jk akifungua kikao cha wakuu wa nchi za sadc leo huku rais robert mugabe wa zimbabwe akitega sikio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Once at a conference, three scientists: an American, a German and a
    Zimbabwean, were talking and bragging about the technological advances
    their respective countries have achieved in the field of medicine.

    Says the American, "In Washington, there was a baby boy born without
    forearms, so we attached artificial forearms on him. And now that he is
    grown, he has become an Olympic boxer and a gold medalist at that!"

    The German replied, "That's nothing to what we have done back in
    Berlin, there was a baby girl born without legs, we attached artificial
    legs on her, she is 3 times marathon gold medalist in the Olympics!!"

    The Zimbwabwean interjected laughingly, "Is that all you have done,
    just gold medalist? In Harare, we had a baby boy born without a head!
    We attached a coconut to his neck and he is now the president!!!

    ReplyDelete
  2. Hivi!, Matatizo yetu nani atayatatua?
    au mpaka na sisi tuwe na Civil war ndio tutaona umuhimu wa kutatua ya kwetu kwanza?

    Huyu JK kaniboa sana kwa kuitisha kikao (Kwa hela ya wapiga kura) kutatua matatizo ya watu wa nchi jirani. na kuleta usumbufu kwenye system ya transport ya mji wa Dar.

    Next Time akafanyie vikao vyake Arusha- Ngurdoto. Ambako Vikao kama hivi havitaathiri shughuli za wananchi. Kwani Ngurdoto ipo nje ya Mji na ipo njia ya kwenda Airport ya KIA. usumbufu utakuwa mdogo ukilinganisha na kikao kikiwa Dar.

    Mimi nimeshaanza kuona kuwa JK hana lolote zaidi ya usanii. Ni Mr. MISIFA... a typical nature ya watu wa pwani...

    ReplyDelete
  3. Jk na wengine mnaowapatia wawekezaji Land/mali bila yakuona mbele angalieni huyobwana wanavyomyayasa sasa,halafu ugomvi tunauamua wenyewe. Wetu atauamua nani ?

    ReplyDelete
  4. Mugabe ndio Jogoo la Africa. Wengine wanawaogopa wazungu kama nini. Saa nyingine lazima kugangamala. Wanamlaumu eti amekaa madarakani muda mrefu mbona Tony blair kakaa sana wazungu hawamsemi? Ghadaffi, Hosni Mubaraka, Omar Bongo, nk. tukitaja wachache mbona hawawekewi vikwazo? Kisa Mugabe kanyang'anya shamba la mzungu ndio anaonekana mbaya! Mwacheni Jogoo awike bwana.

    ReplyDelete
  5. mugabe hajanyang'anya shamba la mzungu... kachukua shamba lake alilokuwa amenyang'anywa na hao wageni

    ReplyDelete
  6. jogoo anawika wakati watu wake wanakufa njaa?we anonymous unachekesha sana.

