Home
Unlabelled
ahhhaaaahhaaaaaa!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hiyo ahahahahaaa Muhdin Issa Michuzi unastahili, maana nafatilia counter hapa chini, leo lazima ile hit ya 1.000.000 milioni moja watu kutembelea blog yako itafika. CONGLATS
ReplyDeleteMichuzi umelalaaaaaaaaaaa, Niko nafatilia hii 1.000.000 tangu asubuhi, nitakupa muda kamili ilipofikia hii 1.000.000, sasa hivi bado wateja 900 tu, na nilivyoona ni kila sekunde una wageni 5 hivi, 1.000.000 itatimu sasa hivi. Mie ntacheki mara 5 ili kuiharakisha namba hii pia. Au?
ReplyDeleteMichuzi, ninayo furaha kubwa kukutaarifu kuwa nimekuwa visitor wa 1.000.000 kwenye blog yako. Nina ushahidi wa picha, ilikuwa Monday, February 12, 2007 saa 7:45:18 za mchana hapa Ubelgiji, sawa na saa 9:45:18 huko Tanzania. Unaniruhusu kuomba zawadi, ingawa halikuwa shindano? Naweza kukutumia ushahidi ukihitaji. Anoni GM
ReplyDeleteSaid Mwamba Kizota afariki
ReplyDeleteMchezaji za zamani wa kimataifa Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Said Mwamba Kizota amefariki dunia jana Jijini Dar baada ya kugongwa na daladala.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Bw. Emmanuele Kandihabi, amethibitisha juu ya kifo cha mchezaji huyo nyota na kuitaja gari iliyomgonga kuwa ni daladala aina ya Isuzu Journey ambalo hadi sasa namba zake hazijafahamika.
Akasema Kamanda Kandihabi kuwa marehemu Kizota aligongwa na daladala hilo wakati akikatiza Barabara ya Dk. Omar Ali Juma pale Temek, karibu na kituo cha mafuta cha Oilcom.
Imeelezwa kuwa baada ya ajali hiyo, Kizota alikimbiziwa katika Hospitali ya Wilaya Temeke ambako alifariki mishale ya saa 2:45 usiku.
Habari zinasema wakati akigongwa, marehemu Kizota alikuwa akitoka kushuhudia mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na Textile Du Pungue ya Msumbiji uwanjani Taifa ambako Simba ililala kwa penati 3-1 na kung�olewa mashindanoni.
Wakati wa uhai wake, Kizota ambaye alikuwa akimudu vyema kucheza nafasi ya ushambuliaji na mlinzi wa kati, aliiwezesha Yanga kutwaa vikombe kadhaa ikiwa ni pamoja na michuano ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati.
Aliwahi kuwa mchezaji bora wa mwisho nchini kuteuliwa na chama cha soka nchini, FAT mwaka 1993.
Miaka hiyo ya `90, pia aling`ara vilivyo ambapo akishirikiana na akina Edibily Lunyamila na Mohamed Hussein katika safu ya ushambuliaji, aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati nchini Uganda ambako huko, wakifundishwa na Kocha aliye marehemu pia kwa sasa, Mrundi Nzoyisaba Tauzany, akaibuka kuwa mfungaji bora.
Kudhidhirisha kuwa Mwamba alikuwa na kipaji cha pekee katika soka, baadaye alibadilisha nafasi ya uchezaji, kutoka kuwa mshambuliaji wa kati hadi kuwa mlinzi wa kati ambako nako, aling�ara sana.
Msimu wa usajili wa 1996/97, Kizota aliziingiza Simba na Yanga katika mgogoro wakati zilipojikuta zikimgombea kama alivyo sasa Athumani Iddi.
Baadaye, mkali huyo aliyekuwa na kipaji cha kukontroo mpira na kupachika mabao ya `video`, akaamua kuchezea Yanga baada ya kuiandikia barua FAT, akikana usajili wake Simba ambako awali, uongozi wa akina marehemu Priva Mtema ulimng�ang�nia kuwa ni wao.
Habari zilisema kuwa Kizota aliyekuwa Yanga damu, aliikana Simba iliyovumishwa kuwa iliahidi kumnunulia gari lakini ikawa ikimyeyusha na ndipo alipoamua kuitosa jumla baada ya kuitumikia kwa kipindi kifupi.
