msanii na kiongozi wa kundi jipya la bongofleva la tmk wanaume halisi sir juma nature akijifua na mistari kambini kwake tmk leo, tayari kwa bonge la tua kutembelea mikoa kumi kuzindua albamu ya 'ndege tunduni' ambayo ni ya kwanza toka sir nature ajitenge na wanaume tmk mwishoni mwa mwaka jana. kijana huyu bado anaongoza wasanii wa bongo wa kizazi kipya kwa kuwa kivutio. kuna siku ratiba yake iligongana na shoo ya koffi olomide na ikabidi akatiwe uchache ili asogeze mbele shoo yake ama sivyo mzee mzima angeumbuka. ratiba kamili ya tua hiyo ni kama ifuatavyo...
TMK WANAUME HALISI ALBUM LAUNCH TOUR 2007


1. Dar es Salaam – Diamond Jubilee Hall Saturday 31st March, 2007

2. Musoma - Magereza Club Saturday 07th April, 2007

3. Mwanza – City Cabana Sunday 08th April, 2007

4. Tanga – Mkwakwani Stadium Friday 13th April, 2007

5. Morogoro – Vijana Club Saturday 14th April, 2007

6. Dodoma – NK Club Sunday 15th April, 2007

7. Mbeya – Dandoo Hall Friday 20th April, 2007

8. Zanzibar – Amani Stadium Saturday 28th April, 2007

9. Moshi - Aventure Club Tuesday 01st May, 2007

10. Arusha – Tripple A Club Saturday 05th May, 2007





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. zichangechange kale kamkangafu kako-"kabenzi" uka-trade inn upate angalau chaser mayai isiyokuzidi umri

    ReplyDelete
  2. Hiyo camp mh! mbona kazi.. kuna bima kweli huko. Kwasababu nyoka akitoka huko sijui itakuaje.

    nadhani hata mwandishi wa habari hamna anayetaka kumtembelea kwenye hiyo camp wamhoji jinsi anavyojiandaa kwa tuor yake...kwasababu walinzi wa hii camp nadhani ni big boas and cobras tu.


    Au ndio mama mwenye nymba alichange bafu basi hilo hata hakutaka kulipeleka kwenye jalala

    ReplyDelete
  3. heheheh hii kali yaani kweli watu bongo wamechoka sana, yaani huyu ndo celebrity... kweli kazi ipo kusaidia jamii ya kitz

    ReplyDelete
  4. huyu jamaa nampendea kitu kimoja tu,haigizi,yupo kama alivyo,anayafagilia maisha ya kibongo halisi,sio kama wale wanaoishi tandale wanashinda masaki.
    au wale waliojilipua eti nakujiona tayari ni wazungu na kukandia maisha waliyotoka.
    na huyo jamaa hapo juu anayekandia usafiri wa mwenzake eti umemzidi miaka wakati yeye hata mkokoteni hana.
    MANYUNYU

