
nipo na mdau maarufu aitwaye 'mzee wa ustawi' kwenye kikao cha harusi hongera baa sinza. hapo chini kuna ujumbe toka ughaibuni ulioletwa sasa hivi...
Habari kaka Michuzi,
Habari za safari ya huko Dumila!! Mimi naendelea vizuri na shule hapa Brest. Vipi hali hapo nyumbani.
Sasa hivi nafuatilia sana habari za JK Boys na nina matumaini makubwa sana kwamba tutafanya vizuri katika mechi ijayo dhidi ya Senegal. Nina rafiki zangu wanatoka Senegal hivyo huwa nawaambia kwamba tutawafunga. Kitu kinachonipa faraja ni kwamba sasa hivi Tanzania tunaogopwa kidogo kiasi kwamba mahasimu wetu wanahaha kutafuta habari zetu kadiri ya uwezo wao, hawa jamaa zangu wamekuwa wakinipa habari za timu yetu kila siku, na wao hizi habari wanazipata toka kwao Senegal, hiyo inaonyesha kwamba wanatuogopa kiasi kwamba wanahaha kutafuta kila taarifa za kutuhusu, wanafahamu kwamba tuliweka kambi Brazil, na hii leo wameniacha hoi baada ya kuja na kuanza kunitajia list yetu kama kocha alivyotangaza, wamenitajia majina yote ya wachezaji walioitwa na Maximo kiasi kwamba nikashangaa sana.
Na sasa hivi nina matumaini kwa kuwa kule Senegal wana kamgogoro ka kiutawala katika soka, kwani waziri anaamua mambo ya kiufundi na wamekuwa wanakosa organisation kidogo, nilisoma jinsi Tony Silva alivyokuwa ana lalamika kuhusu haya mambo, lakini sifahamu kama huko nyumbani wanafahamu kwamba hawa jamaa wana matatizo na pia hawa jamaa zangu wana hofu sana kiasi kwamba wameshaanza kuniambia kwamba wao wanaowachezaji wazuri lakini wanakosa timu( hapo namaanisha kama ilivyokuwa timu yangu ya Real Madrid, kwamba wachezaji wazuri tunao lakini tunakosa timu nikiwa na maana hakuna uelewano uwanjani).
Hivyo ni nafasi nzuri kwa timu yetu kuwaadhibu huko huko kwao. Mimi naamini tukifanikiwa kuwafunga hawa Senegal katika mechi hii basi safari ya Ghana itakuwa imeiva kwani baada ya hapo ni hao wamakonde na BF, na Senegal tena nyumbani, hivyo kazi ni mechi hii inayokuja tu.
Kama utapata nafasi ya kuonana na hao KJ Boys wape salam, mimi nipo pamoja nao daima na kila la kheri.
Remigius
Remigius
Nakuunga mkono mdau!hawa jamaa tunawachinjia hukohuko kwao,ndio dawa.Wanatuogopa sana,nasikia Diof ndio alikuwa amepewa kazi ya kusambaza mikanda ya mechi tulizocheza na Msumbiji na BF,ila watapotea.Maana sasa hv improvement ni kubwa sana tofauti na mechi hizo mbili.Kuku kuku tu, jogoo jina.Hawa jamaa wamebaki majina,recent records zao si nzuri as a National Team.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Taifa Staz!
ReplyDeleteKwa kweli tukiwachinja Senegal nitaamini tuko gado.I am excited but at the same time I am scared to how much time we kept in this,hata Mhe.Rais mwenyewe ana mategemeo makubwa sana na siku hii.I FUCKING CAN`T WAIT,I AM SO READY TO SCREEM RIGHT NOW.
ReplyDelete