victor kinjeketile kingunge ngombale mwiru na mkewe anitha wakipozi na watoto yatima waliowaalika juzi usiki kwenye sherehe yao ya harusi ubungo plaza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Duh! Alikuwa wapi jibaba hadi umri ukaenda hivyo. Saa 9 hiyo bado ulikuwa single!

    ReplyDelete
  2. Wow, hingereni sana, i love the idea of inviting those kids ..iti izi brilianti!...

    ReplyDelete
  3. DEMU BOMBA SANA,BWANA HARUSI KAMA BABU WA KISOMARI!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Hongera bruv kwa kuachana na ukapera naona sasa utatulia, hutafungua sana zipu.wenye wivu wajinyonge.

    ReplyDelete
  5. kwa kweli, si mchezo bwana kaka. haya ndiyo mambo wadogo zako tulikuwa tunasubiri. ufungue mlango kwa ajili ya mambo ya neema hapo mjini>

    ReplyDelete
  6. wewe Mkemia acha ushamba. Hakuna umri wa juu wa mtu kuoa au kuolewa

    ReplyDelete
  7. Inviting kids was so mesmerizing!Big up!
    Ila Anita jishike, tabia haina dawa...sifa za huyo bwana Kinje si njema ktk jamii yetu!

    ReplyDelete
  8. we mkemia wewe ulioa na miaka kumi nini?kia mtu anaoa kwa wakati wae anapokuwa tayari,tuondelee ushamba wako.

    ReplyDelete
  9. anitha is a very nice lady,plz dont break her heart bro..............

    ReplyDelete
  10. Texitile de Pungue yaingusha Simba Tanzania

    Na Ibrahim Bakari (mwananchi.co.uk),12 Feb 2007

    SIMANZI, huzuni na majonzi vilitawala jana kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya Simba kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kwa mikwaju ya penalti.

    Simba ilifungwa penalti 3-1 na Texitile de Pungue ya Msumbiji baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa zimefungana bao 1-1 sawa na matokeo ya mchezo wa kwanza.

    Mchezo huo ilibidi uende moja kwa moja kwenye mikwaju ya penalti kutokana na kuhofia giza kwani taa za uwanja huo hazina nguvu ya kutosha kuendesha mchezo.

    Aliyetia simanzi uwanja mzima alikuwa Nico Nyagawa ambaye baada ya kukosa Yondani na Haruna Moshi kukosa penalti zao, kila mmoja alikuwa na matumaini na Nyagawa kufunga, lakini alipiga kizembe na mpira kuokolewa na kipa wa Pungue, Soares Soares.

    Baada ya Antonio Alberto wa Pungue kufunga penalti ya mwisho, baadhi ya wachezaji wa Simba walianza kuangua kilio huku mashabiki nao wakiwa hawaamini kilichotokea kwani kila mmoja alionekana mwenye huzuni.

    Huku mashabiki wa Yanga wakishangilia, mashabiki wa Simba walikuwa kimya majukwaani wakitafakari, wengine wakishindwa kuteremka kabla ya askari wa FFU kuanza matangazo yao. "Mpira umekwisha sasa tuondoke," lilisikika tangazo la polisi.

    Hata hivyo, mashabiki walianza kujivuta taratibu wengine wakiwa wamekunja mikono kifuani huku wengine wakiwa wameshika tama wakiwa bado hawaamini matokeo.

    Ukiacha hao waliokosa kwa upande wa Simba, ni Victor Costa pekee ndiye aliyefunga penalti yake wakati penalti za Pungue ziliwekwa kimiani na Belazmino Americo, Oscar Joacquim na Antonio. Penalti ya Hopes Changala ilitua mikononi mwa Juma Kaseja.

    Kama ilivyokuwa Msumbiji, Pungue ilikuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya 65, Fernando Cassigo aliipatia timu yake bao safi baada ya kupata mpira mrefu wa Henrique Mathlave na kumtungua Kaseja kutoka mbali.

    Simba ilisawazisha bao hilo dakika ya 87 kwa bao murua la Yahaya Akilimali kwa jitihada binafsi, aliwapiga chenga mabeki watatu na kuachia kigongo cha chinichini kilichokwenda moja kwa moja kimiani.

    Katika mchezo huo uliokuwa wa kibabe, uliochezeshwa na Berhane Dagnew Tesfay wa Eritrea, akisaidiwa na Redae Kiros Mehari na Ghirmai Yohannes Garza, Wimbo wa Taifa la Tanzania ulikosekana na kulazimika 'jukwaa' kuimba wakati Wimbo wa Taifa la Msumbiji uliimbwa kupitia mkanda uliorekodiwa.

