Home
Unlabelled
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
SUPER. THIS IS WHAT EVERYONE OF US IS INTERESTED WITH. TUMECHOKA NA DAGAA. HUU NI UDANGANYIFU MKUBWA. KUKIMBIZANA NA RUSHWA ZA ELFU MBILI HAKUNA MAANA. WALA RUSHWA SIO HIZI ZA KUOMBANA HELA YA CHUMVI. TUPAMBANE NA RUSHWA NA MIKATABA FEKI ZA KUUZA NA KUNUNUA RADAR,NBC,BANDARI TERMINALS, IPTL, RICHMOND, BARRICK, GEITA MINING CORP, AFGEM NA MIOZO MINGINE
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteKazi ipo katika kumvua papa amrani kwa kutumia mshipi, hivi ile report ya Warioba iliishia wapi?
ReplyDeleteKipanya acha mambo yako!!Uliona wapi PAPA akavua PAPA?Hao PCB wenyewe Kiongozi wao ndie PAPA mkuu.Sasa sijui kwa itikadi za Bongo nani anamchunguza!!Labda Jaji warioba atusaidie.Vinginenyo uozo mtupu mtaendelea kushika dagaa milele.
ReplyDeleteAcha hivyo michuzi! nimeandika ujumbe wangu kuhusiana na Rada na uongozi wa awamu ya tatu. Sikuweka tusi hata moja, lakini ujumbe huo umeutia kapuni lakini jumbe zenye kashfa na matusi unazimwaga tu bila soni yoyote.
ReplyDeleteKama unaanzisha mjadala ni lazima uwape uhuru wa kuandika wachangiaji provided that hawamtukani mtu. Nakuomba chonde chonde niweke ujumbe huu na ule wa rada kwenye ukurasa wetu. Natanguliza shukrani.
Afadhali maskini aliye huru kuliko mtumwa tajiri!
Na Profesa Leonard Shayo
TUSIPOKUWA makini na sera za uwekezaji, tutapoteza uhuru wetu kwa wageni! Tayari tumepoteza uhuru wa kujisikia tajiri, na badala yake tumerithishwa ugonjwa wa kujisikia maskini na wanyonge wa kufikiri! Umaskini unaotufanya tupapatikie uwekezaji, kama mkombozi, ni mtazamo wa wageni! Ni mtazamo wa kuyumbisha fikra zetu ili watupore rasilimali zetu! Wenyewe kwa wenyewe, hatuna umaskini! Tusipokuwa makini, hatimaye tutakuwa watumwa mchanganyiko, wa matajiri wachache na maskini wengi! Mbona leo tupo mchanganyiko wa matajiri wachache na maskini wengi, kwa mtazamo wa kibepari, lakini siyo watumwa hasa? Kwa mtazamo sanifu, nchi yetu siyo maskini!
Tunakumbuka enzi zile wanafunzi wa Chuo Kikuu walipofukuzwa kwa kosa la kunena “afadhali wakati wa mkoloni!” Lilikuwa ni kosa la ubinafsi, uliowafanya wanafunzi kujali zaidi maslahi yao, tena ya muda mfupi, kuliko uhuru wa bara la Afrika! Serikali ya wakati ule ilikerwa na tamko hilo la wanafunzi, maana lilikuwa ni matusi ya nguoni kwa uhuru wetu! Hatua ya kuwafukuza wanafunzi iliashiria ukweli kwamba, ni afadhali umaskini na uhuru, kuliko utajiri na utumwa! Iliashiria kwamba, ni afadhali umaskini na uhuru, kuliko utajiri na kutawaliwa!
Kama kungekuwa na kipima joto cha kupima joto la kuridhika kwa mwanadamu, basi maskini wengi wangekuwa na joto kubwa kuliko matajiri, na raia wangekuwa na joto kubwa kuliko watawala wao! Vinginevyo, dunia haingekalika, maana watu wengi ni maskini wa mali, na watu wengi ni raia! Kutokana na wingi wao, maskini wanajilinganisha wenyewe kwa wenyewe, na raia wanajilinganisha wenyewe kwa wenyewe! Kwa kuwa hawana mali za kugombania, wanaishi kwa amani! Mali za kugombania zinakuwepo kwa matajiri walimbikizaji!