    ReplyDelete
  5. Jamani mnajua tunapo toa comments, tuwe makini sana. Nani anayejua Nature kwanini anapendwa sana na watu? Asilimia ngapi ya Watanzania wanaishi maisha ambayo Juma Nature anajaribu kuyaonesha?Mie binafsi nadhani ni 80%. Sasa unataka aoneshe sehemu kama Masaki ni asilimia ipi ya watz wanaoishi maisha ya Ki-masaki kama sio hao kila leo mnao walalamikia kuwa wala rushwa wakubwa!!!Kwa lugha nyingine naweza sema kuwa wanamuziki ni kama waandishi wa habari lengo kubwa ni kutoa taarifa/habari kwa wahusika ambao ni watatuzi wa mambo hayo au wale tulio wachagua wazitumie fedha zetu tulizo zitoa kwa Serikali(taxes)kutatua matatizo ya nchi na sio kujenga hayo majumba yao ya Masaki ambayo nyie mnataka Juma Nature ayaoneshe. Huyo Michuzi mwenyewe mie nakubaliana nae hata picha ile aliyopiga akiwa uswazi huku madimbwi ya maji kibao yakionekanana barabarani kwa mnaojisikia vibaya!Chakarikeni tuijenge Tanzania! Kama upo abroad tuma hizo dollars nyumbani, invest ktk biashara utakuwa umechangia sana kuijenga Tanzania, kwa maana kwamba watu wawili, tatu au zaidi watapata ajira ktk biashara yako/zako. at end You will realize that umewasaidia watu kibao japo huja zitoa hizo fedha direct ktk nchi au serikali lakini utakuwa umechangia sana ktk ujenzi wa nchi yako. Nyie mnao jifanya ughaibuni ndio kwenu hamna lolote, watu tupo huku tunaona watu wanavyostrugle na maisha including watu wenye nchi zao sembuse nyie na Vi-Visa nyenu vyenye restriction kibao!!! Toeni hizo kasumba zisizo endelevu!Hata ulipozaliwa haukuanza kutembea, ulitambaa kwanza then baadae ukaanza kusimama tena mpaka ujishikilie sijui ktk mawe, maana nyumbani kulikuwa hakuna kitu cha kujishikilia labda!then ukaanza kutembea. Kwa hivyo hata huyo Nature ameanza kusima sasa na hilo Benz lake la kifahari! Baadae atakapo anza kutembea mtakuta anamiliki hayo Majumba ya Masaki na Hammmer kama sio ndege kabisa. Na kwasababu hapokei rushwa wala hali fedha za wanyonge inaweza mchukua miaka kibao na labda hato fanikisha kumiliki vitu hivyo. Kuweni makini! Nani anafikiri kuwa UK au USA yote ni kama London na New York! kuna sehemu nyingine zimeshoka. Ila tunaangalia % kubwa imeendelea kuliko sehemu zisizo endelea sasa kwa ku-generalize twasema zimeendelea. Tukazani kuiendeleza tz then 80% ya watz ikiendelea huyo juma nature atahamia upande huo wa masaki!kwasababu uswazi TMK itakuwa 20% tu na Bro Michu atapiga picha kama Posta(City center) kama wadau mnavyotaka. Na mtakuwa mnaicheck hii blog huku Remote zenu zikiwa mikononi badala ya kuwa unaicheck hii blog ukiwa hoi bin taabani kwa kufanya kazi 21hrs per day.Ndio maana watu saa nyingine mna-comments zisizo enda shule sio kwa hamjui vitu ila ni uchovu tu kutokana na hizo kazi zenu za kutumia minguvu mingiiii!!
    Asante sana Watanzania, Tanzania itajengwa na sisi watanzania wenyewe na wala hakuna nchi nyingine yenye huruma wa kutusaidia wataishia kutunyonya resource zetu kwa sayansi na teke linalokujia kwa jina la uwekezaji!!!Bro Michu mie naomba huu ujumbe uweke ktk page kubwa badala ya kuwa kwenye Comments kama nilivyoitoa. Asante in advance kwa kufanya ivyo

    ReplyDelete
  6. we anon hapo juu, mi nasukuma usafiri wa maana, nenda www.crysler.com tafuta gari inaitwa aspen
    we lazima bado uko bongo unawaza mkokoteni

    ReplyDelete
  7. Hapo temeke ndipo alipokulia sasa mlitaka akapige picha Holiday inn au masaki ili iwe nini? nyumbani ni nyumbani hata kama pangoni,jamaa hapo ndio kafika acheni kuponda kujifanya wazungu saana wakati kwenu original its the same,maisha popote as long as you are comfy

    ReplyDelete
  8. He he he Kibla matata full nakuona mtu wangu....iyo ndo life halisi,tmk halisi,wanaume halisi,kamua baba miflex... hawa machekibob na comments zao achana nao,they don't know why unaitwa kibla!!! kudadesa....full kufunika.Hawajui wapi ulitokea, where is TMK??? namiss sana hii life kudadeki.....u talk abt celebrity Lol... huyu ni nyota tuh! wa kibongo kudadesa....

    ReplyDelete
  9. EBANAEEEEE! HIYO ALIYOKALIA SIO BATH TUB KWELI! hALAFU INA KUTU HIYO HATARI !!!!!

    ReplyDelete
  10. Ila kijana punguza bange,mashabiki wako bado wanakuhitaji.