    Kocha wa Simba Madaraka Bendera alisema: "Sina hata la kusema. Timu imecheza vizuri, nashangaa sijui tatizo ni nini...nawataka Simba tutulie tugange yajayo," alisema kocha huyo huku mashabiki wa Simba wakipiga mayowe kuwa hafai.

    Naye kocha wa Pungue, Afonso Sitole alisema Simba ilicheza vizuri isipokuwa tatizo lake ni kiungo. "Ngome na washambuliaji safi, ila kiungo na ndiyo maana tumeweza kupata bao kirahisi," alisema.

    ReplyDelete
  11. Wewe mkemia mpumbafu tuu... Wabongo hatutajiriki kwa vile tunachojua ni kuoa tu. Mwacheni amejijengea maisha, amemaliza mambo yote ya ujana na sasa anaamua kuoa na kutulia. Sasa nyie manaokimbilia kuoa na kuolewa bado wadogo hata mkipata watoto hamjui watakula nini, watasoma wapi. Mwacheni mwenzenu....

    ReplyDelete
  12. HONGERA KWA KUONGEZA WATOTO, NA WANAWAKE TOFAUTI. MAANA WAAFRIKA WANASEMA WATOTO NI UTAJIRI NA WANALETA BARAKA, HATA KAMA UNA WATOTO AMBAO WANA MAMA TOFAUTI.
    KWAHIYO UMEAMUA KUMUOA HUYU NA SIO JACKLINE (YULE MUHAYA) ALIYEKUWA MISS TZ.?
    LAKINI POA MAANA ANITHA SHE IS SO BEAUTIFUL. AND I THINK THIS IS TRUE LOVE, AND MAYBE ANITHA'S LOVE HAS MADE KINJE A CHANGED MAN.
    WELL DONE BROTHER.

    ReplyDelete
  13. Haya hongera mwaya Kinje, ila tunakuombea mola, ubarikiwe na uheshimu ndoa isije ikakushinda kama rafiki zako, Matare Nyerere, Albert Marwa, au Peter Rupia.
    Usituangushe, Kinje please, tunaamini umebadilika, ni mzazi sasa na mtu responsible. Tunakuombea, uprove people wrong.
    Congratulations.

    ReplyDelete
  14. MMependeza, congrats.
    Mke wako kapendeza, furaha mliyo nayo hapo isiishie hapo. Mvumiliane kipindi cha raha na shida, mpendane kikweli kweli na kuaminiana.

    Mmefanya jambo la busara sana kuwa alika hao watoto nao wajisikie. nA HUO msaada mlio toa ni mfano mzuri wa kuigwa na jamii. Mungu awajalie maisha mazuri na mafanikio mengi mzidi kuwa saidia watoto yatima.
    ZAENI MATUNDA MEMA, ZAENI YA HERI, AMEN.

    ReplyDelete
  15. Ww anony wa Sunday 10;15pm acha ujinga. Yawezekana we ndo mpumbafu. Huji kama riziki mafungu saba. Hata ukichelewa kuoa haina maana kwamba ndio utajitosheleza. Umri wa kuoa ukifika oa mambo mengine yatajileta yenyewe unless uwe na matatizo. Futa usemi wako!!

    ReplyDelete
  16. UMRI wa kuoa ni upi? Ni miaka mingapi ufikishe ndio umri wa kuoa au kuolewa maana naona watu wanataka kutoana macho ndani ya hii blog. Nafikiri kwa wanaumme kuoa ni ruksa baada ya miaka 18. Kwa wanawake kuolewa ni ruksa baada ya miaka 15 kama sikukosea kuzingatia sheria za Tz. Hivyo hamna muda maalum wa kuoa baada ya kutimiza miaka 18 wanaume au 15 wanawake. Ni uamuzi wa mtu tu kuoa au kuolewa. Ila kuchelewa kuoa kupo na kuchelewa kuolewa kupo endapo utakuwa unalinganisha na hili zoezi la kuoa au kulewa kufanyika wakati wa ujana. Na miaka ya ujana ni kati ya 18 hadi 35. Sasa kuna kuchelewa endapo utavuka 35 kuoa au kuolewa, lakini sio kosa na ni ruksa kufanya hivyo.