Kwa upande mwingine, kwa uchache wao, matajiri na watawala wapo kwenye vita visivyoisha, vya kulinda utajiri wao, na vyeo vyao! Hawawezi kulala usingizi mnono, kama wa maskini wa mali, anayemudu chakula, malazi na mavazi! Hali ya kuzungukwa na maskini peke yake, ni kero kwa usingizi wa matajiri wa mali! Watawala nao hawawezi kulala usingizi, wakiwa wamezungukwa na umaskini wa raia, maana mamlaka iliyowateua inaweza kusitisha kibarua chao! Yaani watawala, hasa katika nchi maskini wa fikra, wanakuwa na maisha ya hofu, ya kupoteza kazi, kwa sababu huo umaskini unaathiri ufanisi wao!
Hali ya kujisikia maskini ni ugonjwa wa akili, unaosababishwa na virusi vya tamaa ya kuvuna shamba pasipo kupanda mbegu! Ni ugonjwa wa kujilinganisha na watu wengine, kwa kutumia vigezo bandia! Tunasema hivyo kwa sababu, kila mtu ana utajiri wa angalao kitu kimoja, na ana umaskini wa angalao kitu kingine! Kwa mfano, wapo wenye utajiri wa mali, na umaskini wa kukerwa na maisha ya watu wengine!
Pia wapo wenye umaskini wa mali, na utajiri wa kujali maisha ya watu wengine! Wapo wenye utajiri wa fikra, na umaskini wa mali; na wapo wenye utajiri wa kuhudumia jamii, na umaskini wa kujipenda wenyewe! Je, kuna busara gani kulinganisha utajiri wa mwenzio na umaskini wako, badala ya kulinganisha utajiri wako na umaskini wake? Ndiyo maana tunahoji kwamba, hali ya kujisikia maskiini ni ugonjwa wa akili, unaomfanya muhusika asahau utajiri wake, bila kufahamu kwamba, kusahau huko kunawatajirisha wengine! Kama ni kiongozi mkuu wa nchi, anasahau utajiri wa nchi yake, na kuuhamishia ugenini kwa maslahi binafsi!
Harakati za kupigania uhuru wa bara la Afrika zilifanyika bila kujali utajiri wa wakoloni, licha ya hisia za utajiri huo kutunyeshea kama tungeendelea kutawaliwa nao! Tulihitaji uhuru, hata kama ungeambatana na umaskini wa mali! Kwa maana nyingine, jamii za wakati ule zilitambua kwamba, ni afadhali uhuru na umaskini, kuliko utajiri na kutawaliwa, ama utajiri na utumwa! Je, jamii za leo zinatambua hivyo?
Kwa bahati mbaya, kumezuka tabaka la viongozi wengine wanaotafuta utajiri binafsi kwa gharama yoyote, ikiwa ni pamoja na kuuza uhuru wa nchi zao! Kwa viongozi hao, utajiri na kutawaliwa, ama utajiri na utumwa, ni bora kuliko uhuru na umaskini! Tunatakiwa tuwapinge viongozi wa aina hii, kwa nguvu zetu zote, ili tuulinde uhuru wetu! Kwa mfano, tunatakiwa tukatae utajiri unaoambatana na maovu kama ya ubaguzi wa rangi!
Kwa upande wa Tanzania, zipo dalili za kuwepo ubaguzi wa rangi kwenye huduma, na zipo dalili za kuwepo ubaguzi wa rangi kwenye ajira, mishahara na marupurupu, hasa katika maeneo kadhaa ya wawekezaji! Katika maeneo mengi, mishahara wanayolipwa wataalam wa kigeni inatofautiana sana na mishahara wanayolipwa wataalam wa kitanzania, kwa kazi hiyo hiyo! Wakati mwingine, hao wataalam wa kitanzania wana sifa za kitaaluma zinazopita zile za wageni!
