malkia wa mipasho khadija omar kopa akiomboleza kifo cha mwanae omar nyumbani kwake mwananyamala kwa kopa muda mfupi kabla ya kusafirisha maiti kwenza zanzibar na boti ya saa kumi tayari kwa mazishi yaliopangwa kufanyika kesho. omar alifariki usiku wa kuamkia leo hapo nyumbani kwa mama yake baada ya kuugua kwa muda kiasi. jina lake kamili ni omar yusuf doria na amefariki akiwa na umri wa miaka 23, kwa mujibu wa mwanafamilia tulieongea naye pale msibani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Michuzi nimepokea habari hizi kwa mshituko sana, kwani marehemu alikuwa ndio anaibukia katika fani ya taarab na mi nilikuwa mpenzi wa nyimbo zake hasa kupitia pale mahusiano.com, ''sisi wote ni wa mwenyezi mungu na kwake tutarejea''

    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI

    ReplyDelete
  2. poleni sna wafiwa ndio kazi ya mungu na sisi tuanaelekea ukouko.lililobaki ni kumuombea dua marehemu. m/mungu ampe hatima njema

    ReplyDelete
  3. My thoughts and Prayers go out to Khadija and her family , May lord rest his soul in eternal peace.

    ReplyDelete
  4. AMEFARIKI NA UMRI MDOGO SANA , WAKATI SANAA YA MUZIKI WA TAARABU BADO ILIKUWA INAMUHITAJI SANA-MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI

    ReplyDelete
  5. pole sana mama ni mipango ya Mungu hiyo

    ReplyDelete
  6. poleni sana wafiwa ni kazi ya mungu, sote tutaelekea ukouko ,tumuobee dua marehemu,m/mungu ampe hatma njema ,amin

    ReplyDelete
  7. poleni sana wafiwa, ni kazi ya mungu,mungu amlaze mahala pema peponi na ampe hatma njema .amin

    ReplyDelete
  8. Oh no!..Maskini mama yake..

    Nadhani kama mama, Khadija Kopa anawish ange-undo or angebadili kitu alichofanya: Kumuacha mwanae Zanziba mpaka watu wasiokuwa na dini, wajaa laana kumharibu mwanae kiasi kile.. Yule mtoto aliishia kuwa shoga na nadhani tunajua alisumbuliwa na maradhi gani.

    At the end of the day, mimi siko hapa kumnyooshea kidole marehemu, bali kumpa pole mama yake maana mama kupoteza mtoto (kwa njia yoyote ile) ni very very painful.

    Na kwa Omar, mimi namtakia pumziko la milele. At the end of it all, kama alikuwa at peace na Mola wake, ya duniani kayaacha hapahapa, sasa anayatazama ya huko alipo!..

    Amen!

    ReplyDelete
  9. "Inna lahi waina-lilah rajiun" Maskini! Omar nae alikuwa muimbaji wa taarabu kama mama yake. Apumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  10. M/Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.

    Utaendelea kukumbikwa ktk Mipasho.

    ReplyDelete
  11. UTUMWA BADO UNAENDELEA AFRIKA!
    NOUAKCHOTT, Mauritania (Reuters):

    They do not wear chains, nor are they branded with the mark of their masters, but slaves still exist in Mauritania.

    In the Saharan Islamic state, a centuries-old system of bondage is resisting the rise of democracy in the largely desert former French colony.

    Serving hot mint tea

    Herding camels or goats out in the sun-blasted dunes of the Sahara, or serving hot mint tea to guests in the richly carpeted villas of Nouakchott, Mauritanian slaves servetheir masters and are passed on as family chattels from generation to generation.

    They may number thousands, anti-slavery activists say. A shocking anomaly in the 21st century, this is widely accepted in a racially diverse, hierarchical society dominated by a Moorish elite and a brand of Islam that preaches submission.

    "It's like having sheep or goats. If a woman is a slave, her descendants are slaves," said Boubacar Messaoud, who was born a slave and is now his country's leading anti-slavery campaigner.

    He says a 1981 decree outlawing slavery is a dead letter and slavery is alive in Mauritania, with all its manifestations of non-paid work, punishment, forced sex and other abuses.

    Mauritania's military rulers, who are handing over to civilian rule in democratic elections, shy away from discussing the issue and prefer to talk of "vestiges of slavery".

    Some members of the light-skinned elite which has traditionally ruled the country deny slavery exists at all. Questions about it can draw anger, mistrust and silence.

