ionekanavyo dar toka baharini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Wewe kweli fotografa, naona umefanikiwa kuyatoa majengo yote 4 marefu kuliko yote Dar. Ila kama naomba mwanablogu anayejua anifahamishe jengo lipi ni refu kuliko lote.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli na uchumi mifukoni mwa watu ungefanana na majengo haya, tungekuwa mbali sana wabongo

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli na uchumi mifukoni mwa watu ungefanana na majengo haya, tungekuwa mbali sana wabongo

    ReplyDelete
  4. Hio picha hata mi nimeikubali michuzi,anonym wa hapo juu anauliza jengo gani refu kuliko yote, kama nitakuwa sijakosea MAFUTA HOUSE ndio jengo refu kuliko yote,nadhani lina floors 25,kwa hapo linaonekana kwa mbaali sana kule lipo kulia kidogo mwa hizo twin tower za BOT. Bongo kupo juu jamani ohooo,hata mimi naona kuna nikonvice kurudi kule saivi.Na naskia kuna project nyingine ya PSPF inakuja ya kama 25 floors.
    Big up michuzi tupe vitu huko bongo mkuu,aminia, nimeipenda na hio pamba yako na kingo "YOU'L NEVER WALK ALONE"THE KOPES, Tajiri mpya ameahidi kulinda hadhi ya the kopes.

    ReplyDelete
  5. Uchumi ktk enzi hizi za utandawazi haumjali mwananchi wa kawaida! Kwa hiyo tujifunge mkanda maana tutabaki fukara na kushuhudia 'wawekezaji' wakiondoka na rasilimali zetu ghafi!!! Siku hizi wameanza hata kuja kuchukua watoto yatima na kuwafanya ni wao (adoption).
    Wazungu watatuchezea sana, inabidi tujifunze kukataa mambo mengine yasiyo na manufaa kwetu. Sio kuwapa uhuru bila mpaka.

    ReplyDelete
  6. Na Ikulu inazidi kupanuka!

    ReplyDelete
  7. Jengo refu ni PPF Tower ingawa lina ghorofa 17, jengo hili lina kuwa refu kwa sababu floor yake moja ni ndefu sana wakati mafuta vifloor vyake ni vifupi fupi

    ReplyDelete
  8. miaka mi2 mi3 utakuwa huwezi kutautisha bongo na hong kong

    ReplyDelete
  9. miaka mi2 mi3 utakuwa huwezi kutofautisha bongo na hong kong

    ReplyDelete
  10. Hebu Wabongo acheni uzushi hapa kuwa na hivyo vigorofa vitano tu mnataka kufananisha skyline ya Bongo kuwa kama ya Hong Kong baada ya miaka mitatu?? Itachukua miaka mingi sana kabla ya skyline ya Bongo kuifikia ya Nairobi tu hapo ije kuwa ya Hong Kong.

    ReplyDelete
  11. Watu wa huko kunakoitwa mamtoni mpo? Basi hapa ndiyo Bongo. Huyo anayesifia umasikini shauri yake. Sisi bwana huku sisi tupo na Bongo yetu. Maraha na shida ni za kwetu. Jipeni moyo tu kukaa huko nje.

    Ni lazima muelewe kuwa hata ukizaa mtoto, atakua tu. Na huku mambo yanabadilika siku hadi siku. Najua kuwa kuna wengine wanaombea hali ya bongo izidi kuwa mbaya waweze kupata justification ya kukimbia Bongo. Kazi kwenu.

    Mungu awatangulie katika kufanya maamuzi ya busara katika maisha yenu kuanzia sasa. Wengine huku baba zao na mama zao wanakufa, wanashindwa hata kuja kuwazika!. Eti nini? Juu ya nini? Eti sirudi Bongo. Mtajiju!!!!

    Mungu ibariki Afrika,
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  12. Angalau, mambo juu kwa juu sasa, jiji linavyozidi kukua, maghorofa nayo yanakwenda juu, Muhimu wajengee na parking spaces huko huko maghorofani, lasivyo panakuwa hapatoshi!!!! ...nxt Mh. Michuzi tuletee mabadiliko yatokanayo na maghorofa ya kariakoo, zama hizi na zama zileee "kwa masaladi!".

    ReplyDelete
  13. Nyie wote mnazungumzia magorofa mawili matatu ambayo yako dar tu na ktk eneo dogo la Dar nzima sasa mpaka tuwe kama hong kong si wote nyie mtakuwa mmekufa pamoja na watoto zenu pia?

    ReplyDelete
  14. solution ya matatizo ya bongo si kuwa na maghorofa mazuri au kufanya starehe. Kama starehe yeyote aliye popote atafanya. Inatakiwa masuala basic ya maisha yapatiwe ufumbuzi kama maji safi kwa kila mtu, kazi zipatikane kwa vijana, wizi na ujambazi upungue.. Maana watu wanakaa bila amani kabisa na mali zao mfano mzuri ni maeneo ya Mbezi ya morogoro road kuna wezi sana tena wanaua na kujeruhi sanaaaaaaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...