Hayati baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikemea uhuru wa bendera mara nyingi! Alielewa kwamba, uhuru upo kichwani, na kwamba bado walikuwepo watu ambao hawajajinasua kutoka kwenye minyororo ya utumwa na kutawaliwa! Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba, hadi leo, miaka zaidi ya arobaini ya uhuru, bado kuna watu wengi wanaowaogopa wageni! Wanafanya kazi kwa woga, na wanaamini kwamba, uwezo wao ni mdogo kulinganisha na ule wa wageni! Maneno kama uhuru na uraia hayana maana kama tutaendelea kuwaogopa wageni, badala ya wageni kutuogopa!
Kufanya kazi kwa woga ni utumwa! Tunasema hivyo kwa sababu, kama woga ni wa kutoweza kuifanya kazi, basi muhusika anatakiwa ajiuzulu! Lakini kama muhusika ana uwezo wa kuifanya kazi, na bado anaogopa muajiri wake, basi woga huo hauna tofauti na ule wa watumwa, ama ule uliokuwepo wakati wa ukoloni! Tuna hofu kwamba, kama hatua za haraka hazitachukuliwa kutokomeza woga wa aina hii, magonjwa ya moyo yataongezeka, na hivyo kuligharimu taifa nguvukazi pamoja na gharama za matibabu! Mbaya zaidi ni kwamba, uhuru wetu utapotea, na uwezo wetu wa kufikiri utasinyaa, maana woga wa kutoa ushauri utatunyima sababu ya kufikiri!
Athari za wananchi kuwaogopa wageni ni nyingi, na za hatari kwa hatma ya nchi yoyote! Woga unajenga tabia ya kutojiamini, na kwa maana hiyo, unauwa ari ya kuwa huru! Wataalam wanaowaogopa wageni hawawezi kushiriki katika kutayarisha mikataba ya kimataifa, kwa sababu wataburuzwa! Hata kama hawapendi rushwa, watalazimika kuipokea, kutokana na woga wao! Rushwa za aina hii zinaweza kutolewa kama misumari kwenye mikataba, ili wahusika wasidhubutu kuikana siku za baadaye!
Tunaishauri serikali ya awamu ya nne ifadhili tafiti za kubaini viwango vya woga kwa wageni, miongoni mwa wananchi, na hasa wageni wawekezaji! Tunahitaji tafiti za kubaini viwango vya ubaguzi wa rangi katika sehemu zote za ajira, na hasa zile za wawekezaji wageni! Hatukujitoa mhanga kutokomeza ubaguzi wa rangi huko Afrika ya Kusini, na sehemu nyingine duniani, kwa ajili ya kuingiza ubaguzi wa rangi katika nchi yetu! Kwa maana hiyo, tunapendekeza sheria itungwe kwa ajili ya kuwaadhibu watakaopatikana na kosa la ubaguzi wa rangi! Pia tunapendekeza mbinu muafaka zitumike kujenga tabia ya kujiamini, na kufuta kabisa woga wa wananchi kwa wageni! Tusipokuwa makini, tutajenga mila ya kuwaogopa wageni!
Katika soko huria, zipo tekinolojia zinazoweza kutumika kibaguzi kuwabana wafanyakazi! Mfano ni tekinolojia za kufuatilia walipo wafanyakazi, na wanachofanya saa 24, kwa ubaguzi! Hatupingi matumizi ya tekinolojia kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa kazi, lakini tunapinga matumizi ya tekinolojia kuboresha ubaguzi wa rangi!
Ugonjwa wa kujisikia maskini, hasa miongoni mwa viongozi, ndiyo chanzo kikubwa cha kukubali kunyanyaswa na wageni, ikiwa ni pamoja na kujijengea woga usio wa lazima! Ugonjwa wa kujisikia maskini unatufanya tukumbatie pia ubaguzi wa bidhaa tunazozalisha, dhidi ya bidhaa za nje, hata kama ni hafifu! Mfano ni madawa! Je, tuna mikakati gani ya kuhakikisha kwamba, madawa tunayotumia yana lengo la kutibu, badala ya lengo la biashara? Ni dhahiri kwamba, kama lengo ni kutibu, na kama tunatengeneza dawa inayotibu hapa Tanzania, uagizaji wa dawa mbadala, yenye uwezo hafifu ya kutibu, ni uhujumu wa uchumi, na ni kuwanyima wagonjwa haki ya kupona! Tunaweza kusema hivyo kwa bidhaa nyingine zote! Tunashauri kwamba, mamlaka husika zijidhatiti ili zihakikishe kwamba, falsafa ya soko huria na sera za uwekezaji, kwa pamoja havitumiki kwa ajili ya kuuwa viwanda vya ndani! Kwa maneno mengine, tunapinga harakati za kujenga umaskini wa mali ndani ya harakati za kutokomeza umaskini!
