jk akiagana na makamu wake dk. ali mohamed shein pamoja na viongozi mbali mbali waliofika katika wanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere aliopokuwa njiani kuhudhuria kikao cha maadili kwa wakuu wa nchi za afrika kinachotarajiwa kufanyika kesho cape town, sauzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. JK,JK,JK wapi tena uchoki na safari? mtu gani wewe? Wasaidizi wako hawawezi kuwakilisha nchi? kwanini huyo Dk. Shein hasiende?

    ReplyDelete
  2. Hiki chuma nacho kwa safari, hakijambo

    ReplyDelete
  3. Hivi huu mtindo wa kusindikizana kama wanaenda kutoa posa wataacha lini ? Ni upotevu wa muda tuu.

    ReplyDelete
  4. JK vipi na wewe mbona hivyoo jamani? duh huyu jamaa ana mapepo ya kusafiri. ebu wapinzani na viongozi wa dini itisha mkutano wa maombezi kwenye viwanja vya jangwani la sivyo tutampoteza muda si mrefu ahaaaa

    ReplyDelete
  5. nadhani huyu kakete ( whatever the spelling is ) anafaa kuwa rubani than a president 4 sho' maana hili jamaa halichoki damn!! michuzi nawe safari hii vp wanakuacha au ?

    ReplyDelete
  6. mhhhhhh jk tulia baba,wewe kila siku safari unataka kutaliii dunia nzima au?mhhh na wewe michuzi basi hukosi hapo,embu punguzeni misafari,mtaja pata ajali ya ndege bureeeeee.bado tunawahitaji alaghggg.

    ReplyDelete
  7. Hata haipendezi sasa. Kwani hamna wawakilishi wa nje ya nchi mpaka aende raisi kila siku? Kila mkutano ni lazima raisi aende? Huo msafara wa kwenda nae si unacost sana nchi?

    ReplyDelete
  8. Ulimbukeni wao wa kusafiri tu hawana lolote hawa. Halafu wala hawaeleweki kwani watu wanaowaiga akina Bush na Blair hawasafiri jinsi hawa jamaa wanavyo safiri.

    Na hii yote ni sehemu ndogo ya shughuli za uongozi wao, Mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa. Vipi kususu uchumi, elimu, afya, kilimo, ajira na masuala mengine ya jamii?

    Viini macho tu hivi na hata wakienda huko nje kimombo chenyewe hakipandi wanasangaa sangaa kama mabubu. Kaeni nyumbani mfanye kazi.

    ReplyDelete
  9. Hivi waziri wa mambo ya nchi za nje kazi yake nini naomba nieleweshwe.

    ReplyDelete
  10. Anahokwenda kuhudhuria ni kikao cha Madili ya Viongozi wa Nchi. Shein ni Makamu wa Kiongozi wa Nchi. Subirini tu hivi karibuni mtamsikia amesafiri tena.

    ReplyDelete
  11. Michhuzi, JK kakutosa TRIP hii???..
    au tayari upo huko mji wa kapelo?

    Lakini hii hali ya rais akisafiri inabidi viongozi wote wa nchi na mkoa kumsikindikiza eapoti naipinga sana. Hawana Kazi????

    hii protokali inastahili kubadilishwa na hawa viongozi wakaachwa wafanye kazi nyingine. inakuwa ni kikwazo kwa shughuli za maendeleo. Foleni, kazi za hawa viongozi hazifanyiki coz hawapo maofisini na usumbufu kibao kwa wananchi na matumizi mabaya ya muda wa kazi.

    Halafu kuna Anony kanitangulia kauliza swali zuri sana. JK hana wasaidizi kiasi cha kila safari anatinga front mwenyewe?
    au ndio mambo ya kuwa mtu wa watu inabidi kila kona aonekane yeye???

    hapa JK inabidi abadili strategy. otherwise wabongo tumeshaanza kuzichoka "Trip" zake za nje ya nchi

    ReplyDelete
  12. wale jamaa kuli kwa tibaigana wanavitambi si mchezo

    ReplyDelete
  13. Hivi lazima viongozi wote waende airport JK anaposafiri? Huu ni ujinga mkubwa.

    ReplyDelete
  14. Jamani msimseme sana our president haahaaa... hamjui yeye hajakaa nje kabisa katika maisha yake kama sisi???amesoma bongo, akafanya kazi bongo katika maisha yake yote, ivo ndio wakati wake. Da ila huyu jamaa kwa kweli ni kiziwi, hapa hata waandishi wa habari waseme, hawataweza, na anavojua kujitetea????.

    ReplyDelete
  15. Piga ua choma moto galagaza nchi hii haitoki katka umaskini sio leo wal kesho.

