
wadau nawakumbusha kwamba huko dallas kuna mbongo ambaye ana ngazi ya juu katika sanaa ya kujilinda kwa mkono mtupu aitwaye sesnsei rumadha fundi (kati) ambapo sasa ana dani 4 baada ya kufuzu katika staili ya goju kwai. yeye ni mmoja wa wanafunzi bora wa sensei nantambu camara bomani aliyekuwa anafundishia karate shule ya zanaki na hadi sasa dojo lake lipo pale.
eeh bwana michuzi kipindi kile ulikuwa unakuja pale Dojo kupiga picha Sensei bomani akishuka toka unyamwezini. Hebu weka hapa bloguni zile picha basi. Sensei Kheri Kivuli bado yupoo? Nidondoshee picha za dojo hapo huku ughaibuni sijaendeleza dojo tena.
ReplyDeleteEeh bwana michuzi nakumbuka kipindi kile Sensei Bomani akishuka toka unyamwezini basi wewe ulikuwa unakuja pale Dojo kupiga picha na story inatoka Sunday News..hebu tuwekee basi zile picha mie toka niingie ughaibuni Dojo basi tena. Hivi Sensei Kheri Kivuli bado yupo?
ReplyDeleteSorry hapo juu isomeke kama "Sempai" na sio Sensei Kheri Kivuli. labda kama amekuwa sensei siku hizi ila nilimwacha akiwa "Sempai"
ReplyDeleteHii sanaa siku hizi bongo naona imefifia kidogo, Enzi hizo michuzi pale TABORA kuna mtu alikuwa akiitwa WAMDAKI na mwingine MAGEMBE, hawa jamaa walikuwa wababe wa sanaa hiyo na kupiga Chuma, walikuwa wanaingia TABORA JAZZ pale RUMUMBA BAR MTAA WA RUFITA, na msururu wa wapambe nyuma. Yaani enzi hizo ukiwa unajua kuzipiga kavu kavu wewe unakuwa kama mfalme wapambe kibao ila siku hizi imehamia kwenye BONGO FLEVA, kila jambo na wakati wake. Nafikiri hawa jamaa ndio waliompa hamasa huyu kijana kuingia kwenye fani
ReplyDeleteBig up on the promotion to "4 dan"
ReplyDeleteShemeji huyo, kaoa kwetu Iringa!!
Hongera bwana Rumadha sasa ni zamu ya kugawaujuzi huo nafurahi hata mama nasikia naye ni mwanafunzi mzuri sana wa mitindo hiyo
ReplyDelete