Home
Unlabelled
kuwasili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wameelewa kuwa kuwa local star na kuwa international star ni vitu viwili tofauti.
ReplyDeleteWachezaji wanarudi jeuri zao za kujiona nyota zikiwa hoi.Hakuna cha Athman Iddi wala Mwaikimba.Sifa zao mwisho Mwakaleli na Kimanzichana hazivuki mipaka ya hapo.
Wachezaji Waache kiburi wajinoe zaidi.Kujivunia kuwa Yanga Au simba wanakutaka sana si kigezo cha kuwa kiwango chako cha kucheza kiko juu.Inawezekana ukawa kama anayepata markisi 10 ya mia kwenye darasa la wajinga akawa kinara.
Wachezaji wasione kuwa yanga au simba kuwa ni kiwango ambacho ni cha kujivunia sana na mchezaji kujiona kafika kileleni na kudengua kama mwali sababu eti kila timu inamtaka.Kazi bado kubwa kama wanataka kuchezea klabu kubwa zinazolipa mamilioni kwa wachezaji ULAYA.Watumie yanga na simba kama daraja la kujenga uwezo wao kuelekea timu kubwa ulaya badala ya kuzitumia kama sehemu ya kudengua kama wali wasenge hasa wakati wa msimu wa usajili.
Big up staz!Victor Costa nakuona mzee!una kiwango cha juu,basi tu mpira unadunda.keep it up boyz,ushindi wetu marudiano.Inabidi hawa Senegal tukirudiana mechi ianze saa nane na nusu,wachomwe jua watachoka haraka,halafu na humidity ya Dar ilivyo juu tunajipigia kama tano hv kipindi cha pili.
ReplyDeletemsikate tamaa washkaji sisi bado tupo nanyinyi
ReplyDeleteMsikate Tamaa, Tuna imani na nyinyi.
ReplyDeleteTusawazishe makosa ili tusiyarudie.
We pumbavu acha kuongea kama huna akili, izo biashara za usimba na uyanga huko huko kwenu, hapa tunaangalia utaifa,tena inawezekana wewe sio raia,coz hakuna mtanzania anaeongea ujinga kama wako pumbavu kabisa wewe.
ReplyDeletemaoni haya ni kwa ajili ya huyo jamaa aliecoment juu kabisa.
Mambo vipi Michuzi,hope uko pwaa,
ReplyDeletenilikuwa na machache ambayo nilitaka kuwaambia Watanzania wenzangu kuhusiana na timu yetu ya Taifa.
Kwanza nimewasoma Watanzania nikagundua kuwa tatizo moja kwao huwa wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo haliwezekani.
Nakumbuka wakati Marcio ameshuka TZ Alisema kitu kimoja kwamba tusitarajie mabadiliko katika muda mfupi,tunahitaji maandalizi ya muda mrefu, na ndio maana hata Serikali iliamua kugharimia ujio wa Makocha wawili wakubwa Nikiwa namaanisha Marcio kwa ajili ya Timu Wakubwa na Tinoso kwa ajili ya kukuza vipaji vya chipukizi.
Serikali ililifaham hilo na ndio maana ikafanya hivyo, waswahili wanakwambia mkunje samaki angali mbichi, nikiwa na maana huwezi ukamfundisha hii leo Mwaikimba kulenga gori kama mfumo wetu wa soka haukutoa nafasi hiyo kwa Mwaikimba wakati alipokuwa mdogo huko Mbeya.
Sio Mnazungumza Tu kama Wapumbavu kutoa lawama zisizo na msingi kwa Timu yetu ya Taifa ambayo ina muda mfupi toka ipate Kocha ambae hapangiwi Timu na Mtu zaidi ya kuangalia uwezo wa Wachezaji Wetu.
Nataka Niwakumbushe Watanzani Wenzangu kuwa, Timu Kwa Kiasi kikubwa imebadilika,Stars iliyocheza na Burkinafaso pia Msumbijibi si Stars iliyocheza na Senegal coz kama ingekuwa ni ile tungefungwa zaidi ya Goli Nane.
Watanzania Wenzangu naomba tusipeleke lawama kwa yoyote yule,tufaham Stars walijitahidi juu ya uwezo wao,na tufaham hata Wadau pamoja na Serikali wanajitahidi ili kuhakikisha na sisi tunakuwa Gumzo katika soka duniani,tutoe nafasi naamini mabadiliko yatakuja lakini si muda mfupi.
Na mwisho naomba Mtu kabla hajatoa maoni yake yasiyo na kichwa wala Miguu,ajaribu kutafuta historia za Wenzetu walianzaje mpaka kufikia hapo walipo.
Dada Mariam Hassan nina wasiwasi na uraia wako::Wewe ni mtanzania kweli?::Maana naona hapo unasema Watanzania wanapenda mabadiliko ya haraka.... Kwa mtazamo wangu hapo ushajitoa ktk utanzania
ReplyDeleteKocha mzuri lakini wachezaji ndiyo hivyo mwalimu akifundisha wao wanakuwa wanawaza posho baada ya mazoezi na mechi badala ya kuzingatia mafunzo wanayopewa.
ReplyDeleteWachezaji waache utoto na mizaha mazoezini.Hiyo kazi ya mpira ni kazi kama kazi zingine mtu anatakiwa kuwa serious hasa.
Ndio maana unaona wachezaji wa Senegali walikuwa very serious hata walipokuwa wakiingia uwanjani tofauti na wa kwetu ambao huingia kwa mikogo utafikiri ma-miss Utalii.Hwawaingii kikakamavu kabisa!!!
Mimi nina hasira umeme ulikuwa hakuna ikabidi ninunue betri Shs.1600.Nimekula hasara betri zangu kusikiliza mechi redioni.
Timu imekwenda badala ya kuongozana na wataalamu wa soka kwenye kamati ya ufundi,timu imeongozana na vizee vishirikina vitapeli vya Bagamoyo abavyo havina lolote zaidi ya kuganga njaa na ubwabwa kwenye Maulidi.Vimwanga gani hivyo vinapanda Ndege kwenda Senegal? Kama kweli vimwanga si vingeenda na usafiri wa Ungo? Mwanga akiwa kwenye misheni hapandi gari,wala ndege.Hivyo ni vitapeli tu.
Michuzi nina hasira navyo Eti vilisema tutafunga mbili kavu.Ona sasa tumefungwa goli nne bila.Viambieni virudishe nauli vinginevyo Said Mwema vibane hadi vinye.Hupo ni utapeli wa kuaminiwa.