
ni wapi katika bara letu hili utaweza kuona rais wa sasa na aliyepita wakiwa pamoja hivi?
The Tanzania High Commissioner to the United Kingdom H.E. Mwanaidi Sinare Maajar is happy to invite all Tanzanians living in the United Kingdom to a meeting with H.E. Jakaya Mrisho Kikwete on the 17th February 2007 in London.
Meeting will start at 02:00(14:00hrs) at the ROYAL NATIONAL HOTEL GALLEON SUITE
RUSSEL SQUARE
LONDON WC1H 0DG
LONDON WC1H 0DG
FOR MORE INFORMATION
CONTACT TANZANIA HIGH COMMISSION ON 0207-569-1470
Katika jambo hili la kuwaenzi ma-raisi wastaafu Watanzania inabidi tujivunie. Utamaduni huu wa kuwahakikishia viongozi wastaafu maisha mazuri yatawezesha pole pole viongozi wetu Afrika kuwajibika, kutopata tamaa za rushwa na kuwaonea wananchi. Hivyo Tanzania tusione aibu kujisifia angalau katika hili jambo jema la kuwatunza viongozi wastaafu.
ReplyDeleteInaweza kutokea Afrika Kusini pia kwani tumeona picha ya Mandela na Mbeki wakiwa wanatabasamu kwa pamoja. Tofauti kati ya Afrika Kusini na Tanzania ni kwamba tabasamu la viongozi wao ni kielelezo cha kumbukumbu za maumivu waliyoyapata wakati wanapigania maisha bora ya raia wao. Tabasamu la Kikwete na Mkapa ni kielelezo cha kuwatumbukiza watanzania katika lindu la umasikini huku kiongozi mpya analinda uvundo wa yule aliyetangulia. Hakuna maana viongozi wanatabasamu wakati wananchi wanasononeka mioyoni. I think one of them should be in jail.
ReplyDeleteInaweza kutokea Afrika Kusini pia kwani tumeona picha ya Mandela na Mbeki wakiwa wanatabasamu kwa pamoja. Tofauti kati ya Afrika Kusini na Tanzania ni kwamba tabasamu la viongozi wao ni kielelezo cha kumbukumbu za maumivu waliyoyapata wakati wanapigania maisha bora ya raia wao. Tabasamu la Kikwete na Mkapa ni kielelezo cha kuwatumbukiza watanzania katika lindu la umasikini huku kiongozi mpya analinda uvundo wa yule aliyetangulia. Hakuna maana viongozi wanatabasamu wakati wananchi wanasononeka mioyoni. I think one of them should be in jail.
ReplyDeleteNi kweli Rushwa ipo,
ReplyDeleteNi kweli wanachemsha sometimes,
ni kweli nchi yetu ya Tanzania ni maskini, wengi wanaishi chini ya internationa poverty line,
ni kweli Ukimwi unaua sana watu.
LAKINI, ACHA TU NISEME KUWA.
Tunamshukuru sana Mungu kwa kuwa nyerere ametujengea hali ya kuachia madaraka kwa adabu, at least.
Ni wapi kweli Africa utakuwa viongozi kama hawa wanakaa pamoja na kucheka, haijalishi inatoka moyoni ama vipi, lakini atleast tunapata faraja kuwa amani ipo, tukiwaona namna hiyo, viongozi wetu.
Thanks Nyerere kwa kutuachia zawadi kama hii.
japo sisi nchi yetu ni maskini, acha tu tupendane, kuliko kukimbizana.
Thanks God for the blessings.
Mungu mlaze pema peponi Nyerere,
Mungu wabariki viongozi wetu,
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afria.
I'M PROUD OF THEM, AND MY COUNTRY.
WATANZANIA WENZANGU.
ReplyDeleteUondoeni mambo ya kasumba ohoo Mwalimu alitufundisha...acheni hizo watanzania wako hivyo naturaly ingia kwenye historia upate vitu-hilo moja.