Kabla ya kung�ara na jina lake kuwa midomoni mwa wapenda soka nchini, Kizota aliwahi pia kuzichezea Tindo ya Tabora na Pan African ya Jijini.
Mungu ailaze mahali pema peponi.
Said Mwamba Kizota afariki

hiyo aliyoshika nini? sio mkangafu huo? au macho yangu tu sio mbaya lakini picha si zinatoka
ReplyDeleteSote ni wa mwenyezi mungu na kwake ni marejeo; Mwenyezi Mungu ailaze pema peponi Roho ya mwenzetu Said Mwamba Kizota, na awajaalie tahfifu Familia, Ndugu, jamaa na marafiki zake wote kufuatia msiba huu wa Ghafla. Ameen.
ReplyDelete23 kutoa ushahidi kesi ya Ditopile
ReplyDeleteAbadilishiwa shitaka, sasa ni kuua bila kukusudia
DPP asema kesi haziendeshwi kama enzi za Pilato
Na Ester Bulaya (www.uhuru.info),13 Feb 2007
MASHAHIDI 23 wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuru (58)
Miongoni mwa mashahidi hao ni kondakta wa daladala alilokuwa akiendesha marehemu Hassan Mbonde, abiria waliokuwa wamepanda gari hilo siku ya tukio na waliokuwepo eneo la tukio.
Kulingana na taarifa kwenye faili jipya la kesi lenye namba 13/2007, lililofunguliwa Mahakama Kuu, Januari 31, mwaka huu, mashahidi hao 23 ndiyo waliotoa maelezo wakati wa upelelezi wa kesi hiyo.
Chini ya mashitaka hayo mapya, Ditopile anashitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, ambapo anadaiwa Novemba 4, mwaka jana, saa moja usiku, katika njia panda ya Kawe na Bagamaoyo, Wilaya ya Kinondoni, alimuua bila kukusudia Hassan Mbonde.Mashitaka hayo mapya yanafuatia uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kubadilisha shitaka la awali la kuua, kutokana na ushahidi uliopo.Kwa mujibu wa DPP, Lawrence Kaduma, msingi wa mashitaka hayo mapya unatokana na ushahidi uliokusanywa kwa watu walioshuhudia tukio hilo.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaduma alisema ushahidi unaotolewa wakati wa upelelezi ndiyo unaomfanya abadili shitaka.
Kaduma alisema alifikia uamuzi wa kubadili shitaka kwa kuwa mashahidi wote walitoa ushahidi unaofanana, kwa maelezo kulikuwa na malumbano kati ya Ditopile na dereva na pia Ditopile alitukanwa.
Alisema anashangazwa na baadhi ya watu kuhoji uamuzi wa kubadili shitaka na kwamba hafanyi kazi kwa shinikizo au kusikiliza maneno ya watu, bali anachofuata ni sheria.
Kaduma alisema upelelezi unaonyesha Ditopile alitukanwa na katika hali ya kawaida ya kibinaadamu, hakuna mtu ambaye anapenda kutukanwa hivyo alipandwa na hasira na kupelekea kufanya kosa hilo.
"Unajua watu hawajui sheria, kama angeamka na kutembea na bastola kuanzia asubuhi na kusema lazima auwe hapo sawa. Hiyo moja kwa moja ni shitaka la mauaji, lakini yule siyo 'chizi' atoe bastola na 'kushuti', kulikuwa na majibizano, alitukanwa akapandisha hasira, na kwa misingi ya kisheria hakukusudia kwa sababu hakupanga kufanya hivyo, "alisema Kaduma.
Alisema mashahidi waliotoa maelezo yao ni kondakta wa dalalada alilokuwa akiendesha marehemu, abiria waliokuwemo kwenye daladala hilo na watu wengine waliokuwepo eneo la tukio na kushuhudia vizuri tukio hilo.
Aliendelea kusema kuwa hawafanyi kazi kwa kufuata hisia za watu, kwani kesi zinaendeshwa kwa misingi ya kisheria.
"Hatuwezi kuendesha kesi kama pilato, eti watu wakisema kaua basi iwe hivyo, lazima tufuate sheria na ushahidi na vielelezo husika, Yesu aliuawa bila kosa kwa uoga wa Pilato kwa kuwaridhisha wale watu, sasa sisi hatufanyi hivyo," alisema DPP.