    Mnashangaa nini hiyo ndio kasi ari na nguvu mpya? Mtajiju.... nyie

    ReplyDelete
  16. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  17. KIKWETE UNABOA SANA KULIKO HATA NILIVYOKUWA NAKUFIKIRIA,NDO MAANA CKUPIGA HATA KURA,HUCHOKI?HATA SPEECH YAKO YA MIAKA 45 YA UHURU ILIKUWA CHECHE,ACHA HIYO YA CCM 30 YRS,KAA PUMZIKA UDELEGATE WASAIDIZI,NDO MAANA HATA MIRAJI ALIKUSHINDA KUMLEA ULIKUWA UNASAFIRI SANA....

    ReplyDelete
  18. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  19. hivi huyu rahisi kwa nini asitume watu wengine katika shughuli kama hizi,hivi anajua raisi wa nchi kama uganda au kenya mara ya mwisho lini wamesafiri nje ya nchi zao,hivi anajua nini kinaendelea mikoani anapaswa atembelee vijijini kuangalia maendeleo ya nchi,sijui mara ya mwisho lini ametembelea mikoani kukagua shughuli za maendeleo,lakini na sisi watanzania tumelala ndiyo maana watu kama hawa wanatake advantage,sijui ni ushamba wa raisi huyu ama ni nini?na amealikwa vatican nadhani kutakuwa na tripu kibao kabla ya hapo.

    ReplyDelete
  20. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  21. huyu jamaa ni malaya tu, and a big back stabber too. Mkapa was the man. JK ana hazini kubwa sana, he can take the good from all the past presidents and leave all the bad, yet he is bullsh*t.

    ReplyDelete
  22. Yule jamaa aliyoko kushoto kwa Jakaya aogopi anaweza kuzalia hapo kiwanjani

    ReplyDelete
  23. THIS IS WAY TOO MUCH JK. WACHA KUTUDANGANYA SASA UNATAFUTA MAIVENSTOR UONGO MTUPU, LAZIMA IWE WEWE, SHUGHULI NYINGINE WAACHIE WENZAKO UNAJISHUSHIA HESHIMA YAKO SASA, YAANI HUWEZI KUKAA NYUMBANI HATA KAJIMWEZI TAYARI MBIO,SIO LAZIMA KILA UKIKARIBISHWA MAHALI BASI UENDE, UNAWEZA KUSEMA NO THANKS, AU UKAMCHAGUA MWINGINE, BADOA UNAMIAKA MIAKA KAMA MINNE HIVI. NA HAO VIONGOZI WENGINE WACHENI MAMBO YA KIKOLONI KWANI LAZIMA MUMSINDIKIZE NA KUMPOKEA, YAANI MMEJIPANGA KAMA WATOTO WADOGO, MAKAMU WA RAIS , MTUMENI DEREVA AKAMCHUKUWE RAIS KAENI OFFISINI MCHAPE KAZI. YAANI INATIA HASIRA KUONA MMEJIPANGA ETI KUMUAGA ALMOST AKIRUDI HAO MNAJIPANGA TENA KUMKARIBISHA. HOW MUCH DOES JK SPEND IN EVERY TRIP? I AM SURE THE MONEY COULD BE USE TO REMODEL SOME OF THE SCHOOLS AU KUANZISHA SOME PROGRAMS KUSAIDIA VIJANA WETU. STOP SPENDING OUR MONEY FOR NOTHING.

    ReplyDelete
  24. Mimi ndio maana nimeamua nijilipue, niachane na mambo ya kibongo. Huyu jamaa kila siku safari,allowance kibao hapo wanakula wasidizi na yeye mwenyewe. Wakati mkazi wa geza ulole ambaye hawa viongozi wanasema wanataka kumsaidia hana maendeleo yoyote. Kila siku nchi ina punguziwa madeni,misaada kibao lakini zinahiishia mifukoni mwao. Ni kheri niwe mkimbizi kwenye nchi yenye haki kuliko kuona vitu vya ajabu kila siku vinavyoendelea Tanzania

    ReplyDelete
  25. Kweli ukoloni bado upo. Hii kusindikiza na kumpokea kila siku duh... Mwenyewe kila siku anasafiri.
    Sijui kazi hamna za kufanya. Hao maofisa kuchoma mafuta kwenda airport na kurudi... Na masaa ya kumsubiri kumuaga... Time is money and the energy is too much to waste. Kweli hela ya walala hoi inaliwa na wenye walioamka hoi

    ReplyDelete
  26. Kuna wengine wamepanga mstari wa pili hapo nyuma. Yaani i can imagine kama wanapangwa au vipi. It's so sick. Wananchi wako wapi, hivyo vyama vya upinzani vimezorota mna au navyo ndio hivyo hivyo tu, wanataka wachukue wadhifa na wao waanze safari JK ACHA BWANA KUIBIA WANANCHI SIO LAZIMA ULE RUSHWA HATA KUTOKUWA NA MIPANGO MIZURI AMBAYO INADIDIMIZA NCHI NAKO NI KUIBA.

