
hapa bongo tunaziita 'mikangafu' kamera kama hizi ambazo zinatumia filamu. zipo nyingi na studio za kusafisha zipo kila kona. vijana wengi wamejiajiri kwa kazi hii na mambo yao si mabaya sana. wengi tulio katika fani hii tumepita huku na mimi ninazo kamera kadhaa za filamu ambazo bado nazipenda ingawa za dijito zimeshika hatamu kwa sababu zinazoeleweka ...
Hao wanajulikana kama "paparazis"
ReplyDeleteMichuzi--mkanangafu ni ulanzi uliolala, sasa mambo ya kufananisha kinywaji muafaka kama hicho na mambo yanayo pitwa na wakati sio fresh.
ReplyDeletemi nafahamu neno "mkangafu" linatumika,ingawa sijui kama ni rasmi,kumaanisha vitu ambavyo vimepitwa na wakati.Kwa mfano,tangu kuingia kwa Landrover 110 kulifanya Landrover 109 au 89(za miaka ya 60 hizi) ziitwe "mikangafu".Hata leo hii Landrover 110 ni "mkangafu" mbele ya Landrover Discovery.Sidhani kama ni neno baya au labda huyu mwenzetu hapa juu tafsiri yake ndio mbaya.Michudhi kaandika "mkangafu" na sio "mkanangafu";nadhani hivi ni vitu viwili tofauti.Hizo kamera zinastahili kuitwa "mkangafu" kwasababu siku hizi kuna aina mpya na bora zaidi ya hizi,yaani "digital".Michudhi asibanwe ktk lugha anayotumia kuwasilisha ujumbe hapa kama badhi wetu wanavyotaka iwe.Hii ni blog yake na wale hatumpi hata senti kuiendesha ila kazi yetu kulaumu tu,sio vizuri;sometimes we need to advance positive opinions hata kama sio desturi yetu! JJ.
ReplyDeletemzozaji!
ReplyDeleteasante kwa ujumbe ila nomba usome kwa makini nilichosema kabla ya kuhitimisha ama kunitia maneno mdomoni. hakuna mahali niliposema kamera za film mpaka saa zinatoa picha bora kuliko dijito. rejea tena niloandika.
vile vile naomba nipingane nawe kwamba kamera za film zinatoa picha bora kuliko gijito. ingekuwa hivyo maendeleo ya teknolojia yangebakia kwenye film kwani kwa taarifa yako ni makampuni machache yanayoendelea kutengeneza film; wote wamehamia kwenye dijito kama vile kodak, fuji, agfa, hp na kadhalika. wote hao aidha wanatengeneza kamera na software ama accessories kama vile printer au memory cards/sticks.
kubwa zaidi na kwa taarifa yako wewe na wengine ni kwamba nilikuwepo kwenye maonesho ya kila mwaka ya kamera na picha ya 'photokina' kule ujerumani mwaka uliopita na wataalamu wote walisema film inaelekea kuwa extinct kama ilivyokuwa audio casettes dhidi ya cd na dvd. sasa kama film ni bora kuliko dijito kwa nini wasiiendeleze?
kuhusu ubora naomba nisisitize kwamba dijito inazidi kuboreshwa na sasa inapita hata film, kutegemea na kamera yako ikoje. elewa ubora wa picha ya dijito hautokani na kamera pekee, na hata ubora wa filamu hautokani na kamera pekee pia. kwa upande wa dijito ni ubora wa lens zebye optical zoom bora pamoja na zile picture elements (pixels) ambazo kama ni kubwa unapata picha bora pamoja na mpigaji kwani kamera haijipigi.
upande wa filamu pia usitegemee kupata picha bora ukiwa na 'mkangafu' kama vile kodak instamatic inayotumia film ya 110, kufananisha na canon slr yenye kutumia 35mm film, ambayo pia haifui dau kwa kamera zenye kutumia filamu pana kama zile za 120mm ama large format zinazotumika kupigia majengo ama landscape.
usisahau pia kwamba kwenye dijito spidi ya filamu unairekebisha mwenyewe kutokana na mazingira katika upigaji, ambapo filamu ya iso 100 ama 200 ama 400 ukiiweka, basi wewe ni hapo hapo to. naweza kujaza blogu yote na bado nisiwe nimeleza nusu ya faida na hasara ya vifaa hivi - dijito na filamu.
ila yatosha nimkisema kwamba hata mie nainjoi sana nikitumia filamu ingawa usafishaji wake hufanya picha zenye ubora wa chini tofauti na dijito. lakini piga ua, ukweli mchungu ni kwamba kamera za filamu sasa ni kwaheri kama ilivyokuwa kanda za muziki ambazo sasa zinaishia. cha kufanya ni kusubiri tu, baada ya dijito nini kitafuata. lakini ukichagua kubakia kwenye zama za ujima ni uamuzi wako, usije sema hatukukustua juu ya 'mikangafu'
Kweli kaka, watu wamechokoza fani,maana ma pixel ma atomic.Tunakukubali,big up bro.
ReplyDelete