Home
Unlabelled
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
jk na babu mugabe au???
ReplyDeleteNadhani huyu ni mbambe wa Zimbabwe(Mugabe) anamsidikiza JK
ReplyDeleteHuyo ni Jakaya na Dito...Jakaya anampa pole DITO
ReplyDeleteJakaya anampa pole Dito...
ReplyDeleteJakaya kamuita Dito Ikulu...akimpa pole Ikulu...
ReplyDeleteHuyo ni Robert Mubabe wa Zimbabwe. Amekwisha sema kama wapinzani wanaona kuwa wameonewa, basi wakajitundike! Hapa kuna kazi. Ila jamaa mwisho wake waweza kuwa mbaya zaidi ya viongozi wengine wenye sifa kama zake. JK mpe shavu.
ReplyDeleteJakaya na Ditopile...hii ilikuwa jana alipomita ~Ikulu kumpa pole kwa yalio mkuta
ReplyDeleteA.K.A JK ,A.K.A Robert wa Mugabe...Nyundo ya chuma iyo aitetereki
ReplyDeletehii ni Jana..Jakaya alimuta Dito Ikulu ...kupa pole kwa yalio mkuta
ReplyDeleteHUYO NI JK na MUGABE
ReplyDeleteNITUMIE ZAWADI YANGU
MPIGANIA UHURU WA 80'S NA MZEE WA KASI,ARI NA NGUVU MPYA YA KUPUNGUZA AJIRA BINAFSI.
ReplyDeleteNI JK NA MZEE ROBBIE MUGABE,NADHANI JK AMETUMWA NA WAKUU WAKE WA KAZI(BUSH NA BLAIR) KWENDA KUTAZAMA MAMBO YANAVYOKWENDA ZIMBABWE,LAKINI PIA MZEE ROBBIE NI SAWA NA BABA MZAZI KIUMRI,SASA SIJUI KAMA JK ANAWEZA KUMPIGA BITI KUHUSU ALIVYOWAPA KICHAPO CHA NGUVU WAPINZANI WAKE.
ReplyDeleteSASA HIVI ADDIDAS WANA KAMPENI INAITWA 'IMPOSSIBLE IS NOTHING' NAFIKIRI KAMPENI HII INAFANYA KAZI YAKE KISAWA SAWA BONGO,NADHANI PIA KESI YA KINA NGUZA VIKING NA WATOTO WAKE INGEWEZA KUWA YA KUBAKA BILA KUKUSUDIA KAMA TUNGECHANGA MICHANGO YA KUTOSHA KUWALIPA MAWAKILI WENYE TAALUMA.
ReplyDeleteNamwona Mzee Mugabe (Mzee haambiliki wa Zimbabwe) Mtu ambaye haamini kuwa kuna watu wengine waweza ongoza nchi.Katika wazee wajinga waliobaki duniani yuko yeye na Fidel Castro wa Cuba.
ReplyDeleteHamna kitu tena kwenye vichwa vyao.Wamebakia kuwa vituko wa siasa duniani.
Kikwete nakujua huwezi kumeza maneno kiambie hicho kibabu kiondoke. Kama hakijui kiende wapi kipe hifadhi ya kisiasa Tanzania uwasaidie wazimbabwe waondokane nacho.
Wazimbabwe wanaisha jamani mbona viongozi wa Afrika hamna huruma?
Kule kwa Jongwe, Pamberi na Chimurenga, mambo hayo hayakuanza na Robert Gabriel Mugabe.
ReplyDeleteWaingereza walikuwa wakiwatuma masetla wao kwa kuwapa vibali vya kuloea huko. Wafikapo wanapewa na serikali ya kikoloni ardhi yeyote ile iliyokuwa nzuri na kuwafukuza wazawa.
