WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU MH. JUMA AKUKWETI AMEFARIKI DUNIA.
HAYATI AKUKWETI, AMBAYE ALIKUWA AMELAZWA HOSPITALI YA MILPARK JIJINI JOHANNESBURG KUTIBU MAJERAHA ALIYOPATA KATIKA AJALI YA NDEGE YA KULE MBEYA WIKI MBILI ZILIZOPITA, AMEAGA DUNIA SAA NANE ALFAJIRI YA LEO.
KATIBU MKUU OFISI YA RAISI MAMA ROSE LUGEMBE AMETANGAZA HAYO LEO KWA NIABA YA RAIS NA KUELEZEA KWAMBA MIPANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU IMO MBIONI, AMBAPO SERIKALI ITATUMA NDEGE KUUCHUKUA.
MOLA AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI
AMIN



Poleni Familia husika, Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Mungu awatie nguvu muweze kuhumili uzito wa msiba huu.
ReplyDeleteMaskini waziri wetu na wengine amekuwa Victim wa kutokuwa makini kwa watu wanaohusika na ndege ndege hiyo. Kuna habari kuwa ndege yao ilibeba magunia mengi ya mchele wa Kyela.!!
ReplyDeleteINNA LILLAHI WA INA ILAHI RAJIUUN.
ReplyDeleteMwezi mungu amlaze Mahala pema peponi. Amin
ReplyDeleteMungu amuweke pema peponi,Amin
ReplyDeletemungu ailaze roho ya kiongozi wetu mahala pema peponi.na awape nguvu na uvumilivu familia yake katika hiki kipindi kigumu sana katika maisha cha kumpoteza kipenzi wao.ila tu alilolisema bwana limekuwa.KULU NAFSI DHAIKATUL MAUT.
ReplyDeletePoleni sana familia na ndugu wa marehemu Juma Akukweti
ReplyDeleteMwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi - Amen.
inna lillah wainna illahi rajun. poleni sana familia ya marehemu. mwenyezi mungu atawapa subira. inshallah
ReplyDeletePole kwa familia ya marehemu...bwana ametoa na bwana ametwaa... mapenzi yake yatimizwe. Sote tu safarini na yeye Waziri wetu amemaliza safari yake. mungu awatie nguvu familia yake na wawe wavumilivu.
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi na pole kwa familia.Pamoja na hayo,kilikuwa kitendo cha kinyama na kisicho cha kiungwana kumpeleka South Africa muathirika mmoja tu wa ajali huku wengine wakiachwa nyuma na kufia hospitali.Maisha ya kila binadamu yana thamani sawa.Viongozi wetu kama wanataka sana kupata matibabu wanayodhani wanastahili hawana budi kuwekeza katika hospitali za nyumbani na sio kukimbilia nje ambapo wanaume wenzao wamejenga.
ReplyDeleteAnoy wa hapo juu 6:55:42pm you sick uneed help how did u know kama serikali ndio ilimplipia? Do u know him before he was waziri? tuko kwenye msiba so please respect wafiwa
ReplyDeleteAnonymous hapo juu naona hukuelewa mwenzio nia yake. Pengine wewe ni Muisalam au kama ni Mkristo pia hujui "safari" maana yake ni "maisha ya duniani". Hivyo hakutukana wala kumdhalilisha mtu.
ReplyDeleteccm imeanza kutoa kafara.ushirikina mtupu.....
ReplyDeleteKwa nini serikali ipeleke ndege ilhali ATC inakwenda SA kila siku? Serikali zisizokuwa makini ktk matumizi hakika hazitoendeleza nchi na raia wake KAMWE! POLENI SANA WAFIWA WOTE.
ReplyDeleteMungu ampumzishe kwa amani! LAKINI, jana nilikuwa nazungumza na jamaa fulani wakawa na maongezi yaliyoynifikirisha sana... Ajali imetokea na mhusika mkuu ni dereva (rubani) lakini yeye kalazwa, kakatwa mkono, katoka hospitali... Yameisha! Hivi mbona madereva wa mabasi kama Air Msae, Buffalo, nk; ikitokea ajali huwa wanatiwa mbaroni halafu masuala mengine ya uchunguzi yanafuata baadae? Hata kama ni majeruhi, huwa wanaugulia chini ya ulinzi na pingu mikononi. Au kwa sababu udereva wa ndege huwa unafundishwa kwa kizungu ndiyo maana hata namna ya kushughulikia wahusika wake ni ya kizunguzungu?
ReplyDeleteJamani jamani uchunguzi wa ajali upo wapi? sielewi ilikuwaje zaidi. Wenye news tupeni
ReplyDeleteJamaa alikuwa na wake watatu sasa kasheshe kwenye kutoa ubani.Serikali itampa ubani yupi.Ukimpa huyu wengine watanuna na kuhamia vyama vya upinzani.Kazi kwako Rose Lugembe katibu mkuu wa wizara!
ReplyDeleteHii ajali imejaa maswali mengi kuliko majibu. I can be alittle conspiracist sometimes, lakini yote kuanzia moto wenyewe na vifo hivi pamoja na supposedly-maneno yake ya mwisho inaleta mashaka kidogo. Sitaki kusema mengi kwa kuwa sina ushahidi, lakini for some reasons nafikiri kuna idadi kadhaa ya watu waliokufa tanzania miaka ya hivi karibuni because of what they know. I'd like to leave it like that.
ReplyDeleteBwana alitoa na Bwana ametwaa basi jina lake lihimidiwe. Akukweti tulikupenda lakini Yeye kakupenda zaidi. Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yako Pahala pema. Amen
ReplyDeletepoleni sana ndugu wafiwa, mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu. bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.
ReplyDeletePoleni sana. Mungu Amlaze mahali pema peponi. AMIN.
ReplyDeleteKuungua siyo mchezo, ana bahati kuwa alipata nafasi ya kuaga ndugu na marafiki kabla ya kufariki. Lazima alikuwa na maumivu makali sana. Lakini jamani hiyo ajali ya ndege jamani! Imechukua watu wanne sasa wa kwanza alikuwa mpiga picha Dada Theresia Nyantori.
Maskini Juma Jamaldin Akukweti. Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi. Amin
ReplyDeleteWananchi wa jimboni kwako walikukataa mbele ya Kikwete, mkafanya mizwenge na chama chako, ukaukwaa ubunge na hatimaye uwaziri, na katika kujipatia posho ya safari ukaenda Mbeya kukagua soko wakati taarifa za mkuu wa mkoa zilikuwa zinatosha kabisa, ona sasa umetuachia pengo lisilozibika kwa familia na linalozibika kwa uongozi wa nchi.
Mungu ni mwema,jamani semeni yote lakini Mungu akikuhitaji siku zako zikiisha basi hamna atakayeweza kukuongezea hata upelekwe nchi gani!Poleni wafiwa
ReplyDelete