napata lanchi na wadau toka ukerewe leo site gaden. siku hizi kula imekuwa ishu bongo. ukiagizia nyama unatahadharishwa na lifti vale, kuku; mafua ya ndege, samaki nao noma kwani wengine hupakwa mafuta ya kuhifadhia maiti ili wasioze. isitoshe maharagwe nayo nasikia yatawekewa zengwe wakati wowote kuanzia sasa ati kwa sababu pembejeo inayotumika ni kali maradufu hivyo inatia kiungulia. mchicha na kisamvu kadhalika. mbolea ya nanihii ya wafungwa eti ina walakini kutokana na kuzidi magadi ilimradi balaa tupu. waswahili wanasema kufa hatufi ila cha moto twakiona...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. nashukurru kwa ufafanuzi wa msosi,lakin tisa kumi mie bado nafagilia msosi wa bongo bwana,we huku ughaibuni kila kti kimetiwa dawa,yaani embe linadungwa dawa ili liive hali kadhalika chungwa yaani havina ladha kabisa,kuku ndo usiseme wanachomwa sindano kwenye mabawa ili wakue haraka basi hofu tupu ya cancer,aah jamani bongo utakula hata mlenda na sembe na dagaa siku imeenda.

    ReplyDelete
  2. aah basi mi niletee cocacola.... Do! muhudumu kasema inaweza kuwa na cocaine, nikilewa nisilalamike... basi maji je, naambiwa chujio kuu la maji yote Dar umeme ulikatika kwa hiyo kama nikihisi kitu kigumu mdomoni nteme.... mi basi naenda kulala ata kama kuna kunguni....!!!

    ReplyDelete
  3. michuzi acha mizengwe. jana nimepost comment juu ya hii picha naona umeamua kuifuta bila kuiweka humu ndani. sikujua una ukiritimba wa kutaka kuandika yale yanayokufurahisha wewe tu. tafadhali iweke post yangu (unajua nazungumzia post gani. kukukumbushia kidogo ni ile niliyosema hao watu wa ukerewe hakuna haja ya kuwaabudu kwani ni wabongo na huko ukerewe hakuna raha kama watu wanavyodhani kwani stress ya maisha ni kubwa. niliandika kwa urefu zaidi kwahiyo tafadhali weka post yangu humu ndani watu waisome. ama kama hutaki maoni yetu basi hakuna haja ya kusoma hii blogu yako yenye ukiritimba.

    ReplyDelete
  4. Michuzi vipi hapo ndo shemeji nini???????????////

    ReplyDelete
  5. Ha ha haaa. we Michuzi kwa kutuvunja mbavu! jinga kweli kweli. halafu katuni ya ki-mouse ni mwisho. big up braza.

    ReplyDelete
  6. HOYA MICHUZI. MIMI NIMECHOKA NA WEWE KUWAABUDU WATU WA UKEREWE. KWANI WANA NINI? MI MBONA NAONA KAMA WAMECHOKA SANA? UKEREWE? UKEREWE? NJOO HAPA MIDWEST NDO UTAONA KAMA WATU WA UKEREWE HAWANA MAANA...KCKS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...