TAARIFA YA CCM TAWI LA LONDON

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) tawi la London, wanaoratibu shughuli hiyo wamefanya marekebisho kidogo na kufanya uteuzi wa watu ambao watakaokiongzoa kwa muda.
Hii ndiyo taarifa yenyewe:

Mkutano uliokuwa ufanyike tarehe 6 Januari 2007, uahirishwe na ufanyike tarehe 13 Januari 2007 saa 8 mchana, Ukumbi ule ule wa Holiday Inn -Brent Shopping Centre.

Agenda ya mkutano:-
1. Kuwajulisha wanachama watarajiwa, nia na lengo la kuanzisha Tawi la chama cha CCM hapa London.
2. Kuitambulisha kamati ya awali ya Tawi kwa wanachama watarajiwa.
3. Kujiandikisha majina katika orodha ya awali ya wanachama
4. Kuongelea mambo husika yatokanayo na mkutano, kutegemea na muda utaokuwepo kwa maswala endelevu.
5. Kufunga mkutano.

Ndugu Maajar atapokuwa Dar es Salaam kufuatilia maswala ya Kadi za
Uanachama, vitabu, bendera za chama, fomu husika n.k.

Imependekezwa kamati ya muda yenye watu sita (6) ambao wana nia,
dhati, msimamo, uadilifu na muda maana uongozi unahitaji hayo yote.
Mwenyekiti-Sharrif Maajar
Katibu- Richard Mpopo
Wajumbe:
-Yahaya Kiomone
-Said John
-Mariam Kilumanga
-Mariam Mungula
Nategemea tutasonga mbele.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

NB: Tunaomba wanachama tuendelee kujiandikisha na kujiorodhesha katika barua pepe ya chama: ccmlondon2007@yahoo.co.uk.
Ahsante.
Shukuru Hamdani
Katibu Mwenezi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Mbona ni kama cham cha waislamu tuuu . Huko London hamna Christians or atheist?

    ReplyDelete
  2. Ni kweli inaonyesha kuna uislam mwingi hapa. Inaonyesha kuna jina moja tu la kikristo. Inawezekana hapa kuna jambo kubwa limejificha. Hasa ukichukulia kuwa hata balozi hapa uingeleza ni mwislam. Kuna jmbo hapa. Wasdau mnasemaje? Uingeleza hakuna watu wenye itikadi tofauti? Ndo kusema hawapo active katika politics. Na juzi hapa Dunni Haji alikuwepo London. Hii inatupa picha gani?

    ReplyDelete
  3. mimi ninachoelewa Mama MAAJAR anawakilisha Tanzania na wala siyo CCM, je iweje leo mumewe ahusike na chama? sheria inasema kuwa mume au mke wa balozi haruhusiwi kufanya kazi ama kujihusisha na shughuli za siasa akiwa nje ya nchi, Uislamu??? mimi nillkuwa sijaangalia kwa makini hiyo orodha, ngoja niipitie tena.......lol

    ReplyDelete
  4. Inaonyesha ni jinsi gani, wantazania ambao sio CCM hawewezi kupewa kipaumbele ubalozini. Kama Mume wa Balozi ni Kada wa chama tawala. Haingii akilini kwa mume wa balozi kuwa kada wa chama.

    Mheshimiwa Balozi Wakilisha nchi sio chama. Hongera kwa kuwakutanisha watanzania London

    ReplyDelete
  5. Ndugu Maajar kama ni balozi yupo hapo Uingereze kufanya shughuli za serikali na ni walipa kodi ndiyo wanamlipa yeye na bosi wake. Na kama ni mme wa balozi, basi yupo hapo kwa ajili ya mkewe ambaye ni mtumishi wa serikali. Sina uhakika kama anatakiwa ajihusishe na shughuli za chama kisheria kwani hawakilishi wana CCM tu bali ni watanzania wote. Hivyo, ninamuomba aachane kabisa na shughuli za chama kabla hatujampeleka mahakamani. Akumbuke kuwa kufanya hivyo ni kuvunja katiba ya nchi na ni kinyume na sheria za ki-diplomasia.

