
jose chameleon (shoto) wa uganda akitesa kwenye sauti za busara majuzi. huyu bwana hivi sasa hapigi pleibeki kama walivyo wasanii wengi ist afrika mashariki. ana bendi yake ambayo ni mfano wa kuigwa.
kuna wadau wangependa kujua ninavyohesabu wageni. hapo chini ya blogu kuna kitufe cha bluu kama dunia hivi ambacho ukibofya kinakupa data zote ama bonyeza hapa


Kesi ya Dito: Mambo hadharani
ReplyDelete2007-02-16 17:15:27
Na Mwandishi Wetu
Maelezo ya mashahidi yaliyoanza kutolewa kuhusiana na tukio la mauaji ya dereva wa daladala linalomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, yameanika mambo kibao ambayo awali, kamwe hayakuwa yakifahamika.
Miongoni mwa mambo hayo ni kuwa, Mosi, wakati tukio hilo linatokea mnamo Novemba 4 mwaka jana, pale katika barabara ya Bagamoyo, kunako njia panda ya kuelekea Kawe, kulikuwa na watu kibao walioshuhudia na ambao watakuwa mashahidi katika kesi hiyo.
Pili, imedaiwa kuwa mtuhumiwa kabla ya kufanya mauaji hayo, alimzaba vibao kondakta wa daladala hiyo Thomas Mwita.
Pia ikaelezwa kuwa licha ya kumzabua konda huyo, mtuhumiwa alimtishia kwa bastola.
Kitu kingine kipya kilichoelezwa jana ni kwamba mtuhumiwa alieleza mbele ya Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Alfred Tibaigana na Abdallah Msika kuwa yeye si mheshimwa tena bali ni muuaji.
Jambo lingine lililofahamika jana ni kuwa taarifa ya daktari inaonyesha marehemu alipigwa risasi mbili ambazo zilitokea upande mmoja na kwenda hadi wa pili.
Maelezo hayo yalitolewa jana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa na pia mtuhumiwa kubadilishiwa mashitaka.
Mashataka yake yamebadilishwa kutoka mauaji na kuwa kuua bila kukusudia.
Awali, upande wa utetezi uliiomba Mahakama mteja wao apewe dhamana baada ya kubadilishwa mashtaka.
Hata hivyo Hakimu Luguru alitupilia mbali ombi hilo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina uwezo wa kutolea maamuzi kesi hiyo.
SOURCE: Alasiri
Michuzi kazi nzuri sana na nimeona stats zako ni kweli wengi wanaingia na nimeona website nyingine nyingi za kitanzania ambazo nilikuwa sizijui zina link yako. Tuwekee top ten sites zinazoleta watu wengi kwenye mtandao wako.
ReplyDeleteKwanza kabisa mshtakiwa Ditopile, kama mmiliki silaha, na mwanajeshi anajua wazi kuwa unapoweka risasi kwenye chamber, ukatoa usalama, ukavuta trigger, risasi itafyatuka!Kama silaha hiyo ilikuwa ni bastola ya kawaida, na siyo machine pistol, alifyatua risasi mara mbili. Hii inamaanisha kwamba alikusudia kabisa kufyatua risasi ambazo zote mbili zilimlenga barabara marehemu dereva wa daladala. Hapa hakuna kesi ya mauaji bila kukusudia bali ni murder in the first degree!
ReplyDeleteChameleon anapiga mziki wenye rythim nzuri na maneno yake yamejaa falsafa nzuri kuhusu maisha. Kila nikija Bongo lazima ninunue cd zake. Keep it Bro!
ReplyDeleteHongera sana M.I.M (Muhidin Issa Michuzi) kwa ufanisi wa blogu yako. Ina wasomaji karibu kila kona ya dunia.
ReplyDeleteNimejifunza mengi sana kutokana na blogu yako (nimeanzia Sept. 2005 sasa niko May 2006, ninaji'update' yaliyopita ktk blog yako)
Huyu jamaa yupo very very talented, but lini ana tour the US, i am def waiting .,..ANXIOUSLY for his live perfomance, i hear he delivers as well.
ReplyDeleteChameleone come to NEW JERSEY/NEW YORK or WASHINGTON, DC. Watu tunahitaji watu kama nyinyi. Pia how come your CDs sizioni on Stern's Music site.....
Huyu jamaa yupo very very talented, but lini ana tour the US, i am def waiting .,..ANXIOUSLY for his live perfomance, i hear he delivers as well.
ReplyDeleteChameleone come to NEW JERSEY/NEW YORK or WASHINGTON, DC. Watu tunahitaji watu kama nyinyi. Pia how come your CDs sizioni on Stern's Music site.....