"....jamani tumefungwa, jamaa walituzidi kimchezo, lakini tusikatishwe tamaa, jamaa walitutaimu dakika tano za mwanzo za kipindi cha pili wakatupiga bao.... wenzetu wameanza kujiandaa toka utotoni na sie mchakato huo ambao tumeuanza tuuendeleze na mshikamano udumu. tutafanikiwa tu. nafurahi kuona wabongo bado mko nyuma ya timu yetu na inatia moyo kukuta waziri kaja kutupokea..."anasema kocha maximo baada ya kutua leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Oyaaa Maximo kaza buti ndugu yangu, wabongo tuko pamoja nawe na wachezaji wote wa Stars! Hao Senegal wamewekeza kwenye soka kwa zaidi ya miaka kumi sasa mpaka kufikia hapo tulipo. Kwa hiyo sisi bado tuko kwenye mstari, morali wa Watanzania wapenda soka uko pale pale na wadhamini twawaomba wasife moyo!

    Ghana tutakwenda tu, kama wao wameshinda kwao, sisi kwetu pia tutashinda! Tuna mechi mbili za nyumbani so far!

    Taifa Stars oyeeee! Ila wabongo usiku wa juzi tungeshinda sijui ingekuwaje maana baa zilijaa watu na mabendera ya taifa! Angeweza kufa mtu kwenye ajali za barabarani! Khaa kweli wabongo tunapenda sana soka

    ReplyDelete
  2. mambo yaliyotupata kwenye soka ni mambo ya kawaida, hakuna mtu anampeleka mwanae shule ili akafeli ndio maana tulikuwa na matumaini ya kufanay vizuri lakini wenzetu wametumia sana uzoefu waliokuwa nao jambo ambalo lipo hata ulaya timu kubwa nyingi zinapopambana na timu ndogo huwa zinashinda kwa uzoefu, big up maximo kuhiku ni kuendelea kujipanga zaidi nafasi bado tunayo

    ReplyDelete
  3. Mapambano yataendelea tu. Najua mabeki wana kazi ndogo tu ya kurekebisha makosa. Tatizo letu kubwa ni kutafuta washambuliaji nguli zaidi. Ila nafagilia sana midfield yetu mambo si mabaya sana pale.

    ReplyDelete
  4. Hard at it guyz! To 'em (Senegalese) was a purely ''do or die'' game. Any loss or draw was leading dem 2 hell. There was no way out other than ''Jihadizing'' dat match.
    It doesn't matter either wether this was against our Taifa Heroes or Ericsonn's England. This was their FULL SQUAD as they were supposed to win by either means.

    With my poor French knowledge, a plan was according to their coach thru their internal media, to surprise us in the first 10 minutes, a plan dat couldn't materialize up to 38th minute.

    That was a world cup squad against poor and un-experienced Taifa Stars whose group leadership for couple of months has been amazing everybody!
    Think we need extra two matches of the same kind with either Egypt or Cameroon before facing these giants again for more tough exposure.
    It was good and hope we gained something through this match. Now Marcio Maximo know exactly where to rectify..
    BRAVO TAIFA STAAZ, Bravo Tanzania..Tuko Pamoja..

    ReplyDelete
  5. Hapa pia inabidi tujiulize Umuhimu wa ziara ya Real Madrid.Pesa zote hizo tungewekeza kwa vijana ili baada ya miaka miwili tuweze nasi cheka lasivyo tutabaki na matumaini kibao.
    Tumpe kocha wa vijana sapoti ya kutosha Real Madrid hatuitaki wabaki huko kwani hata siku hizi haina mvuto.

    ReplyDelete
  6. Binafsi nina imani na Maximo.
    kikuibwa kinachonipa matumaini nae ni kwamba Wachezaji wana imani nae pia.

    Tumpe sappoti ili Bongo na sisi tung'ae kwenye soka.

    Bado sipati picha ingekuwa vipikama Bongo tungewafunga Senegali ile Jumamosi. Manake ile mechi ilirudisha uzalendo kwa watu wengi sana. inatia imani sana kuona hali ile.

    ReplyDelete
  7. Michuzi,
    Nimekuona na kukusikia ukiinguruma kwenye luninga leo usiku. Hoja zako ni za msingi sana kuhusu visheni ya kandanda hususan soka ya vijana. Ukikutana na JK mwambie kama ulivyoongea kwenye luninga!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...