
bongo, hususan dar, pamekuwa hapatoshi kutokana na kimeo cha popo bawa. wakubwa wanasema hakuna kitu kama hicho sitizeni wanasema kipo. haya, mzee mzima sheikh yahya hussein naye kaingia ulingoni, na leo kasema kwenye luninga ya channel teni kuwa popo bawa wapo na kutoa maelekezo ya namna ya kujikinga naye. tena kasema bayana kuwa popo bawa ni majini yaliyoumbwa na watu toka sehemu fulani ya bongo kwa minaajili ya kukumoana.
infwakti sheikh yahaya amaeonekana akihojiana na baadhi ya waathirika katika kipindi chake cha kila wiki cha 'nyota zenu', ila tu ni kinamama pekee waliojitokeza naye anadai kinababa wanaona noma kukubali kama wameathirika. na magazeti nayo, hasa ya mchana na ya udaku, ni mwendo mdundo tu...
Sasa wengine hatupo Bongo miaka mingi,hivi popo bawa ndio nini?
ReplyDeleteHizi imani za ushirikina sijui zitaisha lini, pamoja ma mapinduzi makubwa ya mawasiliano Tanzania, watu bado wanaimani potufu. Sheik Yahya yeye anatangazia biashara yake lakini kwa kufanya hivyo anachochea hizi imani za kijinga. Wabunge kipindi cha uchaguzi wanakwenda Mbaramo au Bagamoyo!!!
ReplyDeleteHuko kaskazini ya wilaya ya Lushoto (kwetu) wanaamini Kimweli(jumbe, zumbe,mwene au whatever) anafunga mvua na anaweza kuleta mvua. Wakati dunia inajadili global warming wao wanasema hii yote ni Kimweli! Kwa nini wasimjaribu alete mvua wakati wa kiangazi. Tuna safari ndefu
Haya hili tena jipya lisilo na mpango wowote. Kama kuna waumbaji zaidi ya mungu basi, sheikh Yahya Hussein mkali.
ReplyDeleteduu balaa kubwa hili limekushikiyeni tena huko home duu, popo bawa wako bwana tena kwa ma man basi wanapata ugonjwa wa mfedheheko wakipitiwa na popo bawa, someni quran na shikeni ibada kwa sana ndo kinga hiyo shauriyenu aah na wanaosema hawapo basi hao popo bawa huwa wanawatembelea usiku usiku, mungu atakusadiyeni lakin duu, balaa kubwa shikeni ibadaa jaamani eeeh ndo kinga yenu.
ReplyDeleteHivi bado Tanzania kuna watu wanaishi kwa kuuza magazeti?Au wana bishara nyingine, hii ya kuzuga tu?
ReplyDeleteJE KUNA MTU MWENYE AKILI TIMAMU ANAYEAMINI POPOBAWA WAPO? TATIZO NI KWAMBA KUNA AINA FULANI YA WATU KWENYE JAMII YA KITANZANIA AMBAO IMANI ZAO ZINASABABISHA WAWE NA MAWAZO YA KIPUUZI KAMA HAYA. NDIYO HAOHAO WANAOAMINI ETI KWA KUANGALIA NYOTA MTU ANAWEZA KUTABIRI YAJAYO, NYOTA TANGU LINI ZIKAHUSIANA NA MAISHA YA MTU? NDIYO MAANA WANAAMINI POPOBAWA WAPO.
ReplyDeleteKaka Michuzi nashukuru kuna ujumbe nilikupa unifikishie kwa Mwaipaya ukanifikishia shukrani sana, na siku ukija Newala sitotia shaka kuwa mwenyeji wako. Just let me know and I will make sure you have a great time.
ReplyDeleteEbu Michuzi na wewe tuambie, ikitokea ukaingiliwa na popobawa unaweza weka mambo hadharani? au nawe utakaa kimya? Michuzi mimi nakuaminia tupe msimamo wako
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletekukujibu anony wa hapo juu ni kwamba pindi likinitokea, kama kweli kipo kitu kama hicho (mie ni mmoja wa wasioamini kwamba kuna kitu kama hicho), nitajitangaza tena kupitia kwenye blogu yenu hii
ReplyDeleteAsante Michuzi kwa kumjibu Anony 8:19:00. Na yeye sasa atuambie msimamo wake, ikitokea akaingiliwa na popobawa aatasema hadharani au ataminya? Mimi binafsi siamini uwepo wa popobawa.
ReplyDeleteMimi nimepunguza sana kununua magezeti ya Tanzania sababu yamejaa vitu ambavyo haviongezi ufahamu .Yamejaa umbeya mwingi mno.