    ReplyDelete
  11. Ulimbukeni unawasumbua nyie huko ughaibuni!wengine mnacomment upuuzi kwakuwa mlishindwa kufaulu shule ndio maana mkakimbilia huko,sasa mnateseka na kazi za ki kuli na kupata vigari vya mkopo mnajiona mmefika.Msijidanganye,baadhi yenu huku TZ mmeacha ndugu zenu wanaishi maisha magumu kuliko hata hayo mnayodhani Nature anaishi.Hata hizo gari mnazosema zimezidi umri hawana hata ndoto ya kuzinunua,achilia mbali kununua benz.Acheni ulimbukeni!Huyu kijana anauwezo mzuri kulingana na elimu yake,mpeni moyo ajitahidi,na nyie kama mnauwezo sana saidieni na ndugu zenu walio huku.Kuna raha gani ya kuendesha Aspen wakati ndg zako wa damu huku hata nauli ya daladala wanakosa?!Acheni ulimbukeni

    ReplyDelete
  12. hiyo bath tub itakuwa imeibiwa uani kwa "tajiri" mmoja wa TMK. Manaake ukiwa "tajiri" TMK vijana wa kijiweni lazima waanzishe Camp mlangoni kwako. Wanakujumlishia tu hesabu ukilala tu umeuwawa

    ReplyDelete
  13. Hey wewe annoy unayesema watu walio ughaibuni walifell na kukimbilia nje na pia maisha yao ni ya shida huko ughaibuni. Sasa kwa nini mnataka wasaidie ndugu wakati wewe unasema wanaishi kwa shida. Nyie mlio bongo wenye uwezo mngesaidia ndugu zenu walio fell shuleni wakakimbilia nchi za nje.Sidhani kama hao watu waliwaomba hela ya ticket lakini kila siku hamuishi kusema hamsaidii ndugu zenu. Kama wewe ni moja wa wale watu mtoto wa mjomba kaenda majuu basi wote mnafikiri mmekua tajiri utakaa hapa hapo kusubiri akusaidie wakati wewe hata kum wish well alivyokua anaondoka hukutaka. Ulikua unaona wivu.
    Acheni majungu bwana.
    Kwanini nyie tu ndio mnataka msaidiwe? Wakati nyie mnasema wanashida huko sana? Kwanini msisaidie wa kwenu walio nje ya nchi? Hela ni hela it doesn't matter where you spend it. Mtumie ndugu yako hela unayejua anateseka na yupo nje ya nchi na atakushukuru. Wewe si upo bongo unauwezo bwana.

    ReplyDelete
  14. Jamani mjue kuwa wanamiziki wengi tu ughaibuni walikulia kwenye shida pia kuliko mnavyoona kwenye miziki yao. Young gerenration na very few of them kama nicole richie ndio walikulia kwenye raha toka utototni mwao. Majotiry walikulia kwenye hoods. Lakini wakiwa wanatafuta hela hawaji label na hayo maisha all the time.
    Wengi wakishatoka kwenye hoods wanakua hawapigi picha kila siku kuonyesha oh this is the life I grew up in. Wanakubali kuwa ni kweli walikulia kwenye hoods na wanaenda kila siku kujaribu kupeleka misaada kwenye hizo hoods na kuwasaidia vijana wadogo waweze kuondoka kwenye hoods kila siku. Hawaiendekezi hiyo life style. Wanakua so proud kuonyesha na kukubali kweli walikulia katika umasikini lakini look who lakini angalia nimekuwa nani saa hivi.

    Sasa nyie mnaosema kuwa huyu amekulia huku na hataacha maisha ya huku basi wote wa jinga. Nini maana ya maendeleo. Tofautisha culture na maendeleo. You can keep your culture and stay true to yourself but strive for development.