Licha ya kupewa ardhi, walikuwa wanapewa pembejeo za ujasirimali na ulinzi, kulikuwepo na utapeli mkubwa. Aridhi ilikuwa inatwaliwa kwa kuwalazimisha wazawa eti kuingia katika “estate deals” kwa kutia madole shahada zilizokuwa zimeandikwa kwa Kiingereza, lugha wasiyoelewa.
Vibali vya umilikaji wakati mwingine vilikuwa ni vya miaka 99. Masetla wengine walivibadilisha kuwa miaka 999, kama ilivyokuwa huko Kenya!
Wakina Smith walipoona kuwa Uingereza was about to de-colonise “Rhodesia”, walijitangazia uhuru (unilateral declaration of independence) mithili ya Wazungu huko Amerika (USA).
Wazawa wakashika mitutu ya bunduki hadi wakina Jongwe, Pamberi na Chimurenga na wenzao wakatafuta modality ya kuleta uhuru kwa Zimbabwe.
"Modality" hiyo ilikuwa ni pamoja na Uingereza (kwa kushirikiana na Amerika) kutoa fungu la mapesa na uwezekano wa wazawa kununua aridhi iliyokuwa imetwaliwa na Wazungu. Uingereza ilitoa fedha kidogo kwa mara ya kwanza. Amerika ikasita.
Pesa hizo za Uingereza, inasemekana kuwa wakina Pamberi na Chimurenga wachache tu ndio waionufaika.
Kuna uvumi kuwa “vigogo” wa wakina Pamberi na Chimurenga ndio tu walioanza kunufaika.
Modality hiyo ilikuwa sawa na ile Uingereza ilivyofanya huko Kenya kufuatia uhuru wan chi hiyo. Serikali ya Mzee Jomo Kenyatta ilipewa mapesa mengi na Uingereza kununua aridhi kutoka kwa masetla Wazungu.
Lakini wapigania uhuru hawakuweza kupata pesa hizo kwa sababu zilikuwa na masharti. Wengi wa wapigania uhuru hawakuwa na elimu au akaunti za benki kuweza kuzitumia, kama “collaterals” ili kukopa hizo pesa.
Huko Kenya walionufaika ni wachache waliokuwa karibu karibu na Mzee Kenyatta na viongozi wa serikali yake.
Wengine walikuwa ni wale wale walioshirikiana na Uingereza dhidi ya Mau Mau, kama ma-“home guards”, watoto wao wakienda shule, na wakati wa uhuru kuweza kupata mapesa hayo ya kununulia mashamba.
Kenya haikushutumiwa, kama serikali ya Robert Gabriel Mugabe inavyoshutumiwa!
Robert Gabriel Mugabe anashutumiwa kwa sababu ya "his uncompromising position" ya kuipenda Zimbabwe. Lakini msimamo huu umemletea kasheshe!
Vyama vya upinzani (hasa cha Movement for Democratic Change kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai), kwa kushirikiana na wakubwa, vinamwona Robert Gabriel Mugabe kuwa ndiye kitovu cha mabaya yanayoikidhi nchi hiyo nzuri ya Zimbabwe. Na Robert Gabriel Mugabe anajua hizo njama. Amekimbiwa na wakubwa hadi hapo atakapokubali kusalimu! Yeye, anajibu mapigo yaho kwa kusema, “Go and hang!”
Sasa wakubwa wanapitia nchi za Afrika zilizo marafiki na Zimbabwe “to exert soft hammer blows” kumkunja Robert Gabriel Mugabe (kana kwamba Afrika ndiyo the "progenitor" wa makakati huo)!
Mtakumbuka kuwa "within six months" Bush alikuwa na mikutano miwili na JK. Mkutano nyeti wa mwisho uli”ruffle the feathers” za wale Michuzi awaitao, “watani wetu wa jadi”!
Ingawa hatuna undani wa yale yalizozungmzwa na kuafikiwa, nafikiri masuala ya Somalia na Zimbabwe yalizungumzwa, pia.
Mtakumbuka kuwa kati ya si chini ya miezi sita, JK amekutana na Blair mara mbili, pia. Na wa-Tanzania wengi wamekuwa wakijiuliza uliza kwa nini?
