Home
Unlabelled
kingo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
23 kutoa ushahidi kesi ya Ditopile
ReplyDeleteAbadilishiwa shitaka, sasa ni kuua bila kukusudia
DPP asema kesi haziendeshwi kama enzi za Pilato
Na Ester Bulaya (http://www.uhuru.info/kitaifa.htm) 13 Feb 2007
MASHAHIDI 23 wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuru (58)
Miongoni mwa mashahidi hao ni kondakta wa daladala alilokuwa akiendesha marehemu Hassan Mbonde, abiria waliokuwa wamepanda gari hilo siku ya tukio na waliokuwepo eneo la tukio.
Kulingana na taarifa kwenye faili jipya la kesi lenye namba 13/2007, lililofunguliwa Mahakama Kuu, Januari 31, mwaka huu, mashahidi hao 23 ndiyo waliotoa maelezo wakati wa upelelezi wa kesi hiyo.
Chini ya mashitaka hayo mapya, Ditopile anashitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, ambapo anadaiwa Novemba 4, mwaka jana, saa moja usiku, katika njia panda ya Kawe na Bagamaoyo, Wilaya ya Kinondoni, alimuua bila kukusudia Hassan Mbonde.Mashitaka hayo mapya yanafuatia uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kubadilisha shitaka la awali la kuua, kutokana na ushahidi uliopo.Kwa mujibu wa DPP, Lawrence Kaduma, msingi wa mashitaka hayo mapya unatokana na ushahidi uliokusanywa kwa watu walioshuhudia tukio hilo.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaduma alisema ushahidi unaotolewa wakati wa upelelezi ndiyo unaomfanya abadili shitaka.
Kaduma alisema alifikia uamuzi wa kubadili shitaka kwa kuwa mashahidi wote walitoa ushahidi unaofanana, kwa maelezo kulikuwa na malumbano kati ya Ditopile na dereva na pia Ditopile alitukanwa.
Alisema anashangazwa na baadhi ya watu kuhoji uamuzi wa kubadili shitaka na kwamba hafanyi kazi kwa shinikizo au kusikiliza maneno ya watu, bali anachofuata ni sheria.
Kaduma alisema upelelezi unaonyesha Ditopile alitukanwa na katika hali ya kawaida ya kibinaadamu, hakuna mtu ambaye anapenda kutukanwa hivyo alipandwa na hasira na kupelekea kufanya kosa hilo.
"Unajua watu hawajui sheria, kama angeamka na kutembea na bastola kuanzia asubuhi na kusema lazima auwe hapo sawa. Hiyo moja kwa moja ni shitaka la mauaji, lakini yule siyo 'chizi' atoe bastola na 'kushuti', kulikuwa na majibizano, alitukanwa akapandisha hasira, na kwa misingi ya kisheria hakukusudia kwa sababu hakupanga kufanya hivyo, "alisema Kaduma.
Alisema mashahidi waliotoa maelezo yao ni kondakta wa dalalada alilokuwa akiendesha marehemu, abiria waliokuwemo kwenye daladala hilo na watu wengine waliokuwepo eneo la tukio na kushuhudia vizuri tukio hilo.
Aliendelea kusema kuwa hawafanyi kazi kwa kufuata hisia za watu, kwani kesi zinaendeshwa kwa misingi ya kisheria.
"Hatuwezi kuendesha kesi kama pilato, eti watu wakisema kaua basi iwe hivyo, lazima tufuate sheria na ushahidi na vielelezo husika, Yesu aliuawa bila kosa kwa uoga wa Pilato kwa kuwaridhisha wale watu, sasa sisi hatufanyi hivyo," alisema DPP.
Naye Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Prophir Lyimo, alithibitisha kupokea hati mpya ya mashitaka kutoka kwa DPP na kwamba tayari shauri hilo limeshafunguliwa ingawa bado halijapangiwa jaji na kwamba kinachofuatia ni kusomewa maelezo ya awali katika Mahakama ya Kisutu kabla ya kuhamia rasmi Mahakama Kuu, kuanza kusikilizwa.
"Nimeshapokea jalada la kuua bila kukusudia linalomkabili Ditopile, nadhani tayari makarani watakuwa wamefungua na kuwajulisha Mahakama ya Kisutu, ila bado halijapangiwa jaji, bado kusomewa maelezo ya awali huko Kisutu," alifafanua.
Hata hivyo, upande wa Mahakama ya Kisutu ambapo kesi hiyo ilikuwa inakwenda kwa kutajwa, upande wa mashitaka uliokuwa ukiondozwa na Gurvanus Muhume ulidai hauna taarifa ya kubadilishwa kwa hati ya mashitaka na kumuomba Hakimu Mkazi Mkuu Michael Lugulu kuwapa muda wa wiki moja ili wafuatilie.Hata hivyo, Wakili Ringo Tenga anayemtetea Ditopile, alipinga vikali hoja ya upande wa mashitaka na kudai taarifa hizo ni za kweli, hivyo wiki moja ni muda mrefu na kwamba upande wa mashitaka upewe siku mbili kwa ajili ya kupeleka taarifa sahihi juu ya taarifa hizo.
Hakimu Lugulu alikubaliana na upande wa utetezi na kuwapa upande wa mashitaka siku mbili, hadi keshokutwa, ili kuithibitishia Mahakama yake juu ya shitaka jipya.Katika Mahakama ya Kisutu jana kulikuwa na hali ya utulivu na ulinzi mkali kuliko ilivyokuwa ikitokea mwanzo, ambapo ndugu wa Ditopile walikuwa wamedhibitiwa na polisi huku mshitakiwa huyo akichanganywa na wengine tofauti na zamani, ambapo alikuwa akiletwa peke yake.
Ditopile aliwafanya watu waliokuwapo mahakamani hapo kuangua kicheko baada ya kuvaa kofia kubwa nyeusi iliyokuwa imemziba uso hadi pua yake, kwa kukwepa kupigwa picha. Kofia hiyo ilimfanya atembee kwa taabu kwa kuwa hakuwa akiona vizuri.
Ditopile alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Novemba 6, na kusomewa shitaka la mauaji ya Mbonde kabla ya DPP kubadili shitaka na kuwa la kuua bila ya kukusudia.Kwa sasa mshitakiwa huyo anaweza kuachiwa kwa dhamana kwa kuwa shitaka husika lina dhamana na Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Mbona hujatundika maelezo yangu kuhusu kesi ya Dito na vazi lako la carlsberg?
ReplyDelete