    ReplyDelete
  6. Inasikitisha wadau kukimbilia mambo ya dini kwa kuona tu majina ya watu sita.

    Na hata kama kweli wote ni waislamu dini ya mtu si mzani wa kupima kiongozi na uwezo wake wa kuongoza, wadau huo ni udaku na udaku hauna nafasi kwenye jamii inayotaka kwenda mbele.

    Na mkutano wa chama kinachoongelewa ni CCM na sio Hamas. Kwa maana hiyo jambo hilo haliyumkiniki.

    Mijadala ni mizuri kwani inasukama mbele fikra za mtu lakini kama ni ya udaku matokeo ni kinyume.

    Hoja ya mume wa balozi kujihusisha na siasa za chama tawala ndo lingekuwa mjadala bora. Binafsi sijui katiba inasemaje kwenye hili.

    Namaliza kwa kumnakili Jenerali Ulimwengu "Watanzania hatuna budi kujenga utamaduni wa kutoa hoja zetu kwa kutumia mantiki badala ya jazba, na kwa kutumia vichwa badala ya mapafu."

    ReplyDelete
  7. Nadhani Majaar na mkewe watelewa mapema kuwa kuna conflict of interest hapa, na mume attachia hayomadaraka kabla hawajapata kasheshe zisizo na ulazima. Anaweza kuwa na nafasi nzuri tu kama mshauri, lakini namshauri asijiingize kwenye uongozi wa ccm moja kwa moja wakati yupo hapo kwa mwanuli wa serikali, na siyo chama.

    ReplyDelete
  8. Wewe Henry Seif penye ukweli lazima pasemwe. Divesity muhimu ulimwengu huu wa sasa hivi. Hawa watu hawajateuliwa na wanachama wanaoishi London. Aliyewateua sijui ni nani. Na wote but one wakawa waislamu. Na mara mume wa naniniiiihii ni mwenyekiti don't you think something fishy is going on there. Kwanza sijawahi kuona chama kikifungua tawi lake nje ya nchi.

    Kweli serikali ya jamuhuri ya muungano wa ya tanzanaia inarecognize chama kikiwa nje ya ichi? Katiba ya nchi inasemaje? Au ni kwa vile ni chama tawala??? Kwa hiyo watu wanaoishi nje ya nchi wanaruhusiwa kuunda chama chao cha kisiasa na kuja kukisajili Tz pia kikakubaliwa? Na kazi ya hicho chama huko itakua nini? I don't get it.

    ReplyDelete
  9. Msilete mambo ya udini hapa kwa dhana. Kwanza mlishasema Kikwete mdini kamchagua balozi wa dini yake. Pia muelewe kuwa huu ni mkutano kuhusu CCM na si wa Waislam. So udini umetoka wapi. Wanaodai hivi watakuwa watu wa vyama pinzani. Hamueleweki, mara CUF wana udini na leo ccm wana udini. Kama huna cha kuchangia tulia hii siyo sehemu ya ibada.

    ReplyDelete
  10. Yeah, upuuzi mwingi unaendelea TZ siku hizi. Hii ni wazi kinyume na sheria za nchi. Hata CUF mambo wanayofanya kwa miaka kadhaa ni kinyume cha sheria, lakini for some reason (mojawapo ikiwa kwamba vyama vyote hivi ni puppets wa ccm) wanaachiwa waendelee. Tunapoteza muda na pesa nyingi kwenye ushenzi wa kisiasa badala ya kukaa chini kama taifa kutatua matatizo yetu. What happened to 'we should run while they walk'? CCM na wadau wake wanaiangamiza na kuifilisi nchi, enough is enough.