    But anti-slavery campaigners say the master-slave relationship and its social repercussions are branded into the minds of all Mauritanians, just as class consciousness still haunts social discourse in Britain and other European states.

    "There is slavery in our country, in all of our society. You need laws to eliminate it. The fact people try to hide what exists just complicates things," said Messaoud Ould Boulkheir, a black Mauritanian and descendant of slaves.

    In Nouakchott's sprawling, dirt-poor slums, most of whose inhabitants are black, the testimonies about enduring slavery are repeated, and heartfelt.

    "Yes, it's true," said Abdarahman Ould Mohamed Abd, 52, sitting outside his ramshackle hut. "In the interior of the country, it's the worst. You see it in the way some people treat others. Sometimes, they (the masters) have even killed children," the street vendor added, his own surname meaning 'son of Mohamed Slave'.

    Anti-slavery groups, such as SOS-Slaves run by Messaoud, say the fear and secrecy cloaking the issue make it difficult to bring cases of slavery to light, let alone to court.

    But victims periodically surface, such as Matalla, a black Mauritanian who two years ago escaped from members of a Berber warrior tribe, the Reguibat. They were holding him and his family in the isolated deserts of north-east Mauritania.

    "I was born a slave. All my family, all my ancestors were slaves of that group. My aunt, my brothers are still slaves with them," he said with lowered gaze.

    He told Reuters he herded camels for his masters, ate only leftovers from their table and suffered occasional beatings.

    "I have a scar here," he said, pointing to his right cheekbone, "from where they hit me with a stick."

    Anti-slavery activists say it is impossible to tell how many people remain enslaved in Mauritania, a mineral-rich country twice the size of France whose three million population mixes white and black Moors and black Mauritanians of several ethnic groups.

    Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi and Ahmed Ould Daddah, two white Moor front-runners who yesterday faced off in a presidential run-off, last week pledged they would toughen anti-slavery legislation. But uprooting a tradition which has been core to Mauritania's history may be more difficult than political bluster would suggest.

    Historians say slavery developed in Mauritania from the 7th century, when Arab invaders pushed south into sub-Saharan Africa, bringing Islam which explicitly allowed the enslavement of non-believers.

    This blossomed into a trans-Saharan trade that captured black Africans several centuries before the peak of the European-run Atlantic slave trade. Some historians argue the practice of slavery already existed in black Africa.

    Black Mauritanians tell tales of oppression, victimisation

    ReplyDelete
  12. Kun aina yeyote y aUtumwa Tanzania?
    Nadhani hausegeli ni aina ya Utumwa.Hawa watu hawana haki,wanapigwa, wanabakwa kila kukicha na watoto wa wanaofanyia kazi.Wengi wao wanajifunza kufanya ngono kwao,vile vile baadhi ya Baba wa wenye nyumba ndio vile vile.Vipi nani atasikiliza kilio chao?Nani anatetea maslahi yao?
    Demokrasi iko wapi Tanzania wakati kuna tabaka la watu wanaoishi kama watumwa nchini mwao?Kwa nini htauongelei hili?

    ReplyDelete
  13. Yes slavery is an issue in Africa and we quite overstand that, but... how is this slavery issue relevant to Omar Kopa's death?

    ReplyDelete
  14. Poleni sana wafiwa.....Mungu amlaze mahala pema.

    ReplyDelete
  15. Nawapa pole wafiwa. Kwa sisi wazanzibari mbali ya kumkumbuka kwa uimbaji wake lakini pia atakumbukwa kwa ukwaa wake pia.

