Home
Unlabelled
omba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Msiwaonee hao omba omba bure kwani tatizo siyo omba omba ila tatizo ni chanzo cha ombaomba ambao ni utapeli wa wanaodai kuwa wanaiongoza nchi. Rais mwenyewe ni omba omba wa kimataifa kwani leo yuko Marekani, kesho Uingereza, keshokutwa Japani na jana alikuwa Nchi za Scandnavia. Na kila aendapo anaomba. Imefikia anaomba hata wataalamu wa kujadili mikataba akidai kuwa Tanzania haina wataalamu wa kutosha. Rais aache kuomba kwanza halafu hawa jamaa wataacha kwani wanamfuata kiongozi wao. Be fair and honest michuzi. Na ulivyokuwa muoga maoni yangu utayatia kapuni.
ReplyDeleteAnony hapo juu umenikuna kweli na hiyo comment yako! Ni rahisi kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzio hali kuna ji boriti kwenye jicho lako hujaliona. Nasikitishwa sana na kitendo cha raisi kuomba watu wa kujadili mikataba au hata wataalamu wa fani nyepesi ambazo wazawa wanaweza kuzimaliza hukohuko home. Naamini nchi yetu inaa vyuo vikuu kadha wa kadha vinavyozalisha wataalamu wa fani mbalimbali kila mwaka, hivi hawa woooooote kweli hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kuchambua mkataba hadi tukaanike siri zetu za chumbani kwa hawa jamaa ambao bado wana damu ya kikoloni? Mnajua wengi bado hawatutakii mema sie tunaojikongoja kimaendeleo? Hivi mnajua wanajua wazi kuwa waafrika wengi wanafumbuka maacho kwa kuwa wanabukua vyuo vikuu ndio mana wanashinikiza serikali zijitoe kuwadhamini watu kwenye vyuo vikuu ili mambumbumbu ndio wawe wengi? Wanajua wazi kuwa wabongo wengi hawana nguvu za kujisomesha wenyewe wanategemea serikali isaidie, sasa kama serikali inajitoa hata kwenye hio mikopo unadhani nani atasoma? Sasa hawa ndio watu wa kujadili naao kuhusu mikataba iliyofanywa na maswahiba wao! Unadhani watatoa lolote la msaada kama sio kushangilia kuvuja kwa pakacha!
ReplyDeleteTunayo safari ndefu jamani
Anony point kali sana hizo mtu wangu. Kunya anye kuku akinya bata kaharisha. Kama Rais ni omba omba iweje wananchi wake wasiwe omba omba? Ila Rais wetu anatia aibu halafu anajisifu ati anaenda kutafuta misaada, Raslimali kibao tunagawa bure halafu tunaenda kuomba mwe!
ReplyDeletemheshimiwa hapo juu swala sio rais kuomba, na kama ni kuomba serkali yetu imefanya hivo kwa muda mrefu na omba omba wamekuwepo kipindi chote hicho. fikra zangu zinanambia hili tatizo linaonekana kuwa kubwa sana sasa hivi si dar tu bali hata mikoani eg mwanza ambapo omba omba wamekuwa wengi na watot ndio wanaonekana kuwa wengi. wazo linalokuja akilini ni moja tu.... viongozi na jamii nzima kutafuta solution ya tatizo hilo la sivyo maisha ambayo tunayaona kwa majirani zetu kama kenya sasa yapo right in our door steps!
ReplyDeleteKwahiyo na wale ombaomba wa kwenye nchi zingine kama Kenya, Nigeria, just to mention few Marais wao pia ni ombaomba??!! au mnachonga tu kufurahisha midomo?! cha msingi ni kushauri solution juu ya tatizo hili sugu kwa nchi zetu. Wazo kama vile kila tajiri mkubwa akamate ombaomba angalau watatu wakiwa kama kikundi na kuwafungulia mradi and equip them with knowledge on how to run those small businesses, nafikiri kidogo itapunguza tatizo hilo. na hao masikini nao wakifanikiwa wabanwe ili nao wawasaidie wenzao mitaji ya kuanza biashara ndogo ndogo.
ReplyDeletewakale wapi wajameni.............
ReplyDeleteMmmmh naona nembo ya Tigo pale kwa mbele, hili neno nasikia lina maana mbaya sana hapa mjini
ReplyDeleteChuck Palumbo you are runing in a circle. Mheshimiwa hapo juu ametamka bayana kuwa tatizo siyo omba omba, ispokuwa tatizo ni utawala mbaya ambao unataka kutatuwa matatizo bila kujua chanzo cha tatizo. Ndiyo maana ukienda hospitali unapima ili dk ajue tatizo ni nini? Ukishatakiwa, muendesha mashtaka anafanya upelelezi ili awe na kesi nzuri. The same apply kwetu. Rais anaomba, na anapata pesa lakini ana shindwa kuzigawanya inavyotakiwa (missalocation of resources).
ReplyDeleteUtajiri wa nchi hauwafikii hawa omba omba ndiyo maana wanaondoka vijijini kwao na kuja mjini kuomba. Wape ajira, maji, umeme na burudani uone kama utaona omba omba hata mmoja mjini.
Kwahiyo, tatizo siyo omba omba tatizo ni nepotism, tatizo ni incompetence, tatizo ni UTAWALA BORA. Hatuna viongozi.
Mkoa wa Dodoma unaitia aibu Tanzania.Wagogo waambieni wagogo wenzenu waache hiyo tabia ya ombaomba. Kama kwao ardhi mbaya waombe serikali iwahamishie sehemu nyingine.Ardhi Tanzania tele.
ReplyDelete