    ReplyDelete
  11. Nadhani kama walivyotangulia baadhi ya wachangiaji hapo juu, hoja hapa ambayo inaweza kujadiliwa ni nafasi ya mume wa balozi kujihusisha na masuala ya siasa akiwa ubalozini. Mimi sikatai kwa kujihusisha kwake kama hiyo ni haki yake yeye kama SHARIFF MAAJAR. Sasa kwa vile labda hatujui kama utaratibu unamzuia kufanya hivyo basi tuwasikilize watu waliobobea katika nyanja hizi watueleze ukweli hasa ni nini.
    Lakini kwa wale wanaoangalia majina wakaanza kusema hapo kuna udini nachelea kusema hawana hoja ya msingi sana. Sitashangaa wakisema balozi kateuliwa muislam na mume wake muislam, kwanini mume wake asiwe mkristo ili kubalance...
    Kama utakuwa umefuatilia kwa makini hawa wanaonekana kama viongozi (kwa jinsi nilivyoelewa mimi) ni wa muda wakati wakielekea katika uchaguzi.
    Vilevile kila jambo au wazo lazima lianzie kwa mtu mmoja au kikundi cha watu, kwahiyo watoa wazo ndio hao tumewaona. Na kama watanzania wengine waliopo mahali pengine duniani wafikirie jinsi gani ya kuchukua faida za utandawazi ama kwa kufanya siasa au shughuli nyingine yeyote ya kijamii kwa manufaa ya nchi yao bila ya kujali distance.

    ReplyDelete
  12. je hawa jamaa wmo kwenye payroll ya CCM?

    ReplyDelete
  13. Raisi nyerere aliwahi kuulizwa kwa nini anajaza watu mbumbumbu wasiojua kitu kwenye baraza la mawaziri akajibu kuwa wanaojitokeza kugombea ubunge na kupitishwa na wananchi ni mbumbumbu sasa hana ujanja inabidi hao hao mbumbumbu ndio awape uwaziri kuheshimu matakwa ya wapiga kura.

    Njia mojawapo ya kupata watu wasio mbumbumbu ni kupitia wao kujiunga kwenye vyama,kugombea kupitishwa na kuteuliwa.Kama wasomi hawataki kujiunga,kugombea katika hivi vyama tutaishia kupata viongozi mbumbumbu milele.


    Sasa kama na ninyi huko London hamtaki kwenda kwenye vikao mnaitwa hamuendi,mnatakiwa mkate kadi za CCM mpate nafasi za kugombea katika chama na serikali hamtaki mnapiga kelele tu kwenye blogu.Hii si sawa.Mnatunyima wananchi haki ya kupata viongozi wazuri toka Uingereza pia.Nawasihi mjiunge,mkate kadi.Msiwazomee hao wanaoanzisha hicho kitu hata kama mnawaona wajinga au hawajui sheria.Kuna kitu kinaitwa "honesty mistake" ambapo mtu anakosea ila makosa yale yanaleta matokeo yenye faida kubwa kwa jamii au taifa.Hiyo kamati ya muda inawezekana ikaonekana inakosea lakini hata kama wamekosea ni "Honesty mistake" yenye faida kubwa sana kwa watanzania waishio Uingereza na kwa nchi yetu pia.

    Hiyo ni njia nzuri ya kuwaingiza wasomi wetu Uingereza nao wapate njia ya kushiriki katika siasa za Tanzania badala ya kuwa kitu cha watanzania walioko Tanzania tu.
    Huo uongozi ukifika uchaguzi mnauwezo hata wa kuutoa wote mkitaka.La msingi muangalie uwezo wa mtu siyo dini yake,sura,kabila au chochote.Na kwa sababu uongozi huundwa kwa uchaguzi na siyo kujiteua au kuteuliwa (ballot box) itaamua uchaguzi wa tawi ukiitishwa.Pia nafasi za uongozi ni nyingi mno kuna za akina mama,vijana,wazazi na kamati kibao ndani ya chama.Mkiunda tawi mtashanga vyeo ni vingi mno vinavyohitaji watu wengi.Wengi mtajikuta viongozi.

