
jk akiwa na mwanzilishi wa nyumba ya sanaa dar, sister jean pruitt na waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. seif khatibu wakati wa tamasha la chuo cha sanaa bagamoyo. enzi zake nyumba ya sanaa palikuwa na vijana walemavu waliokuwa wakijifunza kazi za sanaa na pia wasanii mbali mbali walikuwa wanapatumia kuonesha na kuuza bidhaa zao. hivi sasa ni naiti kilabu na walemavu hawajulikani walipo. nasikia sister jean ameanza mchakato wa kurejesha hadhi ya nyumba ya sanaa kuwa nyumba ya sanaa na si vinginevyo. na pia hivi sasa anaendesha kituo cha watoto wa mitaani kiitwacho dogodogo senta mtaa wa mansfield. habari zake zaidi bofya hapa
Yaani suti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeachia! Hebu angalieni mkono wa suti (sleeve) - aibu gani hii!!!!
ReplyDeleteHivi anony hapo juu,unayesema suti ya rais 'imeachia' umeangalia vizuri kweli?+au we mwenzetu hujui aina ya suti.Aaahaha ahahha umenichekesha sana!Hii aina ya suti inafanana kabisa na kaunda suti,tofauti yake hizi zina mikono mirefu.Huvaliwa bila shati ndani,hapo mwisho wa mkono wa suti kuna kifungo...sasa huo ndo uwazi kama akifungua kifungo aweze kuivua kwa urahisi.Ndio style yake hiyo ndugu yangu,umeondoka bongo lini?Hata mimi sipo bongo lakini nazijua hizo.Poa,wakati mwingine uangalie kwa makini..halafu utoe maoni yako eeeh,umesikia????
ReplyDeleteNashukuru mungu huyu Bibi amerudi maana manyang'au tayari walishageuza NYUMBA YA SANAA uwanja wa fisi. Kila siku nikipita pale roho inaniuma sana na zaidi ninaposikia serikali imetenga mabilioni kujenga JUMBA LA UTAMADUNI. Watanzania tumuunge mkono bibi huyu kukomboa NYUMBA YA SANAA.Wanautamaduni unganeni nyuma ya bibi huyu mlikomboe jumba lenu.
ReplyDeleteKwa taarifa yenu
ReplyDeletehuyu mama ndiye chanzo cha nyumba ya sanaa kufika hapo na katika makundi yote yanayoigombea nyumba ya sanaa hakuna hata moja linalijali manufaa ya msanii na mzalishaji wa tanzania
Nyumba ya Snaa irudishwe kwa wasanii na si ktk mikono ya waliowahi kuwa pale