Nchi kama Tanzania ni maskini wa tekinolojia, lakini ni tajiri wa mali asili, na ni tajiri wa amani, umoja na utulivu! Kwa maana hiyo, utajiri wetu una thamani kubwa kuliko faida ya kukaribisha wawekezaji wa kutupunguzia umaskini wa tekinolojia na kupokonya uhuru wetu! Je, ni kweli wanatupunguzia umaskini wa tekinolojia? Kwa kuwa dunia imejaa umafia, unafiki na ubinafsi, ni hatari kulala usingizi tukisubiri ukombozi kutoka kwa wawekezaji! Upo uwezekano mkubwa wa nchi yetu kufanywa dampo la tekinolojia zilizopitwa na wakati, na bidhaa za hatari kwa matumizi ya binadamu! Kwa mfano, mitambo iliyookotwa majalalani, katika nchi zilizoendelea, inaweza kupigwa rangi na kuletwa kwetu kama mitambo mipya! Vile vile, vyakula vilivyoisha muda wake wa matumizi vinaweza kupigwa mihuri ya tarehe za mbele, kana kwamba ni safi kwa matumizi ya binadamu, halafu ikaletwa Tanzania! Kwa mfano, hatuoni sababu ya kuagiza ngano kwa ajili ya kuoka mikate, wakati ngano inaota Tanzania! Tunawaomba wananchi waajiriwa kwenye makampuni, na hasa yale ya wageni, wawe walinzi wetu, kwa kutoa taarifa za dhuluma kwa maafisa wa usalama wa taifa!
Hatuwezi kufanikiwa kuulinda uhuru wetu kama hatutajenga tabia ya ya kujiuliza na kujibu maswali kama “kwa nini”, “kwa sababu gani”, na “kwa manufaa ya nani”, kila mara tunapojihusisha na maswala ya kimataifa! Kwa mfano, tunapowapambanisha viongozi wa juu wa nchi na wafanyabiashara wa nje, tunakuwa tunatafuta nini? Waliobuni utaratibu wa “Protocol” hawakuwa wendawazimu! Je, uwekezaji wa vitegauchumi, pasipo uhamisho wa tekinolojia, una faida gani kwa taifa? Tunapendekeza kwamba, wawekezaji watakiwe kuwa na utaratibu wa kuhamisha tekinolojia na utaalam kutoka kwao kuja Tanzania! Watakiwe kuwafundisha watanzania, kwa ajili ya kufanya kazi za wageni baada ya kipindi maalum! Yaani tuwe na muda wa mwisho kwa wageni kufanya kazi nchini, isipokuwa katika maeneo machache kwa hoja zenye nguvu!
Mwandishi wa makala hii ni mtaalam wa kompyuta na Hisabati
nawe profesa kwenda kule,hivi mnategemea kweli watu tupoteze kusoma hilo gazeti lako lenye utumbo?grow up,fanya summary yenye points tupu hatuna muda wa kupoteza sasa unafikiri tukisoma yote nani atawahi kubeba mabox?grow up profesa fake.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteProf. Shayo, anaandika mengi ya msingi na maana kubwa kwa Tanzania yetu leo. Katika kuumba umbo zuri la kile anachozungumzia, Prof. anagusia kwa kutoa mfano wa sababu ya kufukuzwa kwa wanafunzi "wa Chuo Kikuu" hapo tarehe 22 Oktoba, 1966, kama ninavyokunukuru:
ReplyDelete"Tunakumbuka enzi zile wanafunzi wa Chuo Kikuu walipofukuzwa kwa kosa la kunena “afadhali wakati wa mkoloni!” Lilikuwa ni kosa la ubinafsi, uliowafanya wanafunzi kujali zaidi maslahi yao, tena ya muda mfupi, kuliko uhuru wa bara la Afrika! Serikali ya wakati ule ilikerwa na tamko hilo la wanafunzi, maana lilikuwa ni matusi ya nguoni kwa uhuru wetu! Hatua ya kuwafukuza wanafunzi iliashiria ukweli kwamba, ni afadhali umaskini na uhuru, kuliko utajiri na utumwa! Iliashiria kwamba, ni afadhali umaskini na uhuru, kuliko utajiri na kutawaliwa!