    ReplyDelete
  17. Hongereni Sana kwa harusi, mmependeza kweli, lakini niruhusu kusema kitu ' Anitha - Chui hawezi kubadili madoadoa yake or better still - Old habits die HARD' Anitha, you'll need to be a strong lady and always submit your husband in prayers everyday' and God will take care of everything. Nawatakieni Maisha mema!!

    ReplyDelete
  18. Sifuti usemi wangu kwa vile nimeona yote. Kama una mpango na maisha yako uoe na uzae utakavyo. Lakini kama huna mpango na life sio ukimbilie tu kuoa kwa vile umri unaenda mbali. Mimi nakuja bongo kila mara watu oh mtoto wako anahitaji nguo za shule, hela ya shule, oh uncle wako anapata kipaimara, oh uncle wako anaenda form one....Mimi sina mtoto lakini kila mtu ananipa mtoto tu. Kila mtu anataka niwe God father wa mtoto wake. Huyu mtoto wako....mtunze tu hamna tabu kabisa. Kila ukifungua email ni ...mtoto wako hivi , mtoto wako vile....sasa ndio nasema kama hujui utatunzaje mke wako/mtoto wako don't marry/get marriade and make babies just for the sake of it. Kwa vile hiyo ni selfish unataka kujifurahisha, kuishi in a tradition social life wakati hujali huyo unayemuoa au utakayemleta duniani utamtunza vipi, watoto wako watakula wapi, watasomaje.

    Mtu anayeoa kwa miaka 18 anamaisha gani ya kumtunza mke na mtoto? Ni trustfund gani wabongo wanayo ya kuweza kumsupport. Ndio umasikini hautatuisha.

    I am still standing by my opinion

    ReplyDelete
  19. Dah safi sana haswa hapo mlipo amua kuwapa zawadi watoto yatima pesa taslim inaoshesha ni jinsi gani mlivyoguswa na hao watoto na kuna watu maarufu wengine wanaoa au kuolewa bila kutoa msaada wowote ule wanajijali wao tu mmeonyesha mfano mzuri sana.Nawapa hongera ndoa yenu idumu milele na milele.kaka kinje safi sana na dada anitha safi sana.its me reen_minja@yahoo.com

    ReplyDelete
  20. Jamani watu wana vijiba sijaona.
    Kwani huyo Kinje hata kama alikuwa muhuni, player and whatsever. Kuna ubaya gani.
    Infact huko alikopita ilikuwa anavuruga tu, ila kwa Anita kafika Kigoma.Ndiyo maana kamuoa, na pengine ataacha hayo yote yaliyopita. People do change bwana. Mimi ni msichana, lakini Sioni kama kuna big deal ya kuanza ku count mambo ya liyopita, watu huwa wanaganga yajayo, na katika maisha huwezi endelea kama hutasahau yaliyopita

    halafu kuna mwingine anasema oohh, mwanaume mbaya. Kwa taarifa hakunaga mwanaume mbaya bwana, hata mwanamke mbaya. Ni vile tu mtu unavyojiweka, by the way sioni kama huyo kaka mwenyewe ni mbaya jamani. May be kwako, lakini alichompendea mwenzenu wala hujui. TRUE LOVE DOES'NT ASK WHY?

    Baada ya kusoma hayo maoni nimegungua possibly kuna watu wa yao, but mwanaume kuwa muhuni huwa haina aibu sanaaa kama mwanamke akiwa.

    Mimi nadhani hata kama huyo kaka alikuwa muhuni pengine ujana tu, au hakumpata mtu wa kumpepea na kumtuliza, na sasa kafika kwa anita.

    Mimi nampongeza sana huyo anita japo simfahamu. awaombea maisha mema na mvuliane please.

    ANITA YOU ARE THE STRONGEST WOMAN I SALUTE YOU! Na wewe pia Kinje, Kiboko yako ndio huyo ANITA.

    Kila la kheri

    ReplyDelete
  21. hongera sana anitha,,poleni sana dada zangu wote ambao mliitafuta nafasi hii kwa udi na uvumba,,kazi imeisha jamani tuanze maisha mapya,,,,tumsahau kwa sasa ili anitha naye aenjoy na mumewe

    ReplyDelete
  22. Hmm kama Mzee Kinje ameamua kutulia Bwana Asifiwe ...all the best Anitha always put God first in marriage ...that the advise sister...Kinje hongera pia kwa kuaanza unyumba it high time you need to settle too...
    Cograts!!!

    ReplyDelete
  23. h ah aha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...