hii ni mwaka 2005 mwezi septemba kule helsinki, ufini, wakati mie na ndesanjo macha (pili shoto- bonyeza hapa upate mwandani wake mfalme huyu wa blogu za kimatumbi) na wabongo wengine akiwemo maria shaba (mwenye maiki) na mama mwingira (mbele yangu) tulipopanda jukwaani kutumbuiza kwa nyimbo kadhaa ukiwemo ule wa 'geti apu, stendi apu' wa bob marley kwenye hafla ya hisani. mchana wa siku hii ndo nilianza kublogu baada ya ushawishi mzito wa ndesanjo ambaye bila yeye nisingekuwa hapa leo.... ndesanjo bwana awe nawe huko uliko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana Michuzi.
    Nimepitia hiyo link uliyoweka kwenye maelezo, kwakweli uko mbali(the most popular swahili blog in the world!!). Pia ni jambo la busara sana kuwashukuru walikusaidia kufika hapo kama ulivyofanya kwa Ndesanjo.
    Nakuombea mafanikio zaidi, maana tuliombali na nyumbani kwakweli tunafaidika sana na blog yako.
    Kila jema!

    ReplyDelete
  2. Asante Michuzi. Siku hii sitaisahau. Helsinki sitaisahau pia maana ndio ilizaa blogu hii tunayoitembelea hata kabla ya kunywa chai!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...