    Unavyosema anaonyesha hali halisi ya maisha yake. Kwasababu kuwa na mabath tub nje yenye rust hiyo sio life style tunayo accept hiyo ni unhealth. Watoto wakijikata hapo sio vizuri. Au hata kutupa hilo bafu kwenye gari la taka inahitaji hela? Inaoshesha life style yetu ya uchafu, ya kutokujituma sio unasikini. Hapa hii picha kila mtu anachoona ni bafu lenye rust na halitumiki tena lakini badala ya kulitupa au kulipeleka kwa recycle tunaliweka hapo nje tu...Huu si umasikini ni uchafu

    Na pia kama mtu anaendesha benzi hata kama ni yale makabati lakini una gari bongo you can afford to live in a decent room in africa.
    Kama nyie mnaosema tum support at the same time kila siku anishia kuishi kwenye hali ile ile aliyonayo hata kabla hajawa mwanamuziki, tutashtuka na kuwaza may be huyu mtu sio wamaendeleo au ama ana use his money to support another life style kama bangi na drugs vile. Kwa hiyo kama unataka tufurahie kuwa tuna kusupport vizuri show us something. Tutafurahi tukiona mwanamuziki aliyekulia temeke, manzese au wapi kule na leo kwa kuimba na siye kumsupport amehamia au amejenga nyumba yeke kwenye neiborhood nzuri. Natutaelewa sio kila mla rushwa ndio anaweza kuishi vizuri bongo. Tutafurahia sana tu na tutawasupport watoto wetu pia wakitaka kujiunga kwenye hii career. Kama kila siku tunaona album yako na tunanunua na kwenye concert tunaingia laini kila siku bado mtu anarudi kuishi kule kule itatufanya tuelewe kuwa hamna ya sababu ya kusupport anything.

    Tesiendekeze uchafu na kusema haya ni maisha yetu. Umasikini sio uchafu

    ReplyDelete
  15. hey huyu jamaa ana mpinzani kwa bongo fleva.. anayetaka kuamini haya asiyetaka me c mlazimishi, mambo ndo hayo tour ya ndege tunduni inakalibia, embu fikilia inspector ndani, karama ndani c balaa hilo.. big up wanaume halisi hapa vumbi 2 kudadadeki... kamua kibla

    ReplyDelete
  16. wasanii wa kitanzania hawathaminiwi. laitani wangekuwa wanathaminiwa basi kila msanii mwenye akili angekuwa na nyumba yake. kwa vile hakuna anopenda maisha ya kimaskini. nafikiri msela wangu unafagilia maisha ya kuazima nguo ili uonekane bomba sio? lakini si fresh mwanangu. waswahili wanasema
    1. mcheza kwao hutunzwa. kadhalika
    2. mficha uchi hazai

    ReplyDelete
  17. Hili swala la vita baridi kati ya watanzania walioko ughaibuni na walioko home nilisha lisema hapa.

    Mpaka mtu utadhani ni watu wa mataifa mawili wanagombana, inahuzunisha sana ni kama vile mtanzania akisha toka nje basi grade ya kiutanzania ina ongezeka jamani hii inaonyesha jinsi wengine walivyo bado chini sana kimawazo.

    Yaani hata sielewi tunachotaka, (tungekuwa tuna weka hata nic names) maana kuna ma anon wametoa points nzuri hapo juu.

    sijui ni kisomo haba? umasikini? au nini kinachofanya watu wawe na reactions za aajabu????

    Tuache hivi vita sisi wote watanzania kwanza ndoo sababu mojawapo wote tunaingia hapa (kuliko mataifa mengine wanaojua kiswahili)la sivyo kama unasema wewe sio mtanzania tena unafanya nini hapa? pia mjue kwamba popote ulipo ukifa mwili wako unadai uzikwe chini ya ardhi uliyo toka na isipo fanyika hivyo huna amani hata huku uliko iwe peponi au ahela
    Walaah!

    Mungu ibariki Tanzania viongozi na hasa kabisa Eeeeh Bwana watu wake!

    ReplyDelete
  18. Anony wa march19,8;35
    Hatusemi kwamba amekulia hapo hataacha maisha ya hapo..tunachosema ni kwamba hapo alipo ndio pako hivyo sasahivi sasa tunauliza hao jamaa wanasema hapo hapafai walitaka akapige picha msaki?au asafishe kwanza kwa jili ya picha?that wont be his real life then hatufagilii uchafu panapowezakana kusafisha na pasafishwe inawezekana hilo bafu kuna watu wanalihitaji kwajili ya shughuli za ujenzi labda wa vitu vingine then kwa nini litupwe? wajuaje kama lipo kwa muda tu hapo,wenzetu huko mmezoea kutupa kila kitu lakini sio bongo hata wazungu wana recycles ila sisi hatuna pa kuweka kama huko ndo maana unaliona hapo
    hatugalii uchafu lakini tutafika tu huko mnakotaka tufike hata rome haikujengwa kwa siku moja.