    ReplyDelete
  27. namuunga mkono jamaa feb,6;11:27 asilimia zote ni bora kujilipua,sababu mi nimekaa nje na nina ona haki za watu zinavyotekelezwa siyo blabla tu,kama kiongozi unapaswa uwe mfano mzuri wa kuchochea watu wako lazima uwepo physicall siyo kupiga simu kutoka ofisini wakati viongozi wa mikoa ni lazima uwa push ili wasukume maendeleo.mungu ibariki uingereza na viongozi wake.

    ReplyDelete
  28. MI NAFURAHI KUONA KIKWETE ANAVYOSAFIRI KWANI HII INAWAJENGEA WAZUNGU IMANI KUWA WABONGO WAKIENDA INJE WANARUDI.KWAHIYO HIVI KARIBUNI WABONGO TUTAKUWA TUNAPEWA VISA KIRAHISI.KWANI JK NA MICHUZI HAWAZAMII.WAZUNGU WANAFAGILIA KICHIZI.

    ReplyDelete
  29. Jamani mimi napenda kuwapingeni wote hapo juu.

    Kwani JK kusafiri ndio chanzo cha umaskini?

    Na akikaa hapo ikulu anachekeana na wananchi ndio ataleta maendeleo?

    Si ni afadhali aende akakutane na watu mbali mbali angalau watu wakisikia President of Tanzania yupo nchini jina la Tanzania litakuwa linajulikana?

    Eeeh??

    Pili msisahau kwamba rais hawezi kusafiri bila kualikwa. Sasa mataifa yanamwalika kwa dili ambazo anaona zinalipa kwa nini akatae? Ndio manaibu wanaweza wakaenda lakini bila shaka akienda rais wanachukulia much more seriously.

    Kwa hiyo hayo ndio maoni yangu, sidhani kama kuna tatizo kwa Kikwete kusafiri kama anaona mikutano hiyo ina manufaa kwa taifa

    Mawaziri wameshapewa majukumu yao, ndio maana sio lazima awasimamie kama mwalimu wa shule ya msingi. Vile vile Lowassa na Shein wapo kusimamia utekelezaji.

    Nchi yetu inategemea sana vitu viwili:
    (1) Foreign Aid
    (2) Foreign Investment

    Hayo yote hayawezi kupatikana kama Rais anakaa tu akikutana na cabinet yake.

    Ni lazima vifuatwe huko viliko.

    ReplyDelete
  30. Pia ningependa kuongezea kwamba safari za Kikwete zimekuwa za mafanikio.

    Alivyoenda USA May mwaka jana aliteta na Bush akaenda CNBC akatoa interview, akagonga kenge NY Stock Exchange, pamoja na sehemu nyingie kuitangaza bongo. Wamarekani ambao walikuwa hawajawahi kuisikia Tanzania wakaipata pata katika ziara hiyo.

    Alivyoenda China November mwaka jana pamoja na marais wote wa Afrika China ikatoa commitment ya kuongeza sana investment barani Afrika na vile vile kuzidisha maradufu misaada.

    Alivyoenda juzi hapo Davos, akateta na Bill Gates na wale watu wa Google na Google wameahidi kufanya mpango wa kuongeza ajira bongo.

    Juzi ameenda UK akaongea na Blair ambaye ni mwenyekiti wa Tume ya Afrika na bila shaka wameongea mambo fulani ya manufaa.

    Sasa hivi anaenda SA kuongea kwenye mkutano wa mining. Anazungumzia Tanzania inavyotaka kuongeza kodi kwa mining companies ili kuwanufaisha wananchi. Nafikiri hili suala ni muhimu sana ukizingatia umuhimu wa mining sector katika nchi yetu.

    Kwa hiyo kwa kifupi mi naona safari za Kikwete zina manufaa kwa taifa, na mnaosema kwamba atulie tu nchini mnakosea sana tena sana tu.

    ReplyDelete
  31. Kikwete kukaa nyumbani itakuwa ni kuendekeza umaskini!

    Angalau asafiri safiri aombe ombe misaada!

    Embu chekini video hapo chini Kikwete akiomba misaada kiaina:

    http://video.google.com/googleplayer.swf?docid=-4260346984633320902&hl=en

    ReplyDelete
  32. Matokeo ni kuwa sasa hivi hakuna mawasiliano ya barabara kati ya SINGIDA na DODOMA amefanya kitu gani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...