    Chonde chonde nawaomba mjiunge na hilo tawi la CCM na ikiwezekana Marekani,Ulaya,Asia na nchi zote ulimwenguni waliko watanzania fungueni matawi yA CCM na mchague viongozi wa matawi hayo na ikifika wakati chaguzi ziwe za CCM AU SERIKALI MGOMBEE.Tutafurahi kupata wagombea toka nchi mbalimbali.Kwa namna hii tutapata viongozi bora sana mbeleni.Naomba msisusie.Kila mtu amtaarifu mwingine.Kama hamuwezi kwenda andikeni e-mail.Ombeni ruksa za kufungua matawi maeneo yenu katika nchi au majimbo kama mko mbali.Naomba nchi zote duniani igeni mfano wa Uingereza.Jambo hili kama nchi zingine halipo si jambo la msingi siyo lazima watanzania wakati wote tuwe (Copy-cats)tunaweza pia kuwa wa kwanza kuanzisha jambo na wengine wakaiga. Kwani kuna ubaya gani? Si lazima kila kitu tuige wengine.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  14. KWANZA NAWAPONGEZA WALIOTOA WAZO LA KUANZISHA TAWI LA CCM UK,HONGERENI SANA,HAKUNA KIPENGELE CHOCHOTE CHA KATIBA YA NCHI YETU INAYO MZUIA SHARIF MAAJAR KUWA KIONGOZI WA TAWI HILO,NDIO MAANA ATA WAGOMBEA URAIS WANATOKA KATIKA VYAMA,TATIZO TAWI KABLA HALIJA ZINDULIWA TAYARI MMEVUNJA KATIBA YA CCM KIKAO GANI KILIKAA NA KUWATEUWA,KUNA WANA CCM WENGI TU AMBAO WANAKADI ZAO HAI NA WANAISHI HAPA UK WOTE WALIPATA MSISIMKO KWA HABARI NJEMA YA WAZO LENU,WAJUMBE MLIO WACHAGUA KUNA AMBAO HAWANA SIFA NA HATA AWAIJUI KATIBA YA CHAMA SIO WAADILIFU KATIAKA JAMII HAWAFAI KUWA VIONGOZI WATAWI VIONGOZI WACHAGULIWE KWA MKUTANO MAALUM NA SISI WANACHAMA TUWAHOJI KUJUA SIFA ZAO,KUNA BAADHI YA WATU WANAHULKA YA KUJITFUTIA UMAARUFU TU,SWALA LA KUA MJUMBE WA TAWI LA CCM SIO LAMCHEZOMCHEZO,NDUGU MAAJAR JIHADHARI NA WAPAMBE NAAMINI WEWE NI MTU MAKINAI NA UNAJUA TARATIBU ZA CCM KUPATA VIONGOZI WAKE KUANZIA SHINA,CCM SIO BENDI YA MUZIKI KUMCHAGUA KIONGOZI KWA AJILI YA KUKATA KIUNO SANA AU SUTI ZAKE,HAKUNA UBAYA KUWA NA TAWI UGAIBUNI,CUF ILKUA NA TAWI WASHINGON LIMEKUFA KIFO CHA MENDE,KUTOKANA CHAMA CHENYEWE AKINA DEMOKRASI,TATAWAHESHIMU KAMA WAASISI WA TAWI NAKUWAUNGA MKONO KAMA MTACHAGULIWANA WANACHAMA WA TAWI,KWA SASA ILI MKUTANO UFANE FUTENI HILO LA KUWA NA VIONGOZI WALIOJITEUWA KUEPUKA MATATIZO YASIO LAZIMA,KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI ZIDUMU FIKRA ZA WAASISI WAKE,ZIDUMU FIKRA ZA MALIMU NYERERE.SWALA LA UDINI HALINA NAFASI KWA MTANZANIA MWENYE AKILI ZAKE NA HIYO NDIO NGUZO YA UTAIFA WETU.
    FRANCIS NCHIMBI
    GLASGOW SCOTTLAND.

    ReplyDelete
  15. WEWE MICHUZI UNA NINI? TUMETOWA MAONI MENGINE HATUYAONI.
    TUMESEMA KATI YA HAO WALIOCHAGULIWA MMOJA WAO HAFAI, NA JINA LAKE NI MARIAM KILUMANGA.
    MBONA HUKUYATOA MAONI HAYO. KWANI WATANZANIA HAWATAKIWI KUJUA UKWELI? MAANA YA HII BLOG YAKO INAYOSIFIWA NI NINI KAMA UNAFANYIA CHOYO MAONI YA UKWELI.??

