hii ndo silaha yangu bongo. halafu nina shabaha kweli...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Haaa, hiyo kaka michuzi nakufagilia, unajua kwa sasa inabidi tutumie zana hizo hasa kwa wale tuliojaliwa kupata vigari, Unajua Bongo sasa hivi njiani ni Kero, Foleni acha, daladala fujo kibao, waenda kwa miguu nao ndio usiseme akiona hamna gari havuki, akiona gari laja anavuka, sasa naona tuanze na style ya kupiga nati ikizidi ndio tunawadit...

    ReplyDelete
  2. wewe jifanye mtaalam wa kutumia hiyo silaha halafu umfumue huyo jamaa anayekupa masnep hapo sijui utasemaje

    ReplyDelete
  3. Michuzi, hiyo nakuunga mkono, wajua bongo sasa hivi inabidi tuwe na zana kama hizo.... hasa barabarani mzee, si unajua foleni na vurugu hasa kama umejali kupata kigari chako, haaa noma, maana huku daladala kachomeka, mara wapita kwa miguu wameingia barabarna, mara guta, lakini ukiwa nayo hiyo mambo yakizidi watumia tu watu watatulia wenyewe,ikizidi uzalendo una wadit....

    ReplyDelete
  4. misupu umechoka sasa!

    ReplyDelete
  5. Kommando Yosso wamerudi?

    ReplyDelete
  6. Hahahah..Baba yangu anaiita topito..Hadi leo anayo, anasema hata kama ana 9mm, Uzi, yeye hawezi kuacha kuiweka topito karibu...

    ReplyDelete
  7. inafurahisha sana,inaonyesha we michuzi ulikuwa mchokozi kweli!ulivyoishika manati naona jamaa walikuwa hawakusogelei angalia usije ukaanzisha topic mpya na hiyo manati!

    ReplyDelete
  8. Bola Hio Kaka Misupu Huwezi Kumditopilez Mtu

    ReplyDelete
  9. Afadhali umeamua kwenda kuwinda ndege porini kuliko kuweka mada moto kama za kesi ya Dito ili wanablog wajadili.

    Kesi ambayo imejaa vituko eti hadi majaji hawajui wamfanye nini aliyedharau mahakama kwa kupitia mlango wa majaji ambao hawaruhusiwi watu wengine kupita.Au nayo upelelezi haujakamilika? au ushahidi hautoshi?

    Tumeona watu wakihukumiwa hapo hapo mahakamani kwa kuidharau mahakama na kwenda jela.

    Leo hii ya Dito tunaambiwa bado wanawasiliana na kuangalia uwezekano wa kuwachukulia hatua waliohusika.Very interesting

    Hii kesi nimeamua kuitumia kuandika Thesis kwa ajili ya Shahada yangu ya Sheria.

    ReplyDelete
  10. WAW KAKA

    UNANIKUMBUSHA MBALI, NILIKUWA NIKIUA NJIWA NA MANATI LOL.

    KUMBE WASINGETUMIA NDEGE ULAYA KUUA WALE NDEGE WAARIBIFU WA MAZAO, WANGEKUPELEKA WEWE, ILI WATU WAPATE KITOWEO SAFI LOL

    BIG UP KAKA, NAKUFAGILIA SINA ZAIDI.

    MUNGU AKUBARIKI.

    ReplyDelete
  11. Hiyo rafiki yangu kunguru wa zenji wakikuona nayo tu humuoni hata mmoja. Kwa hapo nakuunga mkono kwamba sasa kunguru hawatakusogelea ukiwa unajivinjari na kupata nyama choma Bar za bongo.

    ReplyDelete
  12. Aisee Michu unanikumbusha enzi zangu nikiwa nyamwage.

    ReplyDelete
  13. Nasikia huko Mbozi jamaa wanatengeneza bunduki kiurahisi kama vile wewe ulivyotengeneza manati, cha kusikitisha ni kwamba badala ya serekali kuwa endeleza inawakamata na kuwafungulia kesi

    ReplyDelete
  14. Hivi Michuzi hapo LAPF Millenium Towers-Makumbusho wanaruhusu kubeba manati na kufanya mzaha namna hiyo just in front mbele tu ya car park yao? Ukishika manati namna hiyo halafu ukaingia kichakani utaona tetere wanavyodondoka wenyewe kama kumbikumbi vile!

    ReplyDelete
  15. mh michuzi umetoka kwenye keroro mzalendo uongo?big up home boyz sport club arusha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...