    ReplyDelete
  7. Tujengeni hoja sio jazba. Sisemi kuwa JK hana mabaya aliyonayo, but in this case namvulia kofia. Ni mwenyekiti wa kamati fulani huko SADC, na hivyo ilikuwa muhimu kwake kuitisha kikao kama hiki. It was all over the media. Yanayotokea Zimbabwe yanasababishwa na mamluki na wazungu wao. Hivi kweli, nani yuko tayari dunia hii kuruhusu walowezi kumiliki asilimia 70 ya ardhi yote bora katika nchi yake? Tutaendelea kuwa watumwa wao hadi lini? Sie weusi tungemiliki njia zote za uchumi za wazungu, wangekubali? Mugabe kachelewa tu na ni kwa sababu za kihistoria, kuwa Zimbabwe ilipata uhuru wa bendera miaka ya 80s. Babu yetu Mwl. Nyerere mbona alishafanya hivyo hivyo. Hiyo inflation inayodaiwa ya 1800% ni sababu ya nchi za magharibi kuweka vikwazo vya kiuchumi kwa Zimbabwe. Kwa hiyo sasa wakoloni wako wanachekelea, it worked. Mugabe anachemsha anapopiga wapinzani, dawa ni moja tu, akutane na Vladmir Putin amuulize yeye huwafanya nini. Mtaikumbuka Polonium 210 ipo. Hiyo ndo kiboko, sio kuwapiga hadharani. Wazungu si watu, wana diaspora mlobahatika kukaa na hawa watu mtakubali wazungu ni wanyama. Hawako wazi na society yao iko on the blink of loosing its humanity. They are so exploitative. Nakumbuka mwalimu wangu wa DS, Dr. Kahwa, alikua anafundisha mambo mpaka leo nimekuja kuyafikiria na kuona ni kweli. Wakati ule niliona ni mzushi tu. Katika darasa lake la political economy of capitalism, alisema kuwa, hata mikopo inayotolewa na wazungu ni donor-oriented kuendeleza unyonyaji. pesa zinatolewa katika kujenga jamii katika mambo yasiyo ya uzalishaji, ni asilimia ndogo sana ya mikopo inaenda kwa miradi ya maendeleo. i.e. kujenga kiwanda kwa mfano, bali zinaenda katika kutetea demokrasia, gender balance, utawala bora etc etc. Na hata wakikupa mkopo wa kujenga say, kitulo dairy farm, wanajenga kiwanda cha capacity ya ng'ombe 200.000 na wanajua huwezi fika huko, unatunza ng'ombe 10.000, in the end the thing inacollapse wakiondoka. We are in a viscious cycle, maana baada ya hapo wana point kuwa walipoondoka mradi umeuwawa na corruption. They have no humanity at all. Imagine, ni wangapi walishanyanyaswa katika historia na kuombwa msamaha. Leo hii kwa sababu ni waafrika tulifanywa makoloni na kunyang'anywa raslimali zetu, na pia kuuzwa kama bidhaa kwa mamilioni yetu wakati wa utumwa in exchange of alcohol, beads and money, hakuna hata mzungu mmoja ameomba msamaha kwa hayo. Mugabe you are right, ila fanya taratibu, uma na kupuliza, watakukaba koo kwa kuwapiga wapinzani na kuacha suala la msingi. Wanaimba inflation walioileta wao. Sasa ina maana waafrika wanataka Mugabe arudishe mashamba? Mwafrika gani atafurahia hili? JK initiative was a good one, na sawa sawa wakampa mzee Mbeki kuwa mwakilishi katika kusuluhisha hili, maana wazungu wanamuogopa kama nini. Ana rungu la economic powerhouse ya Africa. Aluta continua JK.

    ReplyDelete
  8. Suala kubwa hapa ni ARDHI, ndiyo nakubali kabisa ni haki kwa hilo, lakini je hapa kwetu TANZANIA/TANGANYIKA ni vipi Raisi anashughulikia kivitendo? Kule wazo-hili TEGETA polisi wanapiga watu kwenye ardhi yao..,Bagamoyo kwao na KIKWETE watu wamepighwa na kufa sababu ya wawekezaji?

    Tofauti ni nini kati ya hawa na Wazungu wa ZIMBABWE?

    ReplyDelete
  9. anonymous wa 9:31 am,
    1) umetoa hoja iliyoenda shule. Hata mie nakuunga mkono kuwa Mugabe anachemsha kwa kumdunda Morgan Tsvangarai na wapinzani wengine. Inaonekana anaendesha ubabe na kutoa "news" kwa mataifa ya magharibi.
    2) Swala la Mashamba-ni haki kuyagawana kwa walio wengi sio kuwaachia walowezi wachache. Tatizo linakuja kama unachukua mashamba na kugawia watu ambao hujawatayarisha kuyatumia kikamilifu. Tunaambiwa kuwa sasa hivi Zimbabwe kuna njaa sana kutokana na hili zoezi-sijui kama ni kweli au ni propaganda za BBC na vyombo vya habari vya magharibi.
    3) Mie siungi mkono viongozi kukaa sana madarakani-nchi yeyote duniani. Naipongeza Tanzania kwa kuweka katiba inayolinda kipindi ambacho mtu anaweza kuwa raisi (miaka kumi inatosha!). Huyu Mugabe amekaa mno bwana-halafu amezeeka. Mbona mwenzie Mandela alikaa kidogo akaachia ngazi?? Ukomavu wa kisiasa lazima uandamane na kung'atuka kutoka madarakani katika muda muafaka.