    ReplyDelete
  16. Tayari watu wameshaanza kutaka kujua kama ni chama kina waislamu tu au kwa nii hakuna Wakristo,sisi hatuna maendeleo wala hakuna Demokrasia ila ni fitina na kubaguana.Hatutaki tawi la chama chochote ila tunachoomba ni Amani kwa Watanzania wote.

    ReplyDelete
  17. Mheshimiwa Koloboi
    Inaelekea wewe ni mkereketwa wa...
    Mimi nina swali moja kwako,je Watanzania wengine walio ughaibuni wanaweza kuanzisha tawi la chama cha siasa badala ya CCM???????????
    ca (Ont)

    ReplyDelete
  18. >a< Jamani Watanzania wote ambao mnaishi Uingereza, mimi nawapongeza hao jamaa ambao walikaa wakafikiri kuwa kuna haja ya kuwa na Tawi la CCM London Uingereza. Kama wangi wanaovyofahamu, kuna Watanzania wengi ambao wanaishi huko Uingereza kwa miaka mingi sana. Na Hao Watanzania, wako wanaojihusisha na vyama tofauti vya siasa kama vili CUF,na CHADEMA. Na isitoshe, viongozi wa vyama hivyo vya siasa, wamekuwa wakienda Uingereza na kufanya mikutano yao na makundi yao husika bila bughudha wala maneno maneno yasiyo na msingi. Pia katika Watanzania hao hao waishio huko Uingereza, wako ambao ni aidha wanachama wa CCM au wapenzi wakereketwa wa CCM.

    >b<. Kinacho nishangaza, ni kwamba pamoja na kuishi huko UIngereza miaka mingi, hatukuwahi kusikia hata siku moja mtu au watu tena hasa hao ambao ni wanachama tayari wa CCM, kuwa na wazo la kuanzisha Tawi huko Uingereza.
    >c<. Jamani, napenda kuwaambia kuwa, hawa watu wanao andika haya ninayoyaita "maneno ya redio mbao", waache huo upuuzi wao, wawaache watu wenye busara wafanye mambo ya busara. Nina uhakika, hao waanzilishi wa mkakati wa kufungua Tawi huko LOndon, Uingereza; ni watu wenye uelewa, na uwezo kitaaluma zao, ambao hawawezi tu kuamka na kufanya kitu bila kuwa wanajua wanachokifanya. Nina hakika wamepita katika ngazi husika na ndio wakafikia hatua hiyo.
    >c<. Mume wa Balozi, au mke wa Balozi, sio wafanya kazi wa Serikali. Wanakuwa na wake zao au waume zao kwa sababu za kindoa, kwamba huwezi watenganisha. Na kwa taarifa yenu, mume wa Balozi au mke wa Balozi, huko Uingereza, anaweza kufanya kazi popote bila "Work Permit".Na kwa taarifa yenu, hata chakula anachokula Balozi, mke wake/mume wake hakinunuliwi na pesa ya Serikali. Balozi anajinunulia chakula na mahitaji yake mengine, mwenyewe kwa kipato chake ambacho ni mshahara wake. Hivyo, watu wanaandika tu pasipo kuwa na uhakika wa msingi wa malalamiko yao.
    >d<.Hakuna sheria inayokataza wahusika, katika maana hii, Watanzania kuanzisha chama cha kisiasa Uingereza na popote pale mradi wanafuata utaratibu husika. Hakuna sheria inayosema, mume wa Balozi, au mke wa Balozi, hawezi kufanya kazi Uingereza, au hawezi kuwa kiongozi wa chama anachotaka.
    >e<. Kama Balozi mwenyewe angekuwa kajiingiza kwenye chama chochote, hapo ndio kungakuwa na kasoro, maana yeye ni mwakilishi wa Rais Kiserikali, na anatakiwa kuwahudumia Watanzania wote pasipo kujali itikadi zao, Kisiasa, Kidini, Kikabila na Rangi zao.
    >f<. WATANZANIA, ACHENI TABIA YA KULALAMIKA BILA SABABU ZA MSINGI. WAACHENI WAPENZI WA CCM WAFUNGUE TAWI LAO, HATA WALE AMBAO WALIKUWA CUF, AU CHADEMA, NENDENI MKAHUDHURIE MKUTANO MKABIDHI KADI ZENU ZA VYAMA MLIVYO NAVYO, MJIUNGE NA CCM. MILANGO IKO WAZI.
    >g<.Katika kila jamii, lazima kuwe na mtu au watu ambao, watakuwa waanzilishi wa jambo lolote. Sasa, wakati muafaka ulifika, ucahaguzi rasmi wa viongozi utaitishwa, na WEWE, NENDA CHUKUA FOMU GOMBEA NAFASI YA UONGOZI.
    >h<. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA"