    ReplyDelete
  16. Omar Kopa: Mtunzi na mwimba
    taarab atakayekumbukwa daima

    Na Mwandishi Wetu

    MTUNZI na mwimbaji nyota wa taarab wa kikundi cha sanaa za maonyesho cha Tanzania One Theatre (TOT-Plus), Omar Kopa (26) alifariki dunia jana mjini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo mchana Zanzibar.
    Katibu wa TOT Plus, Gasper Tumaini alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, Omar alifariki dunia saa 3:00 asubuhi akiwa nyumbani kwa mama yake, Khadija Omar Kopa, Mwananyamala Komakoma, Dar es Salaam.
    Kifo cha Omar kimetokea wiki mbili baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mwananyamala, ambako alilazwa kutokana na kusumbuliwa na homa za mara kwa mara.
    Taarifa za kifo chake ziliwajaza simanzi kubwa mashabiki wa muziki huo wa Zanzibar, hasa eneo la Kwahani, ambako ndiko alikozaliwa na kukulia. Baadhi ya mashabiki walionekana wakiwa wamekaa vikundi wakipeana taarifa za kifo cha msanii huyo.
    Kabla ya kifo chake, uvumi ulikuwa umezagaa Zanzibar siku mbili zilizopita kwamba Omar amefariki. Taarifa hizo ziliwashtua mashabiki wake wengi, ambao walifika nyumbani kwake kuulizia iwapo zilikuwa kweli. Hiyo ilikuwa mara ya tatu kwa Omar kuzushiwa kifo.
    Katika siku za hivi karibuni, afya ya Omar ilionekana kuzorota. Katika baadhi ya maonyesho ya taarab ya TOT Plus, alishindwa kupanda jukwaani kuimba, hali iliyowapa wasawasi mkubwa wasanii wenzake.
    Omar alikuwa mtoto wa malkia wa muziki huo nchini, Khadija Omar Kopa. Enzi za uhai wake, alikuwa mmoja wa wasanii wenye uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo za taarab. Pia alikuwa mahiri wa kupanga mashairi ya nyimbo na kuweka muziki.
    Watu wengi walikuwa wakidhani kwamba mama yake ndiye alikuwa chachu kwake kuupenda muziki huo, ama pengine kumpa mafunzo ya kuwa mwimbaji mzuri.
    Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa. Katika mahojiano na gazeti la Burudani, ambalo ni gazeti dada la Uhuru, Omar alisema wakati anaanza kujihusisha na muziki huo, hakuna aliyekuwa akifahamu kwa vile hakutaka ndugu zake wajue.
    “Baba yangu hakupenda kabisa nijihusishe na muziki kwa sababu wakati ule alikuwa akinisisitizia sana kuhusu masomo,” alisema Omar katika mahojiano hayo yaliyofanyika Februari, mwaka huu.
    Ijapokuwa alianza kujihusisha na muziki huo tangu akiwa Zanzibar, marehemu Omar alianza kupata umaarufu baada ya kujiunga na TOT Plus mwaka 2002.
    Omar alitunga na kuimba nyimbo nyingi za taarab za TOT Plus, ambazo zilikipandisha chati kikundi hicho. Baadhi ya nyimbo hizo aliimba yeye mwenyewe na nyingine aliwapa wasanii wenzake waimbe, hasa zile zilizotakiwa ziimbwe na waimbaji wa kike.
    Baadhi ya nyimbo zilizompatia umaarufu ni pamoja na ‘Tuko beneti’, ‘Nifagilieni’, ‘Sitaki ushambenga’ na ‘Ebwana ndio.’
    Nyimbo zingine alizotunga, lakini zimeimbwa na waimbaji wengine ni kama vile ‘Huna mpango’ na ‘Wema haupo’, zilizoimbwa na Mwanamtama Amir na Aziza Mkumba.
    Wakati akijiunga na TOT Plus, Omar alikuwa kama Malaika aliyeteremshwa na Mola kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikundi hicho kilichokuwa kimepungua makali yake. Pia alikuwa kama vile ameitwa kwa ajili ya kumuongezea nguvu mama yake Khadija.

    Alijiunga vipi na TOT Plus?
    Mwaka 2002 alifika Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria harusi ya mama yake. Baada ya harusi kumalizika, alikwenda kwenye onyesho la TOT Plus.
    Akiwa ukumbini, kikundi hicho kiliporomosha kibao cha ‘Huyu ni wangu’, ambacho kwa kawaida huimbwa na Abdu Misambano. Omar aliombwa apande jukwaani kuimba kibao hicho.
    Baada ya kuimba beti kadhaa za wimbo huo, mashabiki waliohudhuria onyesho hilo walilipuka mayowe ya kumshangilia kutokana na kumudu vyema kuuimba. Ilikuwa vigumu kuitofautisha sauti yake na ya Misambano.
    Mara baada ya kumaliza kuimba wimbo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TOT Plus, John Komba alimfuata Omar na kummwagia sifa kemkem, kisha alimuomba ajiunge na kikundi hicho ili awe mmoja wa waimbaji taarab.
    Siku chache baada ya kujiunga na kikundi hicho, aliibuka na kibao cha ‘Tuko beneti’. Kibao hicho kilibeba albamu ya kwanza aliyorekodi na kikundi hicho.
    Moja ya sifa alizokuwa nazo Omar ni kutunga nyimbo zake kwa kipindi kifupi. Alikuwa na uwezo wa kutunga nyimbo na kuikamilisha kwa siku moja, kitu ambacho kwa kawaida huwa ni kigumu kwa wasanii wengine.
    “Kwa mfano, wimbo wangu wa ‘Nipepee’, niliomshirikisha mama yangu, niliutunga kuanzia asubuhi, ilipofika saa 10 jioni, nikaingia studio kuurekodi,” alisema wakati wa uhai wake.
    Kipaji cha Omar cha kuimba taarab kilitokana na kufuatilia kwake masomo ya Quraan.
    Kabla ya kukutwa na mauti, Omar alikuwa akifanya mipango ya kurekodi albamu yake binafsi ya kwanza ya mahadhi ya mduara yenye nyimbo nne. Nyimbo alizotarajia kuzirekodi ni ‘Raha ya Unguja’, ‘Ngoma ya kinu’, ‘Namuenzi mama’ na ‘Ukweli haufichiki’.
    Alitarajia kurekodi albamu hiyo katika studio za Sophia Record kwa kuwashirikisha wasanii Mohamed Mbange, Samuel Mshana, Aziza Abdul, Khadija na Ababuu.
    Hakika daima Omar ataendelea kukumbukwa na wapenzi wengi wa taarab.