    ReplyDelete
  10. Wewe annoymous wa hapa juu uliondika hoja ndefu kuhusu Zimbabwe na wazungu.usichukulie vitu kwa ujumla(generalised) sio sahihi kusema Wazungu ni wanyama.ina maana ni wote?Sisi weusi wote poa sio?matatizo mengi ya Waafrika kwa asilimia kubwa yanaletwa na sisi wenyewe waafrika ,tuna unyama wetu pia.fikiria hilo na ulifanyie kazi.usitoe comment za kiracist(kibaguzi).Huyo Mwalimu wako alikudanya hapa Mlimani corruption ipo na WaTanzania wenyewe kwa asilimia kubwa waliua uchumi na viwanda.Uvivu na kutowajibika.Tuangalie matatizo yetu na sio kutafuta mchawi wakati wote.Kuhusu utumwa kuna baadhi ya mataifa ndio yalioshiriki na term wazungu kutumika sio sahihi.Kuna WaFinnish,Waswede,Waiceland wote wazungu.ukitumia wazungu ina maana unawajumlisha wote.ila tumia wadutch,wareno,waingereza,waarabu.Na kumbuka Waafrika waliwauliza ndugu zao,na washirikiana na hao wazungu.Sasa sio wanyama?Baadhi ya weusi uliwaambia unatoka Africa wanakukumbusha historia,kwa nini nyie mlisaidia kutuuza?wanauliza.
    Kuhusu suala la ardhi ni haki ya Wazimbabwe weusi kuwa na ardhi yao,ilikuwa lazima kugawia sawa.ila Mugabe anakandamiza upinzani na kufanya kila alowezalo kubakia kwenye madaraka(viongozi wengi wa kiafrika ndio walivyo)ingawa Tanzania kuna mfumo mzuri wa kuachiana madaraka.Nadhani kulikuwa na njia bora zaidi ya kuyagawa hao mashamba.yangegawia kutokana na uwezo wa mtu kuyalima,sijui kama ni logic kumpa mtu shamba la hekari 100 wakati mtu hana uwezo hata wa kulima hekari 2.kumbuka hiyo ardhi unayompa mtu likuwa inalimwa.Lingine la kujiuliza kwa nini huu uamuzi ulichelewa.Wazimbabwe alipigana kwa ajili ya ardhi ambayo ilikuwa imenyang'anywa.Kwa nini baada ya uhuru walikaa kimya?kuna mambo mengi yanasemwa kwa Mugabe kukaa kimya,Na ghafla kuanzisha hiyo process.

    ReplyDelete
  11. mugabe is useless, kwanza hapo hategi sikio kalala

    ReplyDelete
  12. Umri Miaka 83, urais miaka 27, mtu gani huyu mbinafsi ambaye hataki kuachia wengine !!

    ReplyDelete
  13. Pilipili yaliwa shamba nyie yawahusu nini? waacheni wazimbabwe waamue wenyewe maana wamekuwa vilaza mpaka basi waache kwanza wakione hii haihusiani na mambo ya Bongo huyu mchovu Kikwete anapoteza muda bure wa nchi anatakiwa atatue issues za bongo kama rada deals,RVF,consititution changes na mengineyo si uthenge huu!!kuna viongozi kibao wamekaa more than 20 yrs Africa mbona hatusemi(Mu7,Omari Bongo,Ghadafi,Mubarak)....SOON A LATER THE ZIMBWABWEANS WILL DETERMINE THEIR OWN FUTURE!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...