Pili- Jamani huyu JK mbona trip za uk zinafuatana tu. jana watanzania ambao wazazi wao walikupa kula zao leo hii wako kwenye theruji Ukraine.. temperature -18 wewe unakutana tu na watanzania waishio UK. ...U.S.A hawa je ni waganda nini mbona huko upitie kuona watu hawa wanaisheji. Mheshiwa asilimia 58 ya madaktari wa Tanzania ni graduate wa soviet union na Eastern europe hao wa uk kwanza wengi huwa hawarudi....wapiga kura wako huku siyo huko unakokwenda kila siku...chunga mambo miaka 5 siyo muda mrefu.......kasi mpya na mambo mapya.(.Baba leo)///
jk kazidi kila leo yuko uk anataka kukutana na wabongo hatutaki. aende mufindi
ReplyDeleteTumeona Kibaki na Moi, Mandela na Botha
ReplyDeleteKumbe Mkapa handsome kuliko Kikwete
ReplyDeletewote wana ccm sasa kuna nini cha ajabu?wote wanajuana tangu kipindi cha kifimbo,michuzi whats ur point?i dont get it,wanachekelea nini sasa wakati nchi inazidi kudidimia,michuzi najua unajua hakuna mawasiliano kati ya dodoma na singida na huo ni mji mkuu wa nchi kuna kitu cha kuchekelea hapo?na sijui kuna jitihada gani zinafanyika.tanzania siyo dar watu wanahitaji vitu muhimu vijijini na jk huyoo!! london tena na alikuwa huko majuzi,bongo lazima atafutwe mchawi.
ReplyDeleteJamani mwenzenu J.K. kusafiri ni HOBBY yake, mwacheni!!!
ReplyDeleteKUACHA MADARAKA KWA ADABU IBI WEWE ANYN ULIYENITANGULIA UNASEMA. INA MAANA UMASKINI TULIO ACHIWA NA RUSHWA NA ADHA ZOTE ZA KUYAUZA MASHIRIKA YA UMA KWA NJIA ZA PANYA, KUINGIA MIKATABA ILIYO OZA NDIO KUACHA MADARAKA KWA ADABU? BORA HATA MTU UNGANGANIE MADARAKA KAMA UNACHOKIFANYA KINAELEWEKA, NI BORA NA KULIKONI HUKU KUDANGANYIKA KUWA NA NCHI HURU LAKINI SIO UHURU WA KWELI.
ReplyDeleteKweli Afrika Kusini ni mfano wa kuigwa na siyo Tanzania. Botha alimweka Mandela Ndani lakini Mzee Mandela alipotoka ameshikana mkono na Botha. Picha kama hizi za Botha na Mandela wakipata msosi na kufurahi ni nyingi mno. Lyatonga akiwa Raisi anaweza kupiga picha kama hiyo na Mkapa? Mbona hatuoni picha ya Karume na Salmin au kule siyo Tanzania? Nikionacho kwenye hii picha ni furaha ya 10%. RADA Mkapa, na Richmond Kikwete. Kwani nini wasifurahie?
ReplyDeleteDah sasa huyu mshkaji Kikwete noma hii hizi safari za majuu kodi zetu wadanganyika zinazidi kuliwa tu na safari zako na per diem wanazolipana yeye na entourage yake.
ReplyDeleteOya President noma hiyo, watu wanazidi kuwa masikini wewe unaspend mapesa tu kutalii sio?
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletewako kwenye harusi ya kinje nini mwe rais wenu mzaramu kila siku safari london mwee,hawezi kwenda mufindi,nangurukulu nk wadanganyika mmeula wa chuya bora hata njomba che nkapa alikuwa na uchungu na nchi.
ReplyDeleteThis is too much!!Hivi safari moja ya Rais inagharimu kiasi gani, yeye na msafara wake wa akina MICHUZI?
ReplyDeleteWanafunzi wa kitanzania Russia wamesimamishwa shule kwa kukosa ada.Safari moja ya akian kikwete yaweza lipa hizo ada, na posho zao zoote.