ReplyDeleteNina wasiwasi kwa kuwa sekta ya umbeya katika magazeti ya Tanzania inazidi kupewa nafasi kubwa.Hii itaua magazeti mengi ya nchi hii.
Wenye magazeti lazima waelewe kuwa kiwango cha wasomi Tanzania kinazidi kuongezeka na wengi hawapendi vitu vya kimbeya kuvisoma au kusimulia ni watu serious.Na magazeti yao yakidharauliwa ni vigumu mno kuja kurudisha imani sokoni kwenye magazeti yao.
Nawashauri wawe serious na waandikacho.Waangalie "future value" ya magazeti yao badala ya kuangalia only current market value ya magazeti hayo.
kwa mtizamo wangu future value ya magazeti mengi iko hoi hata kama sasa hivi wanapata faida kubwa kwa mauzo yao.
koloboi@yahoo.com
Naomba nimjibu Anonymous wa saa 2:24:00 ambaye ni limbukeni wa kutupwa! Eti unauliza 'Hivi Tanzania watu wanaishi kwa kuuza magazeti'? Hivi kuna nchi ambayo magazeti hayauzwi au ndio kukaa ughaibuni unafikiri watanzania hatujui hilo?
ReplyDeleteKuwa mstaarabu na ufikiri kabla hujaongea. Kama boksi/wazee wamekuchanganya huko ughaibuni pole sana. Huyo kijana anauza magazeti anapata riziki yake. Hata huko ughaibuni kuna vibanda pia vya magazeti....Thamini kwenu na thamini kazi za wenzio...Halafu unavyosema 'Eti Tanzania' kwani wewe kwenu wapi au kubeba maboksi ndio kunakufanya uwe mgeni? Mkataa kwao mtumwa AND THERE IS NO PLACE LIKE HOME!!!UZALENDO MUHIMU JAMANI....
Mkuranga, Mbagala na Temeke kitimoto bei juu, wenyewe wanaamini ni kinga ya Popo bawa. Wanachukua mifupa wanalala nayo, wengine wanajipaka mafuta yaani kazi kweli kweli.
ReplyDeleteNaomba nimjibu Anonymous wa saa 2:24:00 ambaye ni limbukeni wa kutupwa! Eti unauliza 'Hivi Tanzania watu wanaishi kwa kuuza magazeti'? Hivi kuna nchi ambayo magazeti hayauzwi au ndio kukaa ughaibuni unafikiri watanzania hatujui hilo?
ReplyDeleteKuwa mstaarabu na ufikiri kabla hujaongea. Kama boksi/wazee wamekuchanganya huko ughaibuni pole sana. Huyo kijana anauza magazeti anapata riziki yake. Hata huko ughaibuni kuna vibanda pia vya magazeti....Thamini kwenu na thamini kazi za wenzio...Halafu unavyosema 'Eti Tanzania' kwani wewe kwenu wapi au kubeba maboksi ndio kunakufanya uwe mgeni? Mkataa kwao mtumwa AND THERE IS NO PLACE LIKE HOME!!!UZALENDO MUHIMU JAMANI....
Sheikh Yahaya anauza fimbo za kujikinga na popobawa kwa dola 700. Sikujua kama teknolojia ya asili ni ghali kiasi hiki.
ReplyDeleteMichuzi jibu lako safi saba. Huyo mshamba anadai eti bongo kuna watu wanaishi kwa kuza magazeti, inaonekana hasamo hayo magazeti hata huko aliko! Kila sehemu duniani watu wanauza mgazeti na kuishi. Mshamba huyo.
ReplyDeleteKuhusu popobawa, nadhani ni uhuni tu wa kibongo. Mambo mengi sana bongo huwa ni kuvumisha tu. Lakini ni sehemu ya raha ya bongo.
Na wewe anon number moja hapo juu uliyeko ughaibuni, angalia sana. Uwe uanrudi home mara kwa mara. Utakuta vingi zaidi ya popobawa
Miaka ya tisini Popobawa alitamba sana Visiwani, ilifika hatua ya watu kulala nje ya nyumba zao.
ReplyDeletePamoja na kutamba kwa popobawa huyo sikuwahi kukutana na mtu aliekiri kuingiliwa nae... Zaidi ya kusikika kuwa leo alikuwa mtaa fulani, jana alikuwa kule...
Tembeleeni hapa kwa habari na link zaidi za popobawa kwa wale waliotoka Tanzania zamani kabla ya haya mambo hayajavuma sana:
ReplyDeletehttp://en.wikipedia.org/wiki/Popo_Bawa
Awwwww man,Popo Bawa is back?
ReplyDeletelol,I remember back in em days when the "mythical" beast was supposedly in Zanzibar doin his thing to young men.
SO to all men in Bongo:Tighten up em pants!