Nafikiri la Zimbabwe lilizungumziwa, sambamba na ziara ya Mkuu wa Usalama wetu kumtembelea Robert Gabriel Mugabe!
Robert Gabriel Mugabe amefikia wakati wa kuandika mtihani mkubwa us u-“statesman”. Na ushindi kubwa wa kupewa shahada ya u-“statesman” ni ule wa kuokoa nchi (Zimbabwe) kutokana na madhambi ya zamani yanayo-“exacerbate” kuidhalilisha.
Tutumaini kwamba Robert Gabriel Mugabe atashinda mtihani huo kwa kunga’tuka hivi karibuni, siyo kwa sababu ya umri wake. Uongozi wa nchi wakati mwingine “transcends chronological age determinants”.
Tuepukane na "deterministic conclusions when dealing with human conditions; youth does not necessarily endow pre-determined leadership wisdom!"
Pamberi na Chimrenga!
Inasikitisha kwamba wengi wetu tunasahau historia haraka hivi, na inakuwa rahisi kwetu kuwa influenced na vyombo vya magharibi.
ReplyDeleteNitatoa kwa ufupi maoni yangu hapa, lakini ningeomba msome maoni yangu kwenye Jambo Forum, nikitumia jina la 'Keynez' katika topic ya zimbabwe.
Issue ya zimbabwe ni ya kihistoria. Nakumbuka kwenye hii hii blog ya michuzi niliwahi kukumbushia jinsi zimbabwe ilivyokuwa kama symbol ya independence movements za africa miaka ya 60-80, nikasema kuna hatari kwamba tusipoangalia kwa makini tukaacha zimbabwe ianguke kwa pressure za marekani na UK, itakuwa mwanzo na mwisho wa kusahau na kupoteza bure machozi, jasho na damu zilizomwagika miaka ile ili kumkomboa muafrika.
Hatua serikali ya Mugabe ilizochukua katika suala la ardhi, in a perfect word, ilitakiwa kuchukua baada tu ya uhuru, lakini kumbuka, bado south africa ilikuwa chini ya makaburu, z'bwe haikuwa kwenye position, kisiasa, kijeshi au kiuchumi, ya kufanya hivyo. Hapa simtetei kwa nini imechukua this long kufanya maamuzi haya, kuna uwezekano kwamba alijisahau au kama wengine wanavyosema, amechukua hatua hizi ili kupata political support ndani ya nchi (ingawa nakataa kuamini hivyo), lakini ukweli ndiyo huo. Matatizo ya zimbabwe ya kiuchumi yanatokana na sanctions (illegal sanctions) kuliko sera ya ardhi. Ni maamuzi mangapi yanafanyika ndani ya marekani, UK, Australia, ambayo nchi zingine haziyaafiki lakini haziingilii? Inakuwaje z'bwe wafanye maamuzi yenye best interest kwa nchi, maamuzi ambayo ni long overdue, ilete international outcry?
Ningependa waheshimiwa muingie kwenye jambo forum, mimi siyo mshiriki sana kule, mara nyingi ni msomaji zaidi, lakini hii topic baada ya muda mrefu kujizuia kutoa maoni yangu, nadhani ni set the record straight.
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2261&page=6
Rushwa ndio ilinyamazisha viongozi wa Zimbabwe wasishughulikie suala la Ardhi kuanzia walipopata uhuru.Viongozi wa juu wa Zibabwe Waliwekewa mapesa na kupewa Majumba Uingereza,Ulaya na Marekani wakanyamaza.
ReplyDeleteWalipotaka rushwa zaidi kila mwaka kutoka kwa wazungu wenye mashamba Zimbabwe,Wazungu wa Zimbabwe wakagoma ndipo Mugabe akapanda hasira akasema mtatukoma akaanzisha sera za kuwakomoa wakulima wa kizungu Zimbabwe.