    ReplyDelete
  19. Fafanua hilo tawi kwa sheria litaandikishwakama chama cha siasa huko Uingereza? Au jumuia ya Watanzania waishio huko?
    -Nikitaka kuwasiliana nao naomba physical address ya ofisi zao na landline phone

    ReplyDelete
  20. napenda kusapoti maoni ya ndugu aliyemtaja MARIAM KILUMANGA ni kweli binafsi namfahamu sio trustworthy, sasa kama michuzi alishapewa repor halafu hatowi maoni mengine sio poa, kwani kwenye michaguo ya namna hii hasa ya chama tunataka wachaguliwe watu wanaofaa kwa ccm. au siyo.? sitaki kupata dhambi wengine siwafahamu lakini naweza kucomment kwa mariam kilumanga maana namfahamu na hana sifa nzuri.

    ReplyDelete
  21. >a>Napenda kumueleza huyo ndugu ambaye anauliza kama Tawi litasajiliwa kisheria hapa London na anataka anuani ya hilo Tawi ili awasiliane nao:
    >b>Hapa la msingi ni kwamba, Tawi hilo watasajili kama taratibu zinavyostahili,ninavyojua mimi vyama kama hivyo vinasajiliwa chini ya ".....Chapter".Najua unaweza usielewe nilivyoeleza kwa hayo mabano,kama ni hivyo basi samahani inabidi kwenda shule kidogo. Na kama huyo anayetaka aelezwe yote na wahusika kama namna ya kusajili na anuani, basi atoe jina lake na anuani yake hadharani ili wahusika wawasiliane naye. Huwezi kuomba taarifa halafu ufiche identity yako. Huu ni upuuzi na uhuni.
    >c> Nawapongeza viongozi wa muda wa Tawi kwa kufanya kazi nzuri ya kuanzisha Tawi la kwanza nje ya Tanzania. Mnastahili pongezi mno.Ningeshauri pia, vyama vingine kama CUF, CHADEMA, waige mfano huo mzuri, waanzishe Matawi na wao, waache kelele za uvunguni; maana hao wote wanaoandika malalamiko yasiyo na msingi ni hao hao CUF na CHADEMA.
    >d> Nchi haijengwi kwa majungu. Amkeni, msimame kidete mtoe hoja zenu za msingi na sio hoja za kulalamikia maswala ambayo hamjui hata taratibu zake.Nilifikiri mgejihusisha na kusoma ili mpanue uwezo wa uelewa wenu, jambo ambalo lingewasaidia kufahamu maswala muhimu badala ya kulalamika tu kila siku.

    ReplyDelete
  22. .Mzee Michuzi, sasa tunasoma michango ya watu walioenda shule. Mimi nasikia, hao wanaoandika kukashifu juhudi za Watanzania wenzao; hata wakiitwa kwenye mikutano ya Watanzania huwa hawaendi.

