaweza kuku-mingiro au kuku-tibaijuka tukakukuta mitaa ya New York, UN unawakilisha.....
    Natanguliza hongera kwa mama Migi na mzee wake....

    ReplyDelete
  15. Congrats Dr Migiro, We Tanzanians are all proud of you and we sure you will do us proud. God Bless you and all the best

    ReplyDelete
  16. CONGRATS DR MIGIRO, DO US PROUD, GOD BLESS YOU

    ReplyDelete
  17. Huyu angekuwa mama yangu ningewaburuza(mashori)

    ReplyDelete
  18. Huyo twalame anajua kiswahili jamani!!!!!Ukifanikiwa kula mzigo umasikini unatoka NDUKI!!!!!!

    ReplyDelete
  19. watani wa jadi imewauma sana. the nation wameendelea kueneza uzushi ati south korea waliihonga tanzania ile wapate ukatibu mkuu.

    mzee ban ameliongoza ktk polls zote na kuchaguliwa unanimously na general assembly.

    kama ni hivyo kulikuwa na haja gani ya kuhonga nchi ndogo kama tanzania?

    enewei, nampongeza Dr.Asha-Rose Migiro kwa kuchaguliwa Naibu katibu mkuu UNO. Nampongeza Prof.Dr.Eng.Cleophas Migiro kwa kumpa moyo mkewe afanikiwe na apande ngazi ktk taaluma yake na siasa.

    ReplyDelete
  20. Mimi Mama Migiro simpendi kabisa kwa mambo fulani ya kifamilia yetu lakini kwa kuteuliwa kwake nampongeza.Hongera sana mama.

    ReplyDelete
  21. Show me what U gat lil mama???????Kuchagulia sio kazi ngumu sana ila to show the world that you can really bring some changes.

    ReplyDelete
  22. She have been appointed,what nex?Be historical show the world what you have to offer in terms of good leadership.

    ReplyDelete
  23. haya kazi kwenu kina chifupa munaopiga domo tuu elimu hakuna.shule tuu hapa inaongea.hata wasema mambo ya mapenzi but bila shule angeupata?.tunamshauri mtu kama AMINa Chifupa ajiendeleze Walau aipate hata degree!congratulation umetuinua watanzania!

    ReplyDelete
  24. Pongezi Dr. Migiro.

    I would like join my fellow Tanzanians to extend my sincere Hongera to Dr. Migiro. What an achievement!

    But, Mzee Muchizi, how has her appointment to UN been received in Tanzania? Is it talk of the country? I am asking this because I have not read a lot about it from our press instead copious amount of coverage has been devoted on 'U-miss'. To be fair, I only have access to online newpapers e.g. ippmedia etc.

    It is high time people stop aspiring to 'U-miss' and start emulate Dr. Migiro. I think Mzee Michuzi you are in good position to educate people about the great import elimu has in bringing both personal and national progress, since You have attended many such beauty peagents as special guest.
    'U-miss' is a fleeting fad at best and crass exploitation at worst.

    Once again, congrats Dr. Migiro.

    ReplyDelete
  25. CONGRATULATION ASHAROSE MTENGETI-MIGIRO
    NAIFAHAMU SANA FAMILIA YA KINA MTENGETI, NI WAUNGWANA HASA WADOGO ZAKE WANAOITWA RAHMA MTENGETI NA AMINA MTENGETI, POA SANA HAWANA MARINGO NA NI MARAFIKI WAKARIBU SANA KAMA NDUGU NA FAMILIA YA KINA NYERERE.
    MUNGU AKUBARIKI SANA. UMETUFANYA TANZANIA NASI TUSIKIKE SANA ULIMWENGUNI SASA, UBARIKIWE.

    ReplyDelete
  26. mbona comments zangu huzi publish michuzi?tutakukimbia studio kama una ubaguzi!