Naomba kuchangia machache kuhusu kufukuzwa kwa wanafunzi hao:
Moja, si wanafunzi tu wa chuo kikuu (ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa diploma na uganga hapo Muhimbili) waliofukuzwa. Walikuwemo wanafunzi wa Chuo cha Aridhi, Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, na Chuo cha Biashara. Jumla ilikuwa wanafunzi 392.
Pili, wanafunzi hao hawakufukuzwa kwa sababu moja ya kusema "afadhali wakati wa mkoloni."
Tatu, wanafunzi hao hawakusema "afadhali wakati wa mkoloni" katika barua yao iliyosomwa na mwanafunzi Mkoka mbele ya Rais. Maneno (“matusi ya nguoni kwa uhuru wetu”) hayo yalikuwa yameandikwa kibinafsi kwenye kibango alichobeba mmojawapo wa wanafunzi hao.
Nne, kiini hasa cha maandamano hayo kililenga kutoa dukuduku za wanafunzi hao mbele ya Waziri Mkuu kupinga muswada wa Kujenga Taifa Bungeni.
Tano, mazingira (japo tofauti za wakati) ya kutoka uhuru hadi siku hiyo ya Jumamosi 22 Oktoba, 1966, hadi kutangazwa kwa Azimio la Arusha, yalikuwa karibu sawa na ya sasa. Ubinafsi ulikuwa unatanda serikalini na katika nyanja za biashara, kiasi kwamba wengine walikuwa wanaitwa manaiza na wengine akina maganga ama makabwela. Hii ndio ilikuwa inamsumbua Mwalimu, mlilia haki kwa wote.
Sita, kiini hasa cha kupinga muswada huo kilikuwa ni kwa nini wanafunzi wa vyuo vya juu ndio tu waopolewe for national sacrife na huku mawaziri, viongozi wa chama na serikali, na kadhalika waendelee kujinufaisha kibinafsi, ikiwa ni pamoja na kununua hisa katika makapuni ya binafsi na kuwa mamemba wa bodi. kutokana na hali ya namna hiyo, janga la tarehe 22 Oktoba, 1966 lilitokea, baada ya wanafunzi wa vyuo vya juu kukataa kulipwa shilingi 20 kila mwezi wakati wa mafunzo ya kujenga taifa kwa miezi sita, na hapo baadaye wapokee 40% ya mishahara kwa mwezi kwa miezi 18. Simply put, kwa nini wawe the only sacrificial lambs katika kujenga taifa la Tanzania.
Saba, kingine kilichomkasirisha Nyerere ni kwa viongozi wa wanafunzi hao kupuuzia kile alichokuwa amewaeleza kina ubaga katika mkutano wake na hao viongozi sababu za kuanzishwa kwa lazima the new national service scheme. Mwalimu alitumaini wanafunzi wa chuo kikuu wangemsaidia kupambana na kuongezka kwa pengo la matabaka nchini.
Nane, viongozi hao wa wanafunzi walikuwa wakimsakama Waziri Mkuu kana kwamba ndiye aliyehusika na muswada huo...ambao ulikuwa ni wa serikali. Akijieleza kwa ukali mbele ya wanafunzi hao, Rais Nyerere alitamka Waziri Mkuu nimemchagua mimi. Ninyi wanafunzi hamna sababu ya kumsakama Waziri Mkuu wangu. Mnaisakama serikali, ambayo mimi ni kiongozi wake (NOT VERBATIM).