Mugabe ana hasira na mataifa ya magharibi siyo kwa sababu ana uchungu wa Zimbabwe bali ana hasira ya nyumba zake zilizochukuliwa ulaya na Marekani, na Akaunti zake na za washirika wake zilizokuwa frozen Ulaya na Marekani.
Vita ya Zimbabwe ni kati ya viongozi waroho wala rushwa wa Zimbabwe na Wakulima wazungu watoa Rushwa wakikomoana baada ya kushindana dau.Mugabe anatimua wazungu ,wazungu wana-freeze Account na kutaifisha mali za viongozi wa Zimbabwe na ku-frustrate Economic System Za Zimbabwe.Matokeo yake Tembo wawili wakipigana nyasi ndio ziumiazo.Wanaoumia ni wananchi wa Zimbabwe.
Dawa ya tatizo hili ni nini? Wazungu watoa rushwa wameshatimuliwa kilichobaki ni kuwatimua wala rushwa (viongozi wa serikali ya Mugabe) akiwemo Mugabe mwenyewe apishe wengine walete mabadiliko Zimbabwe.
Nchi za Afrika zimchukulie hatua Mugabe na serikali yake wasimchekee chanzo cha mgogoro mzima ni Rushwa pamoja na kuwa Mugabe anajaribu kutumia watu kama "human shield" akisingizia eti anawatetea kuhusu ardhi siyo kweli ni mwongo mkubwa asiye na haya.
Waafrika tufike mahali tuambiane ukweli na tusaidieni.Saidieni raia wa Zimbabwe
Inanifurahisha kusikia mpigania ukombozi huyu mahiri sie Tanzania tunaweza kumpa hifadhi pindi wakoloni watakapomzidi kete ili aondoke kwa kutumia mambo mengine na kuacha swala la msingi likiendelea, waafrika kunyanyaswa kwa utajiri wao. Kwa nini RM unakuwa na huruma hivyo? Anaamua wapigwe mbele ya kamera! Nakupa ushauri wa bure, una state power, kwa hivyo nakuomba uwa "Kolimba", "Katabalo".
ReplyDeleteNa nyie acheni ujinga, mnajua kabisa jamaa ni Mugabe halafu mnasema Dito. Hata hivyo mimi naona labda Mugabe anataka msaada wa chakula [my opinion].
ReplyDeleteNa serikali ya UK na US hawaishi kuharibu nchi zetu. Wanapenda sana tuteseke kwa vile mashamba ya watu wao yamechukuliwa basi wanafanya revenge.
Some of these rich countries have been destroying all these countries from Somali to Iraq. Cause they don't have anywhere to get rid of their bombs. They come up with all these propaganda's just to wipe out our poor countries and future generation.
Imagine you being one of the children of Palestine, day in and day out having to hear the noise of Helicopters, bombs, bullets, etc. This is hell!
It's no joke people are struggling because of these sanctions, they still want to rule the world. In some places things are changing for the better, am really happy to see people like Hugo Chavez trying to create a buzz in order to show and let people know about this modern day colonialization. We all should wise up!
At the same time I must say we are also stupid, all these African rebel groups and governments from war torn countries and democratic governments are also to blame for the rapes, child exploitation, money laundering, greed, etc.
This is another sad story!
AU inapaswa kumuomba Col. Muammar al-Gaddafi kwenda kuzungumza na Mugabe. Ni kiongozi pekee aliyebaki mwanamapinduzi ambaye alikuwa na tofauti za muda mrefu sana na nchi za Magharibi na hivi sasa ameamua kulegeza msimamo wake na wamekubali kumpokea. Pia anaweza kuongea na Mugabe na kumshawishi alegeze msimamo wake na hata kung'atuka madarakani kwa ahadi ya kumpatia nishati na msaada mwingine. Libya ina uwezo huo.
ReplyDeleteJK pamoja na jitihada zake na nia njema aliyonayo, hii ngoma sio siri ni havi sana kwake.