Naye Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Prophir Lyimo, alithibitisha kupokea hati mpya ya mashitaka kutoka kwa DPP na kwamba tayari shauri hilo limeshafunguliwa ingawa bado halijapangiwa jaji na kwamba kinachofuatia ni kusomewa maelezo ya awali katika Mahakama ya Kisutu kabla ya kuhamia rasmi Mahakama Kuu, kuanza kusikilizwa.
"Nimeshapokea jalada la kuua bila kukusudia linalomkabili Ditopile, nadhani tayari makarani watakuwa wamefungua na kuwajulisha Mahakama ya Kisutu, ila bado halijapangiwa jaji, bado kusomewa maelezo ya awali huko Kisutu," alifafanua.
Hata hivyo, upande wa Mahakama ya Kisutu ambapo kesi hiyo ilikuwa inakwenda kwa kutajwa, upande wa mashitaka uliokuwa ukiondozwa na Gurvanus Muhume ulidai hauna taarifa ya kubadilishwa kwa hati ya mashitaka na kumuomba Hakimu Mkazi Mkuu Michael Lugulu kuwapa muda wa wiki moja ili wafuatilie.Hata hivyo, Wakili Ringo Tenga anayemtetea Ditopile, alipinga vikali hoja ya upande wa mashitaka na kudai taarifa hizo ni za kweli, hivyo wiki moja ni muda mrefu na kwamba upande wa mashitaka upewe siku mbili kwa ajili ya kupeleka taarifa sahihi juu ya taarifa hizo.
Hakimu Lugulu alikubaliana na upande wa utetezi na kuwapa upande wa mashitaka siku mbili, hadi keshokutwa, ili kuithibitishia Mahakama yake juu ya shitaka jipya.Katika Mahakama ya Kisutu jana kulikuwa na hali ya utulivu na ulinzi mkali kuliko ilivyokuwa ikitokea mwanzo, ambapo ndugu wa Ditopile walikuwa wamedhibitiwa na polisi huku mshitakiwa huyo akichanganywa na wengine tofauti na zamani, ambapo alikuwa akiletwa peke yake.
Ditopile aliwafanya watu waliokuwapo mahakamani hapo kuangua kicheko baada ya kuvaa kofia kubwa nyeusi iliyokuwa imemziba uso hadi pua yake, kwa kukwepa kupigwa picha. Kofia hiyo ilimfanya atembee kwa taabu kwa kuwa hakuwa akiona vizuri.
Ditopile alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Novemba 6, na kusomewa shitaka la mauaji ya Mbonde kabla ya DPP kubadili shitaka na kuwa la kuua bila ya kukusudia.Kwa sasa mshitakiwa huyo anaweza kuachiwa kwa dhamana kwa kuwa shitaka husika lina dhamana na Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Mpaka hapo ni basi tena jamani marehemu ndo mwenye makosa.
ReplyDeleteSasa huyo Braza Dito anatoka ndivyo sheria bongo zinavyopindishwa.Lakini this will happen to someone else then we will see if they will be treated the same.
Nilibashiri siku za nyuma kwamba mashitaka yatabadilishwa kwa manufaa ya Bwana Ditto! Kuua kwa kusudia ama bila kukusudia ni kuua tu. Uhai wa mtu umekwisha potezwa hata kama lugha gani itatumika!!!
ReplyDeleteInajulikana wazi kwamba kuua bila kukusudia carries a lighter sentence!!! Muheshimiwa anaweza akaruka na kifungo kisichozidi miaka miwili na kwa kuwa ni kosa lake la mwanzo na kwa kuwa alikuwa kibosile basi jail term inaweza kuwa suspended!!!!
Mademu zake kaeni mkao wa kula na muandae majola mengi sana ya kanga kumpamba mshikaji wenu kama mlivyofanya siku za nyuma pale Kisutu kumkinga na paparazi wasimpige picha. Safari hii siyo kumkinga bali zingine mumfunge kiunoni akatike akicheza mdundiko kusherehekea release yake!!!
Tunaamini ni kwamba JK amekwisha andaa position fulani katika moja ya balozi zetu nje akapumunzike jamaa yake.
Hii ndiyo sheria ya Bongo. Rule of law at its best!!!
Damu iliyomwagika itaendelea kumusuta mpaka na yeye atakapokufa kwani hakuna exemption kwa mtu yeyote hata kama alikuwa rais mdogo wa mkoa wa Tabora!!!