shoo kamambe ya kanga na vitenge huko uswidi.
mbongo imam na rafikiye mswidi aitwayed karin pamoja na dada yake imama aitwaye bonita aliye bongo wana kampuni ndogo iitwayo watatu textil inayonunua kanga na vitenge bongo na kuuza uswidi na nchi zingine. Majuzi walishiriki kwenye maonesho ya "mammapappabarn" (kwa kiswahili "MamaBabaMtoto" ) yaliyofanyika mjini karlstad ni harakati zao za kuwaeleza na kuwafundisha waswidi njia bora na rahisi ya kubeba watoto kwa kutumia vitenge na kanga. nimeambiwa shoo ilifana sana na waswidi wengi wamekubali kwamba kanga na vitenge ndo vyenyewe kwa shughuli hiyo.
bofya hapo chini kwa kuona picha za maonesho hayo.<http://www.watatu.com/Shop/Application/Private/showeng.htm>
ama bofya hapo chini ili kuingia dukani kwao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Naona kwa kweli wabongo huko unyamwezini wanaendelea kuipeperusha vizuri bendera ya taifa la watu waungwana hii inapendeza sana na najua lazima huko watakuwa wanapata wateja wa kutosha braza michuzi wape tafu ya kutosha

    ReplyDelete
  2. Only if our girls of today could be proud of such things rather than dressing up all Western and forgeting all that is their own culture. Khanga is beautiful

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...