benki zetu siku hizi zinajitahidi kwa mandhari na huduma kama hii ya nbc tawi la samora. dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Safi sana hii lakini hebu mambo haya yasiishie tu Dar es Salaam yaende hata mikoani pia.Ukilinganisha Dar es Salaam na sehemu zingine utadhani ni dunia mbili tofauti wakati ni nchi moja.

    ReplyDelete
  2. ILA BWANA MICHUZI baadhi ya kina dada zetu wanaofanya kazi kwenye hizo teller wanajiona wako mbinguni. Kuna mmoja anakaa wa kwanza upande wa kushoto sijui kama bado yupo yani anajisikia na ana majibu ya maudhi sijawahi ona, na dharau kali. Ila nisamehe sijui kama wana pangiwa permanent kwenye hizo teller au wanabadilisha kila wakati.

    ReplyDelete
  3. safi sana!
    wahudumu je??

    ReplyDelete
  4. nonsense - with great facilities, come poor customer services, the result is low efficiency.

    many tanzanians do not behave professionally, they think of working in such institutions as big time show off, ujiko.but they forget to deliver on the goods.

    i visited one local bank [name witheld], where a teller was fiddling with her mobile phone replying to text messages, while a queue of customers stretched as far as outside.

    kwa kifupi, watu wanajisikia, lakini wanakosa ufanisi katika uzalishaji na uwajibikaji.kama huamini shauri yako.

    ReplyDelete
  5. Jamani tellers kuzuri na safi kuliko za huku!
    Kweli tuko mbele, sasa huduma vipi?

    ReplyDelete
  6. Ile NBC iliyo kuwa ya Forex Branch ipo wapi???? Naomba mni/unisaidie na mailing address & tel # yao, nilijaribu kutuma several mails inquiring about my acct, sijapata majibu. Nilikuwa na acct pale.

    ReplyDelete
  7. Hiyo kweli ni Benki yetu!

    Shareholding Structure:
    ABSA Group Ltd. 55%
    Tanzania Government 30%
    International Finance Corporation 15%

    Hatuwezi kukohoa! ABSA wataungana na IFC!

    Uchumi wa nchi (ghala) kuhimiliwa na foreigners!

    Angalau Tanzania tungekuwa na 55%!
    tafuteni takwimu sahihi ni pesa ngapi zinazopelekwa Sauzi kutokana na Benki hii peke yake!

    ReplyDelete
  8. Wewe Kaka Mie, kutokuendeea kwa taifa hili kunawezeshwa kwa kiasi kikubwa na watu kama wewe wenye mawazo ya kikomunisti! Unataka tuwe na 55% kwa faida ya nani? Unafikiri tukiwa hata na 110% ndiyo mwananchi wa kawaida atafaidika?

    Sasa hivi benki zinacompete kupata wateja waje wafungue hata akaunti za watoto. Biashara ya mikopo ndiyo wanaadvertise eti hata kama ukifa deni halihamishwi kwa warithi. ATM zinawawezesha watu kuchukua hela hata usiku. Je wakati yalikuwa ma-SU vyote hivi viliwezekana. Angalia NMB ambayo ndiyo ilikuwa ya mwisho kuuzwa haikuwa hata na ka-ATM kamoja mwaka 2003!

    Na je umeshasahau kwamba kuna wakati, kabla ya kuiuza NBC, waziri wa Fedha alieleza graphically deni la NBC lilivyokuwa kubwa? Alisema sijui ukizipanga noti za 10,000 zinaweza kufika kilomita ngapi juu.

    Eti uchumi unamilikiwa na foreigners! Uzalendo bila akili ni bure ndugu yangu.

    ReplyDelete
  9. Kwanza kabisa sipendi kumtukana mtu yeyote hata akisema uozo!
    Andika hoja ya nguvu bila matusi...

    Eti unadai, inter alia, "kutokuendeea kwa taifa hili kunawezeshwa kwa kiasi kikubwa na watu kama wewe wenye mawazo ya kikomunisti!"