    ReplyDelete
  19. Hamna cha cold war wala nini wakati mwingine ukweli unauma. Mshukuru Mungu sana akikusaidia hata utoke siku moja nje ya mahali unapoishi kila siku ili uone tofauti kati ya maisha yako na ya watu wengine. Hata kama unakaa bukoba ukienda mwanza utafumbuka macho na kujifunza moja au mawili. You can't tell the difference if there is nothing to compare with.

    I bet you hilo bath tab halitatumika tena lakini hapo ndio limefika. Na wanaoshangaa sio wanajifanya au kwa vile wako nje ya nchi ni kwa vile wameshajua tofauti.

    Kwa wale mliosoma accouting TZ mnaelewa mwingereza na mmarekani wanatunza vitabu vya uhasibu tofauti kutokana na jinsi wanavyofikiria kuwa utajiti nini. Mmoja wao anaamini kuwa ukiwa na liquid cash nyingi ndio utajiri na mwingine anasema asset ndio utajiri.
    TZ nafikiri tumekuzwa kwa kuamini kuwa asset ndio utajiri pia. Mtu ana magari saba nje ya nyumba hata kama huyatumii ilimradi ana uwezo wa kuyanunua tu basi yatajaa tu nje. Ndio maana matajiri wetu hawalast ni wachache waliogundua ku mix and match ndio wanakua wanatanua kwa muda mrefu ila wengine wanakuja leo wanaondoka leo.

    Nikiendaga TZ nyumbani, wazazi wangu wanakuaga wananishangaa sana kwa vile nikiwa nasafisha nyumba, natupa au nagawa vitu ambavyo naona hawavitumii tena. TZ tunapenda sana kukusanya vitu tu (sijui ndio kuaccumulate wealth!!!) Hata kama mtu anajua fika kuwa kitu fulani hatakitumia tena basi kinawekwa tu. Vitu vingi tu ndani ya nyumba hata paku pita hamna. Kama kuna kitu huwezi kurepair tupa au kama kinatumika lakini hukitumii tena heri ugawe kwa mtu mwingine atakitumia na atakushukuru.

    Nchi za watu hizi tunazoishi ukitembea njiani kumeandikwa no loitering. Miji ambayo utakuta kuna maduka hata ya waswahili au wahamiaji wengi basi ni kuchafu tu pamoja na hayo maandishi kuwa kila mahali. Tumeleta uchafu nchi za watu. Mitaa ambayo wanaishi wenyewe utakuta ni misafi tu. Na mara nyingi nimeona njiani au kwenye subways wenyeji wakiona mtu ametupa kopo la soda au mtu ameacha gazeti chini wao wanaokota na kuweka mahali panapotakiwa. Najiuliza kwanini siye mpaka tulazimishwe au tuambiwe do this, don't do that. Kwanini hatujitumi tuu wenyewe. Wenzetu kuna siku wanaenda kusafisha parks au community swimming pools for free.
    Tuwe na moyo wakujituma jamani.Tusiwe slaves kwasababu watumwa ndio wanasubiri kutumwa

    Michuzi asante sana kwa kutuwekea picha hizi na matukio ya kila siku na watu kuona na kujadili. Naomba muelewe haya ni mawazo yangu lakini simzungumzii mtu wala huyu kaka ila nazungumzia our society in general. Feel free to disagree with me.

    ReplyDelete
  20. Anon hapo juu. Hayo ni maoni yangu nilichogundua baada ya kutembelea sana hii site na kusoma mara kwa mara maoni ya watanzania waliko nje na waliko home wengine wana fagilia na wengine wana dharau kila kitu cha bongo. Sasa sijui kitu gani kina kuonyesha sija toka nje?? pole sana au mnataka nambia mtu hana uhuru wakutoa maoni hapa? Issa sema wewe mwenye hii kitu

    Fo ur info I am out of country for more than 25 solid years but that wont stop me from loving my country/people. U want check me? here u r: mere12muko@yahoo.com

    ReplyDelete
  21. Du insha zinachosha sana, hebu m summerize basi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...