    ReplyDelete
  17. Michuzi na wewe unatupa habari zisizo za kweli. Unasema Marehmu alikuwa na miaka 23 wakati alikuwa ana miaka 26. Vile vile unasema kuwa aliugua muda mfupi wakati inajulikana alikuwa "mgonjwa" siku nyingi. Soma habari chini ziliandikwa na waandishi walioenda shule.

    Omar Kopa: Mtunzi na mwimba

  18. Poleni sana wafiwa

    ReplyDelete
  19. Mii naona umri unatatizo Ukisoma hebu soma na hapa,kuna utata kwenye habari hizi ila kinacho match ni kwamba huyu bwana ametutoka

    Mwimbaji taarab Omary Kopa afariki

    MWIMBAJI nyota wa muziki wa taarab wa TOT Plus, Omary Yusuf 'Kopa' (27) amefariki jana saa 5.00 asubuhi nyumbani kwao Mwananyamala baada ya kuugua ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu.

    Msanii huyo, ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha "Sitaki Ushambenga," alikuwa pia akisumbuliwa na homa ya mapafu na anatarajiwa kuzikwa leo kisiwani Zanzibar.

    Watu wengi walifurika nyumbani kwa msanii huyo, ambaye ni mtoto wa Khadija Kopa, ambaye pia ni mwimbaji maarufu wa muziki wa taarab na hasa miondoko ya Mipasho, kumuaga Omary, ambaye aliibukia kuwa mwimbaji tegemeo wa kikundi cha TOT Plus baada ya kujiunga mwaka 2002.

    Mdogo wa marehemu, Ismail Kibwana alisema kaka yake alifariki wakati wakijiandaa kumpeleka hospitali baada ya kuzidiwa.

    "Omary alikuwa anaumwa kwa kipindi kirefu sasa, na alikuwa anaugulia hapa hapa nyumbani," aliserma mdogo huyo ambaye alisema yeye na marehemu ni watoto wa Khadija, lakini wanatofautiana mzazi wa kiume.

    Mwili wa marehemu Omary umesafirishwa jana saa 10.00 kupelekwa Zanzibar na unatarajiwa kuzikwa leo kwenye makaburi ya Mwanakwerekwe.

    Omary alianzia muziki kwenye kundi la taarab la G- Clef linalomilikiwa na mtoto wa marehemu Issa Matona.

    Baadhi ya nyimbo alizotunga ni "Utalijua jiji", "Mwanamke Mambo", ambao aliimba mama yake Khadija, "Nimemrithia", na "Sitaki Ushambenga".

    ReplyDelete
  20. Ni kazi ya mungu hakuna makosa, mungu amlaze mahali pema peponi. Kwa wapenzi wa mipasho wataendelea kumkumbuka.

    Nimesoma maoni ya watu hapo juu, nafikiri Michuzi wakati mwingine usipotoshe wasomaji. Tukianzia na umri wa omar-mimi sijui nani mkweli kati yako na mwandishi mwingine aliyeandika maelezo kwa urefu kabisa. Pili nafikiri ugonjwa ni ugonjwa tu unabaki kuwa na sifa ile ile, hivyo si vyema kuficha mtu alipatwa na ugonjwa gani, ndo maana ya kuelimishana kwani habari yako imejaa kificho kama Anon wa Monday, March 26, 2007 10:27:00 PM alivyosema. Lakini ili kuwa honest bora ungeandika chanzo cha kifo chake binafsi sijakielewa. Tatu nafikiri wakati umefika tukemee ushoga, hata dini zetu zinakemea. Anon wa Monday, March 26, 2007 4:54:00 PM kasema ukweli mtupu.

