enyi wadau mlio ughaibuni... jengo lipi hili?

kama kawaida mstari mfu ni usiku wa manane ijumaa na mshindi atapata zawadi ya picha aitakayo.

masharti:


1. lazima uwe unaishi ughaibuni

2. kudesa hairuhusiwi

3. jibu swali kama lilivyo (usitie ufundi)

4. endapo washindi zaidi ya mmoja watatoka droo, kura itapigwa na wadau kwa siku mbili

5. zawadi atakayodai mshindi kama haitopatikana (sidhani) itabidi akubali itayofanana-fanana nayo

6. uamuzi wa jopo la majaji ni wa mwisho

7. rufaa itasikilizwa pale palipo na utata wa matokeo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. mzee michuzi....
    hapo ni makao makuuu ya shirika la umeme tanzania(Tanesco) pale dar' mkabala na british councel.....
    by haki-hakingowi.blogspot.com

    ReplyDelete
  2. hapo ni Tanesco mtaa samora

    ReplyDelete
  3. Mzee Michuzi hapo ni makao makuu ya wizara ya nishati na madini Sokoine drive karibu na posta office ya zamani au karibu na kanisa la Azania front

    ReplyDelete
  4. Hili ni jengo ndio makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, Tanzania.

    Tizo

    ReplyDelete
  5. Mzee michuzi hapa ni wizarani,mkwepu street na sokoine dr. karibu na shule ya sekondari forodhani.

    ReplyDelete
  6. Hapo ni Sokoine Drive

    Zamani -Jengo la wizara ya madini na Nishati, mkabala na Bandari

    ReplyDelete
  7. haki umetoka juzi tu huku, ushasahau hivyo jamani hapo sio tanesco. msalimie sheria.
    by nanyika

    ReplyDelete
  8. Sio siri mimi ndo MSHINDI.
    Hapo ni karibu kabisa na British Council, zamani yalikuwa makao makuu ya TANESCO na siku hizi ndo ofisi za wizara ya Nishati na Madini, na jengo la kushoto kwake chini ni ofisi ya TANESCO Ilala. Makao makuu ya Nishati na Madini yalihamishiwa hapo kupisha zile ofisi za Sokoine drive ambazo zimechukuliwa na Ofisi ya Makamu wa Raisi.
    Nimeshinda. Revd. EVM
    email revdevm@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  9. Karibu na posta ya zamani, au jirani na Forodhani Sec school

    ReplyDelete
  10. mzee michuzi hapo ni jirani na posta kwa mbele yake ni bahari
    thanks HAKIM

    ReplyDelete
  11. wizara ya nishati na madini opp posta ya zamani

    ReplyDelete
  12. Hilo ni Jengo lililokuwa Makao Mkuu ya Tanesco,(Barabara ya Samora)hapo mbele kulikuwa na Generator kubwa sijui kama siku hizi imetolewa

    ReplyDelete
  13. Hapa ni Bangladesh

    ReplyDelete
  14. Wizara ya nishati na madini jengo liko mkabala na pale feri (bahari ya hindi).

    ReplyDelete
  15. Jengo hilo ni la Wizara ya Nishati na Madini ambalo lipo Barabara ya Samora karibu linatizamana na Stears ya Barabara ya Samora Wizara hiyo imehamishiwa hapo kutoka kule Posta ya Zamani ambako Ofisi za Waziri Mkuu zimehamia sasa. /Mbongo

    ReplyDelete
  16. Waliosema kwamba ni jengo la TANESCO la zamani wamepatia. Nadhani hiyo Wizara imehamishiwa hapo kutoka katika lile jengo refu mkabala na shule ya sekondari ya Forodhani.
    Makao makuu ya TANESCO yamehamishiwa Ubungo.
    Michuzi wape zawadi zao waliopatia.

    ReplyDelete
  17. HAPO NI NYUMBANI KWA MICHUZI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...