    .Ndio maana hawawezi kutofautisha mikutano ya Watanzania wote, na mkutano wa chama cha Siasa.Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa. Haiwezekani kundi la wanachama wa CCM wamwite akatae aseme hawezi kuwaona kwa kuwa kaenda Uingereza kwa ziara ya Serikali.
    Jamani, haiwezekani utofautishe Serikali na CCM katika mantiki fulani fulani. Hao watendaji wa Serikali, wanfanya kazi zao kutekeleza Sera za CCM na ndio ukweli,maana,Mawaziri,Manaibu wao,Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,Makamishna,na Watendaji wengi,wako katika nafasi zoa kwa tiketi ya CCM. Hata kama CUF wangekuwa madarakani; hao watendaji wangefanya kazi zao kutekeleza Sera za CUF,kwa kuwa wangekuwa pale kwa tiketi ya CUF.
    .Mimi naona ni kweli hao wanaolalamika ama upeo wao wa kuelewa ni mdogo, au basi tuwaite wajinga kwani hakuna hata mmoja ambaye amekuja na hoja yenye ufafanuzi au takwimu kuhusiana na malalamiko yao.Ni jamii ya watu wa kulalamika pasipo na sababu ya msingi.
    .Nampongeza mwana Blogi aliyetangulia kwa kufafanua mambo kadhaa kuhusiana na Watanzania wapenzi wa chama cha Mapinduzi kufungua Tawi huko London.
    .Nampongeza Mhe. Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwakubalia kuwabarikia Tawi lao la Chama huko London,maana ni haki yao ya msingi.Mwana Blogi huyo, amewakumbusha na wao waanzishe Matawi yao ya vyama vyao, na waalike Wenyeviti wao waende kuyabariki Matawi yao.Au basi Warudishe kadi zao za vyama vyao, waingie CCM, na wakati muafaka ukifika wa uchaguzi wa viongozi wa kudumu, wagombee nafasi zitazokuwepo;maana nimesoma hao viongozi waliopo ni waanzilishi na ni wa muda.
    .Taarifa nilizozipata kutoka katika vyombo husika zinaeleza, Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliwaona hao wanachama wa CCM Tawi la London baada ya kumaliza ziara yake ya Kiserikali, ambayo iliisha tarehe 16.01.07.
    Sasa basi kwa kuwa zaira yake Kiserikali ilikuwa imeshakwisha, alikuwa na uhuru sahihi kabisa wa kuwaona wana CCM, marafiki zake, jamaa zake na ndugu zake kama wangekuwa wapo kule London.
    Kwa maana hiyo,hao walalamikaji walipaswa waseme pia ah, haruhusiwi kuwaona ndugu, marafiki, na jamaa zake maana kaenda Uingereza kwa ziara ya Kiserikali.
    .Watanzania wenzetu, wakati umefika wa kuacha malumbano bubu ambayo hayaleti maendeleo.Hudhurieni mikutano mkiitwa,nendeni Ubalozikni kwenu muelimishwe na pelekeni hoja zenu kupitia Wabunge wenu ambao wanakaa katika vikao vya kutunga na kubadilisha sheria, na sio kusemea chini chini kwenye vijiwe.
    .MKUBALI, MSIKUBALI;KUNA SIKU TU MTARUDI NYUMBANI NAWAOMBEENI MRUDI MGOMBEE NAFASI ZA UONGOZI MJENGE NCHI YENU MAANA MNAONEKANA KUTORIDHIKA NA KILA KITU.

    ReplyDelete
  23. basi wote mlio mtaja MARIAM KILUMANGA hamjui kabisa. Na kama hamna la kusema nyamazeni. and get a life.

    ReplyDelete
  24. Nyie wote ambao mnamsema mariamu kilumanga ni waongo na hamfahamu maruiam. Kama kweli unaushahidi kwamba mariam kilumanga afahai basi jitaje wewe ni nani na ushahidi wako unatoka wapi. Sasa wewe unajificha na hautaki kujijulisha basi mie naona yote ni majungu na ni wivu. Mie nafahamu watu fulani fulani ambao wanaweza kuandika uongo kama huu yote haya ni majungu na wivu. Mariam Kilumanga anajitahidi sana kwenye jumuia ya watanzania, na anajitolea sana. Unafiki kama huu ambao unaharibu maisha ya watu kweli ni dhambi kubwa sana. Na mie nasema mtalipata kwani wewe uliandika mabo hayo hauta fanikiwa kamwe utabaki hapo hapo na uongo pamoja na poison letters zako na siku moja zitakurudia.

    ReplyDelete
  25. as for those who are bitching about mariam kilumanga and making viscious comments about the poor soul,why dont you do the running around then and do what she is doing?at least she is trying to play her bit and do something positive for the community.
    WABONGO BWANA mtu akijitolea matatizo.hivi tutaendelea kweli!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...