ukiondoa kupiga mbonji hobi ingine ya wanadumila ni kula.
kuna habari za mvunjiko kwamba huko ughaibuni watu wamekamatwa kwa kukosa makaratasi. hebu bofya hapa dada chemi akupe maelezo zaidi...
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
HII HABARI INATUTISHA TUSIO NA MAKARATASI MZEE TUKIMBILIE WAPI?
ReplyDeleteOooh, napajua sana hapo shopping mall iitwayo CITY CENTER bwana michuzi, panapendeza kweli!!
ReplyDeleteWanakula hivyo wakati kuna joto hivyo. Duh hii kali.
ReplyDeleteYaani wamekuwa deported kwa ndege. Jamani nawaonea wivu wamefaidi! Wengi waliingia Marekani kwa kupitia njia za Panya kwa miguu na sasa wamerudi wamepanda ndege, raha ilioje hiyo.
ReplyDeleteSijui na mimi nije huko kwa miguu wanirudishe kwa ndege maana sijawahi panda ndege.
Bila shaka ndugu zao waliwapokea kama wafalme Airport.
Chonde chonde msio na makaratasi, jiwekeni vizuri msijemkajikuta bongo bila kutarajia.
ReplyDeleteJaribu Mall of Emirates
ReplyDeleteOoooh! Chemi, kiswahili kimeanza kukupotea!
ReplyDelete'... duka iliyokuwa ...'
Hicho sio kiswahili cha mTZ mzawa!!!
Unazikumbuka ngeli za majina ktk sarufi ya Kiswahili?
Michuzi nimesoma blog ya Dada Chemi, Ni nzuri japo hayupo up to date kama wewe. Ila kimoja nimekifurahia ni kwamba anajibu hoja za wanablog wake, tofauti na wewe, unaulizwa mara nyingi lakini hujibu chochote, Inaleta raha kwani inaonyesha Chemi anasoma almost maoni yote ya watu wanaotembelea blog yake. Ile ku'take' trouble ya kujibu pale anapoona panahijaji majibu au malelezo.
ReplyDeleteSasa huyo Chemi anawatisha wasio na makaratasi, au anawaambia wayatafute. Mbona ujumbe wenyewe hauko clear? Nini lengo la kuweka hii info. hapa? Kama yeye anayo, asijaribu ku intimidate wasio nayo. Kila mtu hapa kaja kwa malengo yake, tuache kupeana pressure. Makaratasi hayaokotwi, ni procedure ndefu, na ngumu zaidi kwa wageni wakike/wasichana.
ReplyDeleteAisei Michuzi. Kwanza asante kwa kutoa taarifa hapa kwenye blog. Leo ndo nimeona hapa, nilikuwa na computer problems. Kwa kweli hii jambo la kukamatwa kwa hao wafanyakazi insikitisha kweli. Na sasa hivi hawasiti ku-deport watu wasio na makaratasi, tunaita 'asante bin laden 9/11'. Kuna waafrika nao wamekuwa deported, lakini huwa husikii habari zao kwa vile hawana vyama kama hao wa kutoka Amerika ya Kusini ya kutetea haki zao.
ReplyDeleteKwa anonymous wa 4:12 PM aliyesema nimeanza kusahau kiswahili. Sikatai kabisa. Nimekaa nje ya TZ miaka mingi na naona hata slangs zimebadilika.