    ReplyDelete
  27. HAaaaaa haa anony wa 9;02 unaniua na Richmonduli haaa,michuzi hii blogu yako inanimaliza sana haaaaaa haa

    ReplyDelete
  28. Hongera sana Dr Migiro I wish you all the best.

    sasa kwa first lady ni kituko utavaaje hivyo li T-shirt kama hilo bwana usituaibishe inabidi utafutiwe Personal trainer.
    Alafu mshauri wa mavazi inabidi aachishwe kazi yaani tunahitaji first lady aonekane wa pekee isiwe tabu kumidentifai.

    ReplyDelete
  29. Mama hongera.

    Ukienda UN jitahidi sana kuepuka misimamo binafsi yako ya nchi au bara.Egemea zaidi kwenye masuala ya maamuzi ya pamoja.(Collective stand)ya vikao halali.Kama bado vikao kufanyika waambie press utawaambia baadaye.

    Ukiulizwa na waandishi wa habari kule UN kuhusu msimamo binafsi wako au nchi ulioutoa kama waziri wa mambo ya nje wa Tanzania wambie waziri ni waziri na Naibu katibu mkuu ni naibu katibu mkuu ni watu tofauti,ofisi tofauti na wenye misimamo tofauti yenye mazingira tofauti ya utendaji kazi.

    Ukiulizwa sababu za kuteuliwa.Jibu kifupi mamlaka zilizonichuja na kuniteua zinajua sababu nzuri za kunichagua na sina sababu ya kurudia ila ninachoweza waambia ni kuwa nitajidi kwa pamoja na wafanyakazi wengine wa UN kuhakisha hatuwaangushi mabilioni ya wakazi wa Dunia katika utendaji wa kazi zetu katika chombo hiki muhimu katika maisha yao.

    Maswali mengine ukiona giza Sema tu sijui.Au sina jibu kwa sasa.Uwe makini sharp na mwepesi kujibu.Usinune utawasha moto.Usitukane mtu (be highly composed) hata akuchachafye vipi.Kuna waandishi hawakulelewa na mama zao wamekulia mitaani kutukana mtu kwao nje nje unatakiwa uji-control hasa kwenye press.

    Ukiambiwa kuwa unasemaje kuhusu yale wanayosema juu yako.Jibu kirahisi kabisa kuwa wewe kama naibu katibu mkuu huwezi kuzuia watu mabilioni wasiwe na mawazo yao na maneno yao juu yangu yawe mema au mabaya.Na kama naibu katibu mkuu nawajibika zaidi kwa mataifa si mawazo binafsi na agenda binafsi za watu iwe ndani ya UN au nje ya UN.

    Jitahidi kuwa very brief kwenye press conference.Ukiona wametulia kidogo ukiwajibu maswali kadhaa ukawaona kama wanatafutiza maswali mapya hivi,Waage. Anza mbio mwanangu.Mwenyezi Mungu katuumbia miguu itusaidie kukimbia tukizidiwa. Waambie una majukumu mengine na ukimbie kabla mvua ya mawe haijakunyeshea.

    Nakutakia kila la heri mama.

    Koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  30. HIVI HAKUNA PERSONAL ADVISER AU MSHAURI WA MAVAZI YA FIRST LADY? AAAH! HILO LI T-SHIRT. NA UNENE, JAMANI WASHARUI MPO WAPI???
    HONGERA ASHAROSE MTENGETI. TUNATUMAINI UNATUSAIDIA TANZANIA, KAZI KWAKO SASA, KAZI SIO KUCHAGULIWA, KAZI NI UTENDAJI WAKO WAKAZI, KILA JICHO LA MTANZANIA LIKI KWAKO SASA MAMA, USITUANGUSHE.

    ReplyDelete
  31. Habari zenu nyote mliotoa maoni. Naona kwenye maoni kuna maswali juu yangu. Kwanza, jina langu ni Twalane. Waandishi wa habari wamechemka kidogo. Kiswahili kinapanda freshi tu...Ahsanteni nyote kwa pongezi zenu, na mimi najiunga nanyi kumpongeza mama yangu mpendwa, kwani ni sehemu kubwa aliyoifikia.Mungu amjalie kwenye kutuwakilisha na juu ya yote, kufanya kazi yake vema awezavyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...