Au wadau wa Michuzi Blog mna maoni gani kuhusu hilo?
Vikwazo vya uchumi, utamaduni, na kadhalika, huwekwa na nchi binafsi, makundi ya nchi rafiki, na jumuia ya ulimwengu dhidi ya utawala wowote wa halali au haramu.
ReplyDeleteMadhumuni yake ni kukaza uzi kuumiza utawala wa nchi husika hadi usalimu amri; vikwazo ni silaha (weapons of mass psychology)!
Mataifa makubwa yamekuwa yakitumia silaha hii dhidi ya Zimbabwe. Vikwazo hivyo haviwagusi directly Robert Gabriel na vigogo wa Pamberi ne Chimurenga wenzake, waumiao ni walalahoi wa nchi hiyo; ziumiazo ni nyasi!
Jumuia ya ulimwengu inajua wazi wazi kuwa kunakuwepo na nyufa nyingi za kuepuka vikwazo hivyo. Hili si jambo geni.
Na wakati mwingine, vigogo hutajirika kwa kuwepo na nyufa hizo. Vikwazo vinakuwa ni ujasirimali kwa mpito wa mlango wa nyuma.
Serikali ya Uingereza na Amerika zimekania kukaza nati za vikwazo hivyo dhidi ya Robert Gabriel na wakina Pamberi ne Chimurenga wenzake ili wana-Zimbabwe wajute kiasi cha kuja juu na kuuangusha utawala wa wakina Robert Gabriel na wakina Pamberi ne Chimurenga wenzake.
Itakumbukwa kuwa sisi wa-Afrika tulilia mbele ya Umoja wa Mataifa hadi mbele ya Baraza la Usalama kutaka vikwazo dhidi ya haini Ian Smith na wazungu wachache wenzake wa "Rhodesia" (sasa Zimbabwe) viwekwe. Kilio chetu kikapigwa nyundo na Uingereza na Amerika, hasa Amerika.
Amerika ilipinga vikwazo hivyo, hasa Baraza lake la Seneta, kutokana na sheria iliyojulikana kama “The Bryd Amendment” (Seneta Bryd wa North Carolina) kushauri kuwa ni kinyume cha nidhamu ya biashara ya Amerika kuwazuia wananchi binafsi wake kutofanya biashara na nchi (Zimbabwe) kutokana na vikwazo hivyo.
Amerika ilikataa kuweka vikwazo dhidi ya serikali ya Jenerali Jaruzelski wa Poland ili kuunga mkono msimammo wa wafanyakazi bandarini huko Gdansk, Niezależny Samorządny Związek Zawodowy "Solidarność" (Solidarity Movement) chini ya kiongozi wao, Lech Walesa, kwa kisingizio kuwa vikwazo hivyo vitawaumiza wananchi walalahoi wa Poland.
Lakini vikwazo hivyo vikawekwa kwa Iraq kwa madhumuni kuwa wana-Iraqi wangekuja juu dhidi ya Saddam Hussein na utawala wake, chini ya chama chao cha Baath!
Sasa niandikapo, Uingereza na Amerika zimepania “to tighten the screw” dhidi ya Zimbabwe:
LONDON (Reuters) - Western powers vowed on Tuesday to keep up pressure on Zimbabwean President Robert Mugabe despite threats to expel their diplomats if they continue to criticize his government.
Both Britain and the United States have called for more sanctions against Mugabe's government because of what they say was a violent crackdown on opposition leaders and the severe economic crisis they blame on state mismanagement…
Wengine tunasema :
Afrika, Tuamke! Mapambano Yanaendelea! Pamberi ne Chimurenga! Forward with the Revolution!
masela hayo magazeti yenu hatuna muda wa kusoma kama huwezi kuandika sentensi 10 bora uache tu, tuna mambo mengi ya kufanya ukizingatia tuko hoi kwa kubeba box siku nzima
ReplyDeleteWaachie wenye muda wasome!
ReplyDelete