Mwisho, kuna baadhi ya Watanzania ambao wanafikiria kuwa wanafunzi hao waliandamana hadi Ikulu kukabiliana na Rais. Hasha! Walipofika mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu (mind you, umati wa maandamo ulikuwa umewakumba wana Dar wengine, kama ngoma ya mdundiko) waliambiwa Waziri Mkuu hayupo ofisini.
Kwa hiyo, waliendelea na barabara iendayo Magogoni, kupitia Wizara ya Elimu mkabara na Ikulu, wapinde mkono wa kushoto kurudi vyuoni. Askari wa pikipiki waliokuwa wamewatangulia walisimama na kamanda wao akatoa kauli hii:
Maandamano haya ni ya wanafunzi, tunaomba wale wote wasio wanafunzi kuondoka maandamanoni na kusambaa...Wanafunzi, Rais anapenda kuzungumza nanyi. Karibuni Ikulu (not verbatim).
Mzozo ulizuka kati ya viongozi wa wanafunzi. Kundi moja lilikataa kutii mwito wa kamanda wakisema hawakuja kuonana na Rais, na kwamba kwa kuwa Waziri Mkuu hawakumwona, walikuwa wanataka kurudi vyuoni. Kundi jingine lilifanikiwa kuwatuliza wenzao na kutii kuitikia mwito wa Rais, ambaye alikuwa kipenzi hasa hapo Mlimani.
Wakati mzozo huo ukiendelea, waandamanaji wasio wanafunzi waliondoka...na katika ondoka ondoka hiyo, wanafunzi wengine wa vyuo vikuu hivyo nao walikunja mikia yao na kutoweka kisiri siri!
The rest is a sad story ambayo inataka iandikwe ili ukweli zaidi upatikane, hasa kutoka kwa wale waliokuwa viongozi wa wanafunzi, wanafunzi walioshiriki katika majadiliano ya kutayarisha maandamo yenyewe, na wale wengine ambao katika kushiriki maandamanoni kama wanafunzi wa Chuo Kikuu, ilionekana kwao kuwa "cool". hawa ndio walishawishi wanafunzi wengi kushiriki katika maanadamo hayo kwani the marketing of the idea was at "buddies" level!
Mwalimu Nyerere alikuwa forgiving and compassionate. Wanafunzi hao walisamehewa, na kurudi to their alma mater kutoka “Diaspora”, jina wanafunzi wa Mlimani walilopenda kujiita baada ya kurudi hapo Mlimani. Kati ya wanafunzi hao, wengi wamefanikiwa kuwa viongozi wa juu serikalini na kwinginepo. Visiki havikupenda kuomba msamaha wa kuwa-reinstated. Havikurudi! Kisiki sugu kiliondoka nchini mara na kilipotelea Ulaya.
Toka uhuru hadi hiyo ya tarehe 22 Oktoba, 1966 (tokana na mipango ya maendeleo ya miaka mitatu na mitano iyokuwa inaandikwa kwa misaada na watalaamu wa Benki Kuu ya Dunia, na wataalamu wengineo wa nchi za Magharibi, ilikuwa inaunda mfumo wa kile Prof. Shayo anachoita, “matajiri wachache na maskini wengi!” Napenda kuhusisha hali hiyo iliyozaa “kosa la ubinafsi, uliowafanya wanafunzi kujali zaidi maslahi yao, tena ya muda mfupi, kuliko uhuru wa bara la Afrika” hususani “matajiri wachache na maskini wengi” na hali ya sasa inayomkera Prof. Shayo kuuliza, “ Mbona leo tupo mchanganyiko wa matajiri wachache na maskini wengi, kwa mtazamo wa kibepari, lakini siyo watumwa hasa?”
Wengine wetu tumetoka mbali, been there; seen it!
Hebu haya mambo yapelekeni magazetini watu wengi wayasome hasa kizazi cha miaka ya 1970s. Kuna mengi wanaweza kujifunza
ReplyDeleteNinaelewa kwanini Michuzi hakuweka post yako before kwani kama ndiyo magazeti hivyo unammalizia nafasi tuu.
ReplyDelete