kuna mdau katuma dukuduku lake sasa hivi.....



Ndugu michuzi naomba unitoe dukuduku langu kwa kuitoa hii article kwenye blog yako.
Inatia huruma na uchungu kuona hawa ndugu zetu wa bongo flava.Ingawa wana jitahidi sana kupiga miziki mizuri sana na huku nje tuna farijika tunapo angalia video zao lakini of course wanatutia aibu katika uvaaji.

How comes wewe unasema unaimba bongo flava means muzika wa bongo halafu uvaaji wako unakuwa hauelekei kama m-bongo;una iga akina 2PAC kuvaa minyororo shingoni kama watumwa wa nineteen kweusi na mafulana ya wamerekani maarufu.

Sasa una tangaza bongo flava au amerika flava hii muna haribu sana kwa sababu hakuna mtu wa
au utumwa na kasumba hii ya hawa jamaa naomba jamani muwaelemishe labda hawafahamu.

Tunaona raha tukiwaona kama MR EBO hata rafiki zangu watasha nao angalau wanabuni na kuuliza kuwa huyu ana toka Afrika sio hao wengine tunaoulizwa hawa ni wajamaika au waamerika.

ELIMIKENI NA MAVAZI ONDOENI KASUMBA ZA UTUMWA MAMBOLEO(NEO COLONIALISM) ULOWATAWALA NDANI YA VICHWA VYENU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. MI NAKUUNGA MKONO KABISA NDUGU YANGU... KUIGA KUMEZIDI NA KUNAPOTOSHA MAANA YA KUWA MSANII WA KIBONGO. UNAJUA WASANII NDIO MABALOZI WETU WA KUIWAKILISHA TANZANIA KOKOTE WAENDAKO NA ILI KUIWAKILISHA BONGO HAWANA RADHI BASI KUTOKEA KIBONGOBONGO. INGAWAJE SIJUI KAMA KUNA VAZI RASMI, LAKINI HATA KUVAA VITENGE NK KWA MFANO WANA NJENJE KAMA SIKOSEI AU ILE BENDI FULANI NIMESAHAU JINA WAO HUWA WANAVAA MABATIKI NK.. INAPENDEZA NA KWELI UTAJUA TUU WAMETOKEA AFRICA. WELL KWA UPANDE MWINGINE LABDA TUSIWASAKAME HAWA VIJANA BALI UTAMADUNI WA NCHI KWA UJUMLA NDIO WA KULAUMIWA.. NCHI KAMA NCHI SIJUI KAMA INAWAPA MSUKUMO GANI KIMAENDELEO HIVYO SIJUI KAMA WATAKUWA NA SAUTI YA KUWASUKUMA WAVAE KAMA NCHI ITAKAVYOTAKA. MANAKE SIKU MOJA NILIONA MKWALA WALIOPIGWA DUDU BAYA KWA KUTUMIA MANENO MACHAFU NA RAY C KWA KUTEMBEA NUSU UCHI- LAKINI LABDA NDIO VINAVYOWAFANYA WANAMUZIKI HAWA KUPATA ADMISSION KUBWA WANAPOFANYA MAONYESHO HIVYO KUWAONGEZEA VIPATO.. NADHANI HII MADA ITAKUWA NGUMU..

    ReplyDelete
  2. Jamani, mavazi ya mtanzania ni yapi? Kwanza Bongo ina culture ya miaka ipi? Mama yangu mmasai na baba mmakonde sasa mie nivae vipi? Kama nimekulia DSM sasa niende na kanzu mpaka kaburini? Ningefurahi kuona picha zako za Graduation na harusi nione usivyoiga wazungu au waarabu... signed mpingomweusi ingawa mie ni blackmpingo!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Afadhali umeliona ilo dada yangu mpz Salma maana wa Bongo tunapenda sana kuiga mambo ya wezetu na chaajabu wenzetu wala hawaigi mambo yetu apo mie nachoka zaidi jamani.Tuweni na ustaarabu kwa kuitangaza africa yetu,Mbona tunapendeza tu,ebu angalia Tanzania yetu ilvyo na utamaduni mzuri,Muangalieni Mr Ebo kwani hana pesa ya kununua nguo na kuiga mambo ya wezetu?Haswa kwa wasichana nyie mnaoimba nyimbo na mnalalamika kwamba muzuki wetu hauna soko kwa nje hapana huwa hawapendi wezetu wa nje kununua kwa sababu hatuna tofauti,muangalie Ray c,Jacq Ntuyabaliwe,na wengine wanaovaa nguo kama za wezetu nje hatuna tofauti wqezetu wanavaa nusu uchi na sisi tunaiga hawawezi kununua kwa sababu hakuna tofauti ya radha.TUBADILIKE TUTAFIKA MBALI JAMANI WANAMUSIC WETU.ACHENI KUIGA.reen_minja@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. Michuzi mimi nataka tu kuweka comment kuhusu kazi unayofanya kwa kweli ni umefanikisha katika blog zote kuwafanya watu wajisikie nyumbani. Sifikiri kama kuna blog zenye mtiririko kama huu mimi nimetembelea kadhaa na zote naishia kuboreka. Ila ya kwako naona inaleta aina zote za maisha ya mtanzania...burudani siasa etc. Asante Sana kaka yetu!!

