Home
Unlabelled
mussa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wafanyabiashara 2 D'Salaam wadaiwa kutajirika kwa 'juju'
ReplyDelete*Yadaiwa ndiyo sababu husaidia sana yatima
Na Grace Michael;MAJIRA
MTHAMINI wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo Bw. Deodart Kahanda, ameieleza Mahakama jinsi alivyoambiwa na waganga wa kienyeji, kuhusiana na utajiri wa wafanyabiashara wawili wakubwa jijini (majina yanahifadhiwa), ili aweze kutoa fedha kwa ajili ya kutolewa kivuli cha umauti.
Maelezo hayo aliyatoa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi, Bw. Sivangilwa Mwangesi, wakati akitoa ushahidi wake katika kesi inayowakabili waganga wa kienyeji ambao walimtapeli jumla ya sh. milioni 200.
Akiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Charles Kenyella, majibizano yalikuwa kama ifuatavyo:
Kenyella: Ieleze mahakama, Agosti 8 mwaka juzi ulikuwa wapi na nini kilitokea?
Kahanda: Nilikuwa ofisini kwangu ambapo nilikuta barua iko juu ya meza ikiwa imeandikwa jina langu.
Kenyella: Ulifanya nini?
Kahanda: Niliifungua na kuisoma, ndani iliandikwa hivi: "Habari ndugu yangu inshallah Mungu atakusaidia, wewe hunifahamu ila mimi nakufahamu, jina lako lililetwa na mteja wangu ambaye anataka kukudhuru, hivyo una kivuli cha umauti umetupiwa, njoo haraka ofisini nikutoe."
Kenyella: Nini kiliendelea?
Kahanda: Nilimwomba mkwe wangu ili anisindikize kumwona huyo mtu aliyeandika barua hiyo, kwani nilipata mshituko wa hali ya juu.
Alieleza baada ya kufika walimpigia simu ambayo alikuwa ameiandika kwenye ile barua na yeye aliwaelekeza mpaka mahali alipokuwa ambapo ni Bunju, Dar es Salaam, hivyo alimweleza kuwa kuna mtu ambaye alikuwa anafanya kazi naye ambaye sasa ni marehemu, alikuwa amemtupia kivuli cha umauti kutokana na tuhuma za kumroga.
Kenyella: Kivuli cha umauti ni nini?
Kahanda: Ni kifo, muda wowote unaweza kufa.
Bw. Kahanda baada ya kuelezwa hivyo, alimwomba mganga huyo amwondolee kifo hicho, hivyo aliombwa fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya uganga wake.
Baada ya kutoa fedha hizo, mganga alimtaka atoe tena sh. milioni nane ili zichanganywe kwenye maji ambayo angeogeshwa.
Baada ya kuzitoa alidai kuwa alivuliwa nguo zake na kuvishwa nguo nyekundu na wakati anaogeshwa, mbele yake kulilazwa maiti ambaye alivishwa sanda.
Alipomaliza alirudishwa ndani ambako alisikia sauti nyingi za ajabu zikihoji kwa nini asimuue huyo aliyempa kivuli cha umauti? Yeye alijibu asifanywe chochote, hivyo sauti hizo zilimshangilia na kumsomea Ufunuo wa Yohana na kumpigia kofi.
Alieleza kuwa alioneshwa masanduku ya fedha za nchi mbalimbali na kuambiwa kuwa fedha hizo angepewa yeye kwani ameonekana kuwa mwadilifu, ili asaidie watoto yatima na alitakiwa kutaja mali zake bila kuficha kwani angeficha angegeuzwa mchanga (angekufa).
"Wakati napewa masharti hayo, nilitajiwa akina...na ... (majina yanahifadhiwa) kuwa utajiri huo waliupata kwa njia hizo na ndio maana wanasaidia sana yatima," alidai Bw. Kahanda.
Bw. Kahanda alidai kuwa walizidi kumpa masharti wakitaka fedha kila kunavyokucha, ili aweze kupewa fedha hizo, alipelekwa kwenye makaburi ya Sharifu yaliyoko Kunduchi, makaburi ya Rose Garden, Kijitonyama na ya Kaole, Bagamoyo.
Alisimulia kuwa siku ya mwisho, alimbiwa angekabidhiwa masanduku hayo, hivyo aliambiwa atoe taarifa kwake, ili huyo mganga akifika afunguliwe chumba chake cha kulala ambako zingewekwa fedha hizo na hakutakiwa kulala chumbani mwake kwa muda wa wiki moja, hivyo alilala sebuleni.
Baada ya fedha kwisha ambazo zilikuwa benki ilibidi auze nyumba kwa sh. milioni 60, ili aweze kuwapa hao waganga ili wakamilishe masharti yao na waweze kumpa fedha hizo kama walivyomwambia, kuwa awali walikosea masharti.
Baada ya kuwa ametapeliwa sh. miloni 200, waganga hao walipotea na kila alipowapigia simu walikuwa hawapokei hivyo alifanya jitihada za kutoa taarifa Polisi wakakamatwa.
Awali washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mwaka jana wakikabiliwa na mashitaka matatu ya kula njama, kudai fedha kwa njia za ushawishi wa vitisho na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Wanaokabiliwa na mashitaka hayo, ni Bi. Hawa Shaaban (30) na Bw. Mohamed Mtambo (39) wote wakazi wa Bunju na wako nje kwa dhamana
Muhidin,
ReplyDeleteNilipoiona sura ya Brother Moses/Mussa nilitoa sauti taharuki "..Duuh!.."
Brother Moses/Mussa, ni taasisi si mtu! Brother Moses/Mussa nimemjua tangu nilivyolijua jiji. Watu wanaolijua jiji wanamjua Brother Moses/Mussa. Brother Moses/Mussa siyo mpiga dawa viatu isipokuwa shughuli ile anifanya kuunganisha watu. Zamani kabla ya mambo ya mobile phone hayajaanza watu tulikuwa tukiachiana messages kwa Brother Moses/Mussa. Ukiwa na ujumbe au kitu cha kumuachia jamaa yako unaenda kwa Brother Moses/Mussa unamuachia jamaa halafu anakuja kukipitia. Alikuwa hatozi ushuru wa aina yoyote lakini tulikuwa tunamtilia bakshishi.
Siku moja Muhidin tukiongea kwenye simu hakiambia "..Yule mzungu mwenye duka la miwani kamuhamishia Mussa chini ya mti pembeni ya park ya magari.." Habari hii ilighadhabisha sana. Nilipoenda Dar nikaenda kumuona Brother Moses/Mussa. Nakamuuliza "..Kulikoni leo uko chini ya mti?.." Akaniambia "..Nikiwa hapa au pale riziki yangu naipata, sitaki ugomvi na matajiri.." Nikamuuliza "..Vipi operesheni Machinga itakuathiri?.." Akanijibu "..Hapo ndiyo sijui..Halafu sijui hata tumuulize nani Kama shuushaini nao machinga au vipi.." Nikamwambia "..Nakutakia heri.." Siku nilipokuwa naondoka nikaenda kumuaga chini ya mti. Nikakutana na rafiki yangu wa utotoni Oscar Haule na Kaka yangu John Vaga Mhina wa The Tanzanites wakiwa wanatia soga na Brother Moses/Mussa.
Muhidin, Mpe salamu nyingi sana Brother Moses/Mussa na wanachama wote wa kijiwe chake.
Masalaam,
F MtiMkubwa Tungaraza.