    Niliuliza, je, hiyo ni benki yetu?
    Nikashauri pengine tungekuwa na 55%!

    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!
    ...wenye mawazo ya kikomunisti!

    Maoni yangu hapo juu have nothing to do with kauli yako hiyo. This is, indeed, sad kusikia kutoka kwako!

    Hujui my political-economy background...wala hujui mimi ni nani out there katika dunia hii yetu ya mtandao! Usiparamie ngazi ya chuma na hali umevaa viatu vya chuma!


    Mimi sijui mawazo ya "kikomunisti"! Nifundishe. Na nitakuwa natembelea hii blog kila siku kupata Kujifunza Kozi ya Kikomunisti 101: Profesa Anonymous Mwenye Matusi Yanayonuka wa Wednesday, March 07, 2007 10:18:00 AM.

    Kwa mawazo yako, wageni wakiwa na 110% mwananchi wa kawaida atafaidika.

    Mataifa yaliyoendelea hayafanyi hivyo nchini kwao, nikiwa na maana kwamba benki kubwa na nyeti za nchi hazimilikiwi na mgeni, kama wewe!

    Endapo South Afrika ita-default leo hii, nyasi za Tanzania zitaumia.

    Uzalendo (kama wako huo) wa kuuza nchi yako kwa wageni ni utumwa!

    Mtumwa we! (OOPS)!

    ReplyDelete
  10. Wednesday, March 07, 2007 10:18:00 AM, waweka uzalendo wa wengine kwenye mizani yako na kuonekana wapungua!

    Wa-Tanzania wengi wanakerwa na kuuzwa kwa nchi yao kwa wageni kwa miaka mitatu bila kulipa ushuru wowote, na baada ya hapo kulipa 3%, kama ilivyo kwenye madini, au 30% kwa benki hiyo hapo juu.

    Wa-Tanzania wa namna hiyo watazidi kutetea kuwepo na "fairness in global trade transactions"!

    Wapi Mzee Idi Simba awafundishe wenye kupinga, kama wewe, maana ya uzawa katika kumiliki mali ya Tanzania?

    ReplyDelete
  11. Anony unayempinga Kaka Miye,
    Akili pia bila uzalendo nazo ni bure ndugu yangu. Waliouza NBC kwa million 100 wakati thamani yake ilikuwa ya mabilioni bila shaka walikuwa na akili sana (za darasani)
    Hao wateja watatoka wapi kwa umaskini wa Watanzania, asilimia sabini na tano hawajawahi kuwa na account benki!
    ATM hazihitaji kuwa Makaburu kuweka ni technologia ndio imetufikia sasa hivi. Yaani ulitaka wafunge ATM wakati computer zenyewe hazikuwepo?

    ReplyDelete
  12. We anonymous March 07, 10.18 Kakamie yuko sawa 55% kwa faida ya Taifa, kama tungekuwa na mabepari wetu tungekuwa mbali sana kwani pesa yote ingebaki nchini na kuwekezwa hapa hapa kwa faida yao na ya Taifa kwa jumla. Kwamba wangewekeza kwenye miradi mingine na kutoa ajira, kulipa kodi, umeme, maji nk. mfano IPP media.

    Na kama hujajua Asia Tigers karibu mabenki yao yote yako chini ya serikali zao check it out anzia Taiwan.

    ReplyDelete
  13. Tatizo ambapo lipo Bongo kwa sasa sehemu nyingi ni kwamba watu hawako professional kabisa. Unaenda sehemu unasubiri huduma mtu anakuangalia kwa dharau anakujibu vibaya, yaani hawaelewi chochote kuhusu customer service. Anaona kama anakufanyia favor fulani kukusaidia kumbe that is not it. Inabidi wapewe darasa kuhusu customer service na jinsi ya kuact kama professionals kwenye sehemu zao za kazi ama sivyo wanakuwa wanakimbiza wateja maana mtu unaona kwamba hudhaminiwa kabisa.