Gimme a break, This is too much.
Cheki gozi linavyo dunda dunda uwanjani. Wakati ule, mkataba wa Rada ulimfanya Mkapa awe Mkali kama mbogo kwa walioupinga. Baada ya mambo kuanikwa juani, amekuwa bubu. Ma spin doctor Wanatughiribu kuwa RADA ni tunda la Mwinyi na yeye hakuwa na la kufanya ila kutekeleza. Mbona hatoki kusisitiza msimmo aliokuwa nao wakati ule? Wote tunajua msimamo wa Kikwete kwa wakati huo. Leo naye anasema ni matatizo ya urithi. Kwa nini wasiangue kicheko kwenye picha kufurahia ujinga wa watanzania. Ni mahala gani duniani mtu anaweza kusimamia jambo fulani, alafu kesho akawa na msimamo unaopingana na ule wa jana, na watu wakamwamini? nadhani ni Tanzania!
ReplyDeleteKuna nchi kadhaa katika bara letu unaweza kuwaona viongozi waliopita na waliopo madarakani wakikaa kama walivyokaa Rais Mkapa na na Rais Kikwete. Kwa mfano:
ReplyDeleteSenegal, Marehemu Senghor na Abdoul Diouf na baadaye Rais Diouf na Wade.
Botswana, Rais mstaafu Masire na aliyepo madarakani Mogae.
South Afrika, De Clerk na Mandela, Rais mstaafu Mandela na Thabo Mbeki.
Mozambique, Rais mstaafu Chisano na aliyepo madarakani Guebuza.
eKaribu wote niliowataja hapo juu ni marais wanaotoka katika chama kimoja. Kwa hali hiyo basi huwa wanendelea kuwa maswahiba kwa sababu uanachama wa vyama vyao. Lakini ukiangalia nchi zingine za Afrika ambazo uhusiano kati marais waliotoka na walipo madarakani huwa na mushikeli wanakuwa wametoka vyama tofauti. Kwa mfano
Zambia Rais Kaunda (UNIP) na Chiluba (MMD).
Kenya Rais Moi (KANU) na Kibaki (NARC).
Malawi Rais Muluzi (UDF) na Mutharika(DPP).
Suala la uswahiba wa viongozi linaweza kuwa hitilafu zake. Maswahiba wanakuwa ni watu wa kusameheana. Siyo lazima kila kiongozi aingiaye madarakani amuadhibu aliyemtangulia kwa mapungufu yake. Lakini kuna mapungufu mengine yanayostahili adhabu. Rais Mkapa alipoingia madarakani alikuta kuna mapungufu mengi sana ya serikali ya awamu ya pili/awamu ya ruksa akaunda tume (TUME YA WARIOBA)kuchunguza mapungufu hayo. Matokeo ya uchunguzi wa tume hiyo Baadhi yakawaburuzwa mahakamani na kuadhibiwa akiwemo aliyekuwa Waziri wa Ujenzi Muheshimiwa Nalaila Kiula na Katibu Mkuu Mlingwa ambaye sijui kama bado yupo gerezani akitumikia kifungo chake.
Nyuso hizo za furaha za Rais aliyemaliza muda wake Benjamini Mkapa na aliyepo madarakani Jakaya Kikwete zinaweza kuwa na heri na hitilafu zake. Hali kadhaika zinaweza kuwa siyo kiashirio cha amani na furaha.
Asante na weekend njema,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Namibia, Rais mstaafu Sam Nujoma na na aliyepo madarakani Hifikepunye Pohamba.
ReplyDeleteJamani eeh!kumbe si safari tu,nasikia JK akisafiri yeye na wapambe wake (na wa mkewe) wanafanya shopping ya kufuru,mamilioni ya pesa.Sijui analijua hilo,maana najua hashiki pesa mwenyewe.
ReplyDeleteHalafu na Balozi Maajar alivyoupata ubalozi,haya.........