chuma hicho, goooooooooh!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa


  1. Juhudi za Rais Kikwete kuinua soka zaanza kuzaa matunda

    * Watanzania kuteta na Abramovich, Chelsea kutua Dar
    * Itacheza Kombe la Kikwete kwa lengo la kuinua soka nchini

    Na Eric Toroka (majira.co.tz 9 feb 2007)

    TANGU Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete alipoanza kufanya juhudi za kufufua soka nchini, Watanzania, wahisani, taasisi na kampuni mbalimbali zimejitolea na kuonesha nia ya kumuunga mkono.

    Tumeshuhudia jinsi Rais Kikwete alivyofanya juhudi za kuwezesha kupatikana Kocha Mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars), Marcio Maximo na kuahidi Serikali kumlipa mshahara kila mwezi.

    Juhudi hizo zimeonekaa kuzaa matunda tangu ujio wa kocha Maximo kutoka Brazili ambapo kwa kipindi kifupi tu, Taifa Stars imewabamiza vigogo wa Afrika zikiwamo Bukinafaso na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Haiishi hapo tu, pia tumeona juhudi za Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakitafuta wafadhili kwa ajili ya kuinua soka nchini.

    Moja ya juhudi hizo ni kupata udhamini wa Taifa Stars kwenda kwenye mazoezi ya mwezi mzima jijini Rio de Janeiro, Brazili kutoka kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Benki ya NMB na Kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (METL).

    Kwa upande wa taasisi kutoka nje tumeshuhudia Global Scout Bureau (GSB) ambayo kwa kiasi kikubwa Makamu wa Rais wa taasisi hiyo, Jack Pemba alifadhili pragramu ya kunyanyua vipaji ili kupata wachezaji wa kuwauza Ulaya.

    Tayari taasisi hiyo ya GSB imeshawaleta nchini wachezaji nguli wa zamani wa Uingereza, Darren Barton, John Barnes, na Les Ferdinand.

    Lakini hivi karibuni kumeibuka habari kuwa mmiliki wa mabingwa wa Ligi Kuu England, Chelsea; Roman Abramovich anatarajiwa kukutana na Watanzania waishio Uingereza Mei mwaka huu ikiwa ni mpango wa kundeleza soka nchini.

    Hivi sasa wako katika harakati za kusajili taasisi ya kuendeleza soka nchini itakayojulikana kwa jina la Tanzania Youth Sports Charity Organization (TYSCO).

    Mratibu wa taasisi hiyo isiyo ya kiserikali, Allan Kalinga anasema ina mpango wa kuanzisha mashindano ya aina tatu yakiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuinua soka kwa vijana nchini.

    "Mpango wa makombe haya matatu ni kuwa, kombe moja litakalojulikana kama Kikwete International Cup Tournament ambayo itajumuisha timu kutoka Ulaya na hapa nchini. Kombe jingine litahusisha timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Visiwani na kombe la tatu litashirikisha timu za Wabunge dhidi ya Mabalozi ikiwa ni katika kuchangisha fedha za kufanikisha mradi huu," anasema Kalinga.

    Vikombe hivyo vya mashindano hayo ya Kikwete vinatarajiwa kukabidhiwa mwezi huu kwa Rais Kikwete.

    Katika juhudi za kuhakikisha taasisi hiyo inafanikisha malengo yake, Kalinga anasema wamefanya utaratibu wa kumwona mmiliki wa Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich na kupewa tarehe za Mei mwaka huu.

    Miongoni mwa mambo ambayo wanatarajia kuzungumza na bilionea huyo Mrusi ni juu ya nia ya TYSCO kuendeleza soka la vijana nchini na kuialika Chelsea katika mashindano ya Kikwete International Cup.

    Mbali na hayo, pia Kalinga anasema watamuelezea juu ya vivutio vilivyopo nchini kama njia ya kuinadi Tanzania nje ikiwa ni kuitikia mwito wa Rais Kikwete kuitangaza nchi.

    "Mwakilishi wetu Tanzania ni Muhidin Michuzi ambaye yuko mbioni kusajili taasisi hiyo. Pia katika hayo tumepanga miadi na kupewa tarehe za Mei kuonana na mmiliki wa Chelsea Abramovich ili asaidie mradi huu kupitia 'charity' ya Chelsea London iitwayo Right To Play. Katika mambo tutakayozungumza ni timu ya Chelsea kushiriki kwenye Kikwete Cup na pia kutembelea vivutio vya nchi yetu," anasema Kalinga.

    Anasema: "Ni jambo la kujivunia na la kuungwa mkono na wadau wote wa soka nchini. Mpango mzima wa namna ya kutunisha mfuko wa kampeni hiyo kitaifa kama nilivyodokeza unaonesha nuru ya kuleta mwamko wa kweli kisoka kwa vijana Tanzania.”