    ReplyDelete
  14. Kaka Miye, nitarudia tena kwamba watu kama wewe ndiyo mnayokwamisha maendeleo ya nchi. Mnakuwa na mawazo theoretical amabazo mkiziweka katika practice zina back-fire. Ukweli ni kwamba biashara ya mabenki inawenyewe - hauwezi ukaamka na kujenga majengo na kusema eti na wewe utaji-compare na Stanchart. Mimi sijapinga mabenki genuine yanayoendeshwa katika principal za kibepari - k.m. Azania Bancorp, Dar Community Bank, Akiba Commercial etc. Nachopinga ni pale wananadharia kama wewe mnapoanzisha unsustainable banks za ki-SU (ambazo zimekufa zote)

    Wewe Anon unayelalama 3% ya migodi, tafuta na kukusanya 1Bn USD, wekeza kwenye mgodi, ajiri watu 4,000 halafu zalisha at a rate of return of 15%, alafu ulipe mrahaba wa 50% unaosema. The only way tutafaidi hii migodi ni kwa kuwauzia huduma na bidhaa (goods and services) - tuwepo kwenye value-creation chain ya kuzalisha hizo dhahabu. Kukaa pembeni halafu kutegemea kupewa bila kujishughulisha hakutatusaidia.

    Kuparticipate katika global economy haina maana kwamba tumeuza nchi. Globalization is a force that cannot be stopped. Do yourself a favor and stop resisting it

    ReplyDelete
  15. Wewe anoy unayezidi kumpinga Kaka Miye, you are not a voice of reason at all! You are a voice of unresonableness!

    Eti wauambia ulimwengu out there: Globalisation is deterministic a force: "Globalization is a force that cannot be stopped." You sound as unreasonable as mtu asiyejua kuwa Globalization is a human not a natural force!

    Where there is uneqiality in a society, globalisation shall have to bow to the realities of life!

    ReplyDelete
  16. Globalization ni mfumo ambao unafukuza kazi wazawa ili uajiri wageni kama benki hii ilivyofanya.Imefukuza wazawa wengi kwa kuwapunguza kazi na kuajiri wageni waliojificha ndani ya mtambo unaoitwa Computer.

    Unajua Computer na software zake hutengenezwa na watu wengi huko Ulaya na Marekani.Sasa ili ziuzwe kwa wingi inabidi watu wengi wapunguzwe kazi Africa ili tuajiri hao waliojificha ndani ya Computer wakijiita majina ya Hardware na Software.

    Kama Computer na software inatengenezwa na watu kumi hadi ikamilike,wewe ukipunguza watu kumi ili upate Computer moja maana yake ni kuwa umefukuza wazawa 10 ili uajiri wageni 10 kule Ulaya na Marekani .

    Globalization hasa ni kuwatafutia ajira za maana na soko la maana dunia zima watu wao waiokwama kwa kukosa ajira na masoko madogo katika nchi zilizoendelea.Nchi zilizoendelea zinaogopa sana tatizo la ukosefu wa kazi na masoko katika nchi zao kuwa ni bomu linaloweza kuwalipukia usoni ndio maana wakaanzisha Globalization CHAP CHAP kabla hata nchi zetu zikiwa hazijakaa sawa.

    Technologia imesababisha wazawa kukosa kazi na wageni kupata kazi huko teknologia zitokako.

    ReplyDelete
  17. TAFADHALI JITAHIDI KUANGILIA HIYO PICHA YA NBC SAMORA VIZURI. YOU WILL NOTICE KUNA COUNTER 8, ILA NNE TU NDIYO ZINA WATU. KWA UFUPI HIYO NDIYO CUSTOMER CARE YA NBC. SAD.FONT> KAKA MICHUZI HAKUPATA NAFASI NZURI YA KUPIGA PICHA MPAKA FOLENI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...