    Michuzi endelea kutupa update za nyumbani kwa ufasaha usiogope jamii bali elimisha jamii.

    ReplyDelete
  21. Michuzi, Mimi ni anonymous wa March 26, 2007 5:09:00 PM. Tupo kwenye majonzi, sasa hizi habari za slavery za huyu Mountais and Valleys zinaingiaje hapa kwenye rambirambi?.Tunaomba uzidelete bana, kwa niaba ya wote!

    ReplyDelete
  22. Inasikitisha kuona vijana wadogo hivi wanakufa kabla hata ya kuanza maisha. Kwa kweli ni pigo kuwa sana tena sana haswa katika sanaa ya taarab, kijana alikuwa anakuja kwa spidi kali. Pole sana mama na familia yako yote. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Marehemu Kopa. We will miss you - especially in JIKONI PARTIES

    ReplyDelete
  23. Labda umri huu ni sahihi.

    Naye mama yake mzazi ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Khadija Kopa, alisema kuwa Omar (25) alizaliwa mwaka 1982 Zanzibar, pia aliwahi kuoa na ameacha mtoto mmoja Rukia, mwenye umri wa miaka tisa.

    Chanzo-Tanzania Daima-27/03/2007

    ReplyDelete
  24. When I was just a little girl I asked my mohter what would I be will be pretty will I be rich? that she said to me: "Hey sarah whatever will be will be the future is not for us to see.....

    If only one could control events, if only one could stop things to happen, if only one could see the future, if only.... if only

    The word WHY will always be there because nobody will tell u why things should be as they are....

    Mungu akupe nguvu mama Kopa u r the only one who knows what u have gonne thru do not ask urself WHY? for that is why there is God to answer "THE WHY!!"

    Omar rip

    ReplyDelete
  25. siamini!nilikuwa nampenda sana huyu muimbaji,alikuwa anasauti iliyotulia na kumfanya mtu asinzie.
    MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PANAPOSTAHILI.
    MANYUNYU

    ReplyDelete
  26. inavyoeleweka khadija kopa kazaliwa 1970 sijui huyo alimzaa katika umri gani?

    ReplyDelete
  27. Misupu NUNGANA NA ANNOY WA machi 27 8:15am HUYU MOUNTAIN VALLEY COMMENT ZAKE ZINATAKIWA ZITOLEWE AU ZITAFUTIWE SEHEMU MUAFAKA. MAANA HII NI SEHEMU YA KUWAFARIJI WAFIWA NA KUTOA RAMBIRAMBI KWA WAFIWA.KAMA YEYE ANAHOJA AFANYE KAMA WANAVYOFANYA WENZAKE AKUTUMIE ILI WEWE UIFANYE HOJA RASMI YA KUJADILIWA. AU ANAOGOPA UTAPATA WEWE UJIKO? (finyu mind).
    Malkia wa taarab Mwenyenzi Mungu ndio aliokupa na yeye ametwaa iliyobaki tumshukuru Mungu. Jipe moyo maana huu ni msiba wa milele. Na kama alivyosema annoy wa hapo juu, usibaki kumuuliza Mungu kwanini? kwani tunaamini kuwa kilichopangwa na mungu binadamu hawezi kukibadili
    R.I.P Omary

    ReplyDelete
  28. Hebu tumwache marehemu alale pema peponi. Hivi vitu vya kusema Michuzi kakosea miaka linatuhusu nini?
    Sasa wengine Hadija Coppa kazaoliwa 1970, mtoto wake amefariki na umri 23, 25, 26, or 27 ??!! Marehemu ameacha mtoto umri miaka 9 ??!! Jamani hebu tuwaachie wenyewe kwa wakati huu mgumu. Age is nothing but a number.

    ReplyDelete
  29. Yaani nilikuwa sijui kama mtoto wa malkia amefariki jamaaaaaaaaaani poleni sana wafiwa! sasa cha kushangaza ni kuwa huyu Mt Valley kutoa maoni yasiohusiana na maombolezaji maanaake nini? anamaana gani kusema kuwa mbona hili tatizo tunalifumbia macho? we mt valley mlughalugha wa wapi usiokuwa na utu wala ubinadamu? unadhani nani atakuchukulia serious kuweka hoja yako ktk rambirambi za Omar Kopa? IDIOT

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...