    Akizungumzia lengo lake anasema ni kuanzisha kituo cha kufundisha soka (football academy) katika makao makuu yote ya mikoa Tanzania Bara na Zanzibar.

    Kalinga anasema, kwa kuanzia mpango huo utatekeleza nusu tu ya malengo yake yaani badala ya vijana 50 kila mkoa utatekeleza vijana 25 na kwa kutoa posho ya sh. 50,000 badala ya sh. 100,000 kwa vijana 50.

    Mradi huo ambao si wa kibiashara utakaoshirikisha pia timu kutoka Zanzibar na ambao hautawabana vijana hao katika mikataba ya hila, utakuwa wa kitaifa na utawategemea sana wadau wa soka wa ndani na nje ya nchi katika kutunisha mfuko wa malezi ya vijana hao.

    Kalinga anatoa mwito kwa wadau wote wa soka kushirikiana na waratibu wa mradi huo ili ndoto ambayo taifa hili imekuwa ikiota kuwa juu kisoka, iweze kutimia.

    "Kuandaa timu za vijana ni jambo la gharama sana na ndio maana hata timu zetu kubwa nchini zimeshindwa kuendesha 'academy' zao katika njia ya kuwalipa posho ili kweli wawajibike. Tungeomba timu kubwa na maarufu kuuangalia mradi huu kwa makini na kutoa msaada wowote wa hali pindi watakapoombwa.Tunatarajia timu kubwa zitaacha ubinafsi katika mradi huu," anasema.

    Hata hivyo, anaiomba Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kutoa ushirikiano katika kutoa vibali kwa timu kubwa kutoka nje kuja nchini kucheza soka kama ilivyo mipango ya TYSCO.

    Pia anaongeza kuwa TYSCO inatarajia kuleta vifaa vya michezo vitakavyotolewa kama misaada kutoka kwa wadau wa soka nje ya nchi pamoja na vile ambavyo taasisi hiyo itanunua na kuvileta nchini kwa ajili ya kusambazwa mikoani kwenye timu hizo. Hivyo taasisi hiyo imeomba kusamehewa ushuru wa vifaa hivyo mara itakapoleta.

    Kalinga anasema: "Napenda kuongezea 'plan B' kama 'plan A' ya kuendeleza wachezaji 50 chipukizi itaonekana mzigo, ni kwamba iwapo tutakata namba ya wachezaji chipukizi kutoka 50 hadi 25, hii ikimaanisha ya kuhusisha wachezaji 22, kocha mmoja, meneja mmoja na mhazini mmoja."

    Anasema kutokana na mchanganuo huo, kila mchezaji atapata posho ya sh. 50,000 kwa mwezi ambayo gharama yake kwa malipo ya wachezaji wote ni sh. milioni 250. Kalinga anaongeza kuwa, bajeti hii ni kutokana na utendaji kwa miezi 10 kila mwaka kama mahesabu yao yanavyoonesha.

    Katika ngazi ya mikoa, mradi huo utagharimu kiasi cha sh. milioni 12.5 na ikizidishwa kwa mikoa 23, inafanya jumla ya gharama zote kwa mwaka kuwa sh. milioni 287.5.

    "Kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kufikiwa hata kama Simba na Yanga hawatakubali kucheza mechi," anasema Kalinga.

    Mratibu huyo anaongeza kuwa, kwa kuanzia tu mradi huo utagawa mipira katika timu za shule nchi nzima ambapo zoezi hilo linatarajia kugharimu sh. milioni 57.5 ambapo katika kila mtu itagharimu sh. 100,000 kutoka kwa wachezaji 575.

    Anasema hii inajumuisha mipira, jezi na mambo mengine kwa kila mchezaji.

    Taasisi hiyo inaundwa na A. Kalinga, V. Kinyange, V. Mgoya waishio Uingereza na Muhidin Michuzi.

    "Ni matumaini yetu mpango huu kwa kushirikisha kamati za wafanyabiashara na wadau wa soka kutoka mikoani matunda yake yatakuwa makubwa. Kwa yeyote mwenye maoni na michango atume kupitia barua-e: allankalinga@aol.com," anasema Kalinga.

    Barua-e: toroka27@hotmail.com

    ReplyDelete
  2. Good idea but economically not feasible. Where are you going to get all those money from? What will happen if Abramovich will say no?

    Try to start with a simple but achievable plan and move forward from there.


    Wish you all the best.

    ReplyDelete
  3. Ha ha ha haaa.... Kipa karamba mchangaaaaa........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...