    ReplyDelete
  5. Sio vibaya kuiga, ile tuige vile ambavyo vinafaa na vinavyosaidia kudumisha na kukuza utamaduni wetu. Wazungu na wengine wameiga kwetu, kwa mfano muziki unaopigwa America ya Kusini, Rock etc vina asili ya Afrika. Ukataji wa nywele style ya "punk" umeigwa kutoka Kongo na hata kusuka nywele kumeigwa kutoka kwetu.

    ReplyDelete
  6. WATANZANIA POLENI SANA
    Jamani kwanza huyu dada anaitwa SALMA niambie hilo jina ni la kitanzania au...... sasa kama hata majina yetu ni ya kuiga unategemea mavazi yatakuwaje??? Maji yanafuata mkondo mtu anayeimba malengo yake na mfano wake anajaribu kukopi mwanamuziki successful hiyo kwa bahati mbaya ni saikologiya ya binadamu... wa toto cha ndimu wanacheza mpira lakini kila mtu ana star wake huyu ..Zidane.. huyu Ronaldo... huyu David .Beck.hakuna mtoto anayejifananisha na wachezaji wetu wanao kunywa kimpumu...
    Hivyo hivyo kwa wanamuziki mtu ananza kuimba akiwa saikologikale anajifananisha na most famous singer siyo Dr. Remmy. Na hayo ndiyo maendeleo ... kwa kuwasaidia vitu hivi mvijue nakupa mfano (mtoto wa kiume anapozaliwa mfano wake kwenye maisha ni baba yake... wala siyo mama hivyo hivyo kwa mtoto wa kike anakuwa akiwa anajifananisha na mama yake.. ndiyo maana uwa tunasema wasichana wako sana kwa mama zao au wavulana kwa baba zao) huko siyo kuiga ni human nature.
    Kuvaa kama Mr. Ebbo haina maana eti ni utamaduni wa mwafrica au uzalendo. Aikon ni msenegal aishie marekani na anavaa kama 50...jz... na wengine lakini hiyo haifanyi hapotezi utaifa wake na siku zote anakuambia iam an AFRICAN boy born in Senegal...singing in America Kwa hiyo dada SALMA mie nitafurahi tukiwapata wakina Aikon ambao watapeperusha bendera yetu kuliko wakina Mr. Ebbo ambao wanapiga mitungi bongo na vikoi vyao.
    BY Doctor///

    ReplyDelete
  7. kazi nzuri michuzi maana blog yako inafanya tujisikie tuko karibu sana na nyumbani

    ReplyDelete
  8. Mimi nafikiri watu tunakosea sana tunapowalaumu vijana hawa chipukizi wa muziki.kwani ktk hali ya kawaida kila nchi ina mavazi yao ya kitaifa ila hawavai mavazi yao ya kitaifa ktk muziki,hebu jitazame hapo ulipo umevaa kitamaduniiiiii,cha msingi tupiganie tuwe na vazi la taifa na sio kulaumu tu kwakua umeulizwa hawa ni wajamaika au wachina

    ReplyDelete
  9. Fact ni kwamba wabongo tunapenda sana kuiga. Unakuta eti mtu anajidai yeye kama 2Pac, sijui gengsta sijui nini, yani mambo yasiyokuwa na maana. Ni backward mentality

    ReplyDelete
  10. Yeh hivyo vimeigwa kutokwa kwetu na kufanywa kuwa vya Ulaya sasa. ULaya wamekuja na mtindo wa wanaume kusuka nywele za kilioni. Hamna kitu kinauzi kama hiki lakini utakuta kaka zetu nao sasa wanaiga hii. Na dada zetu pia wanawasuka na watoto wao wavulana kabla wadogo ambao hata hawajaanza kujua tofati ya kuwa wanaume au wanawake. Halafu mtoto hakija kukwambiya yeye sasa anataka kuwa mwanamke unashangaa. Unashangaa nini na wewe ndiyo umeleya hiyo tabia kuwa "he has to do something feminine to look better?" Ni kweli tuangalie tunayoiga. Wamarekani weusi wanaofanya hii mitindo ya kila aina hawana asili au bado hawajaitambua (wanakaribishwa kama waAfrika vile vile lakini mwisho wanajikuta hawawezi kuwa wazungu na vile vile hawawezi kuwa waafrika kwa hiyo wanakuwa in between) lakni sisi tuna asili. Tena asili ya kuwa proud of.

    ReplyDelete
  11. Kwa kuwa Tanzania ina makabila mengi, na kila kabila lina utamaduni wake unaojitegemea, kwa mantinki hiyo HAKUNA UTAMADUNI WA KITANZANIA. Kilichoko ni general practice. Huwezi kuwa na utamaduni uniform kwenye nchi ya kiafrika yenye makabila zaidi ya 200. Narudia, HAKUNA UTAMADUNI UNIFORM WA KITANZANIA. Na pia namuunga mkono anony mmoja wa awali aliyesema kama wazazi wanatoka makabila mawili tofauti, au siajabu wazazi wenyewe walichanganya makabila, kuna utamaduni gani hapo? Kama mnaona watu wanaiga, nyie muwe wa kwanza kuacha kuvaa suruali, na mashati, na muanze kuvaa VINYASI kufunika sehemu za siri, na msivae viatu, na mtembee kwa miguu msipande daladala au magari. Dunia siku hizi imekuwa ndogo kama kijiji, kwa hiyo watu wanatabia ya kwenda sambamba na kinachoendelea duniani kote. Kama wewe binafsi hupendi style fulani, usivae, waache wanaoipenda wavae wapendeze. Tuache kupoteza muda ku discuss nguo za watu, na tupoteze muda kudiscuss tufanye nini tujiongezee kipato, na kusaidia familia zetu.

    ReplyDelete
  12. Ni kweli kuna mambo machache wanaiga,lakini sio sana kama Salma na wenzake wanavyoionyesha.Wala tusidhani ni hawa 'bongofleva' tu wanaoiga,ni watanzania wote, na hata dunia nzima.Wa S.Africa wanaoimba Kwaito unadhani wote wanavaa vikoi?Hata wewe Salma unapoenda kazini au Outing huwa unavaa kimasai au kikabila lako(au Kiafrika?),Kwa sababu hata wewe ni mfano wa kuigwa kwa watoto wako na wa majirani zako.
    Tusikae kuwalaumu hawa vijana kama wanafanya dhambi sana,tukumbuke Yesu alitoa mfano,'asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe......'.Tuwape moyo hawa vijana wajikwamue kimaisha,tununue cassette na CD zao ili kuwapa support,sio lawama zisizo na msingi.Dr Remmy aliyeenda Ulaya na mashanga amefika wapi?lakini angalia Juma nature alipo sasa kimaisha.

    ReplyDelete
  13. Binti yangu tasha ameniambia kuwa wasanii wanavaa kutokana na mitindo yao ya music. Huwezi kupiga BFlava na ukavaa kama mtu wa heavy metal. Pia ukipiga sindimba uwezi kuvaa tai.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  14. BLACK PEOPLE UNITE!!!
    Dada SALMA acha KUJISHUSHA UTANZANIA WAKO!!...Kwa AY kuiwakilisha TZ kwa kutumia muziki wake mpaka kupata airPlay MTV..Kila MTANZANIA HALISI ingefaa Kutoa PONGEZI kwa Kijana huyo na wasanii woote wa BONGOFLAVA...Kwanini wasivae 2PAC na JAY-Z??..wakati Hao ndio walijifunza Kwao...RAIS WETU MWENYEWE ANAVAA SUITS..ambalo ni vazi la WAZUNGU..mbona Hatukusikii ukimkosoa ili naye avae LUBEGA kama Mr.EBBO??
    Before you start Criticizing..Try and Learn about BONGOFLAVA..the Roots of it,The History,The StruggLe these young kids go through to get where they are now..
    KBC-KWANZA UNIT*
    www.myspace.com/mrkbc

    ReplyDelete
  15. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  16. Nafikiri huyu SALMA hajui maana ya utandawazi/globalization, yaani hawa vijana wetu hawawezi kuachwa na wakati. Haya mambo ni ya mpito, mbona zamani watu walivaa mitindo mbalimbali kama bugaluu,nk. I'm very sorry SALMA kwani inabidi uangalie nyuma na mbele kwani maisha ni stages zinapita. Ndo maana hawa vijana wa bongoflava wanaimba nyimba za mapenzi sababu wameshasoma soko lilivyo ni la vijana sanaaaa na mavazi yao vijana ndo hayo kama kata-k, mlegezo n.k. Wakati mwingine tukubali ukweli kulingana na hali halisi. Je kwanini watu wanapanda magari tena ya kisasa badala ya kupanda punda, ngamia, kutumia mguu., Kwanini wewe huvai nguo za kijadi kama za magome, ngozi n.k.

    Waache vijana wafaidi ujana wao, it is a matter of time. Kwanza hii bongoflava inatoweka haraka sanaaa na inaweza potea kabisa, so acha vijana watese ndo wakati wao.

    Lakini tukirudi kwako, tuambie asili ya jina la "SALMA", ni la kabila gani kama sio la kuigwa.

    ReplyDelete
  17. SALMA inabidi uelewe origin ya bongoflava, na jinsi inavyotengenezwa kwani ni kitu kinatengenezwa na mtu mmoja ambaye ni producer anaweka beats anavyoona yeye. Hadi hapo hakuna uasilia. Labda unasemea miziki ya ki-asili ya akina marehemu zawose.

    Kukaa abroad si kukufanya usahau mambo ya kibongo, na kufikiri vijana wa kibongo wako enzi za miaka ya 47. Hata vijijini kuna sat. antenna, MTV wanaona kama kawa. Kama ni mpenzi wa blogu ya Michuzi, recently aliweka kitu toka machakani huko kusini dish linapepea tu kwa mwanakijiji. Ndo nyie mnaochambisha wazeee na ukafikiri